Simulizi na Riwaya Za Saul David bril

Simulizi na Riwaya Za Saul David bril π‘»π’–π’‡π’π’π’π’π’˜ π’Œπ’˜π’†π’π’šπ’† π’„π’‰π’‚π’π’π’†π’π’Š π’šπ’†π’•π’– π’šπ’‚ 𝑺𝑰𝑴𝑼𝑳𝑰𝒁𝑰 𝑾𝒉𝒂𝒕𝒔𝑨𝒑𝒑 π’Œπ’˜π’‚ π’Œπ’–π’ƒπ’π’π’šπ’†π’›π’‚ π’π’Šπ’π’Œ 𝒉𝒂𝒑𝒂 π’„π’‰π’Šπ’π’Š
https://whatsapp.com/channel/0029VaylcIKAInPiI2v4Cc0R

RIWAYA: SIKU 4 ZA LOCKDOWNMtunzi: Saul David BrilWhatsApp: 0756862047SEHEMU YA 40ILIPOISHIA.....k**a alivyotarajia.Aliye...
26/03/2026

RIWAYA: SIKU 4 ZA LOCKDOWN
Mtunzi: Saul David Bril
WhatsApp: 0756862047
SEHEMU YA 40
ILIPOISHIA.....
k**a alivyotarajia.
Aliyesimama mbele yake, akiwa amemkodolea macho ya mshangao alikuwa ni Nisha, mpenzi wa Jordan.
Makuratha alibaki mdomo wazi, aibu na hofu ya kujiachia mbele ya Nisha vilimjaa. Mbaya zaidi alishamwita na jina eti 'Jordan'
SASA ENDELEA....
Ukimya ulitawala pale mlangoni. Makuratha aliona haya. Nisha alimwangalia kuanzia juu mpaka chini, akaona jinsi mwanamke huyo alivyosimama nusu uchi akiwa amevaa taiti pekee mwilini mwake. Hata hivyo, Nisha hakuonesha kushtuka, badala yake alitoa tabasamu la kistaarabu sana, hakujali.
"Hi! tunaweza kuongea kidogo kipenzi?" Alisema Nisha.
Makuratha akaduwaa, macho yake yakitazama huku na kule kwa wasiwasi.
"Ku... kuongea? Hapa?" Makuratha aliuliza huku akijaribu kuweka mkono wake mmoja juu ya matiti yake ili kujisitiri mbele ya mwanamke mwenzake.
"Hapana, siyo hapa mlangoni. Pale panafaa..." Nisha alimuonesha kwa mkono eneo la mapumziko lililokuwa karibu na vyumba hivyo.
Palikuwa na seti nzuri ya sofa, meza ya kioo, na runinga kubwa ukutani. Ni eneo maalum la ghorofa ya kwanza kwa ajili ya wageni kupunga upepo. King G ni hoteli ya kifahari buana.
Makuratha alimeza mate...
"Sa...sawa, ngoja nivae basi, nakuja" Makuratha alisema na kurudi ndani haraka.
Akiwa ndani, alivaa nguo zake huku moyo ukimdunda. Alikuwa na wasiwasi mwingi. Alijiuliza k**a Nisha amemsikia vizuri pale aliposema "My Jordan Surprise" au hakusikia.
Ukweli hakuwa na uhakika jibu lipi ni sahihi, amesikia au hajasikia.
Hata hivyo, asili yake ya ubabe na jeuri ilimrudia.
"Potelea mbali, hata akisikia, kwani nini bana, akizingua namzingua pia. Acha nimsikilize anataka nini" Makuratha aliwaza huku akifunga zipu ya suruali yake. Tayari amemaliza kuvaa.
Alimtazama yule mlinzi kitandani. Mwanaume huyo alikuwa bado amelala fofofo akikoroma mkoromo wa ajabu huku udenda ukimtoka mdomoni na kulowanisha mto aliolalia. Makuratha alimpiga tu jicho la pembeni, wala hakujali hali yake, akatoka nje na kufunga mlango. Hakujua kuidharau hali ile ya mlinzi niko kubwa anafanya. Kosa lenye majuto makubwa hapo baadae.
****
Makuratha alimkuta Nisha ameshakaa kwenye sofa anamsubiri.
Bila salamu wala nini, Makuratha alijitupa kwenye kiti cha pili akaweka pozi kwa namna ya kujiamini sana.
"Nakusikiliza, nikusaidie nini?" Makuratha aliuliza.
Nisha alimtazama kwa jicho la udadisi, akijaribu kumsoma mwanamke huyu, akagundua ana kiburi fulani.
"Naitwa Nisha, binti wa Meya Magi..."
Kabla Nisha hajamaliza kujitambulisha, Makuratha alimkatisha.
"Nakufahamu vizuri Nisha, nenda tu kwenye point moja kwa moja, sina muda please"
Makuratha alikuwa anatafuta shari kwa makusudi kabisa.
Ukweli ni kwamba, anamchukia Nisha kwa moyo wake wote. Sababu kubwa ni wivu wa mapenzi; Makuratha anaamini kuwa Nisha ndiye sababu iliyomfanya Jordan amuache yeye enzi hizo na kumuona sio wa muhimu tena. Hivyo, kumuona Nisha mbele yake ilikuwa ni k**a anamuona adui yake nambali moja kwenye sekta nyeti ya mapenzi.
Nisha alishusha pumzi, akaamua kupuuza jeuri hiyo kutoka kwa Makuratha.
"Vema k**a unanijua. Bila shaka basi unaelewa pia mimi ni nani kwa Jordan, na nina nafasi gani kwake."
Makuratha alicheka kicheko cha kejeli.
"Hahahaha we kuweza... enhe! Nielewe ni nani kivipi? Wewe si ni mwanamke tu k**a nilivyo mimi kwake. Au unajiona nani mwenzangu hebu nambie, malkia au?"
Maneno ya Makuratha yalijaa shombo na dharau za wazi. Lengo lake lilikuwa kumfanya Nisha apaniki, apate hasira, kisha mazungumzo yavurugike.
Lakini Nisha alikwepa mtego huo.
Licha ya kugundua alichokitaka kwa Makuratha hatokipata kutokana na namna alivyompokea, lakini Nisha aliamua kuwa mpole. Hakuelewa ni kwanini mwanamke huyu anamjibu shombo kiasi hicho.
Nisha aliamua kubadili mbinu. Akaona njia pekee ni kumchokoza kwa maneno ili apate ukweli fulani anaouhisi.
Akaanza kwa kusema...
"Nimeona umeingia na mwanaume chumbani kwako muda mfupi uliopita, lakini bado unasema mimi na wewe ni sawa kwa Jordan. Labda sijakuelewa vizuri mrembo. Sawa kivipi? Na huyu mwanaume aliyelala chumbani kwako sasa hivi ni nani? Na Jordan ni nani?"
Swali hilo lilimgusa Makuratha pabaya...
Nisha hakuishia hapo, aliongeza dozi ya pili.
"Umenipokea mlangoni ukidhani mimi ni Jordan, si eti? Tena ukiwa uchi wa mnyama. Jana mmekuja hapa mmevaa nguo za heshima za mapadri na masista, lakini leo mnakaribishana mkiwa uchi. Unaweza kuniambia ni filamu gani mnaigiza? Inaonekana ni kali sana eti eeh?"
Nisha alimsogelea kidogo na kumnong'oneza.
"Yaani una mwanaume ndani chumbani kwako, bado unampokea mwanaume mwingine ukiwa uchi? We dada, mnacheza filamu za ngono eti?"
Maneno hayo yalimchoma Makuratha k**a sindano ya moto. Akajikuta anakosa uvumilivu, na hiki ndicho alichokuwa akikitafuta Nisha. Kumfanya Makuratha apaniki.
"Shika adabu yako Nisha! Kwanza wewe ni nani hadi utake kujua maisha yangu? Kwa nini usimfuate huyo Jordan wako ukamuulize maswali yako ya kijinga?"
Makuratha alisimama, akitaka kuondoka lakini akageuka kumpa Nisha onyo la mwisho.

