08/05/2026
Nyota wa klabu ya Soka ya Al Nassr na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo (41) , Usiku wa Jana aliweka rekodi mpya katika Ligi kuu nchini Saudi Arabia kwenye ushindi wa magoli 4 - 2 dhidi ya Al shabab ambapo Ronaldo alifunga goli 1 kwenye mchezo huo na kufikisha magoli 100 ndani ya ligi hiyo inayozidi kupata wafuasi kila kukicha.
CR7 amefikia Rekodi hii ndani ya michezo 105 pekee , Akiwa na jumla ya Magoli 971 mpaka hivi sasa kwenye safari yake katika mchezo wa soka kuelekea idadi ya magoli 1000.
Cristiano anakuwa mchezaji pekee Aliyewahi kufikia idadi hii ya mabao katika Ligi kubwa 4 tofauti.
— Zaidi ya Magoli 100 ndani Saudi Pro League (Saudi Arabia)
— Zaidi ya Magoli 100 kwenye Premier League (England)
— Zaidi ya Magoli 100 La Liga (Spain)
— Zaidi ya Magoli 100 Serie A (Italia)
— Zaidi ya Magoli 100 kwenye Champions League (UEFA)
The GOAT Himself 🐐
🌍🌎🌏 🌍🌎🌏