Secco Brand.

Secco Brand. Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Secco Brand., Adult Entertainment Club, Dar es Salaam.

  : Aliyekuwa mtangazaji mashuhuri na maarufu nchini kutoka kituo cha kurusha matangazo cha CLOUDS MEDIA, Gardner .G. Ha...
20/04/2024

: Aliyekuwa mtangazaji mashuhuri na maarufu nchini kutoka kituo cha kurusha matangazo cha CLOUDS MEDIA, Gardner .G. Habash (Captain) afariki dunia.

✴️ - Chanzo cha taarifa hiyo ya msiba uliotokea Leo April 20, 2024 kinasema ya kwamba mtangazaji huyo alikuwa alisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu (Pressure).

✴️ - Chanzo hicho kimeendelea kueleza ya kwamba marehemu Gardner alikuwa amelazwa katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo alikuwa akiendelea na matibabu mpaka umauti ulipomfika.

✴️ - Dhati ya pole iwaendee wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyigine. MUNGU ailaze pema peponi roho ya marehemu, AMINA!

  [✍️] :🔸 Sentensi hii fupi ambayo imeundwa kwa maneno manne tu, imebeba maana kubwa sana ndani yake k**a utachukua muda...
13/03/2024

[✍️] :

🔸 Sentensi hii fupi ambayo imeundwa kwa maneno manne tu, imebeba maana kubwa sana ndani yake k**a utachukua muda wako kidogo kuitafakari nami.

🔸 Leo pamezuka hali ya mshangao na tafrani hususani kwa mashabiki na wadau mbalimbali wa burudani ulimwenguni baada ya kuonekana kwa picha ambayo imewanasa 'Mafahari wawili ndani ya z**i moja!'

🔸 Picha hiyo ambayo imewanasa nguli wa muziki & imeshangaza wengi kwani wanaamini kuwepo na 'Bifu' kubwa baina yao, wakina ndani na nje ya muziki. Lakini picha hii imeshuhudia tofauti!

🔸 Hatimaye lile kombe la maji limetufikia mashabiki na sasa ni zamu yetu kkukata kiu iliyotutesa kwa muda mrefu. Hamu ya kuwaona nyota hawa wawili sasa imekidhi.

🔸 Chuki huondoa nuru na kuichosha nafsi, chuki hudhoofisha imani ya yule anayeibeba na kuitunza kifuani mwake. Chuki haiwezi mdhuru achukiwaye bali yule mwenye kuchukia. Kwanini ikutese?

🔸 Japo waswahili pia husema, "Moyo wa mtu ni kichaka!" kwa maana ya kwamba picha tu haitoshi kubeba tafsiri pana ya kwa mmemalizana tofauti zenu na kusameheana lakini tuna amini ni mwanzo mzuri.

[📸] Cc : ! 👍

🔸 Sentensi hii fupi ambayo imeundwa kwa maneno manne tu, imebeba maana kubwa sana ndani yake k**a utachukua muda wako ki...
13/03/2024

🔸 Sentensi hii fupi ambayo imeundwa kwa maneno manne tu, imebeba maana kubwa sana ndani yake k**a utachukua muda wako kidogo kuitafakari nami.

🔸 Leo pamezuka hali ya mshangao na tafrani hususani kwa mashabiki na wadau mbalimbali wa burudani ulimwenguni baada ya kuonekana kwa picha ambayo imewanasa 'Mafahari wawili ndani ya z**i moja!'

🔸 Picha hiyo ambayo imewanasa nguli wa muziki @... & @... imeshangaza wengi kwani wanaamini kuwepo na 'Bifu' kubwa baina yao, wakina ndani na nje ya muziki. Lakini picha hii imeshuhudia tofauti!

🔸 Hatimaye kile kikombe chenye maji kimewafikia mashabiki na sasa ni zamu yao kukata kiu iliyowatesa kwa muda mrefu. Hamu yao ya kuwaona nyota hawa wawili, @... na @... sasa imekidhi.

🔸 Chuki huondoa nuru na kuichosha nafsi, chuki hudhoofisha imani ya yule anayeibeba na kuitunza kifuani mwake. Chuki haiwezi mdhuru achukiwaye bali yule mwenye kuchukia. Kwanini ikutese?

🔸 Japo waswahili pia husema, "Moyo wa mtu ni kichaka!" kwa maana ya kwamba picha tu haitoshi kubeba tafsiri pana ya kuzika tofauti zenu bali tunaamini ni mwanzo mzuri.

Hakika ya kifo ni ahadi pekee ambayo ni lazima kwa kila mmoja itimie kwa wakati wake. Wapo ambao ahadi hiyo huwafika kat...
02/09/2023

Hakika ya kifo ni ahadi pekee ambayo ni lazima kwa kila mmoja itimie kwa wakati wake. Wapo ambao ahadi hiyo huwafika katika nyakati na umri tofauti-tofauti lakini ni lazima kwa kila mmoja kufikwa na ahadi hii.

🔸 Ahadi hii hutimia katika namna mbalimbali. Hutimia kupitia maradhi (ugonjwa), ajali au katika namna ya kiasili ya mtu kuondoka katika mgongo huu wa ardhi pindi wakati wake ufikapo.

🔸 Sote tupo katika foleni ya kuingia katika mlango mmoja. Haijalishi ni nani yupo mbele au nyuma yetu, kila mmoja atapita katika mlango huu pindi wakati wake sahihi unapowadia.

🔸 KIFO ni mawaidha makubwa tuyapatayo sisi tuliobaki hai. Ni ukumbusho ambao hutulazimu kurudi nyuma na kuyatathmini maisha yetu na neema hii ya uzima ambayo kwa mara kadhaa tumekuwa tukidhani ni haki yetu.

🔸 Kuishi ni bahati na kila mmoja atambue hilo. Pindi unapoondoka katika ulimwengu huu, tunapaswa kuamini kuwa umetimiza kusudi la MUNGU la kuwepo duniani hata k**a tumeumia ili kusudi tusije kukufuru.

🔸 Umeacha majonzi makubwa kwa wale wanaokufahamu kiundani (watu wako wa karibu), mashabiki pamoja na watu wote kwa ujumla wake lakini tunaamini kila litokealo ni sababu na funzo pia.

🔸 Pumzika kwa amani! Wewe umetangulia tu nasi tupo nyuma yako. MUNGU aendelee kuwatia nguvu na uwezo wa kuhimili na uvumilivu kwa wale waliosalia katika familia yako. Japo si rahisi lakini hili nalo litapita tu!

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Secco Brand. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share