LIFE Lesson story

LIFE Lesson story Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from LIFE Lesson story, Painting Lessons, Ilala.

LIFE Lesson story is a page specifically established for narrating in swahili language any fictitious or true based story that intends to offer life lessons to the audience.

STORY 04: KISA CHA MFALME NA WAKE ZAKE WANNEHapo zamani za kale palikuwapo na mfalme mwenye nguvu aliyeishi katika nchi ...
31/08/2022

STORY 04: KISA CHA MFALME NA WAKE ZAKE WANNE

Hapo zamani za kale palikuwapo na mfalme mwenye nguvu aliyeishi katika nchi tajiri sana. Mfalme huyu alikuwa na wake wanne. Kati ya wake zake wote, alimpenda na kumjali sana mke wake wa nne. Alimununulia vitu vya dhahabu, almasi na mavazi ya kifahari. Kiufupi mfalme alimpa mke huyu wa nne kila kitu alichotaka na kumfanyia chochote kile alichoweza kufanya.

Lakini pia alimpenda sana mke wake wa tatu. Mke huyu alikuwa mrembo sana, hivyo mfalme alimfurahia na kujivunia kujionesha nae pindi alipokuwa anatembelea nchi jirani. Atahivyo, mfalme aliamini mke huyu atakuja kumuacha na kumwendea mtu mwingine katika siku za usoni.

Vilevile, mfalme alimpenda mke wake wa pili. Mke huyu alikuwa mwelevu na mtu anaejali sana hivyo mfalme alimchukulia k**a mshauri na msiri wake. Pindi mfalme alipopata shida au ugumu wowote katika suala zima la maamuzi, aliweza kumshirikisha naye aliweza kumsaidia mfalme kuvuka mazito na mgumu alokuwa anapitia.

Na mke wa kwanza wa mfalme alikuwa mke mwaminifu sana na alikuwa mke pekee aliyekuwa na mchango mkubwa katika kutengeneza na kudumisha utajiri wa mfalme pamoja na ufalme wake. Mke huyu alimpenda sana mfalme lakini mfalme akuonesha kumpenda, kumuheshimu wala kumjali k**a alivyokuwa akfanya kwa wake wengine, hivyo badala yake alimpuuzia.

Siku moja, mfalme aliugua sana, akawa hoi taabani kiasi cha kukaribia kufa. Mfalme akayawazia sana maisha yake ya kifahari na kustahajabu kwa kusema “hivi sasa nina wake wanne wakinifariji, lakini pindi nitakapokufa nitakuwa pekee yangu”. Mfalme akahofia kuwa mpweke katika maisha yake baada ya kifo, hivyo akamuuliza mke wake wa nne kwa kusema “nilikupenda sana zaidi ya wote, nikakupamba kwa mavazi ya kifahari na nikaonesha kukujari sana wewe. Sasa, niko karibu kufa, je utafuatana nami katika maisha yangu baada ya kifo?” Hakuna namna, siwezi kwenda na wewe” alijibu mke wake wa nne na kisha akaenda zake bila kusema neno jingine. Mfalme akuwaza k**a mke aliemjali sana angeongea maneno k**a hayo, hivyo alihuzunika sana kwani majibu ya mke wake wa nne yaliukata moyo wake k**a vile kisu chenye ncha kali.

Mfalme akiwa kwenye huzuni nyingi baadae akamuuliza mke wake wa tatu kwa kusema “nilikupenda sana katika maisha yangu yote na sasa nina kufa, je utaenda nami na kuwa pamoja katika maisha yangu baada ya kifo?” “Hapana” mke wa tatu alijibu “maisha ni matamu sana na pindi ukifa nitaolewa na mtu mwingine”. Moyo wa mfalme ukazama na kuwa wa baridi sana.

