Sima Stories

Sima Stories Sima stories is a brand name of passionate & ambitious group of individuals who like to tell stories

26/06/2024
03/08/2022

Umeshawahi kufikiria kumshukuru EX wako?

GLORIOUS MISSION - 03Ndugu msomaji k**a hukusoma sehemu ya kwanza na ya pili bonyeza hapaGLORIOUS MISSION - 01https://we...
30/03/2022

GLORIOUS MISSION - 03
Ndugu msomaji k**a hukusoma sehemu ya kwanza na ya pili bonyeza hapa
GLORIOUS MISSION - 01
https://web.facebook.com/simastories/photos/a.115692673481442/327083862342321/
GLORIOUS MISSION - 02
https://web.facebook.com/simastories/photos/a.115692673481442/334739901576717/

AU ENDELEA NA GLORIOUS MISSION - 03

ILIPOISHIA
Na ni kweli, yule askari akasema “naomba niingie dakika moja tu!” Akaruhusiwa kuingia, akaomba anikague kujiridhisha kiusalama. Basi akanikagua na hakukuta silaha wala kitu chochote chenye kuleta mashaka. Kisha akaangalia angalia pale ndani na hakuona dalili yoyote ya kuwepo kwa silaha. Mwisho macho yake yakatua kwenye maboksi mawili, moja lilikuwa na madawa na lingine lilikuwa na vifaa vya huduma ya kwanza na matibabu ya dharura. Akawaambia wale madaktari wafunue boksi moja la mbele ya lingine. Wakafunua, akachungulia kisha akatulia k**a sekunde ishirini hivi, kisha akatikisa kichwa na kusema “samahani sana kwa kuingilia kazi yenu, nilikuwa tu nahakikisha usalama wenu. Samahni sana kwa usumbufu pia ahsanteni kwa ushirikiano wenu na mko salama hivyo wawaisheni hawa watu hospitali” “aaaah haina shida usijali” akajibu Bamdogo Kasim huku akiondoa gari haraka kutoka langoni pale na kuitafuta barabara kuu kwa kasi kubwa sana. Baada ya dakika k**a tatu hivi tulipishana na ambulance halisi ikienda eneo la tukio. Hapa sasa alianza kuendesha gari k**a mwehu huku pikipiki niliyokuja nayo ikitufuata nyuma. Nilihisi kabisa ni mtu wetu pia japo hata sikujua Kasim alimpa funguo muda gani mtu huyo. Tukiwa tunakimbia kwa kasi ile, niliwaza sana, wamejuaje k**a nimetingwa? Ni nani huwa ananifuatilia kwenye misheni zangu wanazonipa? Tunaenda wapi mda huu? Inakuwaje polisi wakijua gari yetu ilikuwa ambulance feki? Bamdogo kaitoa wapi? Pastor Enock tunampeleka wapi? Je yuko upande wetu au ni adui yetu? Vipi yule dada niliyemuacha pale uwanjani hana fahamu yuko salama? Nitamuona vipi tena? Sikupata jibu hata moja, nikasubiri muda uamue.
……………………………………………………..
ENDELEA….
Tukiwa tumeshika barabara ya kwenda Mbeya mjini, bamdogo aliendesha gari kwa kasi kubwa huku akiwa amezima kelele na taa za kuwaka waka za ambulance ile. Yule mtu aliyetufuata kwa pikipiki naye hakuwa nyuma alikimbiza kiasi kwamba akatupita na kuwa mbele yetu, nadhani alijua mpango mzima wa tukio lile. Nikiwa naendelea kujiuliza nini kinafuata baada ya kuchomoka uwanjani, na kulikumbuka tukio lile zima lililokuwa k**a picha ya video, nilishuhudia ghafla yule mwenye pikipiki mbele yetu alikatiza kuingia kibarabara kidogo pale njia panda iendayo mlima Rungwe. Ni njia iliyokuwa na kimsitu cha kiasi mwanzoni kabla ya msitu uliomnene mbele yake. Tuliposogea mbele kidogo, yule mtu alisimama na kutuonesha ishara ya kusimama. Bamdogo Kasim alisimamisha gari na kushuka haraka kisha kutuambia nasi tushuke haraka. Tukashuka na zile siraha na kila kitu chetu. Wakati huo mchungaji Enock alikuwa tayari ameshakuwa wa baridi, miongoni mwa wale madaktari hakukuwa na mtaalamu hata mmoja, wote walikuwa ni wataalamu bandia hivyo hakuna msaada wowote alioupata, mchungaji akaaga dunia.

