04/01/2023
katika maisha yetu humu tunamoishi yanatukuta mambo mengi magumu na sisi tunaoishi maisha yetu ndio tunaojua wapi na nini tunapitia na kipi ni kweli na kipi ni uongo na nini ukweli na nini ni uongo katika maisha yetu,ukipata muda wa walau wa dakika 1 kuweza kufurahi na nafsi yako jitahidi kufanya hivyo kwani kesho unaweza ukapita katika magumu zaidi na ukakumbuka nyakati ambazo ulikuwa umepata muda huru wa kufanya mambo yako na haukuutumia ipasavyo.
Usiogope kuwa peke yako katika ku-enjoy huko kwani watu uja na kuondoka na mwisho wa siku pia wakija wanaweza wakaondoka huku wakikuvunjia heshima yako,wakikukosea adabu,wakakushusha thamani,wakaiondoa amani ya moyo wako na maisha kwa ujumla,kutokuwa na shukurani.
Husiwategemee watu sana katika maisha yako kwani watu huja na kuondoka na hawatokusaidia katika kutafuta hicho ulichokipata ila wao watakunyang'anya chako ulichokipata kwani wao hawawezi na hawana maarifa ya kutafuta k**a uliyokuwa nayo wewe,husitegemee kukupa ila tegemea kukupora ama kunyang'anywa kwa kutumia kila namna sababu wao wana maarifa madogo na ni WADHAIFU kupitiliza.
Usimtegemee mtu anayefanya ujinga ama upumbavu wowote kwako bila ya ridhaa yako na akaonesha kiburi juu yako,majivuno na ubabe k**a ana uwezo wa kukusaidia,mtu huyo mjinga na MPUMBAVU hawezi kukusaidia nae anahitajika kusaidiwa katika kila namna hawezi kukusaidia.
ukimsikia siku anasema anataka kukusaidia huyo ni muongo anakudanganya anataka ajue wapi unapatia mkate wako ili akuharibie.