BeipoaLtd-Digital Marketing Axis

BeipoaLtd-Digital Marketing Axis Like na kushare Ukurasa wangu kwa burudani,maarifa na taarifa za mastaa

Mmnampa %ngap kwa kutoaaaa vipaji vya mzikii katik tasniaaa ya muzik nchin tanzania
26/11/2020

Mmnampa %ngap kwa kutoaaaa vipaji vya mzikii katik tasniaaa ya muzik nchin tanzania

23/10/2020
hellow mambo?!
28/09/2020

hellow mambo?!

Vijana wenzangu wale watu Waliokua wanatuambia Kwa miaka mitano mfululizo tujiajiri sasa wako mbele yetu wanaomba ajira ...
30/08/2020

Vijana wenzangu wale watu Waliokua wanatuambia Kwa miaka mitano mfululizo tujiajiri sasa wako mbele yetu wanaomba ajira hivi tuwafanyeje hawa watu.

šŸ˜‚šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£

Kwanza kabisa niombe radhi kwa mtu ambaye picha hizi zitamletea usumbufu. Tumemchangia miguu bandia dada Jackline baada ...
24/08/2020

Kwanza kabisa niombe radhi kwa mtu ambaye picha hizi zitamletea usumbufu. Tumemchangia miguu bandia dada Jackline baada ya kupoteza miguu yake kutokana na ugonjwa ujulikanao k**a Gangrene au kwa Kiswahili Gangrini. Wengi hawaufahamu ugonjwa huu. Je Gangrini ni nini? Inasababishwa na nini? Dalili zake ni zipi? Je inazuilika?

Dr.Roman Shao Jr. anayesomea udaktari bingwa wa magonjwa ya dharura nchini China anatoa elimu kidogo kuhusu ugonjwa huo.
_____
Gangrini ni hali ambayo tishu za mwili hufa kutokana na kutopata damu ya kutosha. Kwa kawaida damu hutoa oksijeni, virutubisho vya seli na vifaa vya mfumo wa kinga mwilini. Kwahiyo k**a kuna sehemu katika mwili wako damu haifiki vizuri, seli haziwezi kuishi na tishu zako zitaharibika na kufa.

:
Kuna aina tatu za Gangrini.

1. GANGRINI KAVU; Tishu hukosa damu na hivyo hukauka na kudondoka. Hutokea zaidi kwenye vidole.

2. GANGRINI NYEVU; Tishu huvimba na kupata malengelenge.

3. GANRINI GESI; Bakteria huambukiza tishu na husababisha bubu za gesi (gas bubbles ) ndani yake.

Pia Gangrini inaweza kugawanywa kutokana na maeneo inapoathiri. Kwa mfano;

1. GANGRINI YA NDANI; Huathiri ogani za ndani ya mwili k**a utumbo, bandama na apendix etc.

2. FOURNEARS; Huathiri zaidi sehemu za siri hasa wanaume na kupelekea via vya uzazi kuoza.

3. MELENEYES; Hutokea mara baada ya mtu kufanyiwa upasuaji, damu inashindwa kufika kwenye kidonda na hivyo tishu za eneo hilo kufa na kupelekea kidonda kuoza.

4. NOMA; Huathiri uso. Tishu za uso hufa na hivyo kusababisha mtu kuoza uso.

:
Kila aina ya Gangrini ina dalili zake. Japo dalili za ujumla ni pamoja na kuumwa sana kichwa, ngozi kubadilika rangi, maumivu kwenye eneo lililoathirika etc.

; Ngozi kuwa ngumu na kavu, Ngozi kubadilika rangi (kuwa nyeusi), Ngozi kuwa kavu kuliko kawaida.

; ngozi kuwa na majimaji/ Unyevu, Kuvimba kwa eneo lililoathirika, Malengelenge, Ngozi kubadilika rangi na kuwa nyeusi au kijani, Harufu mbaya.

; Maumivu makali sehemu iliyoathirika, Mafua, Homa, rangi ya ngozi kuwa hudhurungi, nyekundu au zambarau, Malengelenge, sehemu iliyoathirika kubonyea k**a sponchi.

:
1. Hitilafu katika mishipa inayosambaza damu mwilini kutoka kwenye moyo (Coronary artery disease).
_
2. Maambukizi ya backteria.

