Tungo Za Rosedory Charles

Tungo Za Rosedory Charles Tungo nzuri toka kwa mtunzi wenu mahiri Rosedory Charles hutojutia muda wako
karibuni.....

MASHAIRI & TENZI %β€οΈπŸ’“πŸ’•πŸ’–πŸ’πŸ’œπŸ§‘πŸ’›πŸ’šWARNINGMwadanamu mwanadamu,mbona unajisahauEwe mwana wa adamu,unayo mengi makuuWajiona wa mu...
09/06/2019

MASHAIRI & TENZI %β€οΈπŸ’“πŸ’•πŸ’–πŸ’πŸ’œπŸ§‘πŸ’›πŸ’š
WARNING
Mwadanamu mwanadamu,mbona unajisahau
Ewe mwana wa adamu,unayo mengi makuu
Wajiona wa muhimu,wengine ynasahau

2.Hauheshimu wazazi,hao waliokuzaa.
Wawatukana walezi,hao waliokulea.
Haumwamini Mwenyezi,mwenyewe wajiendea.
Watokea mavumbini,na mavumbi utarudi.

3.ukae ukitambua,wew Ni kiumbe dunil
Naonawajitanua,watawala duniani.
Ila kaa ukijua,watokea udongoni.
Watokea mavumbini na mavumbi utarudi.

4.Naona wajiamini,watoa roho za watu.
Hujish*tukii moyoni,kuwa wewe nawe mtu
Ufanyayo duniani,talipizwa mara tatu.
Watokea mavumbini,na mavumbi utarudi

5.wajane unawatesa,bila kuwahurumia.
Yatima unanyanyasa,tabu wawazidishia.
Watoto unawatosa,uhai wawaondoa
Watokea mavumbini,na mavumbi utarudi

6.Muda ukishawadia, wa kuenda I badanii.
6.MΓΊda ukishawadia,wa kwenda ibadani.
Sababu wajijazia,sababu waduniani.
Bill ya kujiwazia,pumzi amekupa Nani
Watokea mavumbini,na mavumbini utarud

7.Umeliacha agizo, alilokupa Mwenyezi
Umegeuka gumzo, kwa anasa z's mwilini.
Linakuja angamizo,usipoenda tobani
Watokea mavumbini,na mavumbiutarudi .

8.wanyima watu chakula,kitakupeleka wapi.
Badaye ukishakula,kinageuka makapi.
Riziki kakupa Mola,watu wawanyima vipi.
Watokea mavumbini na mavumbiutarudi.

9.pesa unazitumia,kwa anasa za dunia.
Wapo watu wanalia,njaa zinawalemea.
Njiani ukijipitia ,mate unawatemea
Watokea mavumbini, na mavumbi utarudi.

10.Unajivalia nguo,Tena nguo za aibu.
Waonyesha maungio,na Wala hupati tabu
Usijetoa kilio,Miungu akishusha ghadhabu .
Watokea mavumbini na mavumbi utarudi

11.Mungu kakupa kipaji. Lengo kumtumikia.
Unageuza mtaji ,vibaya wakitumia.
Siku atayokuhoji,kipi utamuelezea.
Watokea.mavumbiniini na mavumbi utarud

12.Hao wakuogopao,watu wa dunia hii.
Wanayouukumu yao,Ni lazima kuitii.
Kamwe hutokwenda naoo, katika yako safar.
Watokea mavumbini na mavumbi utarudi

13.Naona unajichosha,maji watu kunyimia
Leo unajiogesha,huku ukifurahia
Ipo siku yatakuosha,mauti ikikufikia
Watokea mavumbini,na mavumbi utarudi.

14.Sanda imekupania,kwa hamu yakusubiria
Lini we utajifia,ili kukumilikia.
Nini unajivunia, katika hi dunia.
Watokea mavumbini na mavumbini utarudi

15.Hata uwe na kitanda,watu Mia kinalaza.
Mauti ikikudunda, Utalalia jeneza.
Sasa yanini wajilinda, albino kumaliza.
Watokea mavumbini na mavumbi utarudi

16.Hata uwage tajiri, unaetikisa dunia
Wa jumba la kifahari,watu wakusujudia
Nyumba yako Ni kaburi,lazima utaingia.
Watokea mavumbini na mavumbini utarudi.

17.lazima chozi kutoa ,tena utajajutia.
Utatamani kirudia, katika hi dunia.
Ili kujitengenezea,matendo yako ya dunia.
Watokea mavumbini ,na mavumbi utarudi.

18.Mwanadamu mwanadamu,wapaswa kubadilika.
Tambua unahukumu,mbeleni tawajibika.
Wote wako udhalimu,kule umeshasomeka.
Watokea mavumbini ,na mavumbi utarudi.

Mtunzi
ROSEDORY MAMERTUS CHARLES
Facebook:ROSEDORY Charles
Instagram:Rosedory Charles
Email: [email protected]
Phone number
0718685792

Address

Mbezi Mwisho
Dar Es Salaam

Opening Hours

09:00 - 17:00

Telephone

+22559453868

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tungo Za Rosedory Charles posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Tungo Za Rosedory Charles:

Share