Tuliposhuka, pembeni nikaiona gari nyingine aina ya BMW X7 nyeusi, ambayo nadhani ilitusubiri. Tuliposhuka tu ikawashwa, kulikuwa na mtu ndani ya gari hiyo tayari. Tukapanda kisha ikaondolewa kurudi barabara kuu. Ile ambulance tuliiacha pale pale kichakani na mchungaji akiwa amepumzika ndani yake, alipumzika milele. K**a kawaida yule jamaa aliyeendesha pikipiki yangu alitangulia mbele kwa mwendo wa kasi sana. Sisi tulienda mwendo wa kawaida sana, wala dereva yule hakukimbiza sana. Baada ya dakika chache yule jamaa wa pikipiki akapotea kabisa kutokana na mwendo wake kuwa mkali. Kwenye gari hii sasa tulikuwa k**a watu saba, dereva mpya, bamdogo Kasim, wale watu wanne waliojifanya madaktari na mimi. Tukiwa viti vya nyuma ya gari, Kasim alianza kunihoji maswali kwa ghadhabu sana, “kwani unamfahamu yule binti uliyekuwa unamsaidia pale uwanjani? si ungeua wote wawili? Nakuuliza unamfahamu?” aliuliza kwa hasira. “Sasa hapa nijibu ndio au hapana!, wamejuaje yote haya?” nikawaza. Hapo sasa nikatambua hata hawakuwa mbali na nini, walikuwa karibu sana na mimi wakati wa tukio zima bila mimi kujua. Nadhani waliambiwa na mzee kwamba waje kunipa ‘backup’ k**a nitaelemewa.

Nikiwa natafakari haya na bado sijajibu swali, gari mbili za polisi zilitupita kwa kasi. Kila mtu alitulia ghafla na kusubiri nini kinajiri. Muda wote huo sikuwa na maamuzi yoyote katika yaliyofanyika nilikaa kimya kuangalia mipango ilivyopangika. Nikadhani labda kwa sababu wameshatupita na wamepotea basi dereva angebadiri mwelekeo au hata kuficha gari mahali kwa muda. Cha ajabu hata hakuwa na wasi wasi, ndo kwanza akanyanyua mkono wake wa kushoto na kunyoosha kidole cha kati kwenye kioo cha mbele cha gari yetu huku akicheka kwa dharau. Muda wote alivaa ‘earphones’ na kuimba kwa sauti wimbo mmoja uliojirudia mara kwa mara. Ulikuwa ni wimbo wa kimarekani na nadhani aliupenda sana. “I don care.. eeeh eeeh, I don care.. eeeh eeeh, I don care.. eeeh eeeh, life’s fu***ng tough, Ago make’t easy…wana drive.. wana drive to the hell… tomorrow is not there.. use this moment en make it funny” Haya ni baadhi ya maneno ya wimbo ule alioonekana kuupenda sana. Alionekana mtu mwenye uzoefu mkubwa sana wa kukimbiza magari, na hakuwa na hofu.
Baada ya mwendo kidogo, Bamdogo Kasim alipigiwa simu na yule jamaa aliyetangulia na pikipiki. Alimwambia hali ya barabarani, mita k**a mia tano kutoka tulipo sisi kuna askari wa barabarani wanafanya msako. Yeye jamaa wa pikipiki alipapita hapo na aliona moja ya zile gari za polisi imepaki pembeni. Nilianza kuogopa maana yule askari aliyenikagua kwenye ambulance kule uwanjani aliiona vizuri sura yangu na sidhani k**a atakuwa amenisahau. Nikawaza k**a atakuwepo miongoni mwa askari waliobaki na ile gari basi nitaweza kuk**atwa. Kasim akamwambia dereva asimamishe gari, wala hakusikia aliendelea kuimba wimbo wake ule kwa sauti. Staili yake ya Maisha ilinishangaza sana, nadhani aliiga huko kwenye filamu za kimarekani. Mara ya pili Kasim akavuta earphones na kumwambia mbele kuna ukaguzi wa gari zinazopita. Yule jamaa akamgeukia kwa jazba kisha akacheka kwa dharau kiasi kwamba sikuelewa ni mtu wa namna gani. “unaua vibe babu” ndo sentensi yake fupi aliyojibu huku akiendelea kuendesha gari. Ghafla akafunga break, akageuka nyuma akawapa ishara wale madaktari, nao wakavua mavazi yao haraka na kuwa na muonekano wa tofauti kiasi. Nguo zao za kidaktari, vifaa pamoja na miwani zao kubwa vyote vikawekwa kwenye mfuko mmoja na kutupwa haraka sana mtaroni pembeni mwa barabara. Baada ya kuwa sawa, dereva alitoa bahasha nne kwenye kidroo cha dashboard ya gari na kumkabidhi kila mmoja cha kwake kisha wakashuka na kupanda dala dala tofauti kila mmoja.

Baada ya kuwashusha madaktari wale sasa tukabaki watatu, mimi, Kasim na dereva mwenyewe. Tukaendelea mbele na safari, mwendo kidogo mbele sikuelewa alichofanya dereva, alicheza na ile gari na ndani ya sekunde chache akasimamisha gari. Mara hii hakusimamisha kwa taratibu za kawaida za barabarani bali aliiweka katikati ya barabara imegeuka k**a inaingia mtaroni, ilifunga barabara yote. Muda huu hapakuwa na magari, Akashuka, akafungua buti la nyuma la gari na kutoa boksi la vifaa vya ufundi wa magari na ovaroli. Akafungua boneti pale mbele ya gari kisha akaingia chini kwenye uvungu wa gari, baada ya dakika chache niliona moshi ukitoka kwenye boneti. Sikujua hata alifanya nini, japo nilikuwa na uhakika kabisa ule moshi haukuwa wa tatizo. Niliwaza kuna mchezo anacheza ila upi? nia yake ni nini? Sikupata jibu. Bamdogo naye alionekana kupata wasiwasi kiasi na inawezekana ile haikuwa sehemu ya mpango wao.

