24/07/2023
Somo: SIKU ZA MWANADAMU
Katika dunia tunayoishi, zimekuwepo siku za aina nyingi sana, mathalani siku ya watoto,
siku ya akina mama, siku ya wazee n.k. Kwa kawaida, kwa kila siku za aina hii, jamii
hukusanyika na kuadhimisha tukio la hiyo siku. Siku nzima ni mjumuisho wa saa
24. Mwanadamu naye anazo siku zake za kuishi hapa duniani kwa mujibu wa maandiko.
MWANZO 6:1-3.....”Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na
wana wa k**e walizaliwa kwao,2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za
wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote
waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na
mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake
zitakuwa miaka mia na ishirini.”.....Mungu alipomuumba mwanadamu,
hakumwekea ukomo wa maisha yake. Maasi na dhambi zilipoongezeka,
Mungu aliamua kuweka kipimo cha kuishi kwa mwanadamu huyo
aliyemuumba, kwa kuwa hawezi kushindana na mwanadamu milele.
AYUBU 14:1-2... “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za
kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. 2 Yeye huchanua k**a vile ua, kisha
hukatwa; Hukimbia k**a kivuli, wala hakai kamwe”... Mwanadamu hana
siku nyingi za kuishi hata abweteke. Hata hivyo pamoja na uchache wa siku
za mwanadamu, Ayubu anasema zimejaa taabu (magonjwa, mikosi, vifo vya
utata n.k.). Leo Mungu anataka kuuleta ukombozi katika maisha ya watu kwa
Jina la Yesu.
Maandiko yanasema katika ZABURI 103:15...”Mwanadamu siku zake zi
k**a majani; K**a ua la kondeni ndivyo asitawivyo.”
AYUBU 10:20.....”Je! Siku zangu si chache? Acha basi, Usinisumbue,
nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo.”....Mungu leo anataka alete matumaini
kwa uliyepoteza tumaini kwa Jina la Yesu.
Maandiko mengine yanasema katika ZABURI 144:44....”Binadamu
amefanana na ubatili, Siku zake ni k**a kivuli kipitacho..”..
KWA NINI TUJIFUNZE KUHUSU SIKU ZA MWANADAMU?
1. Ni kwa sababu Mungu tayari ametupangia muda wa siku za kuishi, na
hivyo ndani ya siku hizi wapo wanaotaka kuzipunguza ili zisitimie k**a
ambavyo Mungu wetu amekusudia.
Endapo mtu anakufa katika kifo cha utata, maana yake mwanadamu huyu
ambaye ni roho iliyopanga katika nyumba iitwayo mwili, atakuwa
hakuzitimiza zile siku za kushi alizompangia Mungu. Katika 1WAKORINTHO
15:40...”Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari
yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.”....
Maandiko yanasema katika KUTOKA 23:25-26...”Nanyi mtamtumikia
Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako;
nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26 Hapatakuwa na mwenye
kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku
zako nitaitimiza..”.... Kumbe inawezekana kabisa kwa siku zako kutotimia
endapo haumtumikii Bwana. Siku za mtu kuna uwezekano zisitimie. Hata
katika kazi yako, unaweza kujikuta unapunguziwa siku za ajira yako endapo
hujamtumikia Bwana inavyopaswa.
AYUBU 15:20.....”Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote, Hata
hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea.”....
Ndiyo maana katika WAEFEZO 6:10-12 imeandikwa ....”Hatimaye, mzidi
kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni
silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa
maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya
falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo
wabaya katika ulimwengu wa roho.”...tunafundishwa namna ya kushindana
na siku ya uovu. Hii ni ile siku ambyo imewekwa ili kumsababishia mtu
matatizo ya aina fulani.
MHUBIRI 7:1.....”Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa
kuliko siku ya kuzaliwa.”........
Maandiko yanasema katika AYUBU 7:1....”Je! Mtu hana wakati wake wa
vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si k**a siku za mwajiriwa?”....... Kila
mtu ana wakati wake wa vita. Usimcheke yeyote unapomuona anapigana
vita, ukasema eti hajui kupigana, kwa sababu kila mtu anao wakati wake wa
vita. Na kila mtu ni kana kwamba ni mwajiriwa aliye kazini, na usipofanya
vizuri utaondolewa kwenye ajira yako. Yesu vivyo hivyo alisema mkulima
anapoliona tawi lisiilozaa, hulikata na kulitupa nje. Msingi wa kuishi hapa
duniani siyo ufanye kazi, au biashara au kuoa na kuolewa,
lahasha‼. Hayo yote ni ya ziada, bali lengo kuu la kuwekwa hapa duniani
ni KUMTUMIKIA BWANA na hivyo usipofanya vizuri utaondolewa na kutupwa
nje.
