23/01/2021
Karibuni kwenye simulizi mpya kabisa, comment zenu na like ndio zitafanya niendelee kuipost humu. Karibuni
NIMETUMWA: 1
By: Atuganile Mwakalile
Whatsapp: 0714443433
Ilikuwa ni siku ya Ijumaa ambapo wanafunzi siku ya leo waliruhusiwa mapema sana kurudi nyumbani, na walikuwa na furaha sana ya kuwahi kurudi nyumbani k**a kawaida ya wanafunzi.
Berinda na Blenda walikuwa ni ndugu wa mama na baba mmoja ambao walipishana mwaka mmoja tu, hivyo watu wengi waliwaita mapacha na walifanana sana pia walisoma pamoja katika hii shule, kwahiyo siku ya leo ilikuwa ni furaha sana kwa upande wao pia.
Basi waliongozana na wenzao kurudi nyumbani, njiani waliachana na wenzao na kuanza safari wao wawili ya kurudi nyumbani kwao huku wakiongea ongea mambo yao mbalimbali yanayowafurahisha.
Walipokuwa njiani kukaribia na nyumbani kwao, Blenda alihisi haja ndogo na kumwambia mwenzie,
“Nataka nikajisaidia, ngoja niingie hapo”
Mwenzie akasema,
“Mmmh Blenda usiende peke yako, mama alishakataza kabisa hiyo tabia. Ngoja twende wote”
“Jamani na wewe Berinda, si unisubiri kidogo hapo”
“Hapana, mimi ni dada yako Blenda”
“Dada uliyenipita mwaka mmoja tu!!”
Kisha Blenda akacheka na kuingia kwenye kichaka kwaajili ya kujisaidia, wakati huo Berinda alikuwa akimsubiria ila alishangaa kuona ndugu yake amekawia kutoka kwenye kile kichaka ikabidi amfate na kumkuta amesimama huku ameshika karatasi, Berinda akamuuliza,
“Wewe Blenda hilo karatasi ni la nini? Tunachelewa nyumbani”
“Limeandikwa neno moja tu linanishangaza, nimeliokota hapo”
Berinda alisogea na kulisoma, liliandikwa kwa herufi kubwa,
“NIMETUMWA”
Berinda akamuangalia Blenda na kumuuliza,
“Umelipata wapi?”
Blenda alijibu bila wasiwasi,
“Nimeliokota hapo chini”
Akionyesha kwa nyuma yake, walipogeuka hapo nyuma walikuta mwili wa binadamu ukiwa umenyongwa, wakajikuta wakitupa lile karatasi na kupiga kelele halafu wakatoka kwenye kile kichaka.
Walikimbia sana hadi walipofika chini ya mti walisimama huku wakiwa wanahema sana, basi Berinda akamuuliza mdogo wake,
“Inamaana Blenda hukuona? Hukuona pale k**a pana tatizo?”
Blenda alikuwa anahema sana na kusema,
“Sikuona chochote, niliokota tu lile karatasi. Naogopa dada, naogopa sana”
“Inaogopesha sana Blenda, twende tukamwambie mama”
“Mmmmh dada sidhani k**a ni wazo jema kumwambia mama, tusimwambie kabisa kuhusu hili jambo. Mama atatupiga sana”
“Kwanini atupige? Tumeona kitu cha tofauti ni lazima kutoa taarifa”
“Hapana Berinda, tusifanye hivyo tafadhali. Kwanza mama atauliza tulikuwa tunatafuta nini huko porini si unamjua mama alivyo mkali! Halafu atanipiga sana mimi sababu anajua kuwa mimi ni mbishi sana”
Berinda akakubaliana pale na mdogo wake Blenda kuwa wasiende kumwambie mama yao kuhusu lile tukio.
Basi waliondoka pale na kufika nyumbani ambapo mama yao aliwashangaa pia kwa wao kuwahi kurudi,
“Mbon mmewahi sana kurudi? Mmeshadanganyana huko eeeh!!”
“Hapana mama leo tumetolewa mapema”
“Bora umejibu wewe Berinda maana angejibu huyu Blenda nisingeamini kabisa, ni mjanja mjanja sana huyu mdogo wako”
Wale watoto walikaa kimya tu kisha mama yao aliwaonyesha chakula cha wao kuweza kula na kufanya waende kuvua yale mavazi ya shule ili wapate kula.
Wakati Berinda na Blenda wakila, kuna mtu alimfata mama yao kisha mama yao akatoka kwa haraka sana pale nyumbani na kufanya wenyewe wasielewe chochote ila kuendelea kula tu pale.
Walipomaliza kula, Blenda alianza kumwambia dada yake,
“Au mama ameitwa kwenda kuona yule mtu aliyeuwawa?”
“Nadhani itakuwa hivyo Blenda, ila tusifikirie hayo sana yatatuchanganya akili mdogo wangu”
“Kweli dada yatatuchanganya akili”
Basi walipomaliza kula waliondoka zao na kwenda kucheza na watoto wa mitaani.
Waliwakuta watoto wakicheza mchezo wa kukimbia na kujificha, wakaungana nao, kwahiyo na wao walikuwa wanakimbia na kwenda kujificha.
Basi muda huu watoto wote walipatikana kasoro Blenda hadi walianza kuulizana,
“Jamani Blenda ameenda kujifichia wapi? Ni mambo gani haya mtu anajificha hadi haonekani?”