"Sikiliza wewe, siku ukijua nini Jordan anafanya nyuma ya pazia, nina imani utapasuka kichwa. Labda nikushauri tu, achana na Jordan mapema kabla hujakuua kwa presha, maana si....."
Makuratha hakumalizia sentensi yake. Ghafla aliganda na kutoa macho.

Kule mlangoni alimuona Jordan akija kwa kasi. Hua zake zikiwa ndefu ndefu, akafika mbele ya mlango wa chumba cha Makuratha akasimama.
Mlango ulikuwa umefungwa lakini tayari Jordan alisikia sauti ya Makuratha akageuka na kuwaona wamekaa eneo lile la mapumziko.
Jordan alianza kusogea pale walipo. Lakini kwa bahati mbaya hakumtambua Nisha kwa sababu amempa mgongo.

Mawazo yote ya Jordan yalikuwa kwenye ile kazi muhimu waliyopewa na Agent Corma. Hakutaka kupoteza hata sekunde moja.
Alipomfikia Makuratha, hakuhangaika hata kuangalia ni nani mwingine aliyekuwa amekaa naye, akijua fika kuwa Makuratha ni mtu wa mambo mengi, huenda anapiga soga na mwanachama mwingine wa Nairobi fighters.
"Makuratha, tulikuambia ukae karibu na Object 0 uangalie maendeleo yake, wewe umekuja kukaa huku na unaona fresh tu? Hujali wala nini..." Jordan alifoka kwa sauti ya chini huku akitoa simu ya Corma mfukoni mwake.

"Haya, nitupie hizo picha kwenye hii simu sasa hivi tuzitume kwa wakubwa."
Makuratha alitaka kufungua mdomo kumjibu, lakini Jordan hakumpa nafasi.
"Tuna kazi ngumu na nyeti ya kufanya, ninyi mmekaa hapa mnapiga stori na kuchekacheka k**a masheteni ya bichi..."
Alisema Jordan lakini mara ghafla aliganda.
Hatimaye macho yake yalitua kwenye sura ya yule mtu wa pili aliyekaa na Makuratha.
Miguu ya Jordan ililegea. Mapigo ya moyo yakaongezeka ghafla.
"Nisha?" Jordan aliita jina la mpenzi wake kwa mshangao.
Alijikuta akimtazama Makuratha kwa jicho la lawama, kisha akarudi kumtazama Nisha. Jasho jembamba likiwa karibu kumtoka.
Jordan anajua wazi kuwa Makuratha ana mdomo mchafu, huenda ameshamwaga sumu mbaya kwa Nisha.
"Amekwambia nini huyu?" Jordan aliuliza huku akimnyooshea Makuratha kidole chake.
"Nisha, usimsikilize anachosema huyu mwanamke, akili zake anazijua mwenyewe, hachelewi kupigisha watu shoti kwa maneno yake ya kipuuzi. Sikia chochote alichokwambia siyo cha kweli, usimuamini." Jordan alipayuka bila hata mpangilio, akijaribu kuzima moto ambao hata hakuujua umewaka kwa kiwango gani.
Nisha alisimama taratibu kutoka kwenye kochi. Uso wake ulikuwa umetawaliwa na huzuni iliyochanganyika na hasira.
"Unataka kusemaje Jordan? Siyo kweli kuhusu nini? Kwani kuna nini kibaya kimetokea? kuna nini unakificha Joo?" Nisha aliuliza kwa sauti yenye utulivu wa kutosha.
Jordan alizidi kuchanganyikiwa. Alisogea hatua moja mbele karibu zaidi na Nisha.
"Nisha nisikilize mimi, siyo kweli, huyu anadanganya tu ili tugombane."
" Kwa nini tugombane?"
Aliuliza Nisha kisha akamwangalia Jordan kwa jicho la huruma na dharau. Akageuka na kumtazama Makuratha ambaye alikuwa amekaa kimya huku akitabasamu kwa kejeli.
Nisha alihisi kabisa hapendwi pia kuna mchezo mchafu unaendelea nyuma ya pazia ambao hajui ni nini. Alimfyonza Jordan kwa nguvu, kisha akageuka na kuanza kuondoka bila kusema neno lingine lolote.
Kitendo hicho kilimuumiza Jordan. Alitamani kumkimbilia Nisha na kumzuia, lakini ghafla mkono wa Makuratha ulimk**ata kwa nguvu.
Makuratha alimvuta Jordan nyuma na kumnong'oneza kwa ukali.
"Acha ujinga wewe mwanaume. Umefuata nini hapa, picha au Nisha? Kumbuka tuna kazi ya kufanya na mabosi wanasubiri ripoti."
Maneno hayo yalimzindua Jordan.
Alijikuta njia panda... kazi au mapenzi?
Jordan alijua akiharibu kazi ya jaribio la Serum-Z, uhai wake utakuwa hatarini. Ilibidi akubali maumivu na kuchagua kazi mbele ya penzi lake kwa Nisha.
Nisha aliendelea kutembea kwenye korido ndefu huku machozi yakimlenga. Hatua zake zilikuwa nzito. Alitegemea kuwa Jordan angemfuata, angeshika mkono wake, na kumuomba msamaha au kumuelewesha kwa sauti ya mahaba nini kinaendelea. Hadi anafika mwisho wa korido, hakuna kilichotokea, Nisha aligeuka nyuma. Alichokiona kilimvunja moyo mara mbili zaidi.
Alimuona Jordan na Makuratha wakiingia chumbani kwa pamoja.

