Juma Dali

Juma Dali Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Juma Dali, Arts and entertainment, Majengo, Newala.

CHOZI LANGU.Mtunzi;Juma Dali0717 861 372.Sehemu ya 01.Ilikuwa ni majira ya usiku wa manane, nami k**a ilivyo kawaida yan...
08/01/2021

CHOZI LANGU.
Mtunzi;Juma Dali
0717 861 372.

Sehemu ya 01.

Ilikuwa ni majira ya usiku wa manane, nami k**a ilivyo kawaida yangu muda huo ndio muda maalumu wa kurejea maghetoni kwangu, katika pitapita zangu nilijikuta napita moja ya jumba lililopo, mitaa ya uswahilini Uswazi. nikiwa bado naendelea na safari yangu gafla nilisikia maongezi flani yaliotoka ndani ya nyumba ile, kanakwamba walikuwa wanabishana.
Kutokana na kuwa na tabia flani za ushilawadu maana nisijifiche sikutaka maongezi yale yanipite hivihivi. Hivyo nilijisogeza kwa kunyata kanakwamba simba anawinda swala, kwani nilizipiga hatua za polepole mno kiasi cha wenye nyumba kushindwa kunisikia, laiti k**a ungeniona ungeweza jiaminisha labda ni kibaka hivyo nilikuwa kwenye mpango wa kuvamia nyumba ile.
Na kukwapua kile kilicho kizuri kinachopatikana kwenye nyumba ile, lakini la! hasha haikuwa hivyo nilikuwa na lengo kupiga chabo tu na si vinginevyo.
Nilizichanganya kwato zangu hatimae nililifikia jumba lile, nilijisogeza dilishani ili kuyapata kwa uzuri maongezi yote yanayotokea ndani, akili zangu zilinituma huenda ndani kulikuwa na mchezo usio wa kawaida unafanyika.
Mchezo ambao hauna refalii wala rezimeni wala kamisaa wa mchezo, na hauna mashabiki, mchezo ambao hucheza baba na mama tu tena hucheza kwa siri bila ya mtu yeyote kufahamu.
Hivyo nilijitahidi zaidi kujibanza moja ya dirisha ambalo ndimo maongezi yalikuwa yanatokea, nilisogeza vyema sikio langu ili nipate kusikia kile kinachozungumzwa ndani.
nilijitega kwa uzuri sana nadhani hakuna siku ambao nilikuwa makini zaidi kusikiliza jambo k**a siku hii, na niliweza kuyapata kwa uzuri zaidi kabisa maongezi yote yaliokuwa yanaongelewa ndani "mkewngu majali mkewangu" "eenh mumewangu" aliitika kwa sauti ambayo wazi ilionekana kujawa na usingizi mzito, ila kwa kuwa aliitwa hakuwa na budi kuukatisha usingizi na kuamka ili kusikia kile kilichomfanya mumewe kumuamsha.
Alijiamsha na kukaa sawa ingawaje usingizi haukutaka kumuacha kwani bado ulizidi kumng'ang'ania, aliyafikicha macho yake kuondoa usingizi ulikoma kutoka.
Nami kwa ufinyu wangu wa akili kusikia mtu akiamka, nilizidi kukaa sawa sikusikia maumivu yoyote ya mbu waliokuwa wanagema damu yangu tamu niliwacha tu waendelee na shughuli yao zaidi niliwabadilishia mikao tu ili wafaidi vizuri, niliendelea na kazi yangu kanakwamba mpiga picha hivyo nilitaka nisihalibu kazi nikakosa wateja.
Akili yangu ilinituma huenda wanabadilishana upande yaani wanaingia kipindi cha pili cha mtanange usio na refalii nilijitahidi kuvutia taswira, jinsi mtanange huo ulivyo.
Dah! inaelekea ilikuwa mechi ya kukatana na shoka sio mechi ya kitoto niliongeza umakini zaidi ili nipate kusikia kwa uzuri zaidi.
Mazungumzo kwa upande wa ndani yaliendelea "nisamehe sana kwa kukatisha usingizi wako mkewngu" mume alianzisha maongezi "hapana Bidhim mumewangu hata hujanisumbua ni wajibu wako hivyo huna haja ya kuomba msamaha wewe endelea tu baba"alimaliza kwa kupoza sauti, hali iliopekea Bidhim kujisikia faraja.
"unajuwa tokea tufunge ndoa huu ni mwaka wa pili sasa hatuna mtoto na unajuwa ndoa bila mtoto haina maana kwani tunatafuta kwa shida unadhani nani atakuja kurithi hizi mali zote tunazozitafuta, haliakuwa hatuna mtoto na uwezo wa kumlea na kumpa mahitaji yote muhimu tunao".
Bidhim alionekana kuwa na kiu ya kupata mtoto nae siku moja aje kuitwa baba, ila ni ukweli usiopingika ndoa bila mtoto haiwi na radha kifupi haipenezi yaani hainogi, ukizingatia wamefunga ndoa kwa ajili ya kutekeleza abada mojawapo ilioelezwa kwenye vitabu mbalimbli vya muumba wa mbingu na ardhi.
"ni kweli mumewangu hata nami najisikia vibaya kila nikiwaona rafiki zangu wanavyocheza na watoto wao inaniuma mno, ni afadhali umeliwaza hilo ila ulikuwa unafikilia nini?" kumbe hata mke nae alihitaji mtoto "mimi naona sasa ni wakati wa kumtafuta mtoto" "hata nami naunga mkono hiyo kesho twende hospitali tukaangalie uzazi" alichangia "sawa langu lilikuwa ni hilo tu unaweza ukaendelea kupumzika" "haya sawa" kila mmoja alijilaza kivyake.
dah iliniuma mno kumbe yalikuwa maongezi ya kawaida tu hata wale mbu waliokuwa wanafaidi damu yangu niliwapa dozi tena sio ya kitoto, "dah watu wengine bhana mimi nilijuwa kuna mambo yetu wao wanajadili watoto dah" kisha nilimalizia na kusonya.
Sikuona haja ya kuendelea kubaki tena mahali pale hivyo niliamua kuondoka huku nikiwalaumu kwa kunipotezea muda.
Asubuhi ya siku iliofuata waliamka wakiwa wenye afya tele k**a walivyopanga kwenda hospitalini basi ilikuwa hivyo.
Baada ya majibu ya daktali ambayo yalionyesha uzazi wanao hivyo ni maamuzi yao kuzaa walifurahi, yaratibu mipango ya mtoto ilichukuwa nafasi yake.