Baada ya mda mfupi akatoka uvunguni na kufunga buti na boneti kisha akaingia kwenye gari akiwa na vibati vyenye usajili wa gari ile. Hapa sasa nikaanza kutambua kuwa huyu hakuwa dereva tu ila mharifu mwenye akili nyingi. Japo swali langu bado halikupata jibu kamili bado, mpango wake ni nini? Alipofika kwenye gari alifunga vioo vyote vya gari. Vilikuwa ni vioo ambavyo mtu wa nje hawezi kuona waliondani ya gari. Tulikaa kimya kwa dakika k**a tano hivi huku yeye akiendelea kuufuatisha wimbo wake ule na moshi mkubwa ukiendelea kufuka kutokea chini ya gari. Muda wote huu bamdogo aliangalia saa yake, ambapo mwishoni uvumilivu ukamshinda, akamshutua jamaa huku akiuliza unafanya nini?. Dereva hata hakujibu kitu bali akapozi wimbo wake ni kufanya shiiiiiiiiii!!! huku ameweka kidole kwenye mdomo wake k**a vile mtu anayesema tulia usipige kelele utanipeperushia ndege wangu. Tukatulia tena huku yeye akishusha kitu k**a kipazia cheusi pale mbele kwake, akaziba kioo cha mbele. Dakika chache baadaye alitengeneza msongamano mkubwa wa magari njia zote mbili hakuna gari kushuka wala kupanda. Watu wengi kwenye magari walishuka kuja kuangalia kilichotokea. Waliojaribu kuchungulia ndani hawakufanikiwa kuona kitu. Haikueleweka kimetokea nini, wengi wao niliwasikia wakijadili kila mtu akitoa maoni yake. Wakati wote huo sisi kwa ndani tunawaona. Baadhi ya waendesha magari walionekana kukasirishwa sana na hali ile ndipo dereva mmoja wa daladala aliponyenyua simu na kuwapigia askari barabarani wa kile kituo cha mbele kilichokuwa kinafanya ukaguzi. “Hallo afande….., freshi tu kaka….., ndio nimepita hapo sio mda ila hapa mbele kuna tatizo…….., hapa mbele karibu na kona kuna gari imetelekezwa katikati ya barabara njia haipitiki kwenda wala kurudi mzee….. poa poa njooni.” Alisikika dereva yule wa daladala akiongea na askari huku akijaribu kuchungulia ndani ya gari yetu. Sijui hata alisikiaje na spika zake ndogo alizokuwa amevaa masikioni mwake, dereva wetu alipiga tena wimbo wake aliokuwa ameupozi uendelee kuimba, akiwa anapandisha sauti ya kiredio chake kidogo cha mfukoni, akasema “Let the game begin mother f**kers”. Akimaanisha “ mchezo uanze ’ Alionekana ni kijana wa kitanzania mwenye mapenzi sana na umarekani, hasa kwa jinsi alivyojaza matusi ya kizungu kwenye kila sentesi iliyomtoka mdomoni mwake. Alicheka kwa dharau kisha kuiwasha gari na kupiga muungurumo mkubwa huku tairi zikizunguka kwa kasi na kutoa moshi uliongezeka kwenye ule aliousababisha chini ya gari. Hii hali ilifanya watu wote waliokuwa wameizunguka gari ile kusambaratika pembeni na kuipisha. Aliizungusha na kuiweka sawa kuelekea mbele kisha akaiondoa kwa kasi kubwa. Nilishangazwa sana na ujuzi wake wa kucheza na gia na usukani kwa pamoja ndani ya muda mfupi sana. Nilipogeuka nyuma niliona kidude kidogo mithiri ya kibaruti kikiwa chini kinatoa moshi, mpaka leo sijawahi kujua alikuwa amewasha nini kutoka kwenye lile boksi la vifaa. Watu walibaki midomo wazi na mikono kichwani kwa spidi aliyoondoka nayo. Muda huu gari ilitembea kwa kasi kubwa kiasi kwamba ilikuwa k**a inaelea matairi hayagusi barabara. Mbele kidogo baada ya kuimaliza foleni aliyoitengeneza tulipishana na gari zote mbili za polisi nazo zikiwa kasi kurudi kuja sehemu ya tukio. Sijui ni kwa nini hawakutuzingatia, pengine walidhani tumetokea karibu kwa hiyo ile foleni haikutuhusu. Ndani ya hizo gali walikuwa ni wale askari waliotupita mwanzo pamoja na wale wa barabarani. Hata hawakuwa makini na sisi maana sidhani k**a waliona kwamba gari yetu haikuwa na ile pleti ya usajili. Hapa sasa nilipata picha halisi ya plani yake hasa tulipopita kwenye kile kituo cha ukaguzi bila kukuta askari yeyote. Muda wote huu aliendelea kuimba wimbo wake huku akiichochea gari ile ambayo nadhani ilikuwa imefanyiwa maboresho kiufundi ili ikimbie zaidi ya kawaida bila kuchemka. Alipishana na magari mengine k**a vile apishanavyo na mtu anayetembea kwa miguu. Kutokana mwendo ule mkali, sijui k**a tulifuatiliwa tena na wale askari au lah! Maana muda mfupi tulifika karibu kabisa na Mbeya mjini ambapo kukwepa maaskari wa vituo vingine vya mjini aliingia kibarabara cha mtaani na kula kona nyingi mpaka tukaingia kwenye geti moja ambamo alipaki na mlango ukafungwa.