" Why! Why! Why! Jordan" Alisema Nisha kwa sauti ya chini, safari hii akishindwa kabisa kuyadhibiti machozi yasimtoke. Binti wa Meya alilia.
***********
NDANI YA CHUMBA CHA MAKURATHA
Jordan na Makuratha walipoingia ndani na kufunga mlango, walipokelewa na hali ya hewa ya tofauti kabisa.
Walipigwa na harufu kali ya uvundo, iliyofanana na mchanganyiko wa kemikali na nyama iliyoanza kuoza.
"Hii harufu imetoka wapi Makuratha?" Jordan aliuliza huku akiziba pua kwa mkono wake.
Macho yao yalienda kitandani. Yule mlinzi alikuwa bado amelala, lakini mkoromo wake ulikuwa umebadilika. Haikuwa sauti ya mtu aliyelala, bali ilikuwa ni sauti nzito, ya kukwaruza, k**a mnyama anayeunguruma."Alikuwa anaunguruma hivi tangu mwanzo?"

"Mmh hamna alikuwa melala tu kawaida..."

"Umeona sasa haya ndio mabadiliko wazungu wanaka kuona. Hebu tupige picha zingine haraka" Alisema Jordan.
Haraka walimsogelea mlinzi huyo na kumfunua shuka.
Kitu walichokiona katika ngozi ya mlinzi kilikuwa cha kutisha. Mishipa yake ya damu ilikuwa imebadilika rangi na kuwa myeusi tii, ikijichora mwilini mwake k**a ramani. Ngozi yake ilikuwa imepauka.
Jordan hakutaka kuangalia mara mbili. Alipiga picha kadhaa, kisha akazituma zote kwa Bluetooth kwenda kwenye simu ya Agent Corma.
"Baki unamuangalia, nakuja mara moja, napeleka simu kwa Corma ili azirushe Marekani. Usitoke humu ndani" Jordan alitoa maelekezo na kutoka nje akimuacha Makuratha peke yake.
Makuratha alibaki amesimama katikati ya chumba.
Moyo wake ulikuwa ukidunda kwa kasi. Ile harufu na ule mkoromo wa mlinzi vilianza kumtia hofu.
Aliona ni bora aufunge mlango kwa ndani ili mtu mwingine asiingie na kuona maajabu yanayoendelea ndani.

"Yani wazungu jamani, ukute hivi ndivyo wanatengenezaga yale mazombi sijui. Mambo gani haya sasa" Makuratha alilalamika.
Alitembea hadi mlangoni, akashika kitasa na kuanza kunyonga funguo.
Akiwa bado ameshika mlango, ghafla alihisi kitu cha baridi kimemgusa bega lake kulia.
Ilikuwa ni mkono. Mkono mzito, mpana uliokak**aa.
Makuratha aligeuka taratibu, huku akitetemeka kwa hofu kubwa.

ITAENDELEA....

Soma season 4 &5 zote kwa sh 1500/=

Nicheki 0756862047

RIWAYA: SIKU 4 ZA LOCKDOWNSEASON 4Mtunzi: Saul David BrilWhatsApp: 0756862047SEHEMU YA 39ILIPOISHIA...Mawazo yake yaliku...
22/03/2026

