29/07/2025
“Tumeingia Simba sababu ni timu kubwa Afrika, ni timu ambayo inajulikana pande zote za bara hili na hilo ndio tunaangalia zaidi kwenye biashara. Tulikuwa tukiifatilia kwa miaka karibu sita lakini sasa imekuwa kweli. Tunafuraha kufanikisha jambo hili.”
“Huu ni zaidi ya ushirikiano na inatakiwa klabu zote zifaidike na jambo hili. Tunashirikiana na timu nyingi kubwa ambazo tunadhamini hivyo uzoefu huo utatusaidia kufanikisha jambo hili.”
“Nina furaha kwa ushirikiano huu lakini tutafanya kazi kuangalia namna gani ya kufanikisha ushirikiano na vilabu vingine vikubwa ambavyo tunashirikiana navyo.”- Mkuu wa Udhamini wa BetWay Afrika, Jason Shield. NguvuMoja