Tukashuka na kuingia ndani. Nilishangaa sana baada ya kuingia ndani ya jumba lile la kifahari. Nilimuona mzee wangu akiwa na kiongozi mmoja mkubwa wa siasa hapa nchini, waziri ninayemjua kupitia vyombo vya habari na mitandao. Niliendelea kujilundikia maswali kichwani yasiyo na majibu. Hapa mzee kafuata nini? Ina maana na huyu waziri naye anafanya biashara haramu? Kwa nini anafanya biashara ya madawa ya kulevya wakati yeye ndio alipaswa kupambana nayo? Ina maana naye anahusika kusafirisha nyara mbalimbali za serikali? Au ndiye huwa anayemsaidia baba yangu kusafirisha zile pembe za ndovu kwenda nje ya nchi na kuleta madawa? Ana njaa gani huyu waziri mpaka ajihusishe na biashara hizi haramu? Sikupata jibu la maswali yote haya. Nikiwa mkimya nisiyeongea lolote, baba aliniuliza, “Jamin nilikwambiaje kuhusu Jackline?, eeeh nawe ulijibu nini?” Kabla sijajibu kitu, baba mdogo Kasim akadakia.. “kijanaako amezama tena kwenye mapenzi hadi anaharibu kazi” huku akifungua friji lililokuwepo ndani hapo na kutoa pombe kali. “Mapenzi…. Mapenzi… mapenzii.. hahahahaha” aliongea Joseph Charles baba yangu ambaye pia ni bosi wangu huku akicheka kwa ghazabu kubwa. Alinisogelea kwenye sofa niliyokuwa nimekaa, “who is she?, eeeeeeh nilikutuma kumpenda Jackline au ukamuue?”. “hata sio Jack bro” alidakia Kasimu baba mdogo akiwa anajimiminia pombe ile kali k**a anakunywa maji. “ooooh a new girl!!! Bravo” akapiga makofi kunipongeza kwa hasira huku akinizunguka. Aliponizunguka kwa nyuma nilishtukizwa na kofi moja zito alilonipiga kisogoni, pwaaaah!!!! Kofi lile lilinishusha kutoka kwenye sofa mpaka chini ambapo nilifikia magoti. Nikiwa nimebaki nimepiga magoti bila kuongea kitu nimeinamisha kichwa chini, bosi alikuja mbele yangu akatoa bastola na kuniinua kichwa kwa siraha hiyo akiniangalia kwa hasira kali hasa aliposikia neno mapenzi limeharibu hazi aliyonipa. Hapa niliwaza naweza kuuawa kweli japo imani yangu iliniambia baba hawezi kuniua hata iweje. Japo upande mwingine niliogopa kwa jinsi alivyokasirika. Niliwaza siraha zangu sina hata moja mambo yakibadilika kabisa pale ndani. Tuliacha kila kitu kwenye ile gari pale nje. Nilipotupa macho kwa dereva yule ambaye sikumjua hata kwa jina tu, alikuwa anaendelea kuimba kwa sauti huku akiangalia runinga iliyokuwa ikionyesha mashindano ya mbio za magari. Alionekana kufurahia sana bila hata kujali kilichokuwa kikiendelea pale ndani. Yule waziri aliingia chumbani na kutoka na kibrifkesi kidogo kisha kumkabidhi dereva, ambaye aliondoka huku akiimba tu wimbo wake na kutikisa kichwa akionekana kuufurahia kweli kweli. Mzee akiwa ameniwekea bastola kwenye paji langu la uso, akaniuliza tena ni nani huyo mwanamke?? Sikujua cha kumwambia maana binti yule niliyempenda ghafla pale uwanjani hata simfahamu. Nikimjibu hivi mzee angeniona muongo na bado naleta mapenzi kwa kumlinda mtoto wa k**e kitu ambacho kwake ni sumu kwenye kazi. Ikanibidi tu nikae kimya. “Nakupa dakika moja ya kuchagua aidha mapenzi nikumalize mda huu au familia uishi, nakuuliza tena, ni nani huyo binti na nampataje??” Kwa hasira isiyopungua, bosi aliongea.
…………………………………………………………………..
ITAENDELEA…..…..
Ahsante kwa kusoma mpaka hapa, usikose sehemu ya nne ya simulizi hii nzuri…
Je nini atafanyiwa Jamin?, Jackline ni nani? Yule binti vipi?..
Kupata muendelezo wa stori hii au episode iliyopita kwa urahisi tufollow Instagram, Facebook, Twitter, Youtube.. zote jina ni .
Maoni/Ushauri: Whatsapp/Text/Call +255766511619

Uhali gani mwana simas stories? nikiwa naendelea kukuandalia Glorious mission. hebu mjue huyu dada kidogo..
14/01/2022

Uhali gani mwana simas stories? nikiwa naendelea kukuandalia Glorious mission. hebu mjue huyu dada kidogo..