RIWAYA: SIKU 4 ZA LOCKDOWN
SEASON 4
Mtunzi: Saul David Bril
WhatsApp: 0756862047
SEHEMU YA 39
ILIPOISHIA...
Mawazo yake yalikuwa yanawaza starehe anayoenda kuipata chumbani. Laiti angejua kuwa Makuratha hampeleki kumpa mapenzi bali janga kubwa, basi angekimbia kujiokoa wakati huu akiwa bado ana nafasi.
Lakini sasa ilikuwa imechelewa. Tamaa mbele, mauti nyuma.
SASA ENDELEA.....
Makuratha alifungua mlango wa chumba chake na kuingia ndani yeye kwanza, huku nje akimwacha mgeni wake.
Yule mlinzi alisimama mlangoni. Akaangaza macho huku na kule kwenye pande zote za korido kwa tahadhari kubwa ili kuhakikisha hakuna mtu anayemuona akiingia chumbani, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi yake. Haruhusiwi.
Baada ya kujiridhisha kuwa hali ni shwari, aliingia ndani na kuufunga mlango haraka.
Ile anaingia tu na kugeuka, hakupata hata nafasi ya kupumua.
Ghafla Makuratha alimdaka kwa kasi na kuanza kumwagia mvua ya mabusu mazito shingoni na kifuani.
Mlinzi alipagawa. Harufu nzuri ya mwili wa Makuratha na joto lake vilimmaliza nguvu zake zote na kumfanya taratibu aanze kupotelea kwenye ulimwengu wa huba. Mlinzi alijikuta akiegemea mlango huu pumzi zao wote wawili zikibadilika kwa kasi.
Kwa nguvu za ghafla zilizosababishwa na mzuka wa mapenzi, mlinzi alimnyanyua Makuratha juu juu akambeba na kwenda kumtupa kitandani.
Hakutaka kupoteza muda.
Kwa papara, alianza kuziondoa nguo za Makuratha huku mikono yake ikitetemeka kiasi kwa shauku ya kutaka kujilia vyombo vya mwanamke huyu mrembo aliyejilengesha kwenye 18 zake.
Mlinzi wa watu alikuwa amezidiwa. Hakutaka kupoteza muda wa kumuandaa mrembo wala kuleta maneno mengi, yeye aliutaka mchezo ili tu amalize haja zake.
Makuratha alijaribu kutumia mbinu zake za k**e ili yeye ndiye awe kiongozi wa mchezo huo wa kikubwa, lakini mlinzi alimbana kwa nguvu zote.
Kufumba na kufumbua, Makuratha alijikuta tayari ametolewa nguo zake zote za juu. Mwilini alikuwa amesalia na taiti nyepesi pekee ambayo nayo pia mlinzi alikuwa anapambana kuivua kwa nguvu huku akivuta pumzi k**a mtu anayekimbizwa.
"Wait, wait... subiri kwanza we baba!" Makuratha alipiga kelele kwa sauti ya mahaba huku safari hii akitumia nguvu zake zote kumsukuma mlinzi pembeni.
Mlinzi alisogea kando kidogo, akabaki anamtazama Makuratha kwa mshangao.
"Vipi? Mbona unanizuia tena?" Mlinzi aliuliza akihema kwa nguvu, jasho tayari linamtoka.
Makuratha alitabasamu na kumsogelea taratibu.
"Mbona una haraka hivyo? Subiri, ukienda kwa kasi hivyo utaharibu utamu wote. Huu mchezo hautaki hasira wala papara."
Makuratha aliongea kwa sauti laini ya kubembeleza kisha akamsukuma mlinzi kifuani na kumalaza chali kitandani, kisha yeye akapanda na kumkalia kwa juu kiunoni.
Mkao huo ulimchanganya kabisa mlinzi. Kila alipouona mwili laini wa Makuratha na kifua chake kilicho wazi, alizidi kupagawa na kutamani kumrukia tena. Lakini akawa mpole akimuacha Makuratha autawale mchezo, hakujua kufanya hivi ni kosa kubwa la kiufundi.
Makuratha alianza kumvua mlinzi lile gwanda lake la kazi taratibu, kifungo baada ya kifungo, huku akimpapasa kifuani kwa madaha.
"Fumba macho nikupe mambo mazuri ambayo hujawahi kuyapata mahali popote." Makuratha alinong'ona, sauti yake imejaa msisimko wa mahaba.
Mlinzi alitii bila shuruti. Alijilamba midomo yake iliyokauka na kufumba macho, akisubiri kupewa zawadi tamu aliyoahidiwa.
Hiyo ikawa ndiyo nafasi ambayo Makuratha alikuwa anaisubiri.
Kwanza, aliingiza mkono wake haraka kwenye mfuko wa koti lake fupi lililotupwa pembeni ya kitanda.
Alitoa leso yake maalumu kwa kazi ya leo. Leso ambayo tayari nimechanganya na dawa ya usingizi.
Aliishika kwa tahadhari kubwa, kisha kwa haraka akairusha na kuifunika usoni kwa mlinzi, akiziba pua na mdomo wake.
Mlinzi alishtuka. Alipiga chafya mfululizo kutokana na ukali wa dawa hiyo.
"Atsiii! Atsiii!"
Alijitahidi kufumbua macho ili aone nini kinaendelea...
Lakini Makuratha alizidi kukandamiza mkono wake wenye leso puani kwa mlinzi kwa nguvu zake zote, akihakikisha hapati tena hewa safi.
"Unafanya ni...!" Mlinzi aliongea kwa taabu huku akijaribu kuitoa mikono ya Makuratha juu ya uso wake lakini tayari alishachelewa hata sentensi haikuisha. Mwili wake ulilegea ghafla, mikono ikaanguka pembeni, hakuelewa tena kinachoendelea.
Makuratha aliinuka upesi kutoka juu ya mwili wa mlinzi. Alivuta tena koti lake na kuchukua lile bomba la sindano lenye Serum-Z.

Akamtazama mlinzi na kuvuta pumzi ndefu ili kujijaza ujasiri wa kufanya tukio hili la kigaidi.
Bila kusita, alimdunga sindano hiyo kwenye mshipa wa shingoni na kusukuma dawa yote ya kijani ikaingia mwilini kwa mlinzi.

