Kimbia na pakua

Kimbia na pakua Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kimbia na pakua, Art, Dar es Salaam.

02/06/2026

FT: SENEGAL (U-17) 🇸🇳 1 - 1 🇹🇿 TANZANIA (U-17)

⚽️ Mihambo 07'
⚽️ Dione 64'


Dakika 30 zimeongezwa baada ya matokeo ya dakika 90 kutamatika kwa sare ya 1 - 1.FT: SENEGAL 🇸🇳 1 - 1 🇹🇿 SERENGETI BOYS ...
02/06/2026

Dakika 30 zimeongezwa baada ya matokeo ya dakika 90 kutamatika kwa sare ya 1 - 1.

FT: SENEGAL 🇸🇳 1 - 1 🇹🇿 SERENGETI BOYS


02/06/2026

Tazama timu ya Senegal U-17 ilivyotandikwa goli na Serengeti Boys kwenye mchezo wa fainali.


02/06/2026

Shangwe la mashabiki wa Serengeti Boys baada ya mpira kuibgia kambani dhidi ya Senegal.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Ummy Ally Mwalimu kuwa Mshauri wa Rais anayeshughu...
02/06/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Ummy Ally Mwalimu kuwa Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mama na Mtoto. Taarifa hiyo imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kupitia Mkurugenzi wake Shaaban Kissu, ikieleza kuwa uteuzi huo umeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe ya kutangazwa kwake.


Watu saba wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Senkenke, wil...
02/06/2026

Watu saba wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Senkenke, wilayani Iramba mkoani Singida, baada ya lori kupata hitilafu ya mfumo wa breki na kugonga nyuma basi dogo aina ya Coaster.

Ajali hiyo imetokea leo Juni 2, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi wakati lori hilo lililokuwa likishuka mlima Senkenke lilipogongana na Coaster lililokuwa likitoka Singida kuelekea Igunga mkoani Tabora, kabla ya magari yote mawili kutumbukia kwenye korongo kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam–Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amefika eneo la tukio na baadaye kuwatembelea majeruhi waliolazwa hospitalini na kutoa pole kwa familia zilizoathirika. Pia ameagiza uchunguzi wa kina wa chanzo cha ajali hiyo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Peter Luhega, amesema majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu huku baadhi yao wakiwa katika hali ya uangalizi maalumu kutokana na majeraha waliyopata.

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo na miili ya marehemu imehifadhiwa kwa ajili ya utambuzi na taratibu nyingine za mazishi.


02/06/2026

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo amefikishwa tena katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti, John Heche amesema chama hakikuwa na taarifa kuhusu kufikishwa kwake mahakamani, akieleza kuwa kesi iliyomfanya afikishwe mahakamani hapo, tayari ilikuwa imefutwa na mahakama.


02/06/2026

Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara ameitaka Serikali kuweka sheria kali kwa wabadhirifu wa fedha za umma ikiwemo kuwanyonga mpaka kufa ili kudumisha nidhamu.

Ametoa ushauri huo leo Bungeni, wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2026/2027.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 2, 2026 ameondoka nchini kuelekea Shirikisho ...
02/06/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 2, 2026 ameondoka nchini kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya kitaifa inayofanyika kwa mwaliko wa Rais wa Urusi,Vladimir Putin.

Rais Samia ameondoka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo ameagwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kabla ya kuanza safari hiyo muhimu ya kidiplomasia.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria na ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi katika nyanja mbalimbali za maendeleo, uchumi, biashara, uwekezaji na diplomasia.

Pichani ni matukio mbalimbali yakimuonesha Rais Samia akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka kuelekea Urusi kwa ziara hiyo ya kitaifa.


Mkurugenzi wa kampuni ya  Masoud Khalid amerejea salama kutoka katika ibada tukufu ya Hijjah na kupokelewa na Super Star...
02/06/2026

Mkurugenzi wa kampuni ya Masoud Khalid amerejea salama kutoka katika ibada tukufu ya Hijjah na kupokelewa na Super Star, Abdullah Issa.


Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kimbia na pakua posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category