Anaitwa Neerja, dada aliyetoa uhai wake kwa ajili ya kupambania wa wengine 350...katika ndege iliyotekwa huko Pakistani.."PAN AM FLIGHT 73". Bhanot ...

https://www.youtube.com/watch?v=397lDQO4ynQNadhani sasa mitambo imekaa sawa kwa wale wasiopendelea kusoma stories basi w...
07/11/2021

https://www.youtube.com/watch?v=397lDQO4ynQ
Nadhani sasa mitambo imekaa sawa kwa wale wasiopendelea kusoma stories basi wanaweza wakasikiliza huku wakiendelea na mambo mengine. AHSANTE sana kwa kusubscribe na kutufollow kwenye page zetu.🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

BAKI SALAMA NOREEN, ni hadithi fupi inayomhusu kijana PROSPER aliyekutana na rafiki wa k**e kipindi wanasoma shule ngazi ya sekondari. Urafiki wao ukakua na ...

THE GLORIOUS MISSION - 02ILIPOISHIA…………..Watu wakiwa wametawanyika hovyo, tulibaki watatu uso kwa uso, yaani mimi, Jack ...
23/06/2021

THE GLORIOUS MISSION - 02

ILIPOISHIA…………..
Watu wakiwa wametawanyika hovyo, tulibaki watatu uso kwa uso, yaani mimi, Jack na yule mrembo aliyetekwa na Jack. Jack alikuwa ‘siriasi’ sana, aliniangalia kwa hasira akiwa amemtanguliza mbele yule msichana huku yeye amesimama nyuma na bastola yake ikielekezwa kichwani kwa mateka. Yule dada machozi yalimtoka taratibu akiniangalia kwa huruma sana akisubiri msaada wangu. Niliamini roho ingeniuma sana endapo ningempoteza yule mrembo siku niliyompenda. Sikujali k**a angekuwa na mtu tayari wala angenikataa, furaha yangu ilikuwa kumuona anaishi. Nikaamua kujitoa, nikaweka roho yangu rehani kwa ajili ya moyo wangu uliopenda ghafla. Ile nanyanyua mguu kuwafuata walipo….

ENDELEA…….
Ile nanyanyua mguu kuwafuata walipo, Jackiline alimsukuma kwa nguvu yule msichana kuja kwangu. Kutokana na wasi wasi na kuishiwa nguvu yule dada akawa anapepesuka na anadondoka chini smzima mzima. Hapa tayari Jack alikuwa ameshafanikiwa kunishinda vita kwa kupigana na mimi kisaikolojia. Nadhani alishasoma tayari udhaifu wangu kwa muda mfupi sana tuliotazamana. Nadhani zile sekunde chache aligundua namuonea huruma sana yule dada. Kweli, nikashindwa kujizuia, nikapiga hatua tatu mbele haraka sana nikijaribu kumdaka yule dada asidondoke vibaya. Nilifanikiwa kumuweka mikononi mwangu, nikamdaka na kushuka naye chini. Nilikuwa nimefika chini kwa magoti yeye akiwa mikononi mwangu na sehemu ya mwili wake ukiwa umeegemea mwili wangu sehemu ya miguu. Yule dada akawa salama kiasi japo tayari nilikuwa nishajiweka kwenye hatari kubwa maana muda huu tayari Jack alikuwa ameshaniwekea silaha yake kwenye paji langu la uso. Pale akili yangu ilianza kuishiwa mbinu maana bastola yangu iliminywa kwa chini na yule dada aliye mikononi mwangu na tayari muda huo alikuwa ashapoteza fahamu amelegea hawezi hata kujisogeza. Nikaamini Jackline sio msichana wa kawaida. Alikuwa na kasi kubwa sana, akili nyingi na mwenye maamuzi ya haraka sana. Huku watu wakiendelea kukimbia huku na kule na kelele nyingi zikiendelea kusikika hasa akina mama ambao wengine walishiishia kuanguka anguka kila wakikimbia hatua mbili tatu. Wengine walionekana wakitapatapa wakitafuta watoto wao.