Mwanaume huyo alionekana kujitikisa kidogo wakati dawa ile ikiingia. Sekunde chache baadae akaendelea kuuchapa usingizi.
Baada ya kumaliza, Makuratha alimlaza mlinzi huyo vizuri kitandani.
Alichukua simu yake kubwa na kumpiga picha mlinzi huyo akiwa hajitambui.
Kisha, alipiga namba fulani na kuweka simu sikioni.
Simu iliita katika chumba kingine, chumba cha Jordan.
Ndani, Jordan alikuwa amekaa na Agent Corma wakisubiri mrejesho wa kazi waliyompa Makuratha.
Jordan alipokea simu na kuweka 'laudi spika'
"Tayari nimemchoma sindano" sauti ya Makuratha ilisikika.
"Umempiga picha?" Corma aliuliza.
"Ndio, ninazo hapa."
"Basi asiende mbali na huyo mtu. Jordan anakuja hapo sasa hivi kuchukua hizo picha" Corma alitoa maelekezo.
"Sawa" Makuratha alijibu.
Corma alimwangalia Jordan na kutoa ishara fulani ya kuridhika na kazi aliyofanya Makuratha.
"Kazi nzuri. Huyu mtu wa kwanza kuchomwa sindano ataitwa Object 0. Hakikisha mnamfuatilia kwa kila hatua ili tuone mabadiliko yake hatua kwa hatua. Bado tunahitaji wengine wawili kukamilisha sampuli."
Jordan akatikisa kichwa kukubali maelezo muhimu kutoka kws agent Corma.
*******

Upande wa pili, Makuratha alijikuta akitabasamu kwa furaha ya ajabu baada ya kusikia kuwa Jordan anakuja chumbani kwake kuchukua picha alizopiga.
Lile tukio la kushikwashikwa na yule mlinzi pamoja na zile purukushani za kuvuana nguo kitandani zilikuwa zimeamsha hisia zake za mwili kwa kiasi fulani. Damu ilikuwa inamchemka, alihitaji mtu wa kutuliza munkari huo.
Alijua hakuna mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi k**a si mpenzi wake wa zamani, Jordan.
Kwa makusudi kabisa, Makuratha hakuona haja ya kuvaa nguo zake alizozivua.
Aliamua kubaki vile vile akiwa amevalia taiti yake nyepesi. Lengo lake lilikuwa ni kumuandalia Jordan mtego wa wazi. Alijua fika kuwa Jordan akimkuta katika hali ile, hawezi kuchomoka wala kukataa, lazima watafanya kile anachokitaka yeye kabla ya mambo mengine ya kazi kuendelea.
Huko chumbani kwa Jordan, Agent Corma alimkabidhi Jordan simu yake ile aliyounganisha na internet ya starlink.
"Nenda kachukue hizo picha haraka. Tunatakiwa kuzituma kwa Chongo" Alisema Corma.
Huo ndio ulikuwa utaratibu wa kazi waliokubaliana. Picha za maendeleo ya jaribio la Serum-Z zilitakiwa kutumwa kwa mfumo huo. Kutoka kwa Corma kwenda kwa Chongo kisha kutoka kwa Chongo kwenda kwa mabosi wa Mafia kule marekani.
Ndiyo maana Corma aliingia hotelini hapo akiwa na vifaa maalum ikiwemo simu yenye uwezo wa Starlink inayoweza kunasa mtandao licha ya kwamba serikali imezima huduma za internet kwa kipindi hiki chote cha 'lockdown'
Jordan alichukua simu na kuondoka haraka kuelekea chumbani kwa Makuratha.
****"
Baada ya Jordan kutoka, Corma alichukua simu yake ndogo na kupiga namba fulani.
Simu iliita kwa muda mfupi kisha ikapokelewa...
"Kazi imeanza mzee. Tayari tumemchoma sindano mtu wa kwanza na muda si mrefu nakutumia picha zake k**a tulivyopanga" Corma alitoa taarifa.
Chongo alifurahi sana upande wa pili.
"Kazi nzuri sana Corma. Mabosi wapo wanasubiri kwa hamu."
"Powa usijali, naomba kuzungumza na Big Boss mara moja" Alisema Corma.
Chongo alimpa simu Big Boss, yaani Anitha, kiongozi mkuu wa Nairobi Fighters na dada wa damu wa Madam Ande.
Corma alivuta pumzi na kuanza kumsimulia Anitha kilichotokea jana usiku mara baada ya kufika king G hoteli.
"Boss, jana wakati naingia nilikutana na Meya Maginda uso kwa uso."
Taarifa hiyo ilimshtua sana Anitha. Mwili wake ulimsisimka kwa hofu na chuki kwa pamoja.
Kumbukumbu mbaya ya mwanaume huyo aliyemtumia gerezani na kutaka kuitoa mimba yake kwa nguvu ilimjia kwa kasi. Kidonda cha zamani kilifunguka upya. Akakumbuka kuwa ana deni la kulipa kisasi kwa Meya Maginda na familia yake.

"Alikuona? Alikukumbuka? Akasemaje?" Big boss' akauliza maswali mfululizo
*********
Wakati huo huo, katika korido za hoteli ya King G mlango wa chumba cha Makuratha uligongwa utaratibu.
Makuratha alikuwa amesimama mbele ya kioo akijitazama.
Ukimuona ni aina ya mwanamke aliyejaliwa uzuri wa asili wa kuvutia. Ngozi yake nyororo ya maji ya kunde iling'aa katika mwanga wa taa, huku taiti aliyovaa ikilichonga vyema umbo lake namba nane, ikibana vema kiuno chake chembamba na makalio yaliyobinuka vema.
Kifua chake kimebeba matit madogo yaliyosimama wima yakisubiri kupashwa joto na mwanaume. Ni nani mwingine k**a sio Jordan.
Makuratha aligeuka na kumtazama yule mlinzi kitandani.
Alimuona bado amelala fofofo kutokana na nguvu ya ile dawa kutokakwenye leso. Akajiridhisha kuwa hawezi kuamka na kuharibu starehe yake yeye na Jordan.
Maskini kwa bahati mbaya hakuona mishipa ya damu shingoni kwa mlinzi huyo inavyotisha. Mishipa ilikuwa imeanza kugeuka rangi na kuwa nyeusi tii. Makuratha hakuliona hilo.
Alitembea kwa mwendo wa maringo kuelekea mlangoni, akapunguza mwanga wa taa kidogo ili kuleta maadhari ya kimahaba.
Akaweka pozi la mitego, akashika kitasa na kufungua mlango kwa mbwembwe.
"My Jordan... supraiziiiiii....!" Makuratha alisema huku akitanua mikono yake kumkumbatia mgeni wake.
Lakini ghafla, tabasamu lake liliyeyuka usoni.
Macho yake yalitoka kwa mshtuko.
Mlangoni hakuwepo Jordan k**a alivyotarajia.
Aliyesimama mbele yake, akiwa amemkodolea macho ya mshangao alikuwa ni Nisha, mpenzi wa Jordan.
Makuratha alibaki mdomo wazi, aibu na hofu ya kujiachia mbele ya Nisha vilimjaa. Mbaya zaidi alishamwita na jina eti 'Jordan'

