10/09/2020
Kiumbehai
Kiumbehai ni kitu kilicho hai k**a vile binadamu, mnyama, mmea au bakteria.
Kwa upande mmoja viumbehai ni molekuli za mata jinsi ilivyo kwa vitu vingine, kwa mfano udongo, mawe, fuwele au hewa. Kwa upande mwingine mata hii ina mfumo wenye tabia mbalimbali ambazo kwa pamoja zinaunda uhai k**a vile uwezo wa kuzaa, kukua na umetaboli (uwezo wa kujenga au kuvunja kemikali mwilini).
Hata k**a sayansi haijajua kikamilifu uhai ni nini inatambua jumla ya tabia hizo k**a dalili za uhai.
Kiumbehai kinaweza kuwa na seli moja (k**a bakteria kadhaa) au kuwa na seli milioni kadhaa k**a mwanadamu.
Viumbehai vyenye seli moja tu ni vidogo sana: havionekani kwa jicho bali kwa hadubini tu.
Sifa za viumbehai
Kiumbehai ni kiumbe chenye uwezo wa kuzaliana, kukua, kula, kujongea, kuhisi, kupumua, kutoa taka za mwili. Ni lazima awe na sifa hizo ambazo zinaweza kufafanuliwa k**a ifuatavyo:
1. kukua: ni ongezeko la kudumu la sura ya mwili na ukubwa wake. Viumbehai hukua na wanahitaji chakula chenye virutubishi vyote (mlo kamili) ili waweze kukua.
2. kuzaliana: kuzaa au kuzaliana ni mchakato wa kibiolojia ambao viumbe wapya - "uzao" - hutolewa kutoka kwa wazazi wao. Uzazi ni kipengele cha msingi cha uhai wote unaojulikana; kila kiumbe binafsi kipo k**a matokeo ya uzazi.
3. kula: kula (pia inajulikana k**a kuteketeza) ni kumeza chakula, kwa kawaida kutoa viumbe heterotrofu kwa nishati na kuruhusu ukuaji. Wanyama na heterotrofu nyingine wanapaswa kula ili waweze kuishi - "carnivores" kula wanyama wengine, "herbivores" kula mimea, "omnivores" hutumia mchanganyiko wa mimea na wanyama, na "detritivores" kula maozo. Fungi hupunguza vitu vya kikaboni nje ya miili yao kinyume na wanyama ambao humba chakula chao ndani ya miili yao. Kwa wanadamu, kula ni shughuli ya maisha ya kila siku.
4. kujongea: ni kitendo cha kubadilisha eneo au mahali alipo kiumbe huyo
5. kuhisi: ni mchakato wa kukandamiza kwa mujibu wa viumbe vya stimul.every vyema ni nyeti na ina viungo vitano vya mwili kwa ajili ya hisia ambavyo ni macho, masikio, ngozi, ulimi na pua. Pua inatumika kunusia, macho yanatumika kuangalia, ulimi unatumika katika kuonja, ngozi inatumika katika kuhisi na ulimi unatumika katika kuonja.
6. kupumua: kupumua (au uingizaji hewa) ni mchakato wa kusonga hewa ndani na nje ya mapafu ili kuwezesha kubadilishana gesi na mazingira ya ndani, hasa kwa kuleta oksijeni na kusafirisha kabonidaioksaidi.
7. kutoa taka za mwili: ni mchakato ambao taka za kimetaboliki na vitu vingine visivyofaa vinaondolewa kutoka kwa viumbe. Katika vimelea hii hasa hufanywa na mapafu, figo na ngozi. Hii ni kinyume na usiri, ambapo dutu hii inaweza kuwa na kazi maalumu baada ya kuacha kiini. Utoaji taka mwili ni mchakato muhimu katika aina zote za uhai. Kwa mfano, katika mkojo wa wanyama hufukuzwa kwa njia ya urethra, ambayo ni sehemu ya mfumo wa msamaha. Katika viumbe vya seli moja, taka hutolewa moja kwa moja kupitia uso wa seli.
