22/06/2024
Serikali ya Tanzania imezindua rasmi ujenzi wa majengo pacha Jijini Nairobi, Kenya yatakayotumika k**a ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini humo na kitega uchumi ambapo hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi.
Ujenzi huo utafadhiliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF na kujengwa katika eneo la kibiashara katikati ya Jini la Nairobi kwenye eneo ambalo Serikali ya Kenya iliipa Tanzania kwa ajili ya kujenga ofisi zake za Ubalozi.
Akiongea katika tukio la uzinduzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, amesema mradi huo ni sehemu ya mkakati mpya wa Serikali kuhakikisha inatumia maeneo na majengo yake yaliyo ughaibuni kuingiza fedha za kigeni badala ya kutumia fedha za kigeni.
Amesema mkakati wa Serikali unataka kuiondoa Tanzania kutoka kutumia kiasi cha shilingi bilioni 29 kwa mwaka kulipa kodi kwenye Balozi zake ughaibuni na badala yake kuingiza kiasi cha shilingi bilioni 36 kwa mwaka k**a mapato ya uwekezaji k**a huo wa Kenya.