Mfalme akamuuliza mke wake wa pili “Umekuwa ukinipenda, ukinishauri, ukinitia moyo na kuwa msaidizi kwangu, nami nimekuwa nikikugeukia kwa kukuomba msaada nawe umekuwa nami bega kwa bega wakati wote. Sasa ikitokea nimekufa utafuatana na kuwa pamoja nami katika maisha baada ya kifo?” mke wa pili akamjibu “Samahani sana mfalme wangu, wakati huu siwezi kukusaidia tena, lakini nitakachoweza kukifanya ni kuandaa kila kitu kwa ajili ya mazishi yako na mimi kuwepo mbele yako mpaka pale utakapozikwa” . jibu lake mke wa pili lilitoka k**a shaba ya umeme na hivyo kuharibu kabisa moyo wa mfalme.

Sasa, mfalme akabaki mkiwa na mnyonge kwani alikuwa amepoteza matumaini ya kumpata mweza katika maisha yake baada ya kifo. Hii ni kutokana na kukosa ushirikiano kutoka kwa wake zake aliowapenda na kuwajali sana. Mfalme akiwa amebaki mkiwa, mara sauti ikatoka na kusema “Nitaenda na kufuatana nawe mahali popote pale bila kujali ni wapi hata k**a ni katika maisha yako baada ya kifo.” Mfalme akaangalia huku na kule na kumbe ilikuwa sauti ya mke wake wa kwanza ambaye alimjali wa mwisho katika wake zake wote. Alikuwa hana mvuto na amekondeana k**a vile ana utapiamlo. Mfalme akiwa na huzuni zaidi alijisikia aibu na kusema “Nisamehe sana, ninajuta kwamba sikukujali. Nilipaswa kukujari sana pindi nilipokuwa na nafasi na nilitakiwa kukupa umakini na kipaumbele cha kwanza katika maisha yangu.”

Funzo la hadithi hii ni kwamba wote tuna wake wanne katika maisha yetu ya kila siku.

1. Mke wa nne anawakilisha mwili wetu. Tunaupenda na kuupamba kwa mapambo, vipodozi na mavazi mazuri. Tunatumia muda na jitihada nyingi kuufanya uonekane vizuri lakini hautaenda na sisi pindi tutakapo kufa bali utaenda zake bila kusema neno lolote k**a vile mke wa nne alivyofanya.

2. Mke wa tatu anasimama kwa niaba ya vitu tunavyovimiliki k**a vile mali, vyeo, wadhifa, umaarufu au utajiri. Vitu hivi havitafuatana nasi pale tutakapo kufa, bali vitagawanywa na kupewa watu wengine k**a vile mke wa tatu alivyosema kwamba atakwenda kuolewa na mtu mwingine.

3. Mke wa pili anawakilisha familia, ndugu, jamaa na marafiki. Tunawapenda, tunawaamini na kuwashilikisha matatizo yetu kwa ajili ya kutushauri, kutufariji na kutusaidia. Haijalishi ni kwa muda gani watakuwa pamoja nasi lakini kikomo cha kuwa pamoja nasi ni pale tu watakapotuzika. Wanaweza tu kwenda na sisi kwenye maziko yetu na kutuaga k**a vile tu mke wa pili alivyosema atakwenda kuanda mazishi ya mfalme na atakuwepo katika siku ya kumsindikiza na kumzika.

4. Na mke wa kwanza anasimama kwa niaba ya roho zetu. Mara nyingi tunapuuzia kujali roho zetu kwa kujifanya tuko bize na kutafuta maisha, utajiri, furaha na nguvu lakini roho ndiyo kitu pekee kitakachofuatana nasi kwenye maisha yetu baada ya kifo.

Hivyo tuijali miili yetu kwa kuifanya nadhifu na yenye afya. Tufurahie vitu tunavyovimiliki na faraja inayotokana na vitu hivyo. Tuthamini familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa upendo na msaada wanaotoa. Lakini tusisahau kujali roho zetu kwa kujikabidhisha kwa Mungu kwa kufanya ibada, dua, toba na utu wema.

Asante
Usisahau kulike na kushare.

