19/02/2022
*MAMA ETI BABA YETU ATAKUFA LINI.?*
Hakuna siku niliyojisikia vibaya k**a siku moja nipo nyumban, k**a kawaida yangu nilikuwa nimelewa chakar, nimejilaza kwenye kochi. Hapo ni baada ya kumtukana mke wangu na kuwaambia wote waende jikoni.
Ilikuwa ni usiku, baada ya muda njaa ilinibana, nilinyanyuka na kuyumbayumba kwenda jikoni kudai chakula ambacho mke wangu amepika nikiwa sijui hata pesa katoa wapi kwani asubuh sikumwachia chochote.
Baada ya kufika mlangoni kabla sijapiga teke mlango k**a kawaida yangu, sauti ya mtoto wangu wa miaka minne ilisikika akimuuliza mama yake, "MAMA ETI NA SISI BABA YETU ATAKUFA LINI?"
Nilishtuka na kuanza kusikiliza walikuwa wanazungumza nini, "Wewe mtoto nyamaza usiseme hivyo ni vibaya, tema mate chini" mke wangu alimkemea lakini hakujali.
Sasa mbona dada amesema baba yake Jonas amekufa, ameenda kwa Mungu hatarudi tena, kwanini na sisi baba yetu asiende ili tubaki wenyewe?, mtoto aliongea. Mke wangu alijaribu kumkanya lakini hakusikia aliendelea.
Binti yangu wa miaka saba yeye alimkatisha kumuelewesha.
"Baba Jonas anaenda kwa Mungu kwa sababu ni mtu mzuri. Baba yeye hataenda kwa Mungu, ataenda kwa shetan, haendi Mbingun..." alimaliza kumuelewesha mdogo wake, mke wangu alichanganyikiwa zaidi alijaribu kuwakanya lakini yule mdogo aliendelea.
"Heri hata Baba afe maana anakupiga wewe kila siku na sisi, ningekuwa Rambo ningemuua Paap! Paaa! 🤓😳😳Pigo moja tu anakufa, nikiwa mkubwa namuulia mbali……". Aliongea kwa kujigamba.😎
Mtoto aliendelea kuongea kwa msisimko, nilijikuta nasimama wima, pombe ziliniisha, njaa ikakoma, nilianza kutambaa kurudi sebulen, nilishindwa hata kukaa. Niliingia chumban na kuanza kujiangalia kwenye kioo.
Nimefanya nini maisha yangu niliwaza nikikumbuka nilivyokuwa natamani kuwa na familia nzuri, mke mzur na watoto ambao wananipenda. Lakini mtoto wangu mwenyewe wa miaka minne anatamani mimi baba yake kufa! Nilitaman kulia lakin nilijua haitanisaidia, niliingia bafuni na kuanza kujitapisha, nilitapika pombe yote