Baada ya kunibananisha, Jackline akaniangalia machoni kwa umakini mkubwa akitaka kujua ni nani alitaka kujaribu kuharibu misheni yake. Akakiangalia kiziba uso changu kutoka kulia mpaka kushoto kisha akatoa lile tabasamu la kicheko cha dharau na kusema “usijaribu kuwinda mnyama usiyeweza kumuua. Nani amekutuma uniue?” Hakuwa ni mtu mwenye maneno mengi. Sikujibu kitu nikabaki tu namwangalia usoni huku nikiwaza jinsi ya kujinasua kwenye mikono yake. Niliwaza kumlaza yule dada chini na kuweka silaha chini kisha kunyenyua mikono juu naye nimpoteze kimawazo maana nilikuwa na silaha nyingine mfukoni. Jack hakuwa mzembe hata kidogo, nilipotikisika tu akaikandamiza vizuri silaha yake kichwani mwangu kwa sekunde kadhaa kisha akaielekeza kwa yule dada mkononi mwangu. Jasho lilinitoka nikajihisi baridi mwili mzima. Niliikumbuka siku ya kwanza yule mzee wangu aliponifundisha kuua. Siku niliyoua walizi watatu wa super market nikiwa na umri mdogo huku mmoja akiniomba sana nimwachie maisha yake ana watoto na mke wanamtegemea. Nilimuonea huruma sana mlinzi yule kiasi kwamba nilishindwa kabisa kumuua. Ndipo baba yangu mdogo tuliyeenda naye aliponishikisha silaha hatari aina ya SMG kisha kukandamiza kidole changu kwenye kifyatua risasi na kumnyamazisha mtu yule. Roho iliniuma sana, nilikosa raha wiki nzima. Kadri siku zilivyoenda nileindelea kujazwa unyama ambao hata sikuzaliwa nao. Kasim ndo lilikuwa jina la baba mdogo, ndiye aliyenifundisha maisha yale. Sasa siku hiyo niliyobananishwa na Jack niliiona thamani ya maisha hasa pale unapohisi kuna watu wanakutegemea au kuna watu uwapendao na hutaki kuwaacha. Baada ya kukomaa na kuwa katili wa kutisha, sikuogopa tena kutoa uhai wa mtu wala kufa. Ila siku ile naikumbuka sana maana niliingiwa na hofu kuu juu ya kuiaga dunia. Kibaya zaidi mtu ambaye natakiwa kumlinda tayari yuko hatarini na muda wowote anaweza akasambaratishwa vibaya akiwa mikononi mwangu.

Jackline akarudisha silaha kwangu, na kujaribu kuichomeka kwenye kiziba uso nilichokuwa nimevaa kutokea juu ili aishushe shingoni anione uso. Ghafla vikasikika ving’ora vya gari za polisi kwa mbali zikija kwa kasi kulielekea lango la uwanja. Pasipokuwa na uwoga wowote, Jack akaniangalia mimi kisha akamwangalia yule dada kisha akasema “kwa mara yangu ya kwanza namuacha adui yangu aishi, unaonekana una mapenzi ya dhati na huyu mrembo, achana na hizi kazi huziwezi, nenda ukaishi maisha mazuri na huyu binti. Usipobadilika na ukiendelea kunifuatilia basi ipo siku nitakuja kwa ajili yako. Pia kamwambie aliye kutuma kwamba anashindana na mtu mkubwa sana kwenye hii nchi, kamwe hatashinda. Ukinifuatilia tena ntakumaliza wewe, huyo dada na familia zenu zote ndani ya masaa 24 pekee.” Muda huu Jackline alikuwa anarudi hatua moja moja nyuma taratibu. Nilimwangalia kwa umakini sana kuanzia miguuni mpaka usoni nimjue ni mtu wa namna gani. Nilipomchunguza vizuri nikagundua rangi yake ya shingoni haikufanana kabisa na ya usoni. Ina maana ile sura niliyoiona haikuwa sura yake halisi. Tayari gari za polisi zililikaribia sana lango la uwanja huo. Jack aligeuka haraka sana, akatembea hatua k**a kumi za haraka na kujichananya na watu wengine kisha akainama chini kidogo. Alipoinuka akawa mtu mwingine kabisa, hakuvaa koti tena na sura yake sijui aliifanyeje ikawa na utofauti mkubwa. Sikuona sababu ya kupoteza muda maana tayari Jack alishaniuzia kesi kule madhabahuni Pastor Enock alikuwa ameshadondoka. Nikavua kiziba uso haraka na kumlaza chini yule dada kisha nikainuka na kujichanganya na watu wengine. Katika kundi la watu waliokuwa waking’ang’ana kutoka, nikajichanganya nitoke. Nilipotuka macho getini, tayari askari wa jeshi la polisi walikuwa wanaingia baadhi kwa mguu huku wengine wakiwa juu ya mabomba ya gari tatu aina ya “DEFENDER’’. Nikiwa hatua k**a kumi hivi kulifikia lango nilimuona Jack kwa mbali akitoka akilia na kupiga mayowe k**a watu wengine. Mmoja wa polisi waliokuwa langoni wakisaidia watu kutoka nje alimshika mkono na kumtoa nje huku naye akijilegeza mithili ya mtu aliyekosa hewa. Wakati huo mimi nikawa nimefika karibu na alipokuwa ameinama. Nikaona koti lake chini na kitambaa kidogo cheupe kilichofutiwa make nzito iliyokuwa imeibadilisha sana sura ya Jack mwanzo. Nilijaribu kulikanyaga kanyaga lile koti kwa haraka huku nikitembea nikitegemea nitahisi uwepo wa silaha kwenye nguo hiyo lakini sikufanikiwa kuihisi. Kichwani nikajiuliza “Huyu dada amewezaje kupita na silaha pale getini pana askari na isitoshe mda ule kashikwa mkono na askari polisi. Nikaona jinsi anavyok**atwa kirahisi. Cha ajabu yule askari alishindwa kabisa kuzijua mbinu za Jack. Nilishuhudia uwezo mkubwa wa Jack kuigiza hata alipomtoa mpaka nje akamwacha sehemu yenye hewa safi kisha akakimbia tena langoni kusaidia wengine. Sikuamini nilichokiona ni k**a filamu nzuri ya kikorea ya kijasusi au simulizi nzuri iliyoandikwa kwenye kitabu. Kwa baba yangu, ni kosa kubwa kutambulika katika tukio k**a lile. Nilijitahidi sana kukwepesha sura yangu kwa maafisa wa jeshi la polisi na kila mtu niliyemuhisi anahusika na uchunguzi.