Naam hii ndio hadithi yangu ya kwanza kuandika leo nimeileta kwenu je unaionaje tililika mdau je wanandoa hawa walifanikiwa kupata mtoto? swali la kujiuliza hayo na mengine mengi usikose kufutalia kigongo hiki.
Mnaosoma na kupita kimyakimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema k**a inapendeza sema maana huo ndio mtaji pekee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii.

LIKE,COMENT NA SHARE KWA WINGI ILI IWAFIKIE WENGI IFANYE ISOMWE NA WENGI ONYESHA UPENDO WAKO.

Lakini like ukurasa huu ili uwe wa kwanza kuona kila kitakachopostiwa huko pia waalike rafiki zako ili familia izidi kuongezeka.

AHSANTE NA KWA HERI.
CHOZI LANGU NANI WAKULIFUTA?.

JE UTANIPENDA?.Mtunzi;Juma Dali0717 861 372.Sehemu ya 10."karibu mzee chapu" alikalibisha mzee Robert "ahsante mzee mwen...
08/01/2021

JE UTANIPENDA?.
Mtunzi;Juma Dali
0717 861 372.

Sehemu ya 10.

"karibu mzee chapu" alikalibisha mzee Robert "ahsante mzee mwenzangu", alikalibia na kuketi kwenye kiti, "za tokea jana" mzee Chapu alianzisha maongezi ,"aah za tokea jana safi labda kwa upande wako, mmh vipi familia nyumbani inaendeleaje?" "aah familia nyumbani inaendelea vizuri".
"eenh nipe habari" "eenh mzee mwenzangu wewe acha tu" alishusha pumzi na kumuangalia, mzee Robert usoni kisha akaendelea, "nimemuona mwanao akiwa na kijana alafu kilichonishangaza muonekano wao ni wazi kabisa wanaonekana wana uhusiano".
mzee Robert alistuka "kufanyaje" aliuliza kanakwamba hakusikia chochote, "nimemkuta mwanao Vanessa akiwa na kijana" "kwa hiyo kijana mwenyewe unamjua?" aliuliza,
"eenh namjua yule kijana aliefiwa na bibi yake mwaka jana", alikumbuka "nani Kenedy" "eenh huyo huyo" mzee Chapu alidakia.
Kutajwa kwa jina la Kenedy kulimstua sana mzee Robert, aliinamisha kichwa chini kukumbuka jambo, "mzee Robert" aliita mzee Chapu, sauti ya wito ndiyo ilimtoa mzee Robert kwenye tafakali nzito.
"eenh eenh" aliitika kwa kuweweseka "kulikoni mzee mwenzangu" aliuliza mzee Chapu. Baada ya kuona utofauti "hapana" alikanusha,
ili kuficha uhalisia mzee Robert aliamua kubadili mada.
*******
Safari ya dakika arobaini na ushee iliwafikisha nyumbani Vanessa alitamani hata aruke kwenye pikipiki amkimbilie mama yake aliemuona kwa mbali, ila alishindwa kufanya hivyo kutokana kuwa pikipiki ilikuwa kwenye mwendo taratibu ilipungua na hatimae kusimama.
alishuka haraka haraka na kumkimbilia mama yake "mamaaa' aliita kwa sauti kubwa kabla ya kufika "eenh mwanangu" nae aliitika kwa tabasamu pana usoni mwake.
aliacha kuchanja kuni, na kumkimbilia mtoto wake ambae alimkumbatia kwa furaha "waooh ote walisema kwa pamoja kenedy alibaki kuwa mpenzi mtazamaji, taratibu aliachia tabasamu hafifu usoni kwake, hakutoa neno lolote zaidi ya kuwaangalia mama na mtoto walivyojawa na furaha.
"eeenh za siku mwanangu maana nimekukumbuka jamani" alianzisha mazungumzo baada ya kujitoa kwenye kumbatio, "nzuri mama ila nimekukumbuka sana" alisema Vanessa "hunishindi mimi", walisalimiana kwa furaha, Kenedy alifungua mabegi na kuyashusha chini.
Vanessa na mama yake waliacha mazungumzo yao na ote walisaidiana na Kenedy kuingiza mabegi ndani, maongezi mafupi yalichukua hatamu kiasi cha kumfanya Kenedy kusahau kazi yake ya bodaboda, nae alijikuta anaungana nao kupiga soga.
Siku mbili zilipita tokea Vanessa arudi shule, Kenedy hakuacha kumtaembelea mara kwa mara pale alipopata nafasi na pale iliposhindikana alijitahidi kulazimisha angalau amuone Vanessa, kwake aliamini ndiyo furaha pekee kwenye maisha yake.
nako upande wa mzee Robert tokea kuupata ujumbe wa kurudi kwa mtoto wa kaka yake kulimvuruga mno,mawazo mengi yalipita kichwani kwake.
alikumbuka mara ya mwisho kuzungumza na kaka yake mzee Julius kabla ya kifo chake "nitamtunza shemeji pamoja na mtoto, kwani mtoto wako ni mtoto wangu" kauli hii ndiyo iliyomuumiza kichwa, ilikuwa kauli ya ahadi kwa kaka yake kabla ya umauti kuwa atamtunza Vanessa lakini sasa imekuwa kinyume chake aliwaza mno, aaha nimepata wazo" alifurahi sana.

