26/08/2026
Niwaambie tu Ukweli wale mnaombeza Aziz Ki mkisema ni mzee na Yanga wamefanya k**ari mbaya Kumuachia Okello na kumsajili Aziz Ki Mzee iko hivi.
Okello licha yakuwa ana umri wa Miaka 25 yeye alikuwa anakupa pasi nzuri za uhakika Aidha afunge au atengeneze Assist ndio maana kwa muda mfupi alifanya maajabu makubwa lakini tukiongelea ule ukweli ni kwamba kiwango cha Okello bado hakijafika kwa Aziz Ki kwasababu ya Ile Nguvu ya kumiliki mpira
β‘οΈ Mpira wa Tanzania hautofautiani na wa Morocco, Huku mpira sio mchezo wa Miguu tu, Mpira ni Vita Ndio maana Mwezi huwezi kupita bila Red Card. Sasa Okello ni mwepesi sana wa kuhimili mikiki mikiki ya Ligi hii
Aziz Ki ana miaka 30, Na huyu Duke Abuya ana miaka 32 k**a alivyo Shalulile, ni wazi hapa hakuna mzee. Mbona kina Messi, Ronaldo na Pepe wa miaka ya 80 bado wanacheza??
Je, Duke Abuya ambaye Umri wake umesogea kwa uchezaji wake unaweza kumuita mzee?? Au ni k**a vile kijana tu wa miaka 19. Hii inatokana na Fitness ya mchezaji Umri sio kigezo.
Yanga wameamua kujifunza kwa waarabu ambao wao wanasajili wa miaka 30+ lkn wa kazi chafu kuliko vijana wadogo wadogo hawa ambao bado hawajawa na Ukomavu kwenye Football mfano Doumbia
Huyu Abuya, Mudathir na Max hawa ndio viungo bora na hatari zaidi kwasasa Afrika Mashariki k**a kuna mwingine mlete anayejua sekta zote k**a hawa wanalinda, wanakaba, wanachenga kwa kujiamini, wanagawa pasi ndefu na fupi, wanatengeneza mashambulizi na kufunga pia. Huu ni utatu mtakatifu, Fred Ngoma sio mbovu ila kwa hawa ana mengi ya kujifunza...
Eti Ngoma alisajiliwa kwaajili ya Kumkalisha Abuya Benchi, wee mdau unaona hilo linatimia au ni kuikosea klabu heshima?? Follow Rassi Stories kwa habari za michezo na burudani