> Sasa Jipatie season 4 & 5 kwa tsh 1200 tu OFFA

Nicheki 0756862047

RIWAYA: SIKU 4 ZA LOCKDOWNSEASON 4Mtunzi: Saul David BrilWhatsApp: 0756862047SEHEMU YA....38*******TAREHE 30/10/2025 - A...
16/03/2026

RIWAYA: SIKU 4 ZA LOCKDOWN
SEASON 4
Mtunzi: Saul David Bril
WhatsApp: 0756862047
SEHEMU YA....38

*******
TAREHE 30/10/2025 - ASUBUHI.
Mwanga wa jua la asubuhi ulipenya kidogo kupitia mapazia mazito ya chumba cha hoteli.
Nisha aligeuka upande wa pili wa kitanda na kufumbua macho yake taratibu. Alijinyoosha kidogo, mwili wake ukiwa bado unahisi uchovu.
Nisha alihamaki kidogo na kuinua kichwa chake. Aligundua kuwa yuko peke yake chumbani. Mike hakuwepo.
Kitu cha kwanza alichofanya ni kuchukua simu yake iliyokuwa chini ya mto.
Moyo wake ulikuwa na shauku ya kuona jina la Jordan kwenye kioo cha simu. Alitegemea kukuta ujumbe wa pole au simu iliyopigwa bila kupokelewa (missed call). Lakini matarajio yake yakawa ndivyo sivyo.
Hakuna ujumbe wowote, hakuna simu, wala hakuna jibu la ule ujumbe aliomtumia usiku.
Hofu na mashaka vikamvaa.
" Jordan ananini? Mbona kimya kimekuwa kingi kiasi hiki wakati yuko humu humu ndani ya hoteli? Au anahasira kwa sababu ya Mike? Mbona tuliongea tukayamaliza?" Alijiuliza pasipo kupata majibu.
Nisha alitamani kubonyeza kitufe cha kupiga ili amtafute, lakini alisita.
Mlango wa chumba ulifunguliwa na Mike akaingia. Uso wake ulikuwa na dalili za mtu mwenye mawazo mengi.
"Ooh! Kumbe umeamka Nisha" Mike alisema kwa sauti ya chini, akijaribu kutabasamu.
"Vipi hali yako unajisikiaje asubuhi hii?"
"Niko vizuri Mike, namshukuru Mungu napumua vizuri kabisa kwa sasa." Nisha alijibu huku akiificha simu yake haraka chini ya shuka.
Mike alimuangalia kwa sekunde chache, kisha akasema.
"Chakula cha asubuhi tayari. Tunaitwa ukumbini kupata chai, jiandae twende."
Wakati huo huo, sauti ya tangazo ilisikika kupitia spika ndogo zilizofungwa kwenye korido na vyumbani ndani ya King G Hotel.
Ilikuwa ni sauti ya Madam Ande. Sauti hiyo ilikuwa tulivu lakini yenye mamlaka, ikiwaalika wageni wote kuelekea ukumbini kwa ajili ya kifungua kinywa.
Ukweli ni kwamba, Madam Ande hakuwa amelala usiku kucha akimsubiri mumewe. K**a kiongozi na msimamizi wa watu wote hotelini humo kwa sasa, aliamka asubuhi na mapema.
Yeye pamoja na wafanyakazi wachache wa King G waliosalia, waliingia jikoni na kuandaa chai na vitafunwa kwa ajili ya watu wote waliokwama ndani ya hoteli hii (LOCKDOWN). Hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuwapa faraja wageni hao waliokata tamaa.
Nisha alishuka kitandani na kuanza kujiandaa.
Mike alikaa pembeni mwa kitanda akimsubiri.
Macho ya Mike yalikuwa yanamfuatilia Nisha kila alipopita, lakini safari hii hayakuwa macho ya upendo pekee, bali yalijaa maswali kiasi.
Maneno ya Dinna aliyomwambia usiku wa jana yalikuwa yakijirudia kichwani mwake mara kwa mara.
'Mpenzi wa Nisha yuko humu ndani ya King G... Nisha hataki ujue... Anakutumia tu k**a kivuli.'
Mike alijiuliza kimoyomoyo...
"Hivi ni kweli mwanaume wa Nisha yuko humu ndani? Mbona hajawahi kumuona akiongea na mwanaume yeyote kwa ukaribu? Au....mmh! Hapana bana..."
Mawazo hayo yalimfanya Mike ahisi maumivu ya wivu, ingawa alijitahidi kujifanya yuko sawa ili Nisha asigundue.
*****
Baada ya Nisha kujiweka sawa, walitoka chumbani wakiwa wameongozana.
Walitembea hadi kwenye ukumbi mkubwa. Harufu nzuri ya chai ya viungo na maandazi ilitamalaki eneo hilo.
Nisha alimuona mama yake, Madam Ande, akiwa amesimama wima nyuma ya meza ndefu ya chakula, akiwasimamia wahudumu.
Nisha alimwacha Mike na kwenda kumsalimia mama yake.
"Shikamoo Mama"
Madam Ande alimtazama binti yake kwa macho ya upendo.
"Marahaba mwanangu. Unaendeleaje? Hujambo?"
"Sijambo mama, niko sawa kabisa" Nisha alijibu akitabasamu.
"Kweli! Na Mike hajambo...?"

"K**a unavyomuona, ni mzima wa afya. Baba wapi? Hajarudi hata asubuhi hii..."