Aina za viumbehai
Wataalamu wamegawa viumbehai katika makundi matatu kufuatana na muundo wao wa ndani:
• Bakteria na
• Archaea ni viumbehai wenye seli moja wasio na kiini cha seli; wote wanaitwa pia Prokaryota
• Eukaryota ni viumbehai wenye kiini cha seli. Wanyama, mimea na fungi huhesabiwa humo.
Makundi hayo huitwa domeni 3 za uainishaji wa kisayansi.
Virusi viko kati ya viumbehai na vitu visivyo hai; wataalamu wengine husema havistahili kuitwa "viumbehai" kwa sababu haviwezi kuzaa pekee yake, haina umetaboli wake bali unategemea kuingia ndani ya seli na kutumia nafasi za seli kwa kuzaa kwake.
Wanyama (jina la kisayansi ni animalia na hutoka katika Kilatini) ni viumbehai wasio mmea, kuvu, bakteria, protista au arkea. Vile vile tunaweza kusema wanyama ni viumbehai wanaotegemea chakula kutoka sehemu nyingine: wao hawana uwezo wa kujitengenezea chakula chao wenyewe kupitia usanisinuru (nishati ya jua) lakini kutoka kwa viumbehai vingine ama wanyama wengine au mimea.
Kufuatana na aina ya chakula tunatofautisha hasa wanaokula mimea wanaoitwa walamani au walamea (kwa Kiingereza: herbivorous) na wanaokula nyama wanaoitwa walanyama au wagwizi (ing. carnivorous). Kuna pia walavyote (ing. omnivorous) wanaoweza kula kila kitu, ama mimea ama wanyama wengine (ing. omnivorous).
Wanyama wanahitaji oksijeni kwa kupumua.
Wanyama walio wengi hutembea yaani hubadilisha mahali wanapokaa, kwa hiyo wanahitaji milango ya maarifa.
Sayansi inayochunguza wanyama huitwa zuolojia, ambayo ni tawi la biolojia.
Aina za wanyama ni nyingi sana. Mara nyingi aina zao zinatofautishwa k**a ni wanyama wenye seli nyingi (metazoa) au seli moja (protozoa) tu.
Kuna wanyama wanaoishi peke yao, katika vikundi na jamii. Mfano wa wanyama wanaoishi peke yao ni kifaru au nyoka. Wanajumuika kwa tendo la kuzaa pekee. Mfano wa wanyama wa jumuiya ni simba wanaokaa na kuwinda pamoja. Ushirikiano unasaidia kupata chakula bora. Mfano wa wanyama katika jamii ni nyuki na wadudu wengine.
Upande wa mwili hata binadamu ni mnyama na kimaumbile anahesabiwa kati ya mamalia.
Binadamu hutofautisha mara nyingi
• Wanyama wa pori au wanyamapori
• Wanyama wa kufugwa au Mifugo
• Wanyama wa nyumbani (Wanyama-kipenzi)
ingawa lugha hii hutumiwa tu kwa wanyama wakubwa zaidi, kwa kawaida wenye uti wa mgongo (kwa Kilatini: Chordata).
Mamalia ni wanyama ambao wanawanyonyesha watoto wao maziwa kwa kutumia viwele vyao.
Wana damu moto na kupumua kwa mapafu.
Kuna takriban spishi 5,400 za mamalia. Spishi 5 kati ya hizo wanataga mayai, lakini wengine wote wanazaa watoto hai.
Ukubwa unatofautiana sana, kuanzia spishi ndogo aina ya popo mwenye urefu wa sentimita 4 pekee hadi spishi kubwa nyangumi buluu mwenye urefu wa mita 33.
Uainishaji
Mamalia ni ngeli ya faila Kodata.
Ngeli yao hugawiwa katika nusungeli mbili:
• Prototheria ni mamalia wanaotaga mayai au kubeba watoto wao ndani ya mfuko wa mwilini kwa muda fulani baada ya kuzaa
• Theria ni mamalia wa kawaida na spishi nyingi zimo humo.
