15/01/2026
Nyota chipukizi wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania, Lamine Yamal, ameelezea wazi nafasi kubwa ya imani yake ya Kiislamu katika maisha yake, akisisitiza kuwa msikiti ndio chanzo chake kikuu cha utulivu wa kiakili na kiroho.
Yamal, ambaye ana umri wa miaka 18 pekee, amesema kuwa msikiti ni eneo lenye amani ya kipekee kwa mtu yeyote, bila kujali imani yake, lakini kwa upande wake k**a Mwislamu, amani hiyo huongezeka maradufu na kumpa nguvu ya kumudu changamoto za maisha na taaluma ya soka.
Kauli yake imepokelewa kwa mtazamo chanya katika sehemu mbalimbali za dunia, hasa ikizingatiwa umri wake mdogo na kiwango cha juu cha umaarufu alichokipata kwa muda mfupi tangu apandishwe kwenye kikosi cha Barcelona na timu ya taifa.
Yamal ameeleza kuwa katikati ya shinikizo la mashabiki, majukumu ya klabu, na matarajio makubwa aliyopewa, msikiti umekuwa kimbilio lake la kurejesha utulivu wa ndani na kujikumbusha thamani ya unyenyekevu.
Kwa kuzungumza hadharani kuhusu imani yake, Yamal anaungana na wanasoka wengine wakubwa duniani k**a Mohamed Salah na Sadio Mané, ambao wametumia majukwaa yao kuonyesha thamani za amani, heshima na utulivu kupitia dini.
Ujumbe huo, uliojaa hekima, unaweka msisitizo juu ya umuhimu wa maeneo ya ibada katika kujenga afya ya akili, maadili na nidhamu—hasa kwa wanamichezo wanaokabiliwa na presha kubwa.
Yamal, ambaye mara nyingi ametajwa k**a mmoja wa wachezaji waliopo kwenye mstari wa kurithi enzi za wakubwa wa soka duniani, anaendelea kuonyesha kwamba mafanikio makubwa yanahitaji si tu kipaji bali pia misingi imara ya kiroho na kitabia.
Gusa mshua follow me