"Mmh! Babako ananichanganya, nilimpa taarifa zako za kuumwa akasema anakuja usiku huo huo. Lakini wala sikumuona hadi saa hizi"

"Mmmh! Mama jamani ndio umesimama kwa kurelax hapo, hujui nje kumechafuka huko..."

"Hamna, kungekuwa na shida ningeshajua. Wacha ifike saa tano nitampigia DC kumuuliza." Madam Ande aliongea kwa kujiamini.
Baada ya maongezi hayo mafupi, Nisha alichukua sahani yake na kikombe, kisha akaenda kuketi kwenye meza ambayo Mike alikuwa amekaa.
Hata hivyo, wakati anakula, akili ya Nisha haikuwepo kwenye chakula.
Macho yake yalikuwa yakizunguka ukumbini yakimtafuta mtu mmoja tu, Jordan.
Mwishowe, alimuona.
Jordan alikuwa upande wa pili wa ukumbi. Lakini hakuwa ametulia.
Jordan alionekana yuko bize sana. Alikuwa anatembea huku na kule, mara azungumze na Makuratha kwa sauti ya chini, mara aondoke kuelekea mlangoni na kurudi tena. Anatoka kulia, anapotea kwa muda ukumbini anarudi tena kutokea kushoto. Hakuwa na utulivu kabisa.
Hata alipopita karibu na meza yao, Jordan hakumtazama Nisha wala kumuonyesha ishara yoyote ya kumjali. Ni k**a vile hawajuani.
Nisha alibaki mdomo wazi. Hakuelewa ni kitu gani kinamfanya mpenzi wake awe bize kiasi hicho ndani ya hoteli hii ambayo wala haimuhusu. Wote ni wageni.
Hajampigia simu, hajajibu ujumbe, na sasa hata salamu ya macho hampi?
Nisha alikumbuka namna Jordan alivyoingia jana na lile vazi la ajabu la mapadri wa kikatoliki. Imani juu ya Jordan ilianza kutoweka taratibu. Alihisi kuna jambo linafichwa.
Nisha akaweka azimio moyoni mwake kuwa lazima amfuatilie Jordan ili ajue nini kinamsibu.
Watu walipokuwa wanakaribia kumaliza kunywa chai, Madam Ande alikohoa kidogo kusafisha koo na kusimama mbele ya ukumbi.
Ukumbi mzima ukawa kimya, kila mtu akitamani kusikia habari njema ya kuruhusiwa kutoka. Licha ya kwamba tayari wengi walikuwa na taarifa ya kwamba lockdown' inaendelea.
"Ndugu zangu, habari za asubuhi..." Madam Ande alianza kuzungumza kwa sauti ya utulivu.
"....Napenda kuwajuza kuwa nimewasiliana na mamlaka husika huko nje, pamoja na kusikia taarifa katika vyombo vya habari, Hali bado si shwari. Machafuko bado yanaendelea mitaani."
Madam Ande alipumzika kidogo, kisha akaendelea...
"Hivyo, katazo la kutoka nje linaendelea. Leo pia tutaendelea kukaa humu ndani mpaka hapo serikali itakapotangaza. Naomba mtulie na muwe na subira."
Kauli hiyo iliamsha taharuki kwa mara nyingine.
Minong'ono na makasiriko vilianza kusikika kutoka kila kona ya ukumbi. Watu walianza kulalamika kwa sauti.
"Tutaishi vipi humu ndani bila mawasiliano?" Mzee mmoja alilalamika.
"Wamezima internet, wametufungia ndani k**a wafungwa, sasa tufanye nini?" Kijana mwingine alifoka kwa hasira.
Hali ya hewa ukumbini ilibadilika ghafla, kutoka kwenye utulivu wa kifungua kinywa na kuwa uwanja wa manung'uniko na hofu.
Lakini licha ya yote hakuna kilichobadilika. Kifupi 'lockdown' inaendelea.
*******
Baada ya tangazo hilo la kuvunja moyo kutoka kwa Madam Ande, watu walitawanyika ukumbini. Kila mmoja aliondoka akiwa mnyonge, akitafuta kona yake ya kujificha ili kusogeza muda mbele.
Nisha hakutaka kupoteza muda.
Aliamua kuanza kazi yake ya kipelelezi mara moja. Lengo lake lilikuwa ni kumfuatilia yule mwanamke ambaye ameonekana kuwa na ukaribu usio wa kawaida na Jordan tangu walipoingia.
Nisha alitaka kupata nafasi ya kuzungumza naye walau mawili matatu, akiamini kuwa kupitia mwanamke huyo, anaweza kupata pa kuanzia kujua nini hasa kinamsibu mpenzi wake Jordan. Alitaka kujua k**a Jordan ni muigizaji kweli au alumdanganya.
Nisha alipanda ngazi hadi ghorofa ya kwanza.
Alisimama kwenye kibaraza cha juu kinachotazama bustani ya hoteli. Kutoka hapo juu, aliweza kuona kila kitu kinachoendelea chini.
Macho yake yalitua kwa Makuratha.
Mwanamke huyo mrembo na hatari alikuwa amesimama bustanini, akipiga stori na mmoja wa walinzi wa King G Hotel aliyekuwa amevalia sare zake za kazi.
Nisha alijibana kwenye nguzo, akasubiri wamalize mazungumzo ili amfuate Makuratha na kumuhoji.
Hata hivyo, mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea chini yalikuwa mazito kwa kiasi chake, tofauti na Nisha alivyodhani.
Makuratha alikuwa amemfuata mlinzi huyo kwa makusudi kabisa baada ya kumuona yuko katika hali ya upweke na majonzi. Mlinzi huyo alikuwa amejiinamia, akionekana mtu aliyekata tamaa.
"Una usingizi mbona k**a unalala hapa? Hukulala usiku?" Makuratha aliuliza kwa sauti ya k**e iliyojaa ulaghai.
Mlinzi aliinua uso wake uliojaa huzuni.
"Nililala dada yangu, kwani kuna mtu aliyekesha kulinda siku ya leo? Nina mambo yangu tu yananichanganya kichwa."
Makuratha alijisogeza karibu zaidi.
"Yapi hayo kaka yangu? Mbona umenyong'onyea hivyo?"
Mlinzi alivuta pumzi ndefu
"We acha tu, hawa mbwa wamemuua mjomba wangu huko nje. Alikuwa k**a mzazi kwangu, ndiye anayenilea na kusomesha wadogo zangu. Wamemuua kikatili kwenye maandamano wala hakuwa na hatia yoyote. Imeniuma sana dada."

