Saination

Saination Official page of Saination (TZ) Bongo Flavour musician, Novels and Songs writer..

HATIMAE INAANZA KUWA HEWANI.KAA MKAO WA KURA_______________________________________________SIMULIZI MPYA..._____________...
25/12/2025

HATIMAE INAANZA KUWA HEWANI.
KAA MKAO WA KURA
_______________________________________________
SIMULIZI MPYA...
_______________________________________________
MTUNZI: Saination
CONTACT: +255715175518

Simulizi hii inahusisha Kijiji Cha USSIINGIE Kijiji ambacho watu wake wanaishi kwa Imani ya mizimu yao.. Imani hiyo wali rithishwa kutoka kwa mababu zao..

Ishu ni kwamba.. k**a Kuna ukame wa mvua waliamini suluhisho ni kuomba mizimu kwa kutoa kafara ili mvua ije.. vile vile matAtizo yote k**a ya wanyama wakali, magonjwa, radi za madhara, jua Kali n.k waliamini mizimu yao kutatua matAtizo hayo.

BALAA SASA
inatokea mabadiliko ya hali ya hewa na kupeleka mvua kuwa kubwa sana zenye radi nyingi ambazo zilileta madhaera ya vifo.. ni mvua zilizo fululiza kunyesha zikiwa Zina radi nyingi na kuuwa wanakijiji..

Hali ilipekelekea wanakijiji kupata hofu baada ya kiona wenzao wanazidi kufa kwa mafuriko na radi..

Jopu la wazee wakijiji wanaamua kutafuta suluhisho kupitia midhimu Yao.. inakuja kubainika Kuna familia yenye vijana wawili mapacha walio fanana ilihamia pale na hao ndo chanzo Cha maafa Yao... Kwani wao waliamini wakizaliwa mapacha kwenye Kijiji Chao tena mapacha wa kufunana ( IDENTICAL TWINS) ilikuwa ni laana kubwa sana.

Wazee wakiongonzwa na Mzee Kalubandika.. wanaamuru pacha mmoja auwawe.. na hapo ndo matAtizo yanaanza .

Unajua ni nini... KIVULI KIVULI KIVULI... Kijiji kilikumbwa na mauwaji ya kutisha kisa KIVULI... NI KIVULI CHA NANI..
APA UTAMKUTA
Senior Sai (pacha mkubwa)
Sai Junior (pacha mdogo)
KALUBANDIKA (Adui mkuu)

Wote ndani ya KIVULI..
________________________________________________
MAPEMA INAKUJA MPAKA MWISHO...

NIILETEEEEEEE Au?

_______________________________________________SIMULIZI MPYA..._______________________________________________MTUNZI: Sa...
05/01/2025

_______________________________________________
SIMULIZI MPYA...
_______________________________________________
MTUNZI: Saination
CONTACT: +255715175518

Simulizi hii inahusisha Kijiji Cha USSIINGIE Kijiji ambacho watu wake wanaishi kwa Imani ya mizimu yao.. Imani hiyo wali rithishwa kutoka kwa mababu zao..

Ishu ni kwamba.. k**a Kuna ukame wa mvua waliamini suluhisho ni kuomba mizimu kwa kutoa kafara ili mvua ije.. vile vile matAtizo yote k**a ya wanyama wakali, magonjwa, radi za madhara, jua Kali n.k waliamini mizimu yao kutatua matAtizo hayo.

BALAA SASA
inatokea mabadiliko ya hali ya hewa na kupeleka mvua kuwa kubwa sana zenye radi nyingi ambazo zilileta madhaera ya vifo.. ni mvua zilizo fululiza kunyesha zikiwa Zina radi nyingi na kuuwa wanakijiji..

Hali ilipekelekea wanakijiji kupata hofu baada ya kiona wenzao wanazidi kufa kwa mafuriko na radi..

Jopu la wazee wakijiji wanaamua kutafuta suluhisho kupitia midhimu Yao.. inakuja kubainika Kuna familia yenye vijana wawili mapacha walio fanana ilihamia pale na hao ndo chanzo Cha maafa Yao... Kwani wao waliamini wakizaliwa mapacha kwenye Kijiji Chao tena mapacha wa kufunana ( IDENTICAL TWINS) ilikuwa ni laana kubwa sana.

Wazee wakiongonzwa na Mzee Kalubandika.. wanaamuru pacha mmoja auwawe.. na hapo ndo matAtizo yanaanza .

Unajua ni nini... KIVULI KIVULI KIVULI... Kijiji kilikumbwa na mauwaji ya kutisha kisa KIVULI... NI KIVULI CHA NANI..
APA UTAMKUTA
Senior Sai (pacha mkubwa)
Sai Junior (pacha mdogo)
KALUBANDIKA (Adui mkuu)

Wote ndani ya KIVULI..
________________________________________________
MAPEMA INAKUJA MPAKA MWISHO...

NIILETEEEEEEE Au?

MTUNZI: Saination Simulizi: Target.ComEpisode: 02.Whatsapp: +255715175518TikTok: SainationTzInstagram: Saination TzFaceb...
27/01/2024

MTUNZI: Saination
Simulizi: Target.Com
Episode: 02.
Whatsapp: +255715175518
TikTok: SainationTz
Instagram: Saination Tz
Facebook: Senior Sai
YouTube: SainationTz
_______________________________________________________

TARGET.COM

KIGONGO KIPYA KINAANZA K**A HIVI...
_______________________________________________________

"Target, Target, Target, Target............."

"Huyo ndo Muuwaji..
Kill him"

Sauti za afande John na the killer zilizlsikika kwa wakati tofauti...

Bunduki zilikokiwa na zote zikamuelekea the Killer...

Hofu ilitanda maeneo Yale na kupelekea raia wote kulala chini huku wakijua kinacho fuata ni mijegeje..

Cha ajabu the Killer alikuwa kasimama.. huku akishikilia ngao yake ikiwa imechongoka mfano wa ndoano.. huku ikiwa na ncha Kali Kali zenye maandishi ya (.com) yaani DotCom.

"Weka silaha yako chini na nyenyua mikono juu"

Sauti ya Afande John iliamuru hivyo..