3. Majeraha ya bunduki au ajali yanaweza kusababisha bakteria kuvamia tishu zilizo ndani ya mwili.

4. Kisukari.

5. Uvutaji wa sigara au unywaji wa pombe kali kupita kiasi.

6. Kupooza kwa muda mrefu.

7. Unene kupita kiasi.

;
1. Muone daktari unapoona mabadiliko yoyote katika ngozi yako au jeraha lisilopona.
2. Ikiwa ulifanyiwa upasuaji muone daktari k**a maumivu yanazidi katika jeraha au ngozi inabadilika rangi.
3. Jiepushe na matumizi makubwa ya pombe kali na bidhaa za tumbaku.
4. Fanya mazoezi ili kuweka sukari yako iwe katika hali ya kawaida.
5. K**a una jeraha hakikisha utunzaji mzuri wa kidonda ili kuepusha maambikizi ya bakteria.
6. Punguza unene.
7. Kula vyakula vya kuongeza damu.

:
Vipimo hutegemea na aina ya Gangrini na hali yako, lakini inaweza kujumuisha vipimo vifuatavyo:

1. Vipimo vya picha k**a CT-Scan au MRI; Vipimo hivi huunda picha za ndani ya mwili na vinaweza kuonyesha gesi kwenye tishu.

2. Vipimo vya damu - Hivi vinaweza kutafuta ishara ya maambukizi ya damu mwilini.

3. Kupima mtiririko wa damu - hivi huonesha k**a kuna shida katika mishipa ya damu katika kusambaza damu mwilini.

:
1. Upasuaji wa kuondoa tishu zilizokufa (kukata sehemu iliyoathirika k**a vile mguu, mkono au vidole).
2. Kupewa dawa za kuua wadudu ndani ya mishipa ya damu (intravenous therapy).
3. Kuondoa ngozi iliyoharibika (skin grafting).
4. Kuongeza oksijeni kwa wagonjwa wenye matatizo ya kupumua.
5. Kuongezewa damu.

UKUTA UMEFUNUA SIRI YA TANZANIA - Tundu Lissu Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba nchi yetu inatawaliwa...
24/08/2020

UKUTA UMEFUNUA SIRI YA TANZANIA - Tundu Lissu

Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba nchi yetu inatawaliwa na chama cha siasa, yaani CCM. Hata hivyo, wapo wachache ambao walishaanza kuhoji k**a CCM ni chama cha siasa hata kabla mfumo wa vyama vingi vya siasa kuruhusiwa miaka 25 iliyopita. Ukisoma 'The State and the Working People in Tanzania', kilichohaririwa na Prof. Issa G. Shivji na kuchapishwa mwaka '87, utagundua kwamba tayari kuna wasomi ambao walishaanza kuhoji k**a kweli CCM ni chama cha siasa. Chama cha siasa huongoza kwa hoja za kisiasa, sio kwa bunduki, mizinga na mabomu. Chama cha siasa hushinda mijadala ya kisiasa kwa kutumia ushawishi wa hoja za kisiasa na kiitikadi, sio kwa vitisho vya kuua au kuvunja miguu ya mahasimu wake wa kisiasa.

Chama cha siasa huenda kwa wananchi kuwashawishi wakiunge mkono, hakijifichi nyuma ya vyombo vya ukandamizaji vya dola na kuwatisha wananchi. Miaka miwili iliyopita Jakaya Kikwete aliwaambia wanaCCM wenzake waende kwa wananchi wakafanye kazi ya siasa, waache kutegemea kubebwa na Jeshi la Polisi. Hili limewashinda, bila majeshi na bunduki na mabomu, CCM haiwezi kufanya kazi ya siasa. Bila ma-DC na ma-OCD, CCM haiwezi chochote.

Zamani walikuwa wanatuita sisi wapinzani vyama vya msimu vinavyosubiri uchaguzi ndio tufanye kazi ya siasa. Sasa wanatukataza kufanya kazi ya siasa mpaka tusubiri msimu wa uchaguzi. Sasa sisi ndio chama cha siasa, maCCM yamegeuka kuwa chama cha msimu. Wanajifanya walishinda uchaguzi lakini hawadiriki kuturuhusu sisi tulioshindwa kwenda kuongea na wananchi.