Ikabidi watoto wote waingie kwenye msako wa kumtafuta Blenda sasa, wakati wakiendelea kutafuta Berinda akaona kuna jumba ambalo halijaisha yani ni gofu tu akaamua kuingia humo huku akiita,
“Blenda, Blenda, Blenda”
Kweli kabisa Blenda akajibu,
“Nipo humu dada”
Basi Berinda alifata ile sauti ya Blenda ilipokuwa inatoka, alimkuta Blenda amesimama huku ameshika kipande cha karatasi, akamuuliza,
“Umeshika nini hiko?”
“Kimeandikwa k**a kule dada”
“Kivipi?”
Berinda akasogea ili kuangalia, akaona kile kipande cha karatasi kimeandikwa kwa herufi kubwa pia,
“NIMETUMWA”
Berinda akashtuka sana na kumuuliza Blenda,
“Umekitoa wapi?”
“Hapo”
Yani sehemu ambayo Blenda alionyeshea mkono kulikuwa na mwili wa mwanadamu umelazwa pale, na yeye alionekana amenyongwa.
Wote wawili walishtuka kisha Blenda alitupa kile kikaratasi na kukimbia pamoja na dada yake, walikimbia hadi walipofika nyumbani ndio walipumzika.
Berinda akamuuliza pale mdogo wake,
“Ulikuwa unatafuta nini kwenye lile lijumba Blenda? Mbona una hatari hivyo mdogo wangu?”
“Nilienda kujificha dada, hata sikujua k**a nitakutana na jambo k**a lile”
“Kujificha gani huko? Wenzio wote tunajificha karibu, wewe kwanini unaenda kujificha mafichoni k**avile? Ona sasa kwa ambacho tumeona kule? Tumwambie mama?”
“Uwiiii dada hapana, usimwambie mama. Atanipiga sana aniue jamani, mama alishatukataza kucheza michezo ya kujificha, dada usimwambie mama”
“Ni kweli mama katukataza michezo ya kujificha ila wewe nae umezidi, kujificha gani sasa kule? Kila mtoto alikuwa anakutafuta wewe Blenda maana wote walipatikana kasoro wewe, kumbe upo kwenye jumba ambalo lina mauaji. Haya mambo mbona yanatisha, wale watu wamekufa ujue!!”
“Najua ndio dada, ila mimi sikuona chochote wakati nashika lile karatasi dada yangu”
“Inaogopesha na kusikitisha, kwahiyo unasisitiza kuwa tusimwambie mama!”
“Ndio tusimwambie mama”
Basi wakaamua kunyamza maana wakaona wakisema itakuwa ni balaa tupu.
Muda kidogo mama yao alirudi pale nyumbani huku akisema kwa masikitiko,
“Jamani kuna mambo ya ajabu yameingia, kuna mtu amekutwa msituni ameuwawa halafu pembeni yake umekutwa ujumbe umeandikwa kuwa NIMETUMWA tena kwa herufi kubwa, hata sijui ni nani aliyefanya ufedhuli huu. Haya mambo yanaogopesha sana”
Berinda na Blenda walikuwa kimya kabisa, kisha mama yao akawaambia,
“Sasa Berinda utaosha vyombo maana wewe ndio mkubwa halafu Blenda utaenda dukani kununua mafuta ya kura ili nipike chakula cha usiku”
“Sawa mama”
Basi k**a walivyoambia, Berinda alisogea kwenye vyombo na kuanza kuosha vyombo wakati huo Blenda alienda zake dukani alikotumwa.
Hadi berinda alimaliza kuosha vyombo, mdogo wake Blenda alikuwa hajarudi, basi Berinda akaamua kwenda kumfatilia maana alijua wazi kuwa mama yao akijua kuwa hajarudi itakuwa ni msala zaidi.
Basi alienda hadi dukani ila hakumkuta Blenda na aliambiwa kuwa kaondoka muda mrefu tu, akajiuliza kuwa atakuwa kapitia wapi, basi akaanza kupita kwenye njia huku akiita,
“Blendaaa, Blendaaaa, Blendaaaa”
Kuna mahali alipita na kuisikia sauti ya Blenda,
“Nipo huku dada”
Basi Berinda alizunguka nyuma ya nyumba hiyo na kumkuta Blenda akiwa ameshika karatasi, kwanza Berinda alishtuka sana na kuanza kuangaza angaza labda ataona mwili mwingine wa binadamu ila hakuona chochote, akamsogelea mdogo wake na kumuuliza,
“Wewe Blenda, ni nini hiko umeshika”
“Soma dada”
Berinda aliangalia, lilikuwa ni karatasi lililoandikwa kwa herufi kubwa,
“NIMETUMWA”
Basi Berinda akamuuliza,
“Umelitoa wapi?”
“Hapo”
Walipoangalia wakauona mwili wa mtu akiwa amenyongwa k**a wale wawili, hapo waliogopa sana na kuanza kukimbia.
Walikimbia hadi nyumbani kwao huku wakiwa wanapumua sana hata kuingia ndani hawakuingia, ila Berinda alimsema mdogo wake,
“Una nini leo Blenda? Unaokota karatasi za ajabu na kuna mambo ya ajabu”
Mara Blenda akasema,
“Dada umeona ile karatasi pale chini, basi huwa naona k**a vile”
Kisha Blenda akainama na kuokota lile karatasi kisha wakakuta imeandikwa vilevile kwa herufi kubwa,
“NIMETUMWA”
Walijikuta wakiogopa kuangalia hata mahali ambapo wameokota lile karatasi maana walijua lazima kuna mtu kauwawa pia.
Itaendelea….!!!
Kwa mawasiliano 0714443433 au 0765692210
By, Atuganile Mwakalile.