16/04/2022
Wakati akifanya mahojiano na mwanamuziki SIMBA..!🦁]] ameweka wazi kwamba yeye ni moja ya sababu kubwa iliyopelekea tuzo za Tanzania kufa.
SIMBA..!🦁]] anasema kuna tuzo kubwa ambayo alikuwa amenyimwa na alipokuwa amenyimwa tuzo hiyo na akapewa msanii mwingine ndio hapa mashabiki zake walilalamika na mpaka ilifikia hatua mpaka wadhamini wakawa wamejitoa na ukawa mwanzo wa tuzo hizo kufa.
Ikumbukwe kwamba SIMBA..!🦁]] kwenye tuzo za mwaka huu aligoma kushiriki akisema focus yake kwa sasa ni kwenda kimataifa zaidi.