02/08/2022
FURAHA YANGU.
Mtunzi; Juma Dali
0717 861 372.
Sehemu ya 05.
Safari yangu ilikomea nyumbani lakini ilikuwa k**a bahati kwani sikukuta mtu yeyote, nilipitiliza hadi ndani niliingia chumbani kwa wazazi wangu, hata sikujua ni nini nafuata kwenye chumba cha wazazi wangu, nilianza kupekua kanakwamba kuna cha kwangu nilisahau lakini sikupata chochote.
Yaani kila nilichokifanya nilifanya tu lakini ukweli sikufahamu nafanya kwa ajili gani "aaah mbona hamna chochote" nilijisemea baada ya kukosa kile nilichokuwa nakitafuta nilitoka hadi chumbani kwangu ambako nako sikupata chochote akili yangu ilikuwa k**a imechanganyikiwa yaani hakuna nilichokifanya kikatimia sikutaka kuendelea kubaki nyumbani nilitoka tena, akili yangu haikuwa sawa kabisa nililudi tena kijiweni k**a nilivyotoka ndivyo nilivyokuta hakukuwa na mtu yeyote nilikaa kwenye benchi ambalo kila nilipofika nilipendelea kuketi.
Mawazo tele yaliendelea kuusonga ufahamu wangu wa akili k**a kuna siku ambayo nilifanya vitu vya hovyo basi ni pamoja na hii niliingiza mkono mfukoni lakini sikupata nilichokitarajia "dah inamaana nimeacha nyumbani" nilijisemea mwenyewe huku nikiendelea kujipapasa mifukoni "dah leo" nilijisemea na kujisonya mwenyewe tu hakika nilikuwa chizi kasoro kuokota makopo.
Wakati nikiendelea kujisonya sonya nilisikia sauti iliyonifanya niache kile ninachokifanya "oya vipi mbona hivyo mkulungwa" niligeuka na kumtazama mtu alienisemesha "vipi msela mbona k**a umevulugwa" aliendelea kunisemesha.
Lakini sikujibu chochote zaidi ya kumtumbulia macho tu kanakwamba sikumsikia alichozungumza "Edu vipi msela mbona unaniangalia tu mshikaji wangu naongea lakini hunijali kulikoni msela" aliniuliza huku ak**eti karibu yangu sikumjibu chochote badala yake nilikaa kimya na kuendelea kujisonya mwenyewe.
Hali hii ilimshangaza sana rafiki yangu alitamani kujua kinachonisibu lakini alibaki kukaa kimya tu.
Alinitazama kwa dakika kadhaa bila shaka alijiuliza maswali mengi kuhusu mimi alijitahidi kuvumilia lakini moyo wa uvumilivu alimkana na kutomtambua kabisa "Edu mshikaji wangu vipi mbona husemi chochote kulikoni kuna mtu amekuzingua niambie mimi mshikaji wako peter" aliongea kwa upole sana.
Nilibaki njia panda na nisijue nini cha kumueleza kwani moyo wangu ulijaa kisasi ambacho sikikijua ningekilipaje kwani akili yangu ilikuwa mbali nilikuwa nawaza kisasi tu na sio kitu kingine.
Nilimuangalia rafiki ya peter ambaye alikuwa mpole mithili ya maji mtungini nilitamani kumueleza kile kinachonisibu lakini nafsi ilikataa na kunieleza utakuwa udhaifu mkubwa sana k**a nitaeleza kile kilichonikuta asubuhi ataniona ni bwege mzee k**a yule ananipigaje na kumuangalia ama kweli nilikuwa mjinga wa fikra sikuwaza chochote zaidi ya kisasi akili yangu iliniambia usimueleze chochote kaa nalo moyoni kwani ni aibu kubwa sana.
Nilimuangalia Peter ambaye alionyesha kiu ya kutaka kujua kila kinachonisibu, nilimuangalia sana mwishowe nilinyanyuka na kuanza kuzipiga hatua kwa ajili ya kuondoka hali hi ilimshangaza Peter "Eduu" aliniita.
Niligeuka na kumuangalia lakini sikuitika nilibaki kumuangalia tu "vipi lakini msela mbona umebadilika sana leo vipi hauko sawa kabisa" aliendelea kuniongelesha.
Je unadhani kwa hasira alizonazo Edward atafanya nini? usikose sehemu inayofuata.
Mnaosoma na kupita kimya kimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema k**a inapendeza sema maana huo ndio mtaji pekee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii like, comment na share kwa wingi ili tuzidi kusonga mbele pia like ukurasa huu ili uwe wa kwanza kuona kila kitakachopostiwa humu.
Je nini kitaendelea?.
Ahsante na kwa heri.