02/05/2018
Hadithi.. KUNA... Sehemu 06
By. S.Mumwa
Nyie wapumbavu naongea na na nyinyi nijibuni au mumekuwa mabubu pia aibu hii mtaificha kwa mfuniko gani sasa nisikilizeni kwa makini mimi naondoka narudi kijijini staki kuwa sehemu ya laana yenu najua mda umeenda lakini nitafika tu nyumbani iwe leo au kesho na habari zenu zitafika kwa ndugu zenu kwani kuanzia leo mimi siyo ndugu yenu tukikutana popote tupishane tu k**a hatujaonana vile. Mjomba akafungua mlango na kuondoka .........Joy na Ummy walitazamana huku kila mmoja akishindwa hata kunyanyua mdomo baada ya mdaa kidogo kupita walipata nguvu ya kuongea Joy alikuwa wakwanza kuzungumza ............wewe mtoto mjaa laana umeona ujinga wako ulipofikia tutawaambia nini babu na bibi yako....wajomba zako je? Mitoto mingine sijui imezaliwaje jamani hivi wewe ni mtoto wa dada yangu kweli au dada yangu alibadilishiwa mtoto hospitalini jamani .....aibu hii nitaificha wapi mimi jamani.
Ulivyokuwa unapata raha ya kikubwa ulikuwa uliona raha sana saizi unanitukana nina laana eeeeeeeeeh!......we kweli kubwa jinga ulikuwa wapi siku zote kukemea hii laana yangu au na wewe mwenyewe umejaa laana k**a mimi......hilo swala la mimi kuwa mtoto wa dada yako ama laaa kamulize dada yako kule kaburini na usisahau kumwambia kuwa wewe pia hunaimani kuwa ni mtoto wa babu na bibi ......kwanza unanichanganya tu ngoja niende zangu kwa rafiki yangu labda naweza kujua nini cha kufanya juu ya hili na wewe nikirudi hapa nisikukute nenda nyumbani kwako na mwanao sawa wewe kubwa Jinga.....
Ummy akaingia bafuni kuoga baada ya kuoga akavaa nguo na kuondoka kwenda kwa Upendo. Alivyofika kwa Upendo aliingia ndani bila hodi na kumkuta shemeji yake yaani mume wake Upendo kakaa sebuleni anaangalia tv ikabidi shemeji yake amkaribishe ......karibu shemeji yangu naona unamawazo sana umesahau hata kupiga hodi ....karibu ngoja nikuitie rafiki yako .........baby ...baby...unamgeni huku. Shemeji mi nawaacha kidogo. Shemeji nisamehe kwa yote leo sipo sawa kidogo nisamehe shemeji yangu. Usijali shemeji yangu nimekuelewa ....haya mi natoka kidogo ......shemeji yake akatoka. Mbona mwaombana msamaha kulikoni Upendo alimuuliza Ummy .....aaaaah! shost si nimeingia bila hodi ndani kwako ....yaani hapa ninamawazo sijui nifanyaje mimi mwenzio jamani.....Sasa jamani rafiki yangu umepatwa na nini hebu niambie ili nijue nini cha kukusaidia ili kutatua tatizo lako.
Rafiki yangu mjomba kaja nyumbani katukuta mimi na ma mdogo Joy tunabadilishana mate.......Ummy hebu tulia kwanza twende taratibu nipate kuelewa mwenzio umesemaa?wewe na ma mdogo wako mumekuwa mnafanya nini......
Usikose sehemu ya sita ili ujue Upendo atamshauri nini rafiki yake juu ya tatizo lake.