29/08/2014
Neno U.T.I si geni masikioni mwa
wengi, kwani ni wengi leo
utawasikia “naumwa U.T.I”. Japo si
wote hulitumia kisahihi. Wengine
wana tatizo ambalo ni tofauti na
U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe
dawa za U.T.I. Leo nimeona
tubadilishane elimu juu ya hili tatizo,
angalau kila mmoja awe na uelewa
U.T.I ni nini hasa, inasababisha na
nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga.
U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract
Infections, ambayo kwa lugha yetu
ni maambukizi ya njia ya mkojo.
K**a linavyojieleza, kwamba
maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita
ni U.T.I, na si pengine popote. Una
uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu
kingine tofauti nk.
Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni
kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu
hadi kwenye figo.
K**a maambukizi yako eneo la
kutoka kwenye kibofu hadi
kwenye figo(ikihusisha na figo pia),
inaitwa Lower Urinary Tract Infect. Na ikihusisha eneo la juu ya kibofu,
inaitwa Upper Urinary Tract
Infection.
Tatizo hili huwapata wote,
wanaume na wanawake. Lakini
huwapata zaidi wanawake kutokana na tofauti za kimaumbile.
Hii ni kwa sababu kuu mbili, i)njia ya
haja ndogo ya mwanamke iko jirani
zaidi na njia ya haja kubwa ambapo
vijidudu vingi visababishao U.T.I
ndipo vinapoishi, ii) mrija wa mkojo (urethra) wa mwanamke ni mfupi
ukilinganisha na wa mwanaume,
hivyo kufanya iwe rahisi kwa
maambukizi kufika kwenye kibofu
kwa mwanamke kuliko kwa
mwanaume. Visababishi
Tatizo hili husababishwa kwa kiasi
kikubwa na bacteria ambao makazi
yao ya kawaida utumbo mpana, na
hivyo huwa wanapatikana pia
kwenye haja kubwa, mfano Escherichia coli na wengineo. Pia,
linaweza likasababisha na ‘fungus’
na visababishi vingine, japo ni mara
chache sana. Vihatarishi na Njia ya Maambukizi
a)Kwa wanawake
• Kujamiiana –hii huweza kuamisha
bacteria walio kwenye uume moja
kwa moja, ama watokanao na
maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
• Kuchezea ama kuchezewa na
mikono michafu maeneo ya uke
kunaweza kusababisha
maambukizi
• Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza
kuhamisha bacteria walio ktk njia
ya haja kubwa na kuingia njia ya
mkojo
• Matumizi ya pedi za k**e zenye
kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la
uke na kukaribisha bacteria
wanaosababisha maradhi kuzaliana
kwa wingi
Vifuatavyo pia vinaweza
vikachangia • Ujauzito –mara nyingi hushusha
kinga ya mwili ya mjamzito
• Upungufu wa homon ya ya k**e
Oestrogen husababisha bacteria
wasababishao U.T.I kuzaliana
kirahisi b)Kwa wanaume
• Matatizo ya tezi ya kiume
(prostate) mabapo husababisha
mrija wa mkojo kuziba, ama
kutopitisha mkojo vizuri na
kuruhusu bacteria kujenga makazi • Kutotahiriwa, ambapo nyama ya
mbele inaweza kuhifadhi bacteria
wasababishao U.T.I
• Kujamiiana kinyume cha
maumbile huingiza kirahisi bacteria
walio njia ya haja kubwa kwenye njia ya mkojo
• Kujamiiana bila kinga na
mwanamke ambaye ana
maambukizi ukeni
• Kuwa na VVU ambapo
hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi c)Kwa wote
• Kutokunywa maji na vinyaji kwa
wingi –kunywa maji mengi
husababisha mkojo kuzalishwa
kwa wingi, na kukojoa mara kwa
mara na hivyo kusafisha njia ya mkojo
• Kuwekewa mirija inayosaidia
kutoa mkojo nje inaweza pia
kukaribisha maambukizi
• Matatizo ya figo na mengine
kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuziba njia ya mkojo
• Kisukari ambapo hudhoosha
kinga ya mwili na pia kuharibu
mfumo wa figo wa uchujaji Dalili za U.T.I
a) Kwa eneo la chini la njia ya mkojo
i. Hali ya kujisikia kutaka kukojoa
muda wote
ii. Maumivu, au hali ya kujisikia
kuchoma choma wakati wa kukojoa
iii. Kukojoa mara kwa mara na mara
zote mkojo ni mdogo
iv. Mkojo unaweza kuonekana una
ukungu, na mara nyingine unatoa
harufu kali v. Maumivu ya nyonga kwa
wanawake
vi. Maumivu ya rektamu(rectum)
kwa wanaume
vii. Na mara nyingine damu kwenye
mkojo b) Kwa eneo la juu la njia ya mkojo
i. Maumivu ya tumbo(hasa eneo la
juu kwa pembeni –chini ya mbavu)
ii. Homa kali
iii. Kutetemeka na kujihisi baridi
iv. Kichefuchefu na /au kutapika Vipimo na matibabu
Mara nyingi kipimo cha mkojo
kinaweza kuonyesha tatizo.