Wenye hatia huwa na hofu - the guilty are afraid. Wanatukataza siasa kwa sababu wanajua hawakushinda uchaguzi na wanajua wananchi wengi wanajua hivyo. Na wanajua hawana majibu ya hoja nyingi za kisiasa za utawala huu wa kidikteta. Kwenye 'The State and the Working People in Tanzania' kuna makala inayoitwa 'The State and the Party' ambayo inazungumzia uhusiano kati ya CCM na vyombo vya dola, hasa majeshi.

Tangu mwaka '64 lilipoundwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana kati ya chama na vyombo vya ukandamizaji vya dola. Mfano mzuri wa uhusiano huu ni makada wa chama kuingizwa jeshini na kufanywa maafisa wa jeshi, na maafisa wa jeshi kufanywa makada wa chama na kupewa kazi za kisiasa na/au za kiraia. Wafikirie akina Kikwete, Kinana, Makamba, Nsa Kaisi, Kiwelu, Nnauye, Kafanabo, n.k. Orodha ni ndefu sana.

Wakati wa mfumo wa chama kimoja, majeshi yaligeuzwa kuwa Mkoa wa Chama, sawa na mikoa ya kijiografia k**a Dar au Singida. Lengo lilikuwa ni ku-integrate zaidi majeshi katika mfumo wa kisiasa na kiraia ili kuulinda mfumo unaotawala. Katika era ya vyama vingi, majeshi yameondolewa katika siasa kikatiba na kinadharia tu. Katika hali halisi, mambo hayajabadilika kwa kiasi chochote cha maana. Angalia wanajeshi walioko katika nyadhifa za kisiasa za kiraia k**a ma-DC, ma-RC na sasa hata maKatibu Wakuu wa wizara. Wote hawa ni maCCM kwa Katiba ya sasa ya CCM. Angalia wanajeshi walioko katika uongozi wa CCM ambao jana tu walikuwa wanakatazwa na Katiba ya nchi kuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Kwa hiyo, kinachoonekana sasa kwa majeshi kujitokeza hadharani ili kuzuia UKUTA, ni ushahidi wa wazi kwamba CCM haiwezi tena kujenga hoja ya kisiasa kwa wananchi na ikakubaliwa. Sasa ni wakati wa mabavu ya kijeshi tu. Na wala sio utii wa sheria bila shuruti tena. Kwa vile sheria ya mikutano ya kisiasa na maandamano iko upande wetu, sasa ni wakati wa shuruti ya kijeshi bila sheria.

Tukishinda vita hii ya sasa, watesi wetu hawatakuwa ni silaha nyingine yoyote itakayobaki. Tutashinda. Wakati ni UKUTA. Aluta continua!!!!!!

Mwaka 2017 nilivamiwa na polisi Wilayani Tarime wakanipiga na kunivunja mguu kwa kile kilichodaiwa kwamba nimesimamishwa...
24/08/2020

Mwaka 2017 nilivamiwa na polisi Wilayani Tarime wakanipiga na kunivunja mguu kwa kile kilichodaiwa kwamba nimesimamishwa nimekaidi agizo la kutosimama, Wamenisababishia kilema cha kutosikia upande wa sikio langu la kushoto na kwa bahati mbaya wale Polisi walionitendea unyama huo baada ya uchunguzi wa kipolisi kufanyika ilionekana walitenda kosa kisheria na RPC kipindi hicho ANDREW SATTA aliwasimamisha kazi kwa makosa hayo..

Badae Mkuu wa Wilaya GLORIOUS LUOGA aliingiza siasa kwamba aliepigwa ni mdogo wa Heche na Kwaki pindi chote hicho sikuwahi kua mwanasiasa wala kufanya siasa lakini nilitendewa unyama huu na nikakosa haki yangu kwakua kaka yangu ni mwanasiasa wa UPINZANI, Nachoweza kusema ni kwamba serikali inaonea watu na haki haipo tena Tanzania tujitokeze kukemea uonevu huu.

