08/10/2022
Fikra Huru........Mnyaruganda
Nelius Trazias 0748254542
Mnyaruganda... Siku ukipata nafasi ya kukutana na mwanao John mkumbushe
1. Mkumbushe kuwa mwanamke ni kiumbe chenye huruma sana ila asitumie mlango huo k**a fungulia Mbwa, machozi ya mwanamke ni sumu inayoua taratibu.
2. Mwambie John kuwa akila akaondoka akumbuke kuna wengi wamevimbiwa hata baada ya kula, hivyo asijisifu sana hata matokeo hutoka baada ya kufanya mitihani.
3. Mkumbushe John kuwa mwanamke ni kiumbe kinachoamini sana katika uongo kuliko hata ukweli ila haitaji longolongo , hivyo asipende kutembea katika maisha ya kuigiza akivaa raba na suruali za kuazima mwisho wa siku ataumbuka.
4. Mkumbushe John kuwa hakuna mwanamke msaliti hapa duniani ila mwanamke anataka apewe upendo wa kweli na matunzo kidogo ili asimame daima k**a ukuta wa Berlin. Ila wanaume wengi wa sasa kupenda kukwepa majukumu wamegeuza kibao na kuanza kuwaita wanawake Malaya. Duuuuuuh Mungu wa Isaka
5. Mkumbushe John kuwa kila anapomuona mwanamke ampe heshima yake maana kila mwanamke amebeba maono ya dunia. Mara ndiye mwalimu wa familia, mara mwanasheria kwa watoto wake, mara mhasibu akilinda uchumi wa familia, mara Daktari kumuangalie anayeumwa , mara mwandishi akatoe habari na mwenendo wa familia yake n.k, . Mwanamke jipige kifua sema " wanawake jeshi kubwa ".
6. Mkumbushe John kuwa mwanamke ni sawa na bustani ya mbogamboga huitaji