AYUBU 14:15.....”Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake
unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;”.....
Kumbe maisha ya mtu yanaweza kuwekewa “mpaka”, na ambayo
huwezi kuuvuka. Hata uwe na fedha namna gani, huwezi kuuvuka huo
mpaka. Maisha ya yule tajiri na maskini Lazaro yanatufundisha kuhusiana na
huu mpaka. Tajiri akiwa kuzimu na Lazaro akiwa kifuani mwa Ibrahimu, na
katikati yao ulikuwepo mpaka.
2. Ni kwa sababu Tunataka kuzijua idadi ya siku zetu. Ule wakati wa kukaa
mashimoni umekwisha kwa Jina la Yesu. Danieli aliposoma vitabu aligundua
idadi ya siku za kukaa utumwani zimekwisha. Na hata sisi lazima tusome
vitabu na kwamba zile siku za kukaa chini ya utmwa wa shetani zinakoma
kwa Jina la Yesu.
Mungu wa dunia hii (ibilisi) naye hupenda kuweka mipaka ya siku zetu.
Endapo mtu angeweza kuona mbele ya maisha yake na kuziona balaa
zilizoandaliwa juu yake, hakika hayupo ambaye angesukumwa kuja kanisani
ili kumuomba Mungu amuepushie hizo balaa.
3. Ni kwa sababu Tunataka kuzijua siku za mwanadamu ili tujipime
na kujua jinsi gani tumekuwa dhaifu. Wakati mwingi hata waajiriwa
huchekwa pale wanapostaafu lakini huko mtaani unawakuta
hawajajenga hata kibanda cha kuishi.‼ Ni kwanini? Walipokuwa
ajirani walijisahau, wakaacha kujua kuwa siku za ajira zao zimepimwa.
ZABURI 139:4....”Bwana, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku
zangu ni kiasi gani; Nijue jinsi nilivyo dhaifu.”.... Mtunga Zaburi anataka
kuangalia umri wake wa kuishi na kazi alizomfanyia Bwana ili kujua je
zinalingana?
Usifungwe na kazi au ndugu katika kumtumikia Bwana. K**a alivyofanya
Yusufu, vivyo hivyo na wewe ufanye vivyo hivyo, kwa kumuachia joho yeypte
anayekuvuta ili kukurudisha nyuma katika kumtumikia Bwana.
Imeandikwa katika 1WAKORINTHO 3:9....”Maana sisi tu wafanya kazi
pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.”......
Kuna mwingine ni k**a shamba la Mungu, lakini endapo Mungu anataka
kupanda chochote humtumia.
1WAFALME 16:34.....”Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko;
akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa
kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo
Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa
Nuni.”.... Katika siku za mtu ujenzi unaweza kuendelea. Kuna mtu anaishi,
lakini kuna ujenzi anaoendeleza kuufanya ili magonjwa yampate mtu
mwingine. Kuna mtu anaishi lakini ameandaa mpango mbaya katika maisha
ya watu wengine.
Mungu anataka tuwe na siku nyingi, katika ndoa, familia, ajira n.k. Mungu
wetu siyo Mungu wa siku chache. Anapoponya uponyaji anaoutoa unakuwa
endelevu.
Katika siku za mtu fulani, mabaya yaweza kuletwa kutoka upande mmoja
kwenda mwingine.
Imeandikwa katika 1WAFALME 21:29....”Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili
mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale
mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya
hayo juu ya nyumba yake.”.... Mungu alikuwa ameshaahidi mabaya kumpata
Ahabu,lakini kwa kuwa Ahabu alijidhili Mungu akabadili msimamo wake, ila
mabaya yale yakaelekezwa kwa wana wa Ahabu.
Imeandikwa katika MAOMBOLEZO 5:7....”Baba zetu walitenda dhambi
hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.”.... Katika maisha ya
mtu, kuna wakati uovu ulitendwa na waliomtangulia, lakini mateso yanampata
mtu mwingine ambaye hakuhusika na yale maovu.
Ni kweli Mungu alikusudia uishi miaka 120. Lakini shetani naye [k**a
mungu wa dunia hii] anaweza kuingilia kati ilisiku zako hizi zisitimie, endapo
wewe utakuwa mtenda dhambi.
Asoupe Family