mmh je wazo gani alilolipata mzee Robert na anataka kufanya nini kwa Vanessa hayo na mengine mengi usikose sehemu ijayo.
Mnosoma na kupita kimyakimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema k**a inapendeza sema maana huo ndio mtaji pekee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii.

LIKE,COMMENT NA SHARE KWA WINGI ILI IWAFIKIE WENGI ISAIDIE KUSOMWA NA WENGI.
Lakini pia usiache kulike ukurasa huu ili uwe wa kwanza kuona kile kitakachopostiwa huko. Leo jioni tutaanza simulizi mpya iitwayo CHOZI LANGU. hivyo like ukurasa huu ili usipitwe na kigongo hiki.

AHSANTE NA KWA HERI.
JE UTANIPENDA?.

JE UTANIPENDA?.Mtunzi;Juma Dali0717 861 372.Sehemu ya 09.Baada ya muda chakula kilikuwa teali, alimtengea mama yake "wew...
07/01/2021

JE UTANIPENDA?.
Mtunzi;Juma Dali
0717 861 372.

Sehemu ya 09.

Baada ya muda chakula kilikuwa teali, alimtengea mama yake "wewe je mbona hunawi maji" aliulizwa baada ya kuona hana mpango wa kula, "aah mimi sijisikii kula kwa sasa hivi" "hujisikii kula umekula wapi wakati ote tulikuwa pamoja au unaona aibu, sasa unionee aibu mimi".
mama Vanessa hakuacha utani wake, kutokana na kuimbiwa mno wimbo mmoja njoo ule, kenedy aliona isiwe shida alinawa maji, na kujumuika pamoja japo hakujisikia kula kwa wakati, huo alijilazimisha ili kumlizishisha mama yake.
walikula kwa pamoja mpaka chakula kilipoisha, alitoa vyombo na kuvisafisha, na baada ya kumaliza shughuli zake aliludi kuendelea na soga za hapa na pale. Maisha yaliendelea kwa Kenedy kumuuguza mama mkwe, wake hadi pale alipotengamaa vizuri, kitendo cha kuuguzwa kilimfanya mama Vanessa kuzidisha upendo kwa mkwe wake, licha ya kumsomesha mtoto wake na kumsaidia majukumu madogomadogo.
Upande wa Vanessa baada ya kupata taarifa alizidi kumpenda Kenedy na kujiapiza kuwa hatokuja kuwa na uhusiano na mwanaume mungine, kwake Kenedy alimuona ndiye mwanaume bora kuwahi kutokea kwenye ulimwengu huu.
Hivyo hapaswi kumpoteza, mara kwa mara alipopata nafasi ya kuongea nae hakuacha kumsifia, ambapo alivuka mipaka na kwenda mbali zaidi alimfananisha na malaika mwema kwake, hali hii ilimfanya Kenedy kujisika mwenye furaha wakati ote nae hakuacha kumsifia mpenzi wake kwa upendo anaomuonyesha kwake, waliweka ahadi mbalimbali baada ya Vanessa kuhitimu masomo yake na moja ya ahadi walioiweka ni kufunga ndoa, pindi tu Vanessa atakapohitimu masomo yake. waliosema siku hazigandi hawakukosea siku ziliendelea kukatika mithiri ya mshumaa wenye moto.
Hatimae likizo ya awamu ya pili iliwadia walifanya, mitihani ya kumaliza kidato cha tano na kuingia kidato cha sita, baada ya kumaliza mitihani walirejea nyumbani, awamu hii Vanessa hakutaka tena kubaki shule alirudi nyumbani, taarifa za ujio wa vanessa zilimfurahisha sana Kenedy aliona k**a masaa yanakwenda taratibu sana, muda ulifika alikwenda kumpokea hakuamini macho yake baada ya kumuona wake alibaki kujishekesha tu, "waooh" Vanessa alimuwahi alimkumbatia kwa furaha, lakini wanakumbatiana mzee wa makamo kidogo aliwaona aliwaangalia kwa muda kisha akaendelea na safari yake ambae nae alifika kwa ajili ya kumpokea mwanae, hawakufahamu chochote k**a kuna mzee aliwaona, waliendelea na shughuli yao, "eeh wewe ndo umebadilika hivi". Kenedy alionyesha mshangao wake alimuangalia juu chini ni k**a hakuamini "jamani mbona niko kawaida ila wew ndo umebadilika" Vanessa aliongea kwa sauti iliyojaa madeko "kweli umebadilika umekuwa mzuri tofauti na mwanzo", "mmh inawezekana ila mimi sioni k**a nimebadilika najiona niko vilevile" alijikagua.
lakini alijiona yuko kawaida hapakuwa na maongezi mengi zaidi ya kuondoka kuelekea nyumbani upande wa pili baada ya kutoka stendi kumpokea mwanae mzee Chapu alienda nyumbani kwa mzee Robert, alifika na kukaribishwa.

