14/04/2024
SIKUTEGEMEA 01
Dayo de Amos
Maisha ni k**a mtihani usiokuwa na majibu ,Kuna wakati unaweza kudhani Duniani umebakia peke yako, lakini sikuzote kwenye maisha urafiki ni zaidi ya ndugu wa damu, miaka hii wimbi la urafiki limekuwa tishio sana. Miaka iliyopita maisha yalikuwa marahisi kuliko sasa.
Miaka mitano iliyopita ilikuwa miaka mizuri sana Kwa bi dada Sheila maana alifanikiwa kupata kazi katika kampuni ya A-vision iliyokuwapo hapa nchini Tanzania. Na wakati huo alikuwa na miaka kumi na nane tu,
"Hongera sana dada yangu nimefurahi Kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa na kazi nyenye mashahara mkubwa, aliongea rafiki yake Sheila aliyejulikana k**a Sakina.
"Hahaha Sakina bwana, ni juhudi k**a hutojali naweza kukutafutia kazi pale,,
"Hapana ,nitatafuta mwenyewe,,
"Sakina unajua ,tumekuwa pamoja Mimi nawewe tumekuwa pamoja Kwa mda mrefu sana, wewe SI rafiki tu Bali ni ndugu yangu kabsaa, ooh hafu nisindikize chuo cha NIT kwanza,,
"Ooh jamani ,unaenda Kufanya nini?,,
"Kuna mtu nataka nimuone kwanza,,
Basi safari ya kuelekea NIT ilitimia huku lengo la Sheila ni kumwona rafiki yake wa utotoni, ambaye Kwa maisha yake aliamua kujitolea kumsaidia, baada ya safari ya nusu saa hivi Walifika chuoni, Sheila akaenda Moja Kwa Moja kwenye idara ya uhariri. Baada ya kufika alimkuta kijana mmoja ambaye ,Sheila alimwangalia Kwa dakika moja bila kuongea....
"Hei dada ,vipi mbona unashangaa? K**a huna la kuongea ondoka hapa,,
Kitendo hicho Sheila hakukipenda sana hivyo akasema...
"Samahani kaka ,naitwa Mina nipo hapa kuonana na mkurungenzi wa chuo,,
"Ooh bi dada ,hukusoma hapo mlangoni?,, Nenda chumba namba Tano kulia utaona mlango,,
Sheila aliondoka huku akiwa Hana raha kabsa, mara baada ya kutoka akakutana USO Kwa USO na Sakina.
"Vipi mbona mnyonge hivo?"
"Hapana kitu, haya twende nyumbani kwangu,,
Safari ya kurudi nyumbani ikawadia mara hii Sheila hakuwa na furaha k**a mwanzo, baada ya kufika aliingia chumbani kwake, cha ajabu kila pembe ya chumba kulikuwa na picha ya mwanaume mtanashati.
"Wewe Sheila huyu ni nani tena?,,
"Ooh huyu ni mtu niliyeenda kumwona,,
"Nini kilitokea? ,mbona ulikuwa na hudhuni kiasi hicho? Na nilisikia hukumwambia jina lako Kwa nini?,,
"Ooh wewe ulijuaje ? Nilisikia jinsi mlivyokuwa mnaongea,,
"Ooh sawa , alionekana kunisahau kabsa hata hajui ni nani aliyemsaidia kufikia pale,,
"Ooh Sheila labda ungemwambia ukweli angekukumbuka,,
"Sitaki ajue Mimi ni nani k**a amesahau acha iwe hivyo tu,,
Mazungumzo yalikuwa k**a kwamba mwiba mzito ulikuwa ndani ya moyo wa Sheila, lakini Sakina yeye alionekana kuwa na hamu ya kumjua yule kaka. Baada ya hapo Sheila alimsindikiza Sakina kuelekea nyumbani kwao ,na Kisha naye akaelekea kazini kwake, alipofika kazini alimkuta msaidizi wake akiwa na barua mbili.
"Wewe Salma nini hicho,,
"Bosi niliambiwa Kuna barua hizi zinatakiwa kusainiwa ,,
"Sawa ,lete nizione ,hafu Kuna kitu nataka unifanyie ...
"Kitu gani tena ,bosi Sheila ?,,
"Hivi juzi tulijadiliana na mkurungenzi wa idara yetu Kuna nafasi ya kazi alitaka kuitafuta, k**a bado ipo uje unambie,,
Salma aliondoka kwenda kwenye ofsi ya mkurungenzi, wakati huo Sheila alikuwa akipitia barua hizo, mara baada ya kumaliza, Salma alirudi. Sheila alikuwa na hamu sana kujua k**a nafasi bado ipo. Kwa hiyo ilibidi kuumuuliza .
"Nambie bado ipo?, Sheila aliuliza.