"Ha ha ha ha ha haaaaaaa"

The killer alicheka na tayari alikuwa kabadilika... Macho mekundu na mwili wenye milale k**a mwanga wa radi..

TARATIBU

the killer alianza kumsogelea Afande John..

" KILL HIM NOW"
Amri ilitoka kwa mara ya pili...

"PA PA PA PAAAAAAAAAAAAA PAAAAAAA"

MILIO YA RISASI ILISIKIKA...

RISAS zaidi ya 100 zilimlenga sehemu mbali mbali ya mwili wa the killer..

Lakini Cha ajabu the killer alikuwa akipepesuka tu na ajabu zaidi risasi zile ziliyeyuka kwenye mwili wake pasipo kumdhuru...

Shati lake lilikuwa limeungua Vibaya kwa moto wa risasi..

The killer alivua shati... Na kubaki kifua wazi...
Askari wakatahamaki
Raia wakashangaaa

Maneno mbali mbali yalisomeka kwenye mwili wa
The killer... Sehemu ambazo risasi zilipiga na kuyeyuka... Ziliacha maneo haya

".comcomcom comcomcom.................."

The killer alitulia akiwa kasimama na wakati huyo askari walikuwa wameishiwa risasi..

Dakika k**a kumi zikawa zimepita... Na hatimae maneno Yale yalifutika mwilini mwake... Inaonekna mwili ulikuwa umepoa kwa moto wa bunduki..

"Hamuwezi kuniuwa kwa namna yoyote...Mimi sio mtu wa kawaida... Nimepewa order ya kuuwa ... Sasa nauwa muhusika tuu...'"

"Vuuuuuuuuuuuuuup"

Nanga ya minyororo ilirushwa na kumtoboa afande John... K**a samaki kwenye ndoano.. Afande John alivutwa mpk mikononi mwa the Killer...

Afande wote sehemu Ile waliamza kutetemeka wakijua na zamu Yao inakuja...

Mbele ya macho ya watu wote... Afande John alitobelewa kifua.. kwa kifaa kile na the killer akachukua kisu chake na kumchana Kisha kumtoa FIGO zote kitaalamu k**a Daktari...

Hatiame Afande John hatuko nae tena... Na FIGO zake zimetolewa mbele ya watu wote.. tena live bila CHENGA..

Baada ya hapo kutoka ndani akatokea mtu akiwa kavaa mavazi meupo k**a madaktari wa upasuaji... Tena kafunika mwil mzima.. akiwa kashika dell la kisasa lenye barafu ndani emo...

The Kila alipokea deli lile na kuweka pia Figo zile... Zikiwa Figo za watu wawili..

"Hellow Boss.
Mission completed"
The killer aliongea kwenye simu...

Dakika Tano mbele tayari ndege aina ya helkopta ilikuwa imetuwa pale...

The killer na mwenzake waliingia kwenye ndege wakatokomea usawa wa bahari ya Hindi...

Ukimwa ukatanda kidogo... Na sauti za huzuni zikaanza kusikika...

Watu walilia.. kulia maisha ya marehemu.. kushuhudia MAUWAJI ya kikatili.... Na muda huo gari la wagonjwa lilikuwa limefika... Na kuchukua miili Ile kuipeleka monchwari

Waandishi wa habari k**a kawaida Yao walikuwa wakifanya Yao...

________________

SIKU IKAKATIKA NI SIKU NYINGINE TENA...

"Wasi wasi watanda dar..

MAUWAJI ya kutosha yafanyika mbele ya askari.

Wauwawa na kutolewa FIGO.

INVISIBLE MAN AFANYA YAKE..

Mjua mtu aliye kataa kufa.. na KUFANYA MAUWAJI"

Zilikuwa ni headlines siku ile..

Kiukwel nchini sasa wasiwasi ulikuwa mkubwa sana... Na hali Ile ikafanya mkuu wa mkoa pamoja na waziri wa mambo ya ndani na jop la ulinzi wa usalama wote kuitisha kikao Cha Siri .

KIKAONI SASA.
AGENDA IKIWA NI
Kumk**ata muuwaji na genge lake.
Kujua sababu ya kwanini anatoa Figo.. na k**a ni biashara.. inafanyika wapi...
Kujua ni watu waina gani hao ambao risasi hazifanyi kazi kweny mwili wao
Na mengine mengi...

KIKAO KINAANZA..

Mara simu ikaita kwa mkuu wa mkoa..
Kwa kuwa alikuwa bize na mkutano hakuweza kuiipokea...

Iliita na kuiita na kuiita...

" Muheshiwa unaweza kuweka simu Silence"
Mkuu wa mkoa aliombwa na k**anda mkuu wa polisi mkoa..

Akachukua simu ili aiweke Silence mode.. mara akakuta meseji imeingia na imeandikwa

"TARGET"

Ik**aanisha mkuu wa mkoa yupo kwenye Target ya kuuliwa.
Jasho lilimtoka...

Watu wote wakatahamaki baada ya kujua kilicho tokea...
______________________________________________________

"Hawa watu ni wakina nani kwanini wanajiamni..
Na technology ipi wanatumia kupambana na silaha zetu"

Waziri alizungumza...

"Ndriii ndriii ndriiii..."
Simu ikaita tena kwa mkuu wa mkoa...namba Ile Ile mpya...

Pale pale mtu wa INFORMATION TECHNOLOGY..
I.T SPECIALIST akachukua laptop yake ili ahack namba Ile wajue watu hao wapo wapi....

"Haya pokea Mkuu tayari nimeiwekwa namba kwenye system.."

Mkuu wa mkoa akapokea simu..

"Wewe ndio TARGET INAYO FATA.... Tumepewa order ya kuchukua Figo zako.."

Wakati huo tayari I.T specialist alikuwa kainasa location ya Ile namba..

"HALLOW HALLOW "
Simu ilikuwa imekatwa...

"Anahaa tuambie hiyo namba imepigwa wapi"

"Huyu mtu tayari kaisha fika kwenye jengo hilihili...huyu mtu yupo humu tayari..."

Macho yaliwatoka wote na wasiwasi wa uwoga ukawak**ata..
____________________________________________________________

KAZI IMENOGA SASA...

Saination Tz..