Mmh mzee Chapu ameenda kusema nini kwa baba yake mdogo Vanessa na je atachukua uwamuzi gani baada ya kuambiwa hicho anachotaka kuambiwa, hayo na mengine mengi usikose sehemu ijayo.
Mnaosoma na kupita kimyakimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema na k**a inapendeza sema maana huo ndio mtaji pekee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii.
LIKE,COMMENT NA SHARE KWA WINGI ILI IWAFIKIE WENGI NA ISAIDIE KUSOMWA NA WENGI.
LIKINI PIA USIACHE KULIKE UKURASA HUU ILI UWE WA KWANZA KUONA CHOCHOTE KITAKACHOPOSTIWA HUKO.

AHSANTE NA KWA HERI.
JE UTANIPENDA?.

JE UTANIPENDA?.Mtunzi;Juma Dali0717 861 372.Sehemu ya 08.Baada ya kuhakikisha gari, imetoweka kwenye mboni za macho yake...
06/01/2021

JE UTANIPENDA?.
Mtunzi;Juma Dali
0717 861 372.

Sehemu ya 08.

Baada ya kuhakikisha gari, imetoweka kwenye mboni za macho yake alipanda pikipiki yake na kurejea nyumbani, ila kabla alipitia kwao Vanessa kumpa taarifa mama yake, "kwa hiyo ameenda kushukuru", alishukuru baada ya kuambiwa kuwa Vanessa ameshatoka teali.
"sasa mama ngoja nikuache kwanza mara moja tukaangalie mambo mengine" aliaga, "subiri uji basi utoke bila kula", "aah muda wa kula hujafika nitakunywa baadae sasa hivi bado mapema sana" alisema akiiangalia mkokoni kwake k**a anaangali saa ila aibu hakuvaa saa sasa akiangalia nini duh, "baadae ya saa ngapi au unakunywa chai" aliongea mama kwa kulalamika, "hapana sijazoea kunywa mapema nikinywa sasa sitofanya kazi yeyote usingizi tu" "haya sawa kila la heri" waliagana na Kenedy alipanda pikipiki yake na kuondoka.
Vanessa alifika salama shuleni, hatimae alianza maisha ya shule, siku zilikatika mithiri ya barafu.
Vanessa aliendelea na masomo ya kidato cha tano pia kwa Kenedy aliendelea na mishemishe zake k**a kawaida, mara kwa mara alimtembelea mama Vanessa kumjulia hali na hata kumuachia chochote kwa ajili ya kuyaendesha maisha yake.
Familia ya Vanessa haikutaka kabisa kujishuhulisha na Vanessa kwa chochote waliendelea na maisha yao k**a awali, muda wa likizo ulipofika Vanessa hakutaka kurudi nyumbani badala yake aliendelea na masomo ya ziada mpaka pale shule ilipofunguliwa.
siku moja Kenedy akiwa kijiweni alipokea simu iliomstusha, mpigaji alimueleza kuwa mama yake ameanguka gafla "mama! mama gani?" aliuliza kwa taharuki "mama yako mama Vanessa" nae alimfafanulia kwa ufupi "aah sawa kwa hiyo sasa hivi mkowapi" "tuko nyumbani", "sawa nakuja"alikata simu na kuwasha pikipiki yake "mzee baba wapi tena" aliuliza rafiki yake alieitwa Juma, "aaha nakuja kuna abilia mgonjwa kwa hiyo nimepigiwa simu" hakutaka kuweka wazi "aah poa" Juma alikubali "poa mida" alitia gia na kutoka mwendo wa dakika kumi alifika nyumbani kwa mama Vanessa.
Alisimamisha pikipiki na kuingia ndani, hakubisha hata hodi, Baada ya kuingia ndani alimkuta mama Vanessa akiwa amelala hajitambui kwa pembeni yake, alikuwepo jirani yake alieitwa mama Witness "kwa hiyo wewe ndie ulienipigia simu" "ndio" aliitika mama Witness "sasa tatizo ni nini?" aliuliza kwa mshangao "tukiulizana hapa duh mimi hata sijuwi nimefika hapa nikamkuta amedondoka hapo mlangoni nikajitahidi kumuinua na kumlaza kitandani kwa hata sijuwi nini tatizo", alijieleza kwa kirefu "mmh basi tumpeleke hospitali" aliongea Kenedy "hilo ndilo la muhimu" walisaidiana kumpandisha kwenye pikipiki na safari ya hospitali ilianza, kutokana na umbali uliopo mpaka kufika hospitali iliwalazimu kuchukuwa zaidi ya dakika thelathini kufika hospitali.
Baada ya kufika walipokelewa na kupatiwa kitanda moja kwa moja, baada ya uchunguzi wa daktali alisema kuwa anasumbuliwa na malaria, ambayo yalipanda kichwani, Kenedy alichukuwa jukumu la kumuuguza kupitia pesa zake, siku mbili baadae hali ilitengamaa na aliruhusiwa kurudi nyumbani.
"ahsante sana mwanangu bila wewe sijuwi ingekuwaje" alimshukuru Kenedy baada ya kukaa sawa "usijali mama hilo ni jukumu langu kwani wewe ni mama wa pekee kwangu" alimtuliza "hapana kukushukuru pia ni wajibu wangu k**a mzazi ujue umefanya jambo kubwa sana" alisisitiza "haya nami nashukuru kuona unaendelea vizuri kwa hiyo furaha yangu kukuona ukiwa na afya nzuri sababu wewe ndie mama pekee uliebaki" "sawa" bi miriam hukuwa na neno lingine zaidi ya kuitika "ngoja nikakuandilie chakula" aliongeza Kenedy na hakulemba mwandiko alitoka kwenda kuandaa chakula.