"Ndio ipo ila Kuna barua mbili za maombi,,
Wakati hayo yakiendelea nyumbani Kwa Sakina naye alikuwa akijiuliza maswali mwengi sana hasa Kwa nini picha ya yule kijana ilikuwa mle?, Hakutaka kutulia hiyo alichukua tax kurudi chuoni, naye Moja Kwa Moja alienda kwenye chumba cha huyo dokta, mara hii hakumkuta isipokuwa alimkuta mfanya usafi.
"Dada samahani ,huyu bwana Yuko wapi?,, Sakina aliuliza.
"Samahani hatuna bwana hapa, kwanza wewe ni nani?,,
"Ooh samahani ,k**a akija mwambie rafiki yake Sheila alikuja hapa,,
Sakina aliondoka akiacha maagizo Kwa mfanya usafi wa ofsi .wakati huo sheila akiwa na Salma mara baada ya kugundua walituma nafasi ni wachache, ikabidi kumpigia Sakina rafiki yake.
"Haloo Sakina, uko wapi?,, Sheila aliuliza, swali Hilo lilimfanya Sakina kuwa na kigugumizi.
"Ni.....ni.....ni....nipo nyumbani hapa ,vipi kwani Kuna shida Sheila?,,
"Hapana nataka kukwambia kuwa zimebakia siku mbili kufanyika Kwa interview ya kumpata msaidizi wa kukusanya mapato, vipi upo tayari?,,
"Ooh jamani rafiki yangu ndio maana nakupenda, nawezaje kukosa kazi hiyo?, We niambie nini kinatakiwa?,,
"Nakutumia link Kwa whasap yako utaona nini kinatakiwa,,
Baada ya maongezi hayo simu ilikatika ,huku Salma akimuiliza bosi wake, "hivi unauhakika na huyu mtu, mbona anaonekana k**a mhuni mhuni tu"
"Ooh Salma Kwa nini unasema hivyo?,,
"Sheila hata namna anavyoongea tu ,anaongea k**a mtu aliyeridhika na maisha yake,,
"Salma huyu namfahamu vizuri mno, nimesoma naye ,tukaishi naye ,ni mtu mzuri sana, najua vyema anaweza kazi hiyo,,
"Sawa bosi, k**a upendavyo,,
"Sawa Salma niamini Yuko vizuri sana,,
Baada ya maongezi hayo, Salma aliondoka zake, wakati huo chuoni yule mhariri alikuja na alipoingia tu taarifa ikaja.
"Mkuu Kuna mtu alikuwa anakutafuta,,
"Nani huyo?...
"Anaitwa Sheila ...
"Nini Sheila yupi?"
"Mkuu sijui ila alijitambulisha Kwa jina la sheila,,
"Sawa hata simfahamu kabsaaa.,,
Yule Binti alitoka na kumwacha bwana huyo akitafakari Sheila ni nani ,na Kwa nini amtafute?,,
Tangu miaka kumi na nane hawajawahi kuonana na Sheila, wakati huo katika kampuni ya A-vision suala la kumpata msaidizi lilizidi kuwa na kasi ,mara hii Sheila alimpigia Sakina.
"Rafiki yangu ,kesho njoo kwenye interview,,
"Oooh waho! Sawa rafiki na kuna nini cha kuja nacho?,,
"Usijali nitakutumia kwenye whatsapp ,,
Simu ilikata, mara baada ya kukata ,salma akamuuliza tena bosi wake.
"Maadam sheila hivi, unauhakika na huyo mtu?,,
"Jamani, salma usijali bila shaka ukimuona utampenda yuko vema kabsa hana shida na mtu,,
"Sawa, lakini.......,,
"Lakini nini tena ,salma jamani?,,
"Shida sio kwamba sina imani naye sijawahi kumjua lakini ,mbona najisikia vibaya hivi?,,
"Hahahahhahaha,, sheila aliangua kicheko , jamani usihofu hakuna kitu kibaya kwake namwamini sana,,
Wakati hayo yakiendelea Sakina aligeuka kuangalia kwenye dressing yake ,kisha akachagua gauni moja matata, baada ya kulivaa simu ilianza kuita ,alichukua simu yake na kuipokea.
"Haloo, subiri natoka sasa hivi,, aliongea sakina. Kweli alifunga kabadi lake na kisha kuondoka kuelekea nje, alipofika alikuwa kuna gari moja mhimu lilikuwa limepaki.Aliingia kwenye lile gari kisha akaondoka haikujulikana wapi alielekea.
Wakati huo Sheila alimpigia baba yake ...
"Halooo baba ,
"Haloo mwanangu, unaelendeleaje huko?,,
"Baba sisi tuko wazima, sana,,
"Vipi mbona unaongea kinyonge hivyo?,,
" Baba ! Ulisema nikaonane na yule mtu, hanikumbuki kabsa, hata kujua mimi ni nani hakujisumbua kabsa,,
"Mwanangu ,sinauhakika k**a kweli unayoyasema, ulijitambulisha kwake?