0715175518

Simulizi: Target.ComSehemu: 01.Mtunzi: Saination Whatsapp: +255715175518________________________________________________...
26/01/2024

Simulizi: Target.Com
Sehemu: 01.
Mtunzi: Saination
Whatsapp: +255715175518
_______________________________________________________
WAHUSIKA WAKUU.
Sterling---: Saination

Adui Mkuu---- Senior Sai.
________________________________________________________

SONGA NAYO SEHEMU YA KWANZA SASA.

Ni saa 8 mchana katika Jiji la Dar Es Salaam kwenye Soko kuu la Kariakoo... Kila mtu Yuko bize na shughuli yake. Hali ya hewa ikiwa ni jua Kali.. wafanya biashara wapo bize kunadi biashara zao.

Wahuni wako bize kupiga ndole... Huku Matapeli wako bize kumpata mshamba wa kumuingiza mjini.

Watu wakiwa wengi mahali hapa.. zilisikika ni honi za magari..

"Pipiiiii piiii pipiiiii piiiiii"

Huku kukiwa na watu wengi wakipishana kwenye kila mtaa... Sio mtaa wa msimbazi, au uhuru, congo, nyamwezi, aggrey kifupi.. kila sehemu kulikuwa na watu wengi..

GHAFLA Katika jengo Moja mahali hapa.. kunaonekana mtu akidondoka kutoka juu katika gorofa ya nne mtaa wa Msimbazi..

"Jamani Kuna mtu kajirusha kutoka juu "

Zilisikika sauti za watu zikiongea kwa kutahamaki...

"Vuuuuuuuuuuuuuup" kwa spidi ya yaharaka mtu huyo alikuwa akikaribia chini

"'PUPUUUH"

Masikini ya mungu alidondoka k**a gunia chini.

"MUNGU WANGU" Kila mtu alitahamaki..

Na haukupita muda mtu yule akawa kazungurukwa na watu huku akiwa kifudi fudi tena kifua wazi.. tayari alikuwa kakata roho yaani kafariki....

Kila mtu alikuwa ana hamu ya kutaka kujua sura ya huyo marehemu.. kwani alikuwa kalala kifudi fudi.

Polisi kutoka kituo Cha Msimbazi tayari walikuwa wamefika... Na hapo hapo wakatoa tahadhari watu wasimame kwa mbali kidogo...

Polisi Mmoja aliisogelea maiti na kuigeuza Ili marehemu aweze kutambuliwa mahali pale... Huku gari la mgonjwa likiwa linakuja kutoka hospitali ya rufaa Amani...

"NINI HIKI?"
Askari aliuliza kwa kutahamaki baada ya kugeuza Ile maiti...

Maiti ilikuwa imepasuliwa kifuani na kutolewa FIGO zote huku ikiwa imetapakaa damu nyingi...

Pale pale hali ya hatari ikatolewa... Huku sasa kila mtu akifahamu mtu yule kauliwa kikatiri na kutolewa FIGO muda si mrefu...

"Hallow naamuru jengo namba 28 katika mtaa wa Msimbazi lizungurukwe na asitoke wala kuingia mtu."

Askari Chidi alipiga simu kutoka kituo hicho Cha Msimbazi na tayar askari wote wakawa wamefika mahali husika.. na jengo likawa limezungurukwa na askari.

" TUNAAMURU WATU WOTE MLIO NDANI JUU NA CHINI MJIKUSANYE KWENYE SEHEMU YA PARKING KATIKA JENGO HILI.. TUTAWARUHUSU KUONDOKA BAADA YA KUFANYA UKAGUZI KWENYE CCTV CAMERA "

Askari waliamuru.. na watu wote kutoka kweny jengo Hilo wakawa wemesimama kwenye parking huku wakiwa chini ya ulinzi..

Upande wa pili askari Chidi akiendelea kuichunguza Ile maiti .. alizidi kushangaa baada ya kukuta maiti ikiwa imepigwa chata ya muhuli kwenye shingi iliyosomeka... DotCom yaani (.Com)

Pale pale akatambua ni alama iliyo wekwa na muuwaji kwenye maiti hiyo...

Ila the killer akiwa Bado hajajulikana..

Ndani ya control room ya CCTV CAMERA... Askari John Yuko bize kukagua kila camera kupitia kweny tv husika huku akihitaji kujua muuwaji ni nani...

LIVE BILA CHENGA ALIONA TUKIO LOTE LA MAUWAJI YA YULE MTU.. pale pale akaprint picha za yule muuwaji .. Kisha na kuchukua simu kumpgia afande Chidi na wenzake walio kuwa chini ..

"Hallow afande Chidi.. nmepata picha ya muuwaji nashuka chini sasa hivi kuja kuangalia k**a katika watu hao huyo muuwaji yupo"

" Sawa Afande fanya hima"

Chidi alimjibu John

MARA
John alipokata simu... Akaaingia kwenye Rifti na kuanza kushuka chini... Akiwa ana shushwa na Rifti... GHAFLA simu yake iliita... Akaangalia nani anapiga.

Ni namba mpya, akapokea mara..

"Na wewe ni Target unapaswa kufa muda huu, wewe ni Target wa sasa lazima ufe sasa "

"NINI"
Afande John aliuliza.. lakini simu ilikuwa imektwa..

"Hallow hallow'" KIMYA.

GHAFLA

"NDRIIIII" Mlio wa meseji ulisikika... Ile anafungua ndipo akazidi kuchanganyikiwa

"TARGET"

Alisoma meseji hiyo kupitia namba Ile mpya.. hofu ili mshika.. Ila akajipa moyo kwakuwa sehemu Ile Kuna ulinzi mkali...

Muda huo huo alifika sehem ya PARKING huku watu wakiwa chini ya ulinzi..

LIVE BILA CHENGA Alimuona yule muuwaji akiwa miongoni mwa watu walio kuwa chini ya ulinzi.. hakuamini... Huku akiwa kashika picha ya muuwaji yule aliiangalia picha Ile ili ajipe uhakka..

Kisha wakagongana macho na yule muuwaji ... Huku sehemu Ile kukiwa na askari wengi pamoja na raia...