Matibabu ni antibiotic baada ya
daktari kubaini tatizo Madhala yatokanayo na U.T.I
isipopata tiba sahihi
• Inaweza ikasababisha
maambukizi makubwa ya figo
(pyenephritis) ambayo yanaweza
kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha
• Kwa wajawazito inaweza
kuhatarisha maisha ya wote mama,
na motto aliye tumboni
• Bakteria wanaweza kuingia
mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhala
mengine
• Inaweza kusababisha shinikizo la
damu kuwa kubwa kwenye figo na
hata kusababisha ufanyaji wa kazi
mbovu wa figo Tiba mbadala nyumbani kabla ya
kumwona daktari
Unaweza kutibu, ama kupunguza
tatizo nyumbani kabla ya kumwona
daktari pale uonapo dalili ya awali
ya U.T.I, ambayo ni maumivu na kuchomachoma wakaji wa
kukojoa. Fanya yafuatayo
i. Kunywa maji mengi hasa saa 24 za
kwanza baada ya kuona dalili. Hii
itasaidia kuzalisha mkojo kwa wingi
na kusafisha njia ya mkojo ii. Kojoa mara kwa mara na
hakikisha ni hadi mkojo unaisha ili
kibofu kiwe tupu
iii. Kwa maumivu ya mlango wa
mkojo, oga na kuosha kwa maji ya
moto, kutapunguza maumivu Njia za Kujikinga na U.T.I
Kunywa maji na vinywaji kwa wingi
kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara
kwa mara na kutoruhusu bacteria
kujenga makazi kwenye njia ya
mkojo Kojoa kila ujisikiapo mkojo na
usiubane kwa muda mrefu Kwa wanawake
Nenda ukakojoe mara tu umalizapo
tendo la kujamiiana. Hii itasaidia
kutoruhusu bacteria kuingia na
kujenga makazi kwenye njia ya
mkojo. Badili pedi mara kwa mara uwapo
hedhini
Epuka kujisafisha ukeni na maji
yarukayo kwa kasi, pia epuka
kupilizia marashi ukeni, ama
kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu. Hizo huua bacteria
wa asili wa ukeni hali ambayo
hukaribisha bacteria wa maradhi
kuzaliana kwa wingi
Ujisafishapo baada ya kujisaidia
anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bacteria walio
eneo la haja kubwa kuingia njia ya
mkojo
Kwa wale walio katika kipindi cha
ukomo wa hedhi, wanaweza
kushauliana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni
kuwasaidia kujikinga na
maambukizi Kwa wanaume
Kuhakikisha maeneo ya ncha ya
uume ni masafi mara zote, hasa
ikiwa hujatahiriwa kuepusha
kujihifadhi na kuzaliana kwa
vijidudu visababishao maradhi. Kondom wakati wa kujamiiana
nayo ni kinga nzuri