02/05/2026
MLIMA ARARAT: SHAHIDI WA DUNIA YA ZAMANI NA GHARIKA YA NUHU
Katikati ya mashariki ya Uturuki, karibu na mipaka ya Armenia na Iran, kuna mlima mmoja mkubwa unaoinuka kwa utukufu na kimya cha ajabu. Huu ni Mlima Ararat—mlima wenye kilele kilichofunikwa na theluji mwaka mzima, unaoonekana k**a mlinzi wa historia ya kale sana ya dunia.
Mlima huu una urefu wa takribani mita 5,137, na unaonekana k**a jitu la mawe lililosimama peke yake jangwani. Ukiulinganisha na Mlima Kilimanjaro (mita 5,895), Kilimanjaro ni mrefu zaidi kidogo, lakini Ararat unabaki kuwa maarufu zaidi kiBiblia kutokana na hadithi yake ya kiimani na kihistoria.
Kwenye Biblia, Mlima Ararat unatajwa moja kwa moja katika kitabu cha Mwanzo:
“Na Safina ikatua juu ya milima ya Ararati.” (Mwanzo 8:4)
Huu ndio mstari unaoifanya Ararat kuwa mlima wa kipekee sana katika historia ya imani ya Kikristo, Uyahudi na Uislamu.
GHARIKA YA NUHU NA ARARAT
Biblia inasimulia kwamba dunia ilijaa uovu, na Mungu akaamua kuleta gharika kubwa kuangamiza kila kitu kilicho na uhai. Lakini Nuhu alipewa maagizo ya kujenga safina ili kuokoa familia yake na viumbe wa kila aina.
“Bali Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.” (Mwanzo 6:8)
Mvua ilinyesha kwa siku 40 mchana na usiku, maji yakafunika dunia yote, na milima mingi ikatoweka chini ya maji. Baada ya muda, maji yakaanza kupungua, na Safina ya Nuhu ikatua juu ya milima ya Ararati.
Hapo ndipo dunia ilipopata mwanzo mpya.
ARARAT KATIKA HISTORIA NA IMANI
Ingawa Biblia haitoi maelezo zaidi ya tukio hilo, simulizi ya Nuhu lilibaki kuwa msingi wa mafundisho ya Wayahudi, Wakristo na hata Waislamu kuhusu:
Hukumu ya Mungu
Rehema ya Mungu
Na mwanzo mpya wa binadamu
Yesu mwenyewe alilitaja tukio la Nuhu k**a mfano wa nyakati za mwisho:
“Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.” (Mathayo 24:37)
ARARAT LEO
Leo hii, Mlima Ararat bado upo nchini Uturuki, ukiwa na theluji juu yake na miamba mikali inayouzunguka. Ni mlima unaotazamwa k**a:
Alama ya imani
Ishara ya mwanzo mpya wa maisha
Na sehemu yenye siri kubwa ya kihistoria
Wakazi wa maeneo ya chini wanaishi kwa ufugaji, kilimo kidogo na biashara za mipakani, huku mlima huo ukiendelea kusimama kimya k**a shahidi wa historia ya kale sana ya dunia.
HITIMISHO
Mlima Ararat si tu mlima mrefu wa mita 5,137—ni kumbukumbu ya dunia kuokolewa mara ya kwanza, na ishara kwamba hata baada ya maangamizi makubwa, Mungu hutoa nafasi mpya ya maisha.
Follow Historia zilizofichwa
+255671080371 Whatsapp pekee
✍️ Mwalimu Chalema
TANGAZO
KWA ANAETAKA KITABU CHA VIFO VYA WANAFUNZI/MITUME WA YESU KIKO TAYARI TUMA UJUMBE WHATSAPP KITABU KINA KURASA 41 NI SOFT COPY TOLEO LA KWANZA .Mnavyozidi kuniunga mkono, naamini hiyo itafanikisha kutoa na hard copy.maana kiukweli hardcopy ni gharama.
GHARAMA ni 5000/= dollar 2.