MARA

"Target, target , target Targertiiiiiiiiii"

Muuwaji alisema kwa sauti kubwa kumuambia afande John... Askari wote wakawa wamegeuza bunduki zao kumlenga huyo muuwaji...

Muuwaji huku hatujui anaitwa nani... Alichomoa siraha yake yenye umbo la nanga ya meli... Huku pembeni mwa silaha hiyo kukiwa kumeandikwa .com

Afande John alipiga kelele kuwaamuru askari wenzake...

""Huyo ndo muuwaji shoot him"
Bunduki zilikokiwa kwa pamoja.

Upande wa pili nacho ya muuwaji yakabadilika na kuwa mekundu.. .

_____________________________________________________________

KIPI KITATOKEA HAPO.. USIKOSE SEHEMU YA PILI

Simulizi: Target.comMtunzi: Saination Tz.Whatsapp: +255715175518_______________________________________________________S...
26/01/2024

Simulizi: Target.com
Mtunzi: Saination Tz.
Whatsapp: +255715175518
_______________________________________________________
SIMULIZI NI MPYA.
humu Kuna stori Kali ambayo huwez kuikuta sehemu yoyote... Plus maauwaji ya kutosha.
Hiyo imeenda .

TUKUTANE LEO JIONI.

KWA KILA EPISODE.
_________________________________________________________

Habari njema kwa wafatiliaji wa stori za Saination Tz... Natangaza rasmi kuanzia sasa naanza kuachia stori Moja baada Mo...
19/01/2024

Habari njema kwa wafatiliaji wa stori za Saination Tz... Natangaza rasmi kuanzia sasa naanza kuachia stori Moja baada Moja..

Tunaishi nayo Moja Moja Mpaka mwisho..
Kumbuka zipo nyingi tu k**a..

VAMPIRE
PATRIOT
ZAMU YAKO
MAHAK**A YA WACHAWI
KAFARA
ASIYEJULIKANA
LET IT SHINE
Na nyingine nyingi...

Taanza na hii Vampire.

Karibuni kwenye ulimwengu wa burudani...

Simulizi: KAFARA.Sehemu: 03.Mtunzi: Saination WHATSAPP: 0715175518________________________________WAHUSIKA WAKUU..     J...
27/09/2023

Simulizi: KAFARA.
Sehemu: 03.
Mtunzi: Saination
WHATSAPP: 0715175518
________________________________
WAHUSIKA WAKUU..
Joshua Roman.
Mzee Nduli.
________________________________

"HIVI ILE NDOTO INAWEZA KUWA NA MAANA KWELI"

Joshua aliwaza.

Mama akiwa na hofu sasa alimuangalia mtoto wake Joshua Kisha akaanza kulia.

"Mama usilie Bali huna budi kinieleza kwanini umetahamaki baada ya Mimi kupata kazi"

Joshua alimuambia mama ake ..

Taratibu mama, Joshua na Magogwa waliongozana mpk sebuleni Kisha wakaketi.. ndipo mama akaanza kufungua kinywa kuanza kuzungumza.

"Wanangu Joshua na Magogwa nawapenda sana"
"Siko tayari kuwapoteza... Ila kiukweli baba na babu yenu walikufa katika mazingira ya kutatanisha."

"Kule alipo pangiwa Joshua panaitwa KALANGABO..."

NDIPO MAMA AKAANZA KUWAPA STORI YA MAISHA YAKE HUKO KIGOMA.

"KALALANGABO ipo Mkoani KIGOMA... Ni sehemu iliyo anzishwa na Babu yenu mzee Ngabo, kabla Babu yenu hajafa palikuwa pakiitwa kambini... Sehemu ya uvuvi wa dagaa na samaki Aina ya mgebuka.."

"Hivyo upatikanaji wa urahisi wa samaki ulipelekea kuwavutia watu wengi kambini hapo... Na ndipo makazi ya watu yakaanza.."

" Kipindi hicho kila kitu kilikuwa nyuma kwani ilikuwa zamani sana... Wanakijiji kambini hapo WALIAMINI ILI MTU AIISHI MAISHA MAREFU LAZIMA AJIEPUSHE NA VITU VYA KEMIKALI..., kwani watu hao waliamini watu wa Karne za nyuma waliishi mpk miaka 200 na kuendelea kwa sababu kipindi kile hakukuwa na vitu vya kemikali...'"

""Mpaka sasa Hivi watu wa KALALANGABO huwa hawatumii sukari, chumvi, Mafuta ya kupika au kupaka, madawa ya kutibu ya kizungu... Yaani wanakula bado nyama za kushoma au mbichi, na nafaka zisizo changanywa na kiungo chochote...""

"""Mtu akiugua wanatumia madawa ya asili, haijalishi k**a ni maralia au magonjwa mengine sugu"

"Wanakijiji wote wanaamini mtoto akisoma ni sababu ya yeye kuwapelekea maisha ya kileo kijijini kwao... Hivyo watoto wote wa KALALANGABO hawapelekwi mashuleni.."

"Sababu hiyo ilimfanya Baba YAKO awakosee kwani alilazimisha kukusomesha ww nje ya kijiji Cha KALANGABO, maeneo ya Mwandiga"

"Walimkataza lakini akakaidi agizo lao na kulazimisha kuendelea kukusomesha .. ndipo wazee wakijiji waliongozwa na Mzee Nduli wakapanga kumpa Adhabu baba yenu Roman ya kumtoa KAFARA Babu yenu NGABO... Lakini baba yenu akakataa... Pale pale wakatumia nguvu zao za giza na kuwawua Baba na babu yenu... Kisha wakawazika.... Sehemu ya KAFARA... Baada ya kuona hivyo ndipo nilipo amua kukimbia kijijini kule na nyie ILI kuponesha maisha yenu"

Mama aliendelea.

"Sasa mwanangu Joshua umepangiwa kazi ya udaktari kule na wanapinga maswala k**a hayo unajua ni kipi kitafata k**a sio kukuuwa"

"Tafadhari mwanangu usiende kule"

Mama alihitimisha Huku akiwa akimshika mwanae mkubwa
"Nakupenda sana mwanangu tafadhari nickilize"

JOSHUA aliwaza... Kutokana na elimu yake hakuwahi kuamini k**a kuna uchawi kweli...