Ikiwa imefika zamu yangu kupita, akili ilihisi kuchoka kuona maaskari wanazidi kuongezeka na wametanda lango kwa umakini mkubwa wakiangalia watu wanaotoka. Wakati huu kwenye mwili wangu nilikuwa na silaha mbili ambazo mtu akinigusa tu kidogo anazigundua. Niliogopa sana, niliuona mwisho wa mabaya yangu au maisha yangu kabisa. Nikiwa nazidi kulisogelea lango, wale askari wakaanza kuwakagua watu wanaotoka. Na mda huu hapakuwa na msongamano mkubwa sana hivo kwa kundi la askari lililokuwepo ilikuwa rahisi kukagua k**a kuna yeyote ana silaha japo kwa haraka haraka. Nikaona tayari sina namna ya kutoka salama na siwezi hata kutupa silaha zangu maana nilishachelewa, pia nilikuwa siwezi kurudi nyuma kwa sababu watu wanazidi kuisha uwanjani na mlango mdogo wa upande wa pili ulikuwa na ulinzi mkali. Nikapiga moyo konde, nikaamua kujaribu kutoka kiume pale pale lango kuu na silaha zangu mwilini.

Basi nikaanza kupigia hatua kusogea. Zikiwa zimebaki hatua chache sana kuna askari mmoja akawa k**a amenishtukia. Akawa ananiangalia kwa makini sana, wala asitake nimponyoke kwenye macho yake. Pale sasa akili ikaniambia “Jamin, maisha yako sekunde chache zifuatazo yako mikononi mwako, kuwa hai au kusambaratishwa na hizo SMG walizoshika askari hawa. Ukishtukiwa salimu amri uwe hai, au chomoa silaha zako upambane kutunza siri za baba yako.’’ Nikakumbuka siku moja baba aliniambia “Jamin…. Jamin Joseph, piga ua, usije ukatoa siri za babaako, nisitiri mpaka unaingia kaburini mwanangu. Si unaona ninavyowasaidia watu?? Japo ni kweli mali zangu sio za halali lakini ona nasaidia watoto yatima na wale wa mitaani waliokosa kabisa mahitaji na matunzo ya wazazi wao. Jamin, popote unapokwenda jiamini k**a jina lako, usikubali kushindwa, pigana mpaka tone lako la mwisho la damu, kwapigania watu mbali mbali wenye shida kupitia taasisi zangu za misaada”. Kumbukumbu ile ikanipa imani ya kupambana ndipo nikawaza kutoa salaha zangu zote mbili nipambane.