"Kwamba alitoka kuandamana?"

"Sijui, kaka yangu anasema alikuwa ndani, ila nimetoka kuongea na dogo anasema anko alienda kuandamana huko...ila haya mambo"
Makuratha alisogea na kumpapasa shingoni kwa mkono wake laini, akimpa pole.
"Pole sana jamani. Duniani kuna mambo mazito. Hili janga lipite haraka, ndugu zetu wanakufa sana hasa huko Dar ndio usiseme."
Mlinzi alishtuka kidogo. Hakutegemea ukaribu mkubwa kiasi hicho kutoka kwa mwanamke mrembo k**a huyo, tena mgeni machoni mwake. Harufu nzuri ya prafyum ya Makuratha ilianza kumsahaulisha huzuni yake.
Makuratha alizidi kupapasa shingo na mabega.
"Unaonaje k**a tukiingia ndani kwenye chumba changu? Nikakupe faraja nzuri itakayokusahaulisha machungu. Mimi mwenyewe nahisi upweke na nahitaji kampani kidogo" Makuratha alisema huku akirembua macho yake na kung'ata lips za chini.
Mlinzi alimeza mate. Kwa akili za kiutu uzima, alielewa nini Makuratha anamaanisha.
Huzuni ya mjomba iliyeyuka ghafla. Alimtazama Makuratha usoni na kutikisa kichwa kukubali.
Makuratha alitabasamu kidogo. Akageuka na kuanza kuondoka huku akijitikisa makalio yake kwa makusudi ili kuzidi kumchanganya mlinzi huyo.
Bila kuhoji wala kusita, mlinzi aliinuka na kuanza kumfuata nyuma k**a kondoo anayepelekwa machinjioni.
Kutoka ghorofani, Nisha alikuwa akiwatazama kwa mshangao. Hakusikia maongezi yao, lakini aliona lugha ya mwili. Aliona jinsi Makuratha alivyomshawishi mlinzi na sasa wanaingia ndani.
Nisha alihisi kuchukizwa na tabia ya mwanamke huyo, lakini hakujua kuwa kinachoenda kufanyika si ngono, bali ni jambo kubwa zaidi.
Wakati Makuratha anaingia lango kuu la jengo la King G, alipishana na mwanamke mwingine aliyekuwa amevaa kiheshima. Huyu alikuwa Sister Emma, mwenzake kutoka kundi la Nairobi Fighters.

Bila kusimama, Emma na Makuratha waligusanisha mikono yao wakati wanapishana.
Katika mguso huo wa sekunde moja, Emma alimpatia Makuratha bomba la sindano ambalo tayari lilikuwa limejazwa dawa ya kijani kibichi.
Makuratha alilipokea bomba hilo kwa ustadi mkubwa na kuliweka haraka katika mfuko wa koti lake fupi alilokuwa amevaa.
Tukio hili lilifanyika haraka sana, kiasi kwamba hakuna mtu yeyote aliyeweza kuliona, hata yule mlinzi aliyekuwa nyuma.
Mawazo yake yalikuwa yanawaza starehe anayoenda kuipata chumbani. Laiti angejua kuwa Makuratha hampeleki kumpa mapenzi bali janga kubwa, basi angekimbia kujiokoa wakati huu akiwa bado ana nafasi.
Lakini sasa ilikuwa imechelewa. Tamaa mbele, mauti nyuma.
Naam, Tayari Makuratha anayo Serum-Z mfukoni, na mlinzi yuko nyuma yake wanaelekea chumbani.
Kifupi lile jaribio la kisayansi limeanza, na mlinzi huyu ndiye mhanga kwa kwanza.

Mtunzi: Saul David Bril
WhatsApp: 0756862047.

Ndugu msomaji, kwanini usubiri post za bure kwa muda mrefu wakati unaweza kusoma simulizi hii kila siku back to back πŸ˜‡...

Njoo nikuadd kwenye group ambalo kwa simulizi hii tu, tumekuacha mbali sana. Wakati wewe uko season 2 sisi tunamaliza season 5

Si hivyo tu, ndani ya hilo group zipo RIWAYA nyingine kali ambazo hujawahi kusoma popote pale. Mfano:-

1. SIKU NNE ZA LOCKDOWN
2. DO NOT SHOUT - Usipige kelele
3. MAFUTA YA MASAJI
4. SASHA MLINZI WA NAFSI.

Sasa basi kuliko kuendelea kusubiri muda mrefu huku, unaweza kulipa 2000/= HII NI ADA ya mwezi mzima yeye faida zifuatazo...

βœ… Unapata vipande vyote vilivyokupita.

βœ… Nakupa link unajiunga na group unaanza kupata muendelezo kila siku.

βœ… Unasoma stori zangu mpya kali na za kipekee ambazo sijawahi kuzipost popote public.

βœ… Group ni tulivu la kiutu uzima, hakuna chatting. Ni stori baada ya stori.

Kwa 2000/= tu unapata burudani mwezi mzima...πŸ˜‡

Tuma neno Niko tayari kwenda namba
πŸ‘‰πŸΎ 0756862047.

Tafadhali....
Like
Like
Like
Like
Like
*Like hapa chini niweke episode inayofuata*

Address

Kigamboni

Telephone

+255788967317

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Simulizi na Riwaya Za Saul David bril posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Simulizi na Riwaya Za Saul David bril:

Share