11/08/2022
Soma Hii, Hii Itakupa Nguvu Ya Kusonga Mbele Hata K**a Umechoka.
Rafiki Yangu Msomaji,
Vp hali yako?
Uchovu wa akili hauhitaji mapumziko, unahitaji mabadiliko.
Umewahi kutoka kwenye shughuli zako ukiwa umechoka kweli kweli na kujiambia akili yako haiwezi kufanya kitu kingine?
Unajiambia kabisa unachohitaji ni mapumziko.
Lakini kumbuka pale jambo unalopenda linapotokea ukiwa na uchovu huo wa akili, huwa unapotea kabisa.
Na hili liko dhahiri, unajiona umechoka na huwezi kusoma au kuandika,
Lakini ukiingia mtandaoni unajikuta ukiperuzi kwa muda mrefu bila kuchoka.
Au unaweza kuangalia tamthilia nzuri na unayoipenda kwa muda mrefu bila kuchoka.
Kuchoka kwa akili siyo k**a kuchoka kwa mwili.
Mwili ukichoka lazima upumzike.
Lakini akili ikichoka haihitaji mapumziko,
Bali inahitaji ubadili kile unachofanya.
Kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu ndiyo kinaleta sana kuchoka kwa akili.
Na kufanya kitu usichopenda ndiyo kunazidisha kuchoka huko.
Panga kubadili yale unayofanya katika vipindi fulani.
Na pale unapojiona umechoka, panga kufanya kile unachopenda.
Uchovu unapotea kabisa.
Zaidi, pale unapojiona umechoka, jiambie hujachoka na akili yako itakaa sawa.
Kazi zetu nyingi zama hizi siyo za kutumia nguvu bali akili.
Na akili ina uwezo mkubwa kuliko unavyoutumia sasa.
Kazana uweze kutumia uwezo wa akili yako zaidi.
Anza kwa kutokubali umechoka na hilo litaondoa sehemu kubwa ya uchovu.
Halafu kwa kupanga kubadili yale unayofanya, utaweza kufanya mengi zaidi.
Kila Lakheri.
@ we love you