05/12/2023
Ndege ya Korean Air Flight 858 mali ya serikali ya korea kusini ilikumbana na hali mbaya Novemba 29, 1987 ilipolipuka angani kutokana na bomu lililotegwa na maajenti wawili raia wa Korea Kaskazini ndani ya chumba cha abiria cha ndege hiyo.
Tukio hilo la kusikitisha lilisababisha hasara na vifo vya abiria wote 104 na wafanyakazi 11 waliokuwa kwenye ndege hiyo.
Kwa kufuata maagizo ya serikali ya Korea Kaskazini, inaelezwa kuwa maajenti hao walitega kilipuzi hicho wakati ndege hio ipo katika kituo cha kwanza cha kusimama huko Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu, kabla ya wao kuteremka kutoka kwenye ndege hiyo ambayo ilikuwa inatoka Baghdad Iraq ikielekea Seoul Korea Kusini.
Wakifuatiliwa hadi Bahrain, washambuliaji hao wawili (mwanaume na mwanamke) wakigundua kuwa walikuwa karibu kuk**atwa, walimeza vidonge vya sumu vilivyokuwa vimefichwa kwenye vipisi vya sigara sigara.
Mwanamume alikufa kwa sumu hiyo ya vidonge huku mwanamke Kim Hyon-hui akinusurika na baadaye kukiri wazi kwamba alikuwa amekuhusika na shambulio hilo.
Kufuatia kesi yake ya shambulio hilo alihukumiwa kifo nchini Korea kusini, lakini baadaye alisamehewa na Rais wa Korea Kusini Roh Tae-woo. Msamaha huo ulitolewa kwa misingi ya kwamba mwanamke huyo alikuwa amekubali makosa na kuwa tayari kwa adhabu zote.
FM facts