01/05/2021
MWANANGU
Mwanangu nakwita kwema,
Sauti itokeako,
Hadhi fani taaluma,
Uzidi ya babayako,
Adili usiwe nyuma,
Wengi wajifunze kwako,
Uniitike mwanangu,
Urithi wangu simali,
Nihai leo mzima,
Naghani hili andiko,
Kesho juwa litazama,
Namara sitakuweko,
Neno hili nalituma,
Liwe mkumbushi wako,
Uniitike mwanangu,
Urithi wangu simali
Nahifadhi ujesoma,
Mana kesho zamu yako,
Kuzisuka tungo njema,
Zikafunze nduguzako,
Wewe ndo yangu alama,
Nawe uweke yakwako,
Uniitike mwanangu,
Urithi wangu simali
Mwanangu yangu kalima,
Iwe k**a tajilako,
Utunze yamgu heshima,
Vinanda tupia huko,
Tungo usitie ngoma,
Yakataza maandiko,
Uniitike mwanangu,
Urithi wangu simali
Hata mambo yakikwama,
Linda ninenayo kwako,
Taasisi hatachama,
Nawenye pesa kuliko,
Kamwe wasije kutuma,
Kuiponza fani yako,
Uniitike mwanangu,
Urithi wangu simali,
Wala sijeshikatama,
Wabezapo tungo zako,
Yalisha nikuta nyuma,
Tazama yangu mafiko,
Kesho yako utavuma,
Mrithi huwa kuliko,
Uniitike mwanangu,
Urithi wangu simali,
Tungo yakufika tama,
Arshadi ndio niko,
Karibu kuweka koma,
Nilifanye pumziko,
Lamwisho ninalosema,
Halahala dini yako,
Uitike wito wangu,
Mwanangu mtii mola.
By
Abuu.ArshadTAZA@