Duh hivi wanaume wenye moyo k**a Kenedy wapo au ndo walishafariki maana mmh si kwa kujitoa huku. ila nina wasiwasi naa hili penzi sidhani k**a litafika salama ila niseme mengi mwisho wakafika salama mpaka ndoa.
Mnaosoma na kupita kimya kimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema k**a inapendeza sema maana huo ndio mtaaji pekee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii.

LIKE,COMMENT NA SHARE KWA WINGI ILI IWAFIKIE WENGI NA ISAIDIE KUSOMWA NA WENGI,ila onyesha upendo wako kwa kulike ukurasa huu ili familia izidi kuongezeka.

AHSANTE NA KWA HERI.
JE UTANIPENDA?.

JE UTANIPENDA?.Mtunzi;Juma Dali0717 861 372.Sehemu ya 07."mama mama!" Vanessa aliita "eenh wewe vipi mbona furaha sana a...
05/01/2021

JE UTANIPENDA?.
Mtunzi;Juma Dali
0717 861 372.

Sehemu ya 07.

"mama mama!" Vanessa aliita "eenh wewe vipi mbona furaha sana ametokea wapi wakati ulikuwa unalia muda si mrefu" aliuliza hukuelewa furaha ile inatokea wapi mara Kenedy alijitokeza nae,
mama alibaki na maswali tu baada ya kumuona Kenedy nae ana furaha k**a ilivyo kwa vanessa.
Alichokisema Vanessa ndicho kilimstua mama "kufanyaje"
"ndiyo hivyo mama Kenedy ameniahadi hivyo kuwa ataniendeleza",
mama alimuangalia sana Kenedy alionekana kutabasamu muda ote, "kweli Kenedy alichokisema mwenzio" aliuliza "ndio mama nimeona si vizuri kusitisha ndoto yake mimi nimeshindwa kuendelea na yeye pia asiendelee hapana kwa hiyo nitamuendeleza kwa kuwa sasa kiasi najiweza".
mama hakuamini alimuacha Vanessa na kumkumbatia Kenedy "hongera sana na ahsante sana k**a umelifikilia hilo haiwezekani ote msisome sasa watoto hao itakuwaje",
mama aliongeza utani kila mmoja alicheka, waliongea wengi ikiwa ni pamoja kupanga mipango ya shule, siku ziliyeyuka mithiri ya mshumaa uwakao na hatimae, siku ilifika ya Vanessa kwenda shule.
kenedy alifika na pikipiki yake kumfuata ili kumsindikiza stendi kwa ajili ya kwenda shuleni "ukasome huko sio kucheza si unanona mama yako hali yangu" alimsisitiza mwanae akimuaga.
"usijali mama nitasoma kwa bidii ili nije nikusaidie siku moja" alimuondoa hofu mama yake "haya kila la heri mwanangu masomo mema ila nitakukumbuka sana maana nimekuzoea sana nitajisikia upweke lakini basi nenda ukapambanie maisha yako ya hapo baadae",
"ahsante maamanami nitajitahidi kusoma kwa bidii" waliagana na Vanessa alipanda kwenye pikipiki safari ya kuitafuta stendi ilianza mwendo wa taratibu ulimfanya mama kuwasindikiza kwa macho mpaka pale walipolamba kona na kumfanya ashindwe kuwaona tena kwani uwezo wa macho yake uliishia hapo, alibaki na majonzi.
Safari iliendelea hatimae walifika kituo cha mabasi, wakiwa wanasubiri gari ili Vanessa aendelee na safari yake maongezi ya kupeana moyo na kufarijiana yalichukuwa nafasi "ukasome kwa bidii ili tuje kuwa na familia bora hapo baadae si unaona maisha yenyewe".
Kenedy alijalibu kumuasa "usijali nitasoma kwa bidii ila na wewe usinisahau ukapata mwingine" Vanessa alionyesha wivu "hapana siwezi kukusahau kwanza natoa wapi jeuli ya kukusahau mrembo wangu malkia eenh".
aliongea na kumshika shavu kisha aliendelea "labda wewe tu ndio unisahau maana hamchelewagi kupata wengine huko shuleni",
"hee jamani huyo mungine atatoka wapi moyoni kwangu uko pekeyako tu babaa" aliongea kwa kudeka sauti ndogo iliotokea puani sauti hiyo ilimmaliza nguvu Kenedy "mmh haya k**a kweli nitafurahi sana japo mmh mshaka".
"mashaka ya nini mumewangu mtarajiwa", kitendo cha kumuita mumewangu kilimmaliza kabisa Kenedy fikra zilimpelekea mbali na kujiona teali wamefung ndoa fikra zilimpeleka mbali na kujiona wako kwenye kwenye bustani nzuri ya maua iliopambwa na maua yenye rangi tofauti pembeni kulikuwa na Vanessa akiwa ndani ya shela jeupe akisindikizwa na tabasamu nono lililoupendezesha uso wake nae akiwa ndani ya suti yenye rangi nyeusi kina kona kulionekana watu mbalimbali wakisherekea harusi yao wengi wao walionekana kujawa na furaha.
mama nae alipendeza na gauni lake la kitenge huku akisaidiwa na tabasamu pana osoni kwake kuukamilisha uzuri wake mabaharia nao hawakuwa nyuma walicheza na kuimba hari ilifanya harusi kuwa yenye kuvutia kwa kila mmoja na kumfanya asijute kuhudhulia harusi hiyo.
lakini isivyokuwa fikra zake zilikuja kuzimwa na mlio wa honi za gari zilizopigwa kwa fujo kanakwamba aliekuwa anapiga honi hizo hana akili timamu, dakika mbili tu zilitosha kabisa basi la kampuni ya MACHINGA LUXURY COACH kuwasili kwenye viunga vya stendi hiyo, ilisimama na wasafiri ote akiwemo na Vanessa walipanda ndani bila kucha viatu vyao Kenedy alimsaidia kum'bebea begi lake na kupeleka ndani.
Ila hakuacha kumsihi kuhusu kuwekeza zaidi akili yake kwenye elimu na mambo mengine aachane nao "usijali kwanza shule yenyewe ya wasichana tupu sasa mambo hayo yatatokea wapi",
aliendelea kumuondoa wasiwasi "tahadhari lazima hata barabarani tu tunashauliwa kuwa makini kwa hiyo wewe umakini unahitajika"
"usijali kipenzi changu mimi ni wako tu kikubwa nitunzie tunda langu" walipata nafasi ya kuongea kidogo kabla ya gari haijatoka alimpa kiasi kidogo cha pesa akaanzie maisha , hatimae gari iliondoka taratibu na kutokomea.