Kwani kwa taaluma yake anaamini kitu chochote ambacho hakionekani kwa ushahidi wote ule hicho kitu hakipo duniani au sehemu yoyote...

"HIVI kweli kuna uchawi?""
Joshua aliwaza

Na ndipo akapata jibu la kumlidhisha mama ake.

"Mama Serikali huwa wana ajiri mara moja tuu... Nisipo lipoti kazini basi Sito ajiliwa tena serikalini"

"Okay nimepata wazo naomba niende nikalipoti kazini kwani kituo nacho enda ni kipya hakuna muhudumu yoyote... Baada ya miezi kadhaaa taomba ruhusha ya kuhamishwa HUKO ili tuwe salama"

"Nikifika kule tajaribu kuishi namna wanavyotaka wanakiji mpk takapohamishwa"""

Joshua Alihitimisha na mama akakubali kwa shingo upande na maandalizi ya safari yakaanza....

Hatimae siku zikakatika na siku ya Safari ya kwenda Kigoma ikawadia. Joshua akiwa tayari kakata tiketi ya gari Moshi...taratibu jioni hiyo alifika kwenye kituo Cha Treni mjin hapa Tabora.

Magari ya mpanda, Kigoma na Mwanza yakiwa kwenye njia zake usiku huo yalianza kuondoka kwa ZAMU ZAMU.

Hatimae gari la kwenda Kigoma likafika ZAMU yake ya kuondoka kwani lilikuwa la MWISHO kutoka kwenye stesheni ya Tabora.

Joshua akiwa na shauku alikuwa akiuliza kila kituo ambacho Treni ilisimama...

Hatimae ikapita......

Ilalangulu.. Mabama... Ussoke... Urambo... Kaliua. Kombe... Ussinge....

Ikiwa Ussinge ndo kijiji Cha mwisho Cha Tabora uelekeo wa Magharibi... Sasa treni ilianza kuingia vijiji vya KIGOMA...

Nguruka.... Maragarasi... Luguvu... Uvinza... Kazurimimba... Kandaga... Kalenge...Luiche..

Ikiwa sasa ni asubuhi.. Treni ilifika mjini Kigoma.. na hapo ilikuwa kwenye kituo Cha Luiche.

Joshua sasa alianza kuchungulia dirishani Treni ikiwa moto kuelekea kweny kituo Cha mwisho.. akiwa ananona michikichi Mingi akiipita.

Mwishoe Treni ukifika mwisho wa Safari.. pembezoni kwa ziwa TANGANYIKA.

Alishuka na kuja kwenye kituo Cha daladala Kisha akpanda gari linalo enda KIBIRIZI.
Ilichukukua k**a dk 15 akawa kafika mwisho wa gari.. KIBIRIZI.. Kisha akaoneshwa gari la kwenda KALALANGABO... Na akaketi kiti Cha mwisho kwenye hiyo daladala.

Hatimae gari likaanza kuiachia KIBIRIZI na kuitafuta KALALANGABO.

Kitu Cha ajabu ndani ya gari alianza kuona abiria mmoja mmoja kwa ZAMU kuanzia abiria wa mbele KWA dereva simu zikiita kwa ZAMU ...

"Ndriiiiiiii. Ndriiiiiiii"
Abiria aliipokea Simu yake..

"Umekuja na mgeni?"
Abiria wa Kwanza akajibu

"Sijaja nae"

Kisha akakataa simu..

Abiria aiyefuata nae akapigiwa simu na kuulizwa swali lile lile

"Nipo mwenyewe"
Alijibu.

Aliuulizwa tena abiria mwingine swali lile na jibu likawa lile lile.

Haikujulikana aliyewapigia simu abiria hao na kuwauliza swali la Aina moja alikuwa no Nani...

Mwishoe akapigiwa simu abiria aliyekuwepo karibu na JOSHUA na alijibu yupo mwenyewe.

Cha ajabu Joshua hakupigiwa simu.. lakini alishangaa namna watu walivyo pigiwa simu mmoja mmoja.

Na mwishoe gari likaanza kupanda kakilima ILI lianze kuingia KALALANGABO.

Likiwa sasa limemaliza kilima na kuanza kutaka kuingia KALALANGABO GHAFLA gari likazimika.

Dereva alijitahidi kuwasha gari lakini Bira mafanikio likagoma kuwaka.

Mwishoe akapata wazo la kushusha abiria mmoja mmoja nakujaribu kuwasha gari..

Gari liligoma kuwaka.. mara ilivyo fika ZAMU ya Joshua kushuka GHAFLA gari likawaka .....

Ndipo konda. Na dereva wakaamua kupelekea abiria na kumuacha Joshua akisimama peke ake.

Gari likiwa limetokemea na kuingia KALALANGABO.... Joshua akiwa kasimama pale mpakani mwa KIBIRIZI na KALALANGABO..
Akaanza kupapasa macho yake mahali pale.
Kwa mbali alishuhudia makaburi mawili maeneo Yale.

Live bila chenga alimuona mtu mrefu kutoka makaburini pale akiwa kavaa mashuka meupe...

Na akaanza kumsogelea Joshua...

________________________________
ITAENDELEA

LIKE
COMMENT
SHARE
_______________________________

Usikose kipande Cha nne kwani kuna vitisho vya hali ya juu vya kichawi..

Simulizi: KAFARA.Sehemu: 02.Mtunzi: Saination WhatsApp: 0715175518..............................................WAHUSIKA...
19/09/2023

Simulizi: KAFARA.
Sehemu: 02.
Mtunzi: Saination
WhatsApp: 0715175518..............................................
WAHUSIKA WAKUU.
Kinara:- Joshua Roman
Adui:- Mzee Nduli.
___________________________

Taratibu nikadondoka chini na kuishiwa nguvu, kwa shida nikashuhudia maiti Ile imewekwa chini kando kidogo mahali gari lilipokuwa limesimama.

Mara watu wale walitokwa na kucha ndefu na kumsikia mkubwa wa wale watu akisema.

"Hii maiti ni ya JOSHUA ROMAN NGABO, "

"Tumeisha itoa KAFARA"
"Ni muda sasa wa kula nyama yake"

MARA
Walianza kuifakamia Ile maiti kwa kukata kata viungo vyake na kuliwa nyama na wale watu.