• Amfibia ni kundi la wanyama wenye uti wa mgongo na damu baridi ambao wanaanza maisha kwenye maji na baada ya kupita metamofosi wanaweza kuendelea kwenye nchi kavu katika kipindi cha pili cha maisha yao. Vyura, salamanda na nyoka wanafiki wamo katika ngeli hii.
• Jina la kisanyansi "amfibia" linaunganisha maneno mawili ya Kigiriki ἀμφί amphi yaani "pande zote mbili" na βίος bios yaani "maisha" kwa jumla "maisha pande zote mbili" yaani ndani ya maji na kwenye nchi kavu.
• Chanzo cha maisha yao ni mayai yaliyotegwa kwenye maji. Amfibia mdogo anatoka kwenye yai katika umbo la ndubwi anayeishi ndani ya maji bila miguu na kupumua kwa yavuyavu ikiwa na mkia. Inaendelea kubadilika na kukuza miguu hadi kutoka kwenye maji ma kufikia umbo la mnyama mzima anayepumua kwa mapafu.
• Spishi chache zimeendelea na zinaweza kuzaa bila maji. Wadogo wanafikia umbo la ndubwi na kuendelea na metamofosi ndani ya yai hadi kutoka kwa umbo mzima. Spishi kadhaa zinatunza mayai ndani ya mwili hivi zinazaa wadogo hai.
• Amfibia ni wala nyama wanakula viumbe vidogo hasa wadudu.
• Kuna takriban spishi 5,700 za amfibia.
• Ndege ni wanyama wenye uti wa mgongo (chordata) na miguu miwili wanaozaliana kwa kutaga mayai.
• Biolojia inawapanga katika ngeli ya Aves.
• Ndege wameenea kote duniani kuanzia Aktiki hadi Antaktiki.
• Ndege mdogo huwa na sentimita 5 tu na ndege mkubwa ana urefu wa mita mbili na nusu.
• Ndege huwa na manyoya, mdomo bila meno, mayai yenye ganda gumu, moyo wenye vyumba vinne na mifupa myepesi ambayo ni imara.
• Ndege walio wengi wana uwezo wa kuruka hewani na maumbile yao yanalingana na kusafiri hewani. Ila tu aina chache zimepoteza uwezo wa kuruka kwa mfano mbuni, ngwini na ndege kadhaa wa visiwani.
• Aina nyingi za ndege huwa na misafara ya kila mwaka, kwa mfano korongo mweupe husafiri kila mwaka kati ya Afrika na Ulaya.
• Reptilia (kutoka Kilatini "reptilis" mwenye kutambaa; pia: mtambaazi, mtambaachi, mnyama mtambaaji[1]) ni kundi la wanyama wenye damu baridi, ngozi ya magamba badala ya nywele au manyoya wakipumua kwa mapafu. Siku hizi wataalamu hupendelea jina Sauropsida.
• Wanazaa kwa njia ya mayai; wengine wanatega mayai na wadogo wanatoka nje bila ngazi ya kiluwiluwi au kwa spishi kadhaa mayai yanaiva ndani ya tumbo la mama na wadogo wanazaliwa hai.
• Kibiolojia ni ngeli ya vertebrata. Jina limetokana na maumbile yao maana wanatambaa na tumbo juu ya ardhi; ama kwa miguu mifupi k**a mijusi au bila miguu k**a nyoka.
Kwa leo somo letu linakomea hapa. Bila shaka umeweza kuwafahamu wanyama kwa ujumla. sasa tutaanza kumchambua myama mmoja baada ya mwengine.
Kupata kusikiliza na kuona video pamoja na picha kwa kila kinachoelezewa. Subscribe youtube channel yetu ya au bonyeza link hii
Tafuta video zilizoandikwa Wajue Wanyama. Upate kujifunza wanyama na maisha yao.
mpaka siku nyingine, Bye Bye.
Pata simulizi za sauti na kazi mbalimbali kutoka kwa Multi-talented boy Molito