"Aanh baba kiukweli hanitambui kabsa,,
"Sawa niachie mimi nitalifanyia kazi,,
Baba aliongea akiahidi mkumsaidia binti yake.
"Maadamu ,ulikuwa unaongea na nani?,,
"Salma usijali ni baba,,
"Maadamu wewe ni k**a dada kwangu siku ya leo hauko sawa ,shida nini?,,
"Salma hakuna shida pengine uchovu make mambo ya kushughulikia nayo ni mengi, ndio maana niko hivi,,
Sheila aliamua kutoka nje kupinga upepo huku akikumbuka njinsi alivyotolewa maneno na yule mhariri.
Akiwa pale simu iliita namba ilikuwa namba ya Sakina ,
"Sakina ,unasemaje kipenzi,,
"Uko wapi?, Nipo ofsini vipi kuna shida?,,
"Hapana ,ila nimeshindwa kukalili yale maswali ,nifanyie mpango wanipitishe free tu,,
"Sakina hiyo haiwezekani ,kumbuka kwamba mimi sio meneja wa hii kampuni, kwa hiyo nimekutumia maswali jiongeze na wewe,,
"Kuna kitu nakifatilia hapa, ndio maana nikakuomba,,
"Ok sawa nitajaribu,, Sheila alikubali hapo papo akainuka kuelekea kwa mkurugenzi wa kampuni. Bwana Albert
"Mkuu samahani ,aaaa nimeona nikueleze jambo mhimu sana, make nimejaribu kufanya utafiti juu ya hawa watahiniwa wetu, mmoja tu ndio naona mwenye vigezo,,
"Ooh sheila, unajua hatuwezi kufanya jambo kwa njia hii labda ni hakikishie unamwamini na anasifa zote tunazozihitaji?,,
"Bosi usijali k**a kuna changamoto juu ya utendaji kazi wake bila shaka nitakudhibitishia hujakosea kunchagua,,
"Sawa, lete jina lake,,
Sheila alimpatia form ya Sakina ,na kuondoka, alipotoka tu akakutana na Salma.
"Salma kuna nini?,,
"Hapana, nilitaka kujua uko sehemu gani?,,
"Oooh! Jamani usiwe na wasi wasi juu yangu, leo twende tukale cha kula jioni pamoja,,
"Sawa maadamu wangu"
Baada ya makubaliano hayo kila mtu alikuwa na furaha sana. Wakati huo sakina alikuwa zake maeneo ya resort akila bata.hakuwa na wasi wasi plani zake ni kumjua yule kaka na namna gani anahusiana na Sheila. Alikuwa akipiga picha namna ya kumvutia kijana yule, baada ya kufikilia kwa mda alipata jibu na aliamua kurudi nyumbani.
Ilipofika majira ya asubuhi sakina aliamka mapema alijiandaa kisha akaita tax na safari kuelekea A-vision iliwadia, baada ya kufika alimfuata Sheila ofsini kwake.
"Ooh sheila mambo vipi mwana?,,
"Sakina?, Umefika saa ngapi?,, Aliuliza sheila."
"Mda so mrefu, vipi hapa panaonekana full bata , pananifaa sana,, aliongea sakina.
Salma akatia neno."Ndugu samahani itabidi uende kule. Chini subiria tu huko tafadhali,,
Kitendo hicho hakukipenda sana bibie Sakina.
"Sheilaa hii ni nini?, Na huyu ni nani?,,
"Sakina, sikia nenda tu kule isije ikaharibu mpango wetu,, sheila aliongea. Hata hivyo sakina aliondoka kuelekea kwa watahiniwa wenzake. Baada ya mda wote waliitwa tayari kwa kufanyiwa interview, Baada ya interview Sakina alionekana kukosa furaha, Sheila alimfuata.
"Vipi tena mbona uko hivyo?,,
"Kwani wewe unataka niweje?, Mbona kila siku niko hivi?,, Alijibu sakina kwa dharau, hata sheila alilitambua hilo. Hata hivyo hakutaka kuendelea kumuuliza, aliondoka kuendelea na kazi zake baadae alikuja bwana Albert.
"Sheila mtu wako kajitahidi kwa kuwa uko hapa ni rahisi sana kwako kuangalia mwenendo wake,, aliongea bwana Albert.
"Hakuna shida boss ,najua utampenda,, alijibu sheila.
Baada ya maongezi hayo Bwana Albert aliitisha kikao cha dharula katika ukumbi wa kikao ,timu nzima ya A-vision ilifika,
"Nimewaiteni hapa kwa lengo moja tu ,hii weekend tutakuwa na tour tutaenda uturuki kwa ziara kwa hiyo kila mtu ajiandae na hili naliacha kwako Sheila,, aliongea boss Albert.
