KWAYA Katoliki

KWAYA Katoliki 0754664092

MATUKIO KATIKA PICHA  - ITAGA TABORA▪︎ Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, ame...
07/07/2024

MATUKIO KATIKA PICHA - ITAGA TABORA

▪︎ Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, ametoa Sakramenti ya Kipaimara kwa Waamini 106 wa Parokia ya Mtakatifu Anthony wa Padua - Itaga Jimboni Tabora Julai 07, 2024.
KWAYA Katoliki
Beatus Benedicto
Malimbu
www.radiomaria.co.tz

Godfrey Mahonge

HERI YA KUMBUKUMBU YA UPADRE▪ Karibu umtakie Neno la Baraka na Matashi mema Mhashamu Christopher Ndizeye Askofu wa Jimbo...
05/07/2024

HERI YA KUMBUKUMBU YA UPADRE
▪ Karibu umtakie Neno la Baraka na Matashi mema Mhashamu Christopher Ndizeye Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama, leo hii anafanya Kumbukizi ya Miaka 23 ya Upadre.
▪ Familia ya Radio Maria Tanzania inakutakia heri sana Baba Ndizeye umefanyika baraka kwa Taifa la Mungu, nasi tunakuombea heri katika maisha yako.
Mama Maria azidi kukubeba.
www.radiomaria.co.tz

Je, ni nini hivi ndani ya picha hii ?Vitaje kwa uelewa wa Taifa la Mungu
05/07/2024

Je, ni nini hivi ndani ya picha hii ?
Vitaje kwa uelewa wa Taifa la Mungu

MATUKIO KATIKA PICHA - TABORABalozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania Askofu Mkuu Angelo Acattino akimvalisha Pallia Tak...
05/07/2024

MATUKIO KATIKA PICHA - TABORA
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania Askofu Mkuu Angelo Acattino akimvalisha Pallia Takatifu Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Mt.Theresia wa Mtoto Yesu Jimboni Tabora na kuhudhuriwa na Mababa Maaskofu, Mapadre, Watawa wa k**e na kiume,Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Tabora na Waamini walei.
www.radiomaria.co.tz
KWAYA Katoliki
Beatus Benedicto

Zinapatikana kwa Sh.Elfu 14, tunatuma mzigo sio Moja moja . Karibuni tujivunie ukatoliki wetu.
30/05/2024

Zinapatikana kwa Sh.Elfu 14, tunatuma mzigo sio Moja moja . Karibuni tujivunie ukatoliki wetu.

19/05/2024

Njoo Roho Mtakatifu tujaalie Paji la
1. Hekima
2. Akili
3. Elimu
4. Nguvu
5. Shauri
6. Ibada
7. Uchaji wa Mungu

Picha hii ni kutoka Kituo cha Hija Kiabakari Jimbo Katoliki Musoma, kwa Hisani ya Padre Wojciech Adam ambaye ni Mhifadhi kituo hiki na Paroko Parokia ya Huruma ya Mungu - Kiabakari.


KWAYA Katoliki Malimbu

MASOMO YA MISA KILA SIKU ZA JUMA KUU. Bonyeza Alama ya WhatsApp Hapo Chini, uje inbox
27/03/2024

MASOMO YA MISA KILA SIKU ZA JUMA KUU. Bonyeza Alama ya WhatsApp Hapo Chini, uje inbox

Matukio katika picha - Tabora Tanzania ▪︎ Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, ...
27/03/2024

Matukio katika picha - Tabora Tanzania

▪︎ Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, March 26, 2024 aliadhimisha Misa Takatifu ya kubariki Mafuta ya Wakatekumeni, Wagonjwa na kuiweka Wakfu Krisma Takatifu.

▪︎ Misa hii aliiadhimisha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Tabora Mjini, na kuhudhuriwa na Mapdri wote wanaofanya Utume Jimbo Kuu la Tabora.

MfollowKWAYA Katoliki
Mtakatifu Rita Wa Kashia

Godfrey Mahonge

HABARI PICHA - DODOMAWakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kubariki mafuta ya wagonjwa, wakatekumeni na kuweka wakfu K...
21/03/2024

HABARI PICHA - DODOMA

Wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kubariki mafuta ya wagonjwa, wakatekumeni na kuweka wakfu Krisma Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la Dodoma.

Misa imeadhimishwa na Mhashamu Beatus Michael Kinyaiya OFM Cap, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dodoma.
mfollowKWAYA KatolikimfollowMtakatifu Rita Wa Kashia

DAR ES SALAAM;Mhashamu JUDE THADDEUS RUWA'ICHI, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DAR ES SALAAM ametoa wito kwa Wakristo wakat...
21/03/2024

DAR ES SALAAM;

Mhashamu JUDE THADDEUS RUWA'ICHI, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DAR ES SALAAM ametoa wito kwa Wakristo wakatoliki na wananchi wote kushiriki mbio za riadha zinazoandaliwa na Jimbo, ili kuwasaidia wahitaji, kuboresha kituo cha hija PUGU na Maktaba ya MWL. NYERERE.

Askofu Mkuu RUWA’ICHI amesema hayo leo Machi 21, 2024 wakati akizindua rasmi maandalizi ya awamu ya pili ya mbio hizo za riadha maarufu k**a PUGU MARATHON 2024 zinazotarajiwa kufanyika Mei 18, 2024 kuanzia saa 12 asubuhi katika viwanja vya kituo cha hija cha PUGU jijini DAR ES SALAAM.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano Kanisa Kuu la Mtakatifu YOSEFU jijini DAR ES SALAAM, Askofu Mkuu RUWA’ICHI amesema gharama ya kujisajili ni shilingi elfu 30, na kwamba kutakuwa matembezi na riadha ya umbali tofauti kadri ya uwezo wa mshiriki.

Aidha ameongeza kuwa, katika mbio za mwaka jana walifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 117 na laki 5, ambacho kilitumika kununua mashuka 50 kwa ajili ya Hospitali ya Kardinali RUGAMBWA, kulipa ada ya watoto wasio na uwezo, kuweka umeme katika nyumba iliyotumiwa na Hayati Baba wa Taifa, MWL. NYERERE alipokuwa akifundisha PUGU pamoja na maboresho ya kituo cha hija.

Naye Meneja wa Kidigitali kutoka Benki ya MKOMBOZI, FILEMON TESHA akielezea namna ya kujisajili amesema, usajili unafanyika kupitia simu ya mkononi, mawakala wa benki hiyo na katika matawi yao yote nchini.

  Katoliki
21/03/2024

Katoliki

SONGEAKatika picha ni Mapadre, Mashemasi, Watawa, Waseminari na Waamini, wakishiriki Misa ya kubariki Krisma  Takatifu k...
21/03/2024

SONGEA
Katika picha ni Mapadre, Mashemasi, Watawa, Waseminari na Waamini,
wakishiriki Misa ya kubariki Krisma Takatifu kutoka katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Matias Mulumba Kalemba, Songea.

▪︎Misa inaadhimishwa na Mhashamu Askofu Mkuu Damian Denis Dallu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea.follow Mtakatifu Rita Wa Kashia FollowKWAYA Katoliki

Address

United Republic Of Tanzania
Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KWAYA Katoliki posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category