Ghafla kabla sijatoa silaha nikasikia mlio wa gari ya kubeba wagonjwa maarufu k**a ‘ambulance’ ikija kwa kasi na kuingia pale langoni. Ikiwa inaingia, ilipita katikati yangu na yule askari aliyekuwa ananiangalia kila hatua kwa kunihisi ninahusika na shambulio lile. Nikaamua kuitumia nafasi hiyo kumkwepa askari huyo. Nikainama kidogo ili nimzunguke asinione tena. Ile nataka kuinama ile gari ikapunguza kasi na kushusha kioo upande wa dereva. Nikaiona sura ya baba Kasim ambaye ni mdogo wa bosi wangu, baba yangu mzee Joseph Charles. Nikagundua haraka sana kwamba Kasim amekuja kuninasua pale, hivo nikaamua kujiongeza. Kwa sababu gari ilikuwa na mwendo mdogo, nikajibamiza ubavuni mwa mlango upande huo wa dereva nikadondoka chini. Akasimamisha gari haraka, ile nikiwa najaribu kuinuka akafungua mlango kwa nguvu akanibamiza nao kwenye ubavu wa kichwa nikaanguka chini. Hapa nilielewa kuwa anataka niwe nimezimia. Nikajilegeza k**a mtu aliyepoteza fahamu. Ghafla walishuka watu wasiopungua wanne wakiwa wamevaa mavazi ya kitabibu. Wakanibeba haraka sana na kuniingiza ndani ya ambulance hiyo, kisha milango ikafungwa gari ikaendeshwa kwa kasi kubwa kuelekea upande wa uwanja ambapo jukwaa lilijengwa kwa ajili ya mkutano ule mkubwa wa injili. Wakati gari inaelekea kwenye jukwaa, Kasim akaniambia “Jami najua unanisikia hapo, toa haraka silaha zako, picha na simu muziweke chini kabisa ya hilo boksi la madawa na funguo za pikipiki uliyokuja nayo nipe haraka sana.” Ikafanyika hivyo. Gari ilipofika karibu na jukwaa ikasimamishwa haraka, kisha wale watu wanne wakashuka na kumbeba Pastor Enock na kuja naye kwenye gari. Askari wote walikuwa wametapakaa pale hawakuwa na shaka yoyote maana walijua ni kwa ajili ya huduma ya kwanza na kumuwahisha hospitali. Gari ikageuzwa haraka na tukaanza kutoka uwanjani hapo lakini tulipofika langoni yule askari aliyekuwa ananiangalia sana akasimamisha gari nikiwa namuona kabisa kwa mbali. Bahati nzuri gari ile ya kubeba wagonjwa ilikuwa haioneshi yanayoendelea ndani ya gari hiyo. Bamdogo akaniambia “Jami legea na ulale k**a huna fahamu haraka”. Nikafanya hivo, kwa kweli sikumuangusha, na wale madaktari wakajifanya wako busy sana kutoa huduma ya kwanza kwangu na Pastor Enock. Akaja yule askari akamuuliza bamdogo Kasim dirishani k**a anamfahamu kijana aliyembeba kwenye gari. Bamdogo akakataa hanifahamu, ila niwajibu wake kumbeba mtu yeyote anayedhani anahitaji msaada wa dharura na isitoshe yeye ndiye aliyesababisha ajali. Nikiwa hapo ninaendela kuigiza kupoteza fahamu nikawaza. Ina maana Kasim anataka kunikana? Kwa nini? Jibu likaja kwamba inawezeka amenikana ili kuleta uhalisia, kwamba ni ajali tu sio ndugu pia nadhani aliogopa kukubali maana pengine angekubali kunifahamu angeshtukiwa na yeye na timu yake yote aliyokuja nayo. Na k**a angeshtukiwa basi gari yote ingekaguliwa na silaha zingek**atwa na ndio ungekuwa mwisho wetu uraiani. Na ni kweli, yule askari polisi akasema “naomba niingie dakika moja tu!” Akaruhusiwa kuingia, akaomba anikague kujiridhisha kiusalama. Basi akanikagua na hakukuta silaha wala kitu chochote chenye kuleta mashaka. Kisha akaangalia angalia pale ndani na hakuona dalili yoyote ya kuwepo kwa silaha. Mwisho macho yake yakatua kwenye maboksi mawili, moja lilikuwa na madawa na lingine lilikuwa na vifaa vya huduma ya kwanza na matibabu ya dharura. Akawaambia wale madaktari wafunue boksi moja la mbele ya lingine. Wakafunua, akachungulia kisha akatulia k**a sekunde ishirini hivi, kisha akatikisa kichwa na kusema “samahani sana kwa kuingilia kazi yenu, nilikuwa tu nahakikisha usalama wenu. Samahni sana kwa usumbufu pia ahsanteni kwa ushirikiano wenu na mko salama hivyo wawaisheni hawa watu hospitali” “aaaah haina shida usijali” akajibu Bamdogo Kasim huku akiondoa gari haraka kutoka langoni pale na kuitafuta barabara kuu kwa kasi kubwa sana. Baada ya dakika k**a tatu hivi tulipishana na ambulance halisi ikienda eneo la tukio. Hapa sasa alianza kuendesha gari k**a mwehu huku pikipiki niliyokuja nayo ikitufuata nyuma. Nilihisi kabisa ni mtu wetu pia japo hata sikujua Kasimu alimpa funguo muda gani mtu huyo. Tukiwa tunakimbia kwa kasi ile, niliwaza sana, wamejuaje k**a nimetingwa? Ni nani huwa ananifuatilia kwenye misheni zangu wakinipa? Tunaenda wapi mda huu? Inakuwaje polisi wakijua gari yetu haikuwa ambulance feki? Bamdogo kaitoa wapi? Pastor Enock tunampeleka wapi? Je yuko upande wetu au ni adui yetu? Vipi yule dada niliyemuacha pale uwanjani hana fahamu yuko salama? Nitamuona vipi tena? Sikupata jibu hata moja, nikasubiri muda uamue.
……………………………………………………..
ITAENDELEA….
Ahsante sana kwa kusoma mpaka hapa. Endelea kufuatilia Episode inayofuata (ya 03) ndo kwanza kunakucha moto umeshika moto USIKOSE.
Kupata muendelezo wa stori hii au episode iliyopita kwa urahisi tufollow Instagram, Facebook, Twitter, Youtube.. zote ni .
Maoni/Ushauri: Whatsapp/Text/Call +255766511619

Address

Kinondoni
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 22:00
Tuesday 08:00 - 22:00
Wednesday 09:00 - 22:00
Thursday 09:00 - 22:00
Friday 08:00 - 22:00
Saturday 08:00 - 22:00
Sunday 08:00 - 22:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sima Stories posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share