Baada ya kuongea hayo kila mtu alifurahi sana, wakiwa anapongezana alikuja Mariam msaidizi wa Albert.
"Sheila nataka kuongea na wewe, njoo ofsini kwangu,, baada ya kuongea hivyo aliondoka ,wakati huo John yeye alikuwa zake pembeni akiangalia mchezo kwa kuibia , baada ya kuona tukio la mariam alimfuata Sheila.
"Dada naitwa John ,bila shaka wewe ndo sheila?,,
"Ndio ,nambie,,
"Ooh ! Hongera sana ,sikuepo hapa kwa mda ,niko kitengo cha mawasiliano niko chini ya mariam,,
"Oooh sawa, nafurahi sana kukufahamu ,bila shaka tutakuwa timu,, aliongea sheila.
"Ndio bila shaka, kuwa makini,,
Baada ya maongezi hayo, sheila ilibidi kumfuata mariam, baada ya kufika.
"Sheila nimeandaa mipango yote ya safari ,kisha nimetoa order kwenye moja ya hotel iliyopo mji wa agharibi ,hii hoteli inagharama mzuri sana kwa siku wanatoza dola 1560$ tu,,
"Ooh sawa nimependa wazo lako lakini je boss atalikubali?,, Aliuliza Sheila.
"Kuhusu boss usijali ,mwambie ni mpango wangu atapenda mandhari ya hoteli hiyo wala usijali sawa?,,
"Sawa, k**a unavyotaka,,
"Nimefurahi kukujua natumai tutakuwa timu,, ( walishikana mikono kuonesha kuwa wamekubaliana).Baada ya hapo Sheila alirudi kwa marafiki zake, alipofika tu simu yake ikaita namba ilikuwa boss Albert, alipisha pembeni kuipokea, hakuchukua mda kisha akapanda kuelekea ofsini kwa boss.
"Mkuu nimekuja,, aliongea Sheila.
"Huyo mfanya kazi wako mwambie kesho aanze kazi mara moja, mpangie majukumu yake ipasavyo,,
Baada ya sheila kupokea maelekezo hayo alirudi kwa marafiki zake, salma alikuwa wa kwanza kutaka kujua alichoambiwa na boss.
"Maadam sheila nambie boss kasemaje?,,
"Salma usijali ni suala la kiofsi wala hakuna jambo geni kabsa,,
Wakati hayo yakiendelea ,sakina yeye alikuwa njiani kuelekea Chuoni kuonana na yule mhariri, baada ya kufika moja kwa moja alienda kwenye ofsi ya mhariri. Sakina alibisha hodi kisha sauti ikasikika
"Karibu, ingia,,
Sakina aliingia kwa macho ya soni.
"Mkuu habari,,... Sakina alisalimia
Yule mhariri hakuelewa shida ya yule mdada ambaye hakuwa kumuona hata siku moja.,kabla hajajibu msaidi wa mhariri akafika.
"Mkuu.....,ooh kuna mgeni kumbe,,
"Ooh hakuna shida sharifa, nambie kuna shida?,,
"Hapana ,ila ....ila.... Au malizana na mgeni wako kwanza,,
Sharifa aligeuka kuondoka kabla hajafunga mlango ,akasikia sauti ikimuuliza ...
"Sharifa huyu mdada unamfahamu?,,
Ndio bosi, ndo yule mdada aliyekuja siku za nyuma akikuulizia, anaitwa Sheila,, baada ya sherifa kujibu aliruhusiwa kuondoka.
"Kwa hiyo wewe ndo yule binti unayenitafuta?,,
"Aah! Ni.... Ni nikweli,,
"Sawa niko hapa sema sasa,,
"Aanh najiua umenisahau si rahisi kukumbusha kwa nini nimekuja kwako, tumetoka mbali sana labda je unanikumbuka?,,
"Aanh ndio ,nakumbuka lakini sheila siikumbuki sura yake, lakini huwa nasikia sheila kutoka kwa baba yangu ,tofauti na hapo siwezi kusema uongo simfahamu kabsa sheila alivyo,,
"Hahaha(sakina alicheka kidogo huku akinyanyuka kwenye kiti), nikweli kabsa lakini nambie nini kilitokea siku hiyo?"
"Siku gani? Na ilikuwaje?,, Mhariri alikuwa na hamu ya kujua
"Namba yangu hii hapa ( alitaja namba)"
Baada ya kutaja namba aliondoka kuelekea nyumbani, baada ya kufika alimkuta sheila akimsubiria.
"Ulikuwa wapi?, Nimekusubiria ,mbaya hupokei simu,, aliongea Sheila.
"Ooh samahani ,sikuiona missed call yako, hata hivyo usijali niko hapa sasa, nambie .......,