"Kwachaaa kwachaaa"

Watu wale waliendelea kutafuna sehemu mbali mbali ya Ile maiti.

Muda huo huo nikiwa naona giza giza pale chini nilimshuhudia yule dereva wa gari akiwa kasimama k**a anasubili nikate roho achukue mzoga wangu.

"Bro pindi wakianza kugombania na kutafuna fuvu la hiyo maiti na wewe utaanza kukata roho... Hivyo tachukua maiti YAKO k**a kiini macho (MGOMBA) niipeleke kwenu wakaizike"

Kwa shida nilimsikia dereva huyo akisema.

Nilijitahidi kunyenyuka ILI nikimbie lakini nikashindwa... Kwa tabu nikawaona sasa wale watu wakianza kugombania fuvu la Ile maiti baada ya kiwili wiki chale kukimaliza kukitafuna.

Kwa kutumia vidole vyao virefu waliligawa lile fuvu vipande vipande na kuanza kulitafuna nalo.

"Kwachaaa kwachaaa"
Mlio ule niliusikia namna walivyo kuwa wanavunja vunja mifupa ya lile fuvu kwenye midomo yao...

Baada ya dk kadhaaa maiti Ile ikawa imeishia tumboni mwa wale watu.

"Khrooo khrooo" watu wale walikoroma na sasa wakaanza kuniangalia mimi wakinitamani mahali hapa nilipokuwa chini.

GHAFLA.
Sasa wale watu wakiwa wanatembea kwa mwendo wa kunyata nyata walianza kunisogelea mahali nilipokuwa.

"KAFARA KAFARA KAFARA ya nyama hii ni TAMU."

Watu wale waliimba Huku sasa wakiwa wananikaribia... Muda huo huo nilianza kuhisi k**a naishiwa pumzi.

MARA.

nikakurupuka kutoka usingizini kumbe nilikuwa naota.

Naangalia saa ni saa moja asubuhi.
------------------------------------------
Joshua Roman akiwa kitandi peke ake nyumbani kwao maeneo ya ISEVYA, Manispaa yaTABORA. muda huo huo mdogo wake alikuwa kaamka kitambo.

"Kaka kaka umeingia mtandaoni?"

Ni Sauti ya Magogwa Roman, ilimstua Joshua pale kitandani.

"Hapana mdogo wangu sijaingia"

Roman alijibu Huku akimuangalia mdogo wake aliye kuwa anaingia chumban.

"Umepata kazi kaka"
"Nini"
"Umechaguliwa na Serikali kwenye kazi uliyo omba ya udaktari wa binadamu"

Magogwa alisema.

"ASANTE MUNGU"
Roman alishukuru.

Pale pale alifungua simu yake Aina ya NOKIA C20 na kujiridhisha yeye mwenyewe.

Alikuta kituo Cha kazi ni Cha KALALANGABO, kilichopo nje kidogo mwa mji wa Kigoma. Kwa wenyeji wa KIGOMA ni mbele ya KIBIRIZI mwambao wa ziwa TANGANYIKA.

Roman alifurahi sana, akamwita mama ake ampashe habari njema.

"Mama nimepata kazi"
"Kweli mwanangu?"
"Ndio"
"Umepangiwa wapi"
"KALALANGABO, Mkoani KIGOMA"
Roman alijibu.

"Unasema Nini"
"Umepelekwae KALALANGABO"
"Kule alizikwa Baba yenu pamoja na babu yenu"
"HAIWEZEKANI WEWE UENDE"

Mama alitahamaki na jasho zikamtoka GHAFLA...Roman aliposikia habari za Baba na babu yake... Akavutwa taswira juu ya ndoto aliyo iota siku hiyo.

"HIVI ILE NDOTO INAWEZA KUWA NA MAANA KWELI?"
Alijiuliza......

___________________________
Kipi kitafata.

LIKE
SHARE
Comment.

___________________MPYA___________________Simulizi: KAFARA.Mtunzi: Saination Sehemu: 01.WhatsApp:+255715175518__________...
16/09/2023

___________________MPYA___________________
Simulizi: KAFARA.
Mtunzi: Saination
Sehemu: 01.
WhatsApp:+255715175518
___________________________

WAHUSIKA WAKUU.
Joshua Roman Ngabo
Adui:- Mzee Nduli....…........................................

Nikiwa nipo katika hali ya Sintofahamu najikuta nipo kati kati ya msitu mnene Huku nikiwa sifahamu nimefikaje na huo msitu ni wa wapi.

Hali Ile iliniogopesha sana.

"Buuuuuuu buuuuuuu"

Ni sauti za ajabu zikiwa zinajirudia rudia ndizo nilizo zisikia.

Nilitulia kwa lengo ya kuzisikia vizuri.

"Buuuuuuu buuuuuuu buuuuuuu "

Nilikuja kugundua Sauti hizo ni za ndege Aina ya bundi.

"Mama angu nimekufa sasa"

Niliwaza moyoni... Huku moyo ukiwa unaenda mbio.

GHAFLA.
Upepo ulianza kuvuma kwa Kasi sana katika pori hili.... Huku kimbunga kikali kikiwa kinavuma na kupelekea kuinamisha matawi ya miti katika msitu huuu.

kimbunga hicho kilikuwa kinakuja usawa wangu... Nilitamani kukimbia lakini miguu ilikuwa mizito.

MARA.

"Haaaaaaaaaa kheeeeeeeee haaaaaaaaaaaaaa."

Ilikuwa ni Sauti ya kicheko kikali Huku mtu simuoni....

Hofu ilizidi kunishika moyoni.

Mara Sauti Ile ilianza kusikika.

"Unaitwa JOSHUA ROMANI NGABO"

"Si ndio nakuuliza wewe"

Sauti Ile iliniuliza Huku mtu nikiwa simuoni.

"Ndioo ndioo"

Nilikubali na tena nikitikisa kichwa kuwa jina Hilo ni langu.

Huku nikiwa nawaza mtu huyo anayeniuliza Yuko wapi na kanijuaje.

"Unakuja kufanya Nini Huku?"
Sauti hiyo iliendelea.