STORY 03: KISA CHA WATUMISHI WATATU NA TALANTA Kulikuwako na bwana mmoja aliyekuwa na watumishi watatu aliyowaamini sana...
01/05/2022

STORY 03: KISA CHA WATUMISHI WATATU NA TALANTA

Kulikuwako na bwana mmoja aliyekuwa na watumishi watatu aliyowaamini sana. Siku moja bwana huyu alitaka kusafiri kwenda mbali katika nchi ya ugenini, hivyo akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao. Mmoja akampa talanta tano, mwingine talanta mbili, na mwingine talanta moja. Kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri zake.

Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi. Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi. Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alikwenda akachimba shimo ardhini na kuificha ile fedha ya bwana wake.

Baada ya muda mrefu, yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao. Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta nyingine tano zaidi. Akasema, ‘Bwana uliweka kwenye uangalizi wangu talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta tano zaidi.’ Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’

Yule mwenye talanta mbili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, uliweka kwenye uangalizi wangu talanta mbili. Tazama nimepata hapa talanta mbili zaidi.’ Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako.’

Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unayevuna mahali usipopanda na kukusanya mahali usipotawanya mbegu. Kwa hiyo niliogopa, nikaenda, nikaificha talanta yako ardhini. Tazama, hii hapa ile iliyo mali yako.’ Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu. Vyema basi, ingekupasa kuweka fedha yangu kwa watoa riba, ili nirudipo, nichukue ile iliyo yangu na faida yake.

Basi mnyangʼanyeni hiyo talanta, mkampe yule mwenye talanta kumi. Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa. Nanyi mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje, kwenye giza, mahali ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

Hadithi hii inatufundisha mambo makuu matano:

1. Uaminifu ni mtaji. Usipokuwa mwaminifu kwa kitu kidogo, huwezi kuwa mwaminifu kwa kitu kikubwa. Mtumishi alipewa talanta tano akazalisha kumi na Yule aliyepewa mbili akazalisha nne walikuwa waaminifu kwa bwana wao ivyo wakapewa nafasi ya kuwa waangalizi na wasimamizi wa vitu vingi.

2. Mungu hakupi unachotaka bali unachostahili kulingana na uwezo wako. Hivyo lazima uridhike na unachopata. Mtumishi wa kwanza alipewa taranta tano kwa sababu anajituma sana, na watatu akapewa talanta moja kwa sababu ni mvivu sana.

3. Mwenye kingi uongezewa, asiyenacho, hata kile kidogo alichonacho unyang`anywa. Hivyo, usiridhike na kidogo ulichonacho bali kitafutie namna ya kukiongeza. Mtumishi aliyepewa talanta moja na kushindwa kuizalisha alinyang`anywa na kupewa mtumishi mwenye taranta kumi badala ya mtumishi mwenye talanta chache nne

4. Adui wa mafanikio yako ni hofu, uvivu wa kufikiri, kudharau aina ya kipawa ulichonacho (pesa, kipaji, ujuzi, kiwanja, nguvu kazi, shamba, kitendea kazi k**a vile simu n.k), kudharau udogo wa kipawa ulichonacho (mfano, elfu kumi siyo mtaji), na kukadria vibaya uwezo wako (mfano; biashara zina wenyewe, uongozi tuwaachie wasomi). Yule Mtumishi wa tatu alikadriwa na Bwana wake kwamba kwa kumpa talanta moja angeweza kuzalisha talanta nyingine lakini alikuwa mwoga wa kuthubutu, mvivu, aliona taranta moja haitoshi kwa uzalishaji na alijiona uwezo wake mdogo wa kuizalisha hiyo talanta moja ndiyo maana akaishia kuifukia kwenye ardhi asije akaitumia akadaiwa.

5. Mtu asiye na faida hafai kitu. Hivyo usimkumbatie, bali mtupilie mbali na maisha yako na mbali na mipango yako ya kimaendeleo. Mtumishi aliyepewa talanta moja na kushindwa hata kuzalisha robo au nusu ya hiyo talanta hakuwa na faida yeyote kwa bwana wake ivyo akatupwa nje, kwenye giza, mahali ambako kuna kilio na kusaga meno.