RPC akaonekana ndie mwenye makosa kuwawajibisha watu walioniga Mtu anaetokana na Mpinzani JOHN HECHE, Kilichofuata ni RPC kuhamishwa na polisi wale kurudishwa kazini, nilijiuguza kwa msaada wa familia yangu mpaka nikapona Mungu ni mwema leo naweza kutembea.
Heche Enock

KWENYE MAISHA UTANI UKO ATA ENZI ZA  MABABU ZETU WALIKUWA WANATANIANA ATA KWENYE MISIBA PIA  TUNAONA UTANIkiukweli Adam ...
17/08/2020

KWENYE MAISHA UTANI UKO ATA ENZI ZA MABABU ZETU WALIKUWA WANATANIANA ATA KWENYE MISIBA PIA TUNAONA UTANI

kiukweli Adam MCHOVU umezingua Sana na umekosea ningekuona MJANJA ungekausha kimiya tu au ungesema tu izo bangi tunafutaga wote kuliko ayo mahamuzi uliyoyachukua kumkata mtama mwenzako mbele za watu na viongozi wa serakali moja kwa moja umewaaminisha watu wewe kweli bangi kwa kile ulichokifanya kuchukua Sheria mkonni wewe Ni MTANGAZAJI MAHARUFU Sana umejifunjia heshima yako badilika mzee baba hayo siyo maisha mzee baba umetia aibu Sana mbele ya viongozi wa serekali wamekuamini na ndio maana wamekupa nafasi ya kuendesha tamasha ilo matokeo yake umefanya kitu Cha KIJINGA sana fikila ulichokifanya kumkata mwenzako mtama angeangukia kichwa au sehemu mbaya na angekufa wewe ungekuwa wapi asaivi ata kisheria UNGETAKIWA uk**atwe Adam MCHOVU kwa kosa la udhalilishaji na kuchukua Sheria mkononi WANAUME AWAISHI ivyo

ACT WAZALENDO NA CHADEMA TUTASIMAMISHA MGOMBEA URAIS MMOJAKIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kati...
17/08/2020

ACT WAZALENDO NA CHADEMA TUTASIMAMISHA MGOMBEA URAIS MMOJA

KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, chama chake pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vitaungana ili kusimamisha mgombea mmoja wa kiti cha urais.

Hayo aliyasema juzi jijini Mwanza wakati akizungumuza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano mkuu wa wajumbe wa chama hicho Jimbo la Nyamagana wakupata mgombea ubunge kwa jimbo hilo.

Zitto alisema vyama vya upinzani vyenye nia ya dhati kushirikiana kwa sasa ni viwili, hivyo anawahakikishia Watanzania vitasimamisha mgombea mmoja wa urais ambapo mchakato wa kisheria unafanyiaka ili kufikia maafikiano.

ā€œHadi sasa sisi tunajua kitu gani kinachoendelea, tumejipanga ninachotaka kuwakikishia tu ni kwamba tutakuwa na mgombea mmoja wa upinzani.

ā€œMazungumuzo bado yanaendelea, yapo vizuri na dhamira yetu ni hiyo, hatuwezi kuwavunja moyo Watanzania, wanataka mabadiliko, na wanataka vyama vishirikiane nasi tutashirIkiana na hiyo ndiyo kauli ambayo naomba muwafahamishe wananchi,ā€ alisema Zitto.

Kuhusu minong’ono ya kutoelewana kwa baadhi ya vyama vya upinzani, Zitto alisema hiyo inatokana na utofauti wa maono, sera na mikakati na hivyo kutokuelewana wakati mwingine ni jambo la kawaida.

Alisema kuelekea Uchaguzi Mkuu chama chake kitakuwa tayari kushirikiana na vyama vyenye sera makini tu na si vinginevyo.

Kuhusu mfumo wa k**ati kuu ya chama hicho kupitisha majina wa wagombea baada ya kura za wajumbe, Zitto alisema mfumo huo ni wa kurithi kutoka kwenye katiba ingawa ni lazima ifikie hatua vyama vya siasa viheshimu maamuzi ya wanaopiga kura ngazi ya chini.

Alisema hoja ya chama chake kuheshimu maamuzi ya wajumbe ni nzuri lakini kwa sasa ni vigumu kuitekeleza kwa sasababu ndani ya katiba ya vyama vyote maelekezo ni kwamba k**ati kuu ndiyo inatakiwa kufanya maamuzi.
Chanzo: Mtanzania Digital Jumapili Agosti 16, 2020

Address

Dar Es Salaam
00255

Telephone

+255766202020

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BeipoaLtd-Digital Marketing Axis posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to BeipoaLtd-Digital Marketing Axis:

Share