Nukuu zenye kutia moyo

Nukuu zenye kutia moyo katika maisha binadamu razima afarijiwe,atiwe moy na apongezwe.

Nukuu za kutia moyo
hii page unaweza kuwasiliana kwaajili ya biashara za matangazo ya mtaandaoni post kwenye page hii kwa garama nafuu tembelea ukurasa huu mara kwa Mara ama tuna ujumbe mfupi kupitia page hii ya zenye kutia moyoo

09/10/2019

Biashara gani naweza anzisha kwa mtaji mdogo sana?

25/09/2019

THE BLACK HOE OF AFRICA
WRITER: Benedctor Zacharia
YEAR:2018
PUBLISHED: UNPUBLISHED
Utangulizi
Demokrsia ni neno lakigreek lenye maana ya kuwa huru.
Kwahiyo demokrasia ni hali ya mtu kuwa huru ktk kufanya shughuli bali mbali paspo kuingiliwa na mtu yeyote ili mladi tu havunji sheria mama(katiba) za nchi

22/09/2019

next week tutaanza kutoa makara kupita vitabu mbali mbali ikiwemo THE BLACK HOE OF AFRICA
Get Ready.
Kikubwa tu nikutembelea ukursa wetu.Search tu zenye kutia moyo kisha ulike utapata makara hizo kwa mda mwafaka kuanzia wiki ijayo

Nina ndoto kubwa sana Nabado nina safari kubwa tu kuzifikia"Women don't wait to empowered by men if still having power@"
12/09/2019

Nina ndoto kubwa sana
Nabado nina safari kubwa tu kuzifikia
"Women don't wait to empowered by men if still having power@"

06/09/2019

K**a una biashara yako Fanya mipango tangaza naasi katka ukursa huu
Andika tu NUKUU ZENYE KUTIA MOYO kisha like page hili

I LOVE MY COUNTRYTanzania Tanzania Tanzania  Mungu tudumishie upendo sisi wa Tanzania
06/09/2019

I LOVE MY COUNTRY
Tanzania Tanzania Tanzania
Mungu tudumishie upendo sisi wa Tanzania

REST IN PEACE hon.Robert MugabeHakika umetutumikia sisi waafrika kwa moyo wako Wote nenda ukapumzike hakika tumeona dham...
06/09/2019

REST IN PEACE
hon.Robert Mugabe
Hakika umetutumikia sisi waafrika kwa moyo wako Wote nenda ukapumzike hakika tumeona dhamira ya mwenyezi Mungu kukubariki mpaka miaka 95 lengo lilikuwa ushuhudie mabaya ya waafrika kusini wanavyo wafanyia wa Afrika wenzao kawape habari wakina j.k nyerere ,Mandela pamoja nawengine wambiee kumekucha tena S.A

27/08/2019

Mke wangu mimi elimu yake ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasibu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho.

Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.

Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nishafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili k**a yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumuacha afanye "miujiza" yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina katika hati ni yetu wote wawili lakini ndani ya nafsi yangu nakiri hakuna chakwangu hapo.

Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anatamani kuwajengea nyumba wazazi wake, nikaridhia ombi lake. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia k**a kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu k**a nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.

Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia maneno mengi nikamsikiliza sana nikamuambia....

“Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma?

“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili k**a mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho,keshokutwa nitakua k**a fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani yeye atakua milionea.

Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga.Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki.Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga k**a unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vya kwao na wenza wao!”

Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua k**a natania wakidhani k**a nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.

Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wa k**e alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitisho kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakayeendelea kumsumbua mke wangu nitasahau k**a ni ndugu yangu, basi wewe kuanzia sasa nimekwisha kusahau!”

Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha kuhusu msimamo wangu.
Mwaka huu wote ada ya chuo ya mdogo wangu aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anaomba kupitia mgongo wa Mama ili Mama aniombe nimpe.Najua zinaenda wapi nabaki nacheka tu moyoni.

Mdogo wangu nimemsamehe ila natamani ajue kuwa mke wangu ni jembe,ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, akili yangu ni ya darasani tu ila kwa Biashara huyu mwanamke hapana.

Wakati mimi nikiiangalia Tsh 100,000 naona raundi kadhaa za bia Baa,yeye anaiona k**a mtaji wa Biashara itakayozalisha mamilioni.

Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, Si kweli,mimi sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu ataondoka na mali zake.Biashara tunazomiliki sasa sitaweza kuziendeleza na hata nikiwapa ndugu zangu hawataweza kuziendeleza!

: Kuna Wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya Wanawake lakini ni wachache tu wanaweza kukubali.



**credits to unknown author

Daa!!Pole sana jamaa k**ando ushamba wakisi sihivi sasa mpaka mtoane damu
27/08/2019

Daa!!
Pole sana jamaa k**ando ushamba wakisi sihivi sasa mpaka mtoane damu

Address

Moshi
MOSHI

Opening Hours

Monday 00:00 - 23:59
Tuesday 00:00 - 23:59
Wednesday 00:00 - 23:59
Thursday 00:00 - 23:59
Friday 00:00 - 23:59
Saturday 00:00 - 23:59
Sunday 00:00 - 23:59

Telephone

+255753989689

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nukuu zenye kutia moyo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Nukuu zenye kutia moyo:

Share