Asante
Usisahau kulike na kushare

Uenda ukawa unajiuliza1) LIFE Lesson story  ni nini? na  inajihusisha na nini?LIFE Lesson story ni ukurasa wa Facebook u...
29/04/2022

Uenda ukawa unajiuliza

1) LIFE Lesson story ni nini? na inajihusisha na nini?
LIFE Lesson story ni ukurasa wa Facebook unaojihusisha na kusimulia hadithi, matukio, au jambo fulani na pia kueleza kinagaubaga funzo la maisha linalotokana na simulizi hizo.

2) LIFE Lesson story imeanzishwa na nani na ni lini?
LIFE Lesson story imeanzishwa kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 14'th March 2022 na mwasisi wake akiwa ni Abdon Richard.

3) LIFE Lesson story imeanzishwa kwa kusudi gani?
LIFE Lesson story imeanzishwa kwa lengo la kutaka kuendeleza na kudumisha utamaduni wetu wa kusimuliana hadithi uliokuwepo tangu enzi za mababu zetu. Lakini pia kututaka kudumu katika kujifunza kupitia simulizi za maisha ya wengine na siyo kutegemea dhana ya kutenda makosa k**a njia pekee ya kujifunza.

4) Nifanye nini ili nipate kuwa mfuasi wa ukurasa huu.
Ili uwe member wa ukurasa (Page) huu kwanza unatakiwa kutembelea ukurasa wetu pindi unapokusogelea katika akaunti yako ya facebook au kwa kuclick link hii (https://www.facebook.com/LifeLessonstory/),
pili unatakiwa kulike ukurasa wetu na hii itakufanya usipitwe na kila aina ya simulizi kemukemu. Jinsi ya kulike ukurasa wetu, nenda juu kabisa ya ukurasa wetu, halafu bonyeza kitufe cheupe kilichoandika (LIKE) na baada ya kubonyeza kitaweka rangi ya blue na hapo utakuwa tayari member wa ukurasa huu.

STORY 02: KISA CHA MWANAMKE AKIMNYONYESHA  MZEE GEREZANI Hapo zamani kidogo  katika utawala wa 14 wa Louis huko Ufaransa...
01/04/2022

STORY 02: KISA CHA MWANAMKE AKIMNYONYESHA MZEE GEREZANI

Hapo zamani kidogo katika utawala wa 14 wa Louis huko Ufaransa, kulikuwepo na mzee maskini aliyefahamika kwa jina la Simoni. Mzee huyu alikuwa na binti yake wa pekee aliyeitwa Pero ambaye naye alikuwa na mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni.

Sasa kutokana na hali duni ya maisha, mzee huyu alipatikana na hatia ya kuiba kipande cha mkate na hivyo alik**atwa na kupelekwa mahak**aini kwa ajili ya kusomewa mash*taka pamoja na hukumu yake. Hata hivyo, sheria za makosa ya uharifu katika kipindi hicho cha utawala wa 14 wa Louis zilikuwa kali sana, hivyo mzee huyu maskini alipewa hukumu ya kifo kwa njaa; kwa maana ya kufungwa jela bila kupewa chakula wala maji hadi pale atakapokufa.

K**a ilivyo desturi ya ndugu kuwatembelea wapendwa wao waliopo magerezani, basi Mzee huyu alipoanza kuitumikia hukumu yake, binti yake 'Pero' alihakikisha kila siku anaenda kumtembelea baba yake kwa lengo la kumfariji na kumjulia hali. Kulingana na matakwa ya hukumu, Pero aliruhusiwa kumtembelea baba yake kila siku lakini kabla ajaenda kumwona alikaguliwa kwa umakini kiasi kwamba hakuna chakula chochote angeweza kwenda nacho.