"Tulimuambia baba ako Roman amtoe KAFARA baba ake NGABO akakataa, alifanya kosa kubwa sana kutaka kuishi kinyume na utaratibu wetu..."

"Hivyo alivyo kataa kutoa KAFARA kwa babu ako NGABO ndipo tukauwa wote baba na babu ako."

"Mama ako akakimbia mbali na wewe Pamoja na mdogo wako ikawa pona pona yenu"

"Sasa umerudi tena etiiii"

Sauti Ile iliendelea safari hii ikiniuliza.

Kiukweli nilikuwa sijui chochote hali Ile ilinifanya nikae kimya tuu.

"Sasa ili uishi kijijini hapa lazima utoke KAFARA ya mama ako na ndugu yako."

Sauti ili ilinistua...
"Nini!?"
"KAFARA YA MAMA NA NDUGU ANGU"

Nilijikuta nikipwayuka kuiuliza sauti Ile..

"Siwezi kutoa KAFARA kwa mama na mdogo angu"

Safari hiii nilijibu kwa kujiamini nikiwa tayar kwa lolote.

"Huwezi kutoa KAFARA"
"HAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA"

Sauti Ile ilicheka kwa nguvu Huku nikiisikia kwa ukaribu zaidi...

Mara Moshi mkubwa ulienea mahali hapa.

GHAFLA

wakatokea watu watatu k**a kimbunga mbele yangu.

Watu wale walikuwa warefu sana Huku wakiwa na kucha ndefu waliovaa mavazi meupe....

Taratibu walianza kunisogelea... sijui wakiwa na nia gani...

Nilijikuta nikipata nguvu na kuanza kukimbia kuokoa maisha yangu....

Baada ya dk 15 mbio zangu zilinifikisha kwenye kijiji ambacho haraka haraka sikuweza kukifahamu... ikiwa ni saa 12 jioni..

Kila mwanakijiji alivyo niona alianiambia

"lazima UTOE KAFARA ili uwe salama wewe..."

Niliogopa na kuanza kukaa nao mbali...

Nilifika hadi kwenye kiwanja Cha shule vijana wakiwa wanacheza Mpira.

Walipo niona tuuu waliacha na kuja mbele yangu...

"TOA KAFARA, TOA KAFARA, TOA KAFARA."

Walisikika Huku wakiniambia niliogopa sana na kujiuliza njia pekee ni kuondoka kwenye kijiji hicho ambacho bado sijakijua.

Niliuliza wapi stendi ya magari Yanayo ended vijiji vingine niliambiwa... Ilikuwa k**a km 5 kutokea kijijini hapo ndipo unaifikia barabara..

Baada ya dk 45 ikiwa imefika saa moja jioni nilifika barabarani.

"Mhhhhhhh mhhhhhhh"
Nikiwa napumua kwa kasi nilijipa moyo taweza kupata gari lolote niondoke mahali hapo.....

Mara nikaona gari likiwa linakuja..

Moyoni nirifurahi nikiona sasa nimepona...
Gari lilifunga breki mbele yangu.

Nakuja kushangaa naona picha yangu ikiwa kwenye bodi ya gari lile tena juu ya sanduku la maiti.

Alishuka dereva akaniambia...
"Samahani bro nimefata maiti ya huyo jamaa anaitwa JOSHUA ROMAN NGABO"

MUDA HUO AKIONESHA PICHA ILE KWENYE GARI.

"Umewaona watu mahali hapa wameleta maiti hii ili niipakie kwenye gari niipeleke kwao"

Dereva yule aliniuliza.

Nilibaki nimemkodelea macho kwani maiti anayo iulizia huenda nikawa Mimi.

MARA NIKASH*TUKA NILIPOSIKIA KELELE ZA WATU ZIKIIMBA KUTOKEA KIJIJINI KUJA HAPA BARABARANI.

"Akalale akalale akalale akalale akirudi bahati yake"

Sauti zile ziliiimba Huku zikiwa zimebeba maiti juu juu inayo fanana na mimi kila kitu ikiwa wazi ikiletwa mahali hapa..

Pale pale nguvu ziliniishia nikaanza kulegea taratibu kudondoka chini sasa nikijua ndo MWISHO wa maisha yangu.

____________________________
ITENDELEA
LIKE
COMMENT
SHARE.

Ili niachie kipande kinacho fuata haraka

SUPER STAREp 03..Coming soon....Kaa mkao wa kula.. kupata SIMULIZI hii nzuri kutoka kwa mtunzi wako Senior Sai ...Wanawe...
08/08/2023

SUPER STAR

Ep 03..

Coming soon....
Kaa mkao wa kula.. kupata SIMULIZI hii nzuri kutoka kwa mtunzi wako Senior Sai ...

Wanaweza kunicheki Whatsapp 0715175518.. k**a utahutaji Moja ya simulizi zangu mpaka mwisho..

Kumbuka simulizi nilizotunga na kukamilika mpaka sasa ni

PATRIOT
MAHAK**A YA WACHAWI
VAMPIRE
ZAMU YAKO
KAFARA
na SUPER STAR...

huku simulizi nyingine nyingi mpya mpya nikiendelea kuzichora.

SIMULIZI: SUPER STAR.Sehemu:. 02.Mtunzi: Senior Sai (+254) 715 175 518.________________________________________________W...
26/12/2022

SIMULIZI: SUPER STAR.
Sehemu:. 02.
Mtunzi: Senior Sai
(+254) 715 175 518.
________________________________________________
WASHIRIKI WAKUU

Saleem Idriss
Salum Idrliss
Wazili Mkuu...

________________________________________________

GHAFLA
SIMU IKAKATWA

"HELLOW HELLOW"

Wazili Mkuu aliendea kuzungumza peke ake kwenye simu.

Akaja kugundua simu tayari ilikuwa imekatwa...

"Nimuue mke wangu?

Huyu mwanamke anatafuta Nini kwangu, tokea nizaliwe sijawahi fanya unyama wa namna yoyote... Ewe Mungu wangu ninusuru kwa hili nilipitiwa tuuu"

Alijikuta akiwaza...

Hatinae dakika kadhaa zikapita.. akafika kwake..

