24/12/2021
BEAVER
Fundi seremala wa kwenye maji.
Beaver ni aina ya mnyama anayepatikana kwenye kundi la wanyama jamii ya panya (rodents). Katika maeneo mbalimbali ya mito na maziwa ya huko Amerika na maeneo ya Ulaya utakutana na fundi seremala huyu wa kwenye maji.
Beaver ni k**a seremala ama ni k**a mkandarasi kwani hutengeneza makazi yake kwenye maji kwa kutumia utaalamu. Yeye na binadamu ni viumbe pekee wanaoweza kutengeneza bwawa. Hutumia miti na mawe kutengeneza bwawa ambapo pia hujenga makazi yake kwa miti ndani ya bwawa. Kutokana na shughuli hiyo ya ujenzi beaver wana meno magumu yaliotengenezwa na kiwango cha madini ya chuma ambayo hutumika kukatia miti pia kula ambapo hutegemea magome ya mti k**a chakula chao.
Uwezo wake anaweza kuukata mti wenye unene wa cm 15 kwa dakika 50 tu.Ukataji wa mti ni wa kitaalamu kabisa k**a unavyoona pichani ili mti udondokee anapotaka.Ujenzi wake pia ni wa kimahesabu sio wa ovyo. Ili aweze kuzuia maji hulaza miti kwenye maji yanayotiririka kwa angle ya 30 ili kuyaruhusu maji kutiririka ili yasiondoke na mti baadae huanza kupanga mawe na kuyashikilia na tope ili kuziriba maji huku wakiacha upenyo mdogo kuruhusu maji yapite kiasi yasijaze bwawa. Miti hubebwa kwa meno huku mawe hubebwa kwa miguu ya mbele. Beaver wana uwezo kujenga bwawa linaloeza kufika hadi mita 100.
Ukiacha na shughuli ya ujenzi beaver ni waogeleaji wazuri. Wakati binadamu ana uwezo wa kuchukua asilimia 15 tu ya pumzi ili kujaza mapafu kwa kuvuta mara moja, yeye anaweza kujaza asilimia 75 ya mapafu yake hivyo kumwezesha kukaa ndani ya maji kwa dakika 15.
š«Explore