Hata hivyo, baada ya miezi minne kupita tangu mzee aanze kutumikia hukumu yake, mamlaka husika ya magereza ilipatwa na mshangao mkubwa kumwona mzee huyo akiwa bado hai, mwenye afya njema tena bila hata ya kupungua uzito. Sasa kutokana na Pero kuwa mgeni wa kila siku na wa pekee wa mzee katika mahabusu hiyo, Mamlaka ikaingiwa na wasi wasi na hivyo kuanza kumpeleleza mwanamke huyo.

Katika upelelezi wao, mamlaka ilipata mshangao zaidi walipomkutaniza mwanamke huyo mdogo akimpatia baba yake ziwa ili anyonye maziwa ambayo ni maalumu kwa ajili ya mtoto wake mchanga. Kitendo alichokuwa amefanya mwanamke huyu kilikuwa ni kitendo cha kustahajabisha sana na kilikuwa akikubaliki na wala akiendani na maadili ya jamii yeyote hata sasa, hivyo kesi ilifunguliwa mahak**ani dhidi yake.

Baada ya mahak**a kusikiliza kesi pande zote mbili k**a ilivyo desturi ya sheria; upendo na huruma ya mtoto huyu wa k**e kwa baba yake uliweza kugusa na kurahinisha moyo wa jaji hivyo mahak**a ikaamua kutoa msamaha kwa mzee yule na kumwachia huru.

Funzo la hadithi hii ni kwamba “Upendo ni siraha kubwa yenye nguvu ya kufanya mapinduzi ya kitu chochote kile kilichoshindikana kwa sababu ndani ya upendo kuna baraka za mwenyezi Mungu.” Hivyo tudumu katika upendo.

STORY 01: KISA CHA MTU MMOJA NA NYOKA KATIKA MOTO  Palitokea mtu mmoja aliyejawa na huruma na moyo wa kusaidia wengine. ...
15/03/2022

STORY 01: KISA CHA MTU MMOJA NA NYOKA KATIKA MOTO

Palitokea mtu mmoja aliyejawa na huruma na moyo wa kusaidia wengine. Siku moja mtu huyu katika pita pita zake, alimuona nyoka mmoja aliyekuwa katika hatari ya kufa kwa moto uliokuwa umemzunguka pande zote. Basi mtu huyu alimuhurumia nyoka yule na kuamua kuokoa maisha yake.

Sasa katika harakati za kutaka kumuokoa na kumweka huru na moto, haraka haraka alimshika nyoka yule kwa mkono tayari kumtoa kwenye moto lakini zoezi hili halikufanikiwa kwani nyoka yule alimung`ata, jambo lililopelekea kumwachia kwa haraka kutokana na maumivu makali aliyoyapata. Hivyo nyoka yule alianguka na kubaki tena kwenye moto unaowaka.

Hata ivyo mtu huyu hakuchoka na wala hakukata tamaa kumwokoa nyoka yule licha ya maumivu makali aliyoyapata kutokana na kung`atwa. Hivyo aliangalia huku na kule na kufanikiwa kupata fito ndefu ya chuma na kuitumia kumtoa tena nyoka yule katika moto unaowaka na hatimaye kuokoa maisha yake.

Basi, Mtu mwingine aliyekuwa ameona kile kilichotokea akamfuata na kumuuliza kuwa “Huyu nyoka amekung`ata na kukusababishia maumivu makali, sasa kwa nini unajaribu kuokoa maisha yake?. Yule mtu akamjibu akisema “Asili ya nyoka ni kung`ata lakini hilo aliwezi kubadili asili yangu ambayo ni kusaidia”

Funzo la hadithi hii ni kwamba: “Usibadili asili yako kisa mtu fulani amekuumiza. Usipoteze uzuri wa moyo wako bali uendeleze hata kwa mtu yule yule aliyekuumiza lakini kwa kujifunza kuwa mwangalifu ili usije ukaumizwa tena.

Address

Ilala

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LIFE Lesson story posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to LIFE Lesson story:

Share