"Piiiiii piiiiiiiiiiiiii"

Honi za gari lilimfanya mlinzi wa nyumba kufungua geti... Wazili Mkuu akaingia kwake na kushuka katika gari...

Baada ya kusalimiana na mlinzi Kisha akaingia mpk sebuleni hakuamini alicho kiona Mr Idriss..

Kiukweli sebule Ile ilikuwa imepambwa kweli kweli.. huku kukiwa na ugeni mzito...

Pasipo hata kutegemea alimkuta kiongozi MKUU ambaye ni Mfalme wa Sasa wa KUSADIKIKA Mfalme Sai akiwa na familia ya wazili Mkuu wakiwa wanamsubili mlengwa ili afanyiwe pati kwa kuteuliwa kuwa Wazili Mkuu...

AKASTAAJABU WAZILI MKUU...

"USISHANGAE ni Mimi Mfalme wako nimeletwa na walinzi wangu hapa kwako baada ya tafrija hii kuisha watanifata kwani wao wameondoka"

Wazili Mkuu aliinama chini kumpa heshima Mfalme wake.

"Asante Mfalme kwa kuniamini na kunipa madaraka makubwa ya kuwa Wazili Mkuu...nakuahidi sito kuangusha"

Usijali naomba usimame.... Mfalme Sai alimuamuru wazili Mkuu..

Wazili Mkuu alisimaa Kisha wakaketi kwenye sofa na familia nzima... Yaani mke wa wazili Mkuu pamoja na watoto wake watatu na pati ikaanza.

Kiukweli Jioni hiyo ilikuwa ni furaha sana mahali hapo kwani wote walikunywa na kula pia nakuburudika kwa mziki laini sana...

Hatimae usiku ukaangia , watoto pamoja na mke wa Wazili Mkuu wakaenda kupumnzika...

Mke wa Wazili Mkuu bi Aisha akiwa chumbani kipindi huko alikuwa bize na simu yake anaperuzi mitandao ya kijamiia huku akiwa anafatilia habari kem kem za juu ya wanachi wamepokea viip taarifa za waziri Mkuu wao mpya..

Wengi walionekana kumpongeza na wengine wakisema waampe muda tuu kwani hata wa kwanza wazili Mkuu alionekana mzuri kumbe alikuwa ni muhaini kwa kuuuwa familia ya Aliyekuwa Mfalme baba ake na mfamle wa Sasa Sai Haroun... Mwisho wa siku akaambulia kunyongwa.

HUKU SEBULENI.

MAZUNGUMZO KATI YA MAFALME NA WAZILI MKUU YALIENDELEA...

"Muheshimiwa Wazili Mkuu mteule.. nimekuamini kutoka CV yako uliyo nayo ndo maana nikaamua kukuteuwa wewe katika nafasi hii"

"Nashukuru sana Mfalme wangu tena"

"Usijali Ila kumbukuka kuheshimu wananchi,
Uheshimu katiba na dini yako,
Uheshimu wazfa wako,
Hivyo jitahid kufanya kazi kwa weredi.. kumbuka kashfa au kosa lolote lile, likiwa ubadhilifu wa pesa, uroho wa madaraka na hata unyanyasaji wa kingono au skendo yoyote Ile itakufanya wewe usiwe wazili Mkuu... Na itapelekea kuweza kunyongwa k**a ilivyo kuwa kwa wazili Mkuu aliyepita pamoja na wazili wa afya au kufungwa kifungo....

Hivyo kuwa makini sana na kazi yako"

MFALME ALIHITIMISHA..

"NIMEKUELEWA MFALME WANGU""
WAZILI MKUU ALIJIBU.

Kisha Mfalme akapiga simu jumba la kifalme na haikupita muda msafara ukawa umetia nanga kwenye nyumba ya wazili Mkuu.. Mfalme aliingia kwenye gari maalum Kisha safari ya kurudi ngome ya kifamle ikaanza...

Huku wazili Mkuu akiwa kainamisha kichwa mpka magari yote yakatokomea.. Kisha ageuka nyuma aiingie ndani ili aende akapumnzike...

GHAFLA UMEME UKAWA UMEKATIKA SEHEMU ZOTE..

kukiwa Giza Totoro wazili Mkuu alianza kuogopa.. sio kitu Cha kawaida kwa UMEME kukatika hasa kwenye nyumba za viongozi wakubwa serikalini.

Ukiona hivyo jua Kuna kitu kibaya kimetokea mtandaoni... Hivyo serikali hatua ya kwanza huzimisha UMEME nchi nzima ili kitu hicho kisiwafikie watu wengi kabla hawajaanza kukifatilia mtandaoni ili kukibaini, na wahusika washikiliwe.

Wazili Mkuu akiwa anatetemeka... Na mwenye hofu aliingia chumbani na kumkuta mke wake kawasha mishumaa huku akiwa kakasirika Simu ikiwa mkononi.

" Viip mke wangu kulikoni"
" Habari zako mme wangu za kuteuliwa kuwa Wazili Mkuu zimezima mtandaoni, sasa Kuna video ya ngono Ina trendi mtandaoni... Kila mahali ukipita ni yenyewe tuu... Wanachi wako bize na video hiyo.. siyo Facebook, YouTube, Instagram, tiki Tok, ni yenyewe tuu ILA MIMI SIJAFUNGUA BADO LINKI ZA VIDEO HIYO AU KUOMBA CONNECTION WATU WANITUMIE B"

"NAOMBA NIONE HIYO VIDEO.". WAZILI MKUU ALISEMA,

KISHA AKAPEWA SIMU HUKU AKIWA NA WASIWASI AKAFUNGUA LINKI YA VIDEO HIYO KUPITIA FACEBOOK..

"MAMA ANGU" ALIJIKUTA AKIJISEMEA MOYONI YEYE MWENYEWE TENA AKIWA NA HOFU TELEE BAADA YA KUIONA VIDEO ILE.

MARA SIMU YAKE IKAITA, ANAANGALIA NAMBA ILIYO PIGA HAPO AKAZIDI KUCHANGANYIKIWA.

___________________________________________________

ITAENDELEA

LIKE
SHARE
COMMENT

Address

Mikocheni
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Saination posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share