Mjue Mtunzi

Mjue Mtunzi ?

KITABU KIPYA.Baada ya ukimya wa muda mrefu, mwandishi HASSAN MBONECHE anayo furaha kukutangazia ujio wa kitabu chake kip...
25/04/2026

KITABU KIPYA.

Baada ya ukimya wa muda mrefu, mwandishi HASSAN MBONECHE anayo furaha kukutangazia ujio wa kitabu chake kipya cha MSAMAHA WA RAIS.

Kitabu hiki kitakuwa madukani kuanzia tarehe 26/04/2026. Bei ni Tshs. 7,000/=

Kitapatikana katika maeneo yafuatayo;

DAR ES SALAAM

Kona ya riwaya, Kinondoni—0655428085

Kwa George, Posta—0755454152

MAKAMBAKO

APM Bookshop—0762282599

ARUSHA

Kwa Ally Said—0757690302

MOSHI—0673056571

Nje ya maeneo hayo unaweza kutumiwa popote ulipo.

Kuandika ni jambo moja, kujua kundika ni jambo mbali. K**a ilivyo kusoma na kujua maana ya kile ulichosoma.Lugha ni chom...
17/04/2026

Kuandika ni jambo moja, kujua kundika ni jambo mbali. K**a ilivyo kusoma na kujua maana ya kile ulichosoma.

Lugha ni chombo cha mawasiliano; tunawasiliana kwa kutumia ishara, sauti, maandishi kwa njia nyingi na mbinu mutawalia.

Bahati imenifanya kuwa mwandishi - mwandishi wa vitabu. Kwa ushairi na mjazo.

Bahati hiyo hiyo imenikutanisha na watu wenye kustahiki umufti katika uandishi; kwa fasaha na akili kubwa waliyonayo.

Watu weledi wanaojua kuchagua maneno wazungumzapo. Wanaojua kudhibiti hisia ukikabiliana nao. Watu walio tayari kujifunza hata herufi moja yenye manufaa kwao binafsi na tasnia ya uandishi wa vitabu katika ujumla wake.

Tasnia ya vitabu tangu zamani imekumbwa na nak**a za choyo, hasad na ulafi kutoka kwa wanaosimamia uchapaji na usambazaji.

Pengine tunaweza kuwaita wanaoshikilia nguzo ya uandishi wa vitabu.

Ukelele wa mabadiliko umekuwepo tangu enzi za kina Saadan Abdu Kandoro, Shafi Adam Shafi na waandishi wa zama hizi.

Hofu imepumbaza mapambano haya; yakakosa mnyororo wa mwendelezo kutoka kizazi kimoja kwenda cha pili.

Huibuka tu kundi likalalamika, likahanikiza mabadiliko kisha likafa kifo cha asili.

Ni k**a majilio ya radi yanyakuavyo usikivu wa mwanadamu kwa ghafula. Kisha kukapiga kimya.

Mimi na wenzangu tunataka kuukata mduara huu wa utesi na unyonge.

Tumeanza kwa kukutana kujadili chanzo cha matatizo yetu. Kwa sababu mwenye akili za desturi hutazama alipojikwaa si alipoangukia.

Kwa kutaniko letu la kwanza lililofanyika Dar es Salaam, Aprili 12, 2026. Tumejadili mengi.

Jumla ya tuliyojadili ni mamna gani tutazitumia akili, kalamu na sauti zetu kuukabili huu utesi.

Ni mtu mjinga tu ataacha kufanya hiki tunachokifanya kwa mustakabali wa fani nzima ya uandishi wa vitabu.

Hatutaki baada ya miaka 100 ijayo wajukuu zetu waone aibu kutaja majina yetu kwenye meza za majadiliano, kuwa babu zao tulipata kuwa waandishi wa vitabu; kwa sababu tu majina yetu yatakuwa katika orodha ya watu waoga.

*** Imeandikwa na Hafidh Kido

MSHINDI WA KWANZA wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu katika tamthilia, kwa mwaka 2026, ni mwanachama...
14/04/2026

MSHINDI WA KWANZA wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu katika tamthilia, kwa mwaka 2026, ni mwanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira (Uwaridi), Bw. Hamisi Kibari

Hii ni mara ya pili kwa Bw. Kibari kushinda tuzo hii. Mara ya kwanza (2023) alishinda nafasi ya kwanza katika riwaya. Hii inafanya jumla ya TUZO nne ( Laura Pettie 2024; Maundu Mwingizi 2025) kukusanywa na waandishi kutoka UWARIDI.

Hongera sana Hamis Kibari. Hongera Uwaridi.

Address

Masaki
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mjue Mtunzi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category