Haya Vanessa huyo shuleni je mambo yatakuwaje ni kweli Vanesa ataweza kulitunza penzi akiwa shuleni na je Kenedy ataweza kuvumilia kwa kipindi chote Vanessa atakachokuwa shuleni bila ya kumsaliti. Hayo na mengine mengi usikose sehemu ijayo.

Mnaosoma na kupita kimyakimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema k**a inapendeza sema maana huyo ndiyo mtaji pekee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii.
LIKE,COMMENT NA SHARE KWA WINGI ILI ISOMWE NA WENGI ONYESHA UPENDO WAKO KWA KULIKE UKURASA HUU ILI UWE WA KWANZA KUONA KILE KITAKACHOPOSTIWA HUMO.

AHSNTE NA KWA HERI.
JE UTANIPENDA?.

JE UTANIPENDA?.Mtunzi;Juma Dali0717 861 372.Sehemu ya 06.Alitoka na panga, Vanessa kuona panga aliona sio pakukaa tena a...
03/01/2021

JE UTANIPENDA?.
Mtunzi;Juma Dali
0717 861 372.

Sehemu ya 06.

Alitoka na panga, Vanessa kuona panga aliona sio pakukaa tena alitoka nduki "shenzi sana na usirudi tena hapa wewe mtoto mdogo unifundishe mimi cha kufanya mali za baba yako unazijuwa wewe sasa rudi tena utamfuata baba yako aliko mpumbavu na nusu wewe" Vanessa alikimbia sana baada ya kuona yuko mbali aliamua kusimama "eeenh kweli dunia hadaa walimwengu hadaa ananitimua k**a hanifahamu eeenh mungu yupo atalipa yote haya " alijisemea kujipa matumaini "hee hata viatu nimesahau" aliongea akijalibu kujikagua.
alikuwa anahemea juujuu hakuwa na lingine zaidi ya kurudi nyumbani alizipiga hatua za kichovu kurudi nyumbani alifika nyumbani na kupokelewa na mama yake, ambapo baada ya kumuona mama yake aliangua kilio "nini tena" alijiuliza mama vanessa aliacha hata kuchambua maharage na kumlaki mwanae "jamani nini tena mbona unalia kulikoni" Vanessa hakuongea chochote zaidi ya kuzidi kuporomosha machozi mama alijikuta kwenye wakati mgumu maana hakuelewa kipi kinachomsibu mtoto wake "jamani nini mbona hunielezi nmekumbwa na nini" alimuuliza huku akimfuta machozi lakini pia nae machozi hayakuwa mbali kwani machozi yalikuwa yakimlengalenga.
Baada ya kutulia Vanessa alieleza kila kitu hakutaka kuficha chochote alieleza k**a ilivyotokea "kufanyaje" mama alimuuliza kanakwamba hakusikia vizuri "mama ndio hivyo nilivyokuambia amenifukuza tena kwa panga" bi Miriam alimkumbatia mwanae na kujitahidi kum'bembeleza "lakini si nilikuambia mimi nilishaona mbali lakini sikutaka kukuzuia sasa umejionea mwenyewe kwa hiyo ndio ujifunze, usijali utasoma japo kwa shida hivyo hivyo" aliendelea kumtuliza lakini wakiwa kwenye harakati za kutulizana ilisikika sauti ikibisha hodi "karibuu" mama alitoka kuangalia nani aliebisha hodi "ooh Kenedy karibu mwanangu" alimkaribisha kwa tabasamu "ahsante mama" nae alikaribia "umepotea sana nyumbani ama ulisafiri" alishusha lawama "aah hapana mambo ni mengi tu mama" Vanessa nae kusikia jina la Kenedy alitoka ndani "duh kumbe na wewe ulikuwa ndani" Kenedy alionyesha kushtuka huku tabasamu pana likiupendezesha uso wake, lakini Vanessa hakujibu chochote zaidi kumtumbulia macho tu.
Hali ilimshangaza sana Kenedy "kulikoni mbona hunijibu" kimya "jamani mwenzio si anakuuliza" mama alidakia kimya, Vanessa hakuona sababu za kuendelea kubaki mahali pale aliamua kuingia ndani Kenedy alibaki na maswali mengi hakuelewa kwanini Vanessa hakumjibu chochote hivyo alibaki kumtazama tu "mama kulikoni mbona sielewi" aliuliza Kenedy "mmh mwanangu we acha tu" "kulikoni sasa niache niache kivipi" aling'ang'ania.
mama Vanessa hakuona sababu ya kumficha tena alimueleza mwanzo mwisho "hee hivi wazee wengine wakoje ila hii yote ni kutokukaa darasani" alishangaa "basi ndio hivyo kwa hiyo huenda ndio chanzo cha kutokukuchangamkia" "aaha sawa"aliitikia kisha nae akaingia ndani alipita moja kwa moja hadi chumbani ambapo alimkuta Vanessa analia, mama Vanessa hakusema chochote kwani aliujuwa uhusiano wao na mara kwa mara Kenedy alijitoa kuwasaidia yeye aliendelea na shughuli zake alizokuwa anazifanya awali.
upande wa ndani, "Vanessa kulikoni mbona unalia tu" alivunja ukimya baada ya kukaa kwa dakika kadhaa ila Vanessa hakuongea chochote zaidi ya kulia tu alijitahidi kum'bembeleza mwisho alitulia, "haya niambie nini tatizo" aliuliza kanakwamba hajuwi chochote "Vanessa alieleza kila kitu hakutaka kumficha chochote, Kenedy alisikitika sana story yake ilimuumiza sana "usijali kwa kuwa mimi sitoendelea na shule nitakusimamia maana k**a ni vincenti nashikashika kwa hiyo nitakuendeleza ili utimize ndoto, haiwezekani tusisome ote" aliongea kwa kirefu, Vanessa alistuka "unastuka nini sasa" aliuliza baada ya kuuona mstuko "kweli utanisomesha?" aliuliza k**a hakusikia vizuri "ndio ila usinisaliti kwani nakupenda sana" Vanessa alifurahi sana alimrukia na kumkumbatia kwa nguvu "ahsante sana kipenzi changu" alishukuru hawakuongea mengi sana waliamua kutoka kwenda kumueleza mama yao.

haya Kenedy amekubali kumsomesha Vanessa unadhani nini kitatokea na je mama atalipokeaje hilo hayo na mengine mengi usikose sehemu ijayo.
mnaosoma kimyakimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema k**a inapendeza sema maana huo ndiyo mtaji pakee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii.
LIKE,COMENT NA SHARE KWA WINGI ILI IWAFIKIE WENGI ONYESHA UPENDO KWA KULIKE PAGE HII ILI UWE WA KWANZA KUONA CHOCHOTE KITAKACHOPOSTIWA.

Je nini kitaendelea?
AHSANTE NA KWAHERI.

JE UTANIPENDA?

JE UTANIPENDA?.Mtunzi;Juma Dali0717 861 372.Sehemu ya 05.Alikubali japo kishingo pande "kwa hiyo utaenda lini huko" mama...
03/01/2021

JE UTANIPENDA?.
Mtunzi;Juma Dali
0717 861 372.

Sehemu ya 05.

Alikubali japo kishingo pande "kwa hiyo utaenda lini huko" mama alimuuliza mtoto wake "mimi nataka niende kesho" aliongea kwa furaha "sawa kila la heri" aliongea hayo akiamka kwenye mkeka walipoketi, vanessa alimtazama sana mama yake alimuonea huruma vile anavyopambana pekee kumtimizia mahitaji yake "usijali mama nasi ipo siku tutafurahia maisha k**a wengine" alijisemea mwenyewe akinyanyuka kumfuata mama yake ndani.
siku iliofuata majira ya jioni aliondoka kuelekea kwa baba yake mdogo k**a alivyopanga ambae baada ya kufariki baba ndiye alipewa jukumu la kumlea na familia, lakini baada tu ya kukamilika shughuli na taratibu zote za mazishi hakutaka kushughulika na chochote kile badala yake alizichukuwa mali zake na kujimilikisha huku akimuacha mirithi halali wa mali mtupu bila ya msaada wowote.
safari ya takribani lisaa limoja ilimchukua vanessa kufika nyumbani kwa baba yake ambapo alipokelewa na mama yake mdogo mke wa baba yake "karibu mwanangu" alimkalibisha akitoka jikoni ila uso wake haukuonyesha tabasamu bila shaka hakulizishwa na ugeni uliofika nyumbani kwake "karibu" alimkalibisha kwenye mkeka "ahsante" alikalibia akiketi kwenye mkeka.
salamu fupi ilifuata ambapo baada ya salamu Vanessa hakutaka kuzunguka sana alimuulizia baba yake "ameenda kijiweni kwao wanakochezaga bao" baada ya majibu hayo kwa Vanessa alimuita mwanae aliejulikana kwa jina la John "john...johhnn" "eeeh"aliitika "njoo" haraka John alifika, baada ya kufika alimsalimia dada yake Vanessa"kamuite baba" "wapi" aliuliza John "kwa mzee Chamkono wanakochezaga bao kule" alimueleza "aah haya" John kuambiwa hivyo alichukuwa berenge lake kwake alikuwa anafananisha na gari alitoka nduki kuwahi ni honi za mdomo tu ndizo zilizosikika dakika kadhaa tu alifika alikoelekezwa pia muda mfupi tena alionekana John akiwa ameongozana na baba yake mzee Robert.
Vanessa baada ya kumuona alistuka lakini hakutaka kuonyesha mstuko wake waziwazi, walifika "oooh Vanessa mwanangu leo umekumbuka nini hadi kuja kututembelea maana tokea afariki kaka yangu ni mgumu kukanyaga huku au mama anakukatazaga" aliongea hata kabla kukaa "John kaniletee kiti" john alizama ndani kisha akatoka na kiti cha kijani "rudisha hicho kachukue chekundu huko uniletee, kijani wewe mtoto mbona huna adabu halaa" aling'aka ni wazi alichukia bila shaka mzee Robert alikuwa shabiki wa wekundu wa msimbazi.
John kugomewa tena mbele ya dada alijisika vibaya alichukia ingawaje hakusema lolote alizama ndani na kuleta kiti kilichotakiwa chekundu alimkabidhi baba yake kisha akatoweka kwenda kuendelea na michezo yake "eenh habari za siku nyingi binti yangu maana tumepoteana sana" mzee Robert alifungua maongezi "aah mmh safi tu" kisha aliamkia, Vanessa k**a kawaida yake hakutaka kuzunguka alieleza kile kilichompeleka ambapo mzee Robert alionyesha kuchukizwa na taarifa alizopewa "kwa hiyo umekuja kuniambia nikusomeshe si ndio" aliuliza mzee Robert kwa dharau huku akiwa amekunja uso "ndio baba" nae Vanessa alijibu bila hiyana "kwa hiyo mama ameshindwa kabisa kukusomesha" aliuliza tena "ndiyo hana pesa kwa sababu niliko sasa ada yake ni kubwa tofauti na mwanzo na mama hana hizo hela za kunilipia ada" alijibu kinyonge "mmh swala la kukusomesha mimi sina hela kwa sasa hela niliokuwa nayo nataka kujenga na nyingine nimcheze mdogo wako John si unamuona alipo pale mkubwa sasa hela ya kukusomesha wewe sitakuwa nayo utanisamehe mwanangu sawa" alimaliza hivyo kwa maelezo yaliojitosheleza "lakini baba kwanini john usimcheze mwakani halafu pesa zilizopo akanisomesha" "hivi una akili kweli yaani nimuache alalie siyo" aliongea kwa kufoka hali hii ilimuogopesha sana Vanessa "ndio alafu baba mimi sasa nimekuwa kwa hiyo nina uwezo wa kujiendesha kwa hiyo mali za marehemu baba yangu unikabidhi" aliamua kuvunja ukimya "hivi wewe mtoto una akili hivi tokea afariki alipofarikia baba yako pale mpaka leo mali ziwepo tu, kwa hiyo mama yako ndivyo anavyokuambaia eenh" mzee Robert aling'aka hasira zilimshika kiasi cha mikono yake kutetema "sasa ni hivi toka kwangu usinivunjie adabu toka kabla sijachukuwa aamuzi mengine" aliamua kumtimua bila haya kwake Vanessa aliona k**a utani lakini mzee Robert alimaanisha kweli kile alichokizungumza, alinyanyuka kwenye kiti na kuzama ndani "sasa nikukute hapo ndipo utanijuwa vizuri mimi ni nani" aliongea akiwa anaingia ndani.

Je unadhani mzee Robert anaenda kuchukuwa nini otea? hayo na mengine mengi usikose sehemu ijayo.
mnaosoma na kupita kimyakimya hamtendi haki k**a simulizi haipendezi sema k**a inapendeza sema maana huo ndio mtaji pekee unaonifanya niilete kwenu simulizi hii.

LIKE,COMMENTI NA SHARE KWA WINGI ILI IWAFIKIE WENGI PIA USISAHAU KULIKE UKURASA HUU ILI UWE WA KWANZA KUONA KILE KITAKACOPOSTIWA KILA SIKU.

je nini kitaendelea?

AHSANTE NA KWAHERI.
JE UTANIPENDA?

Address

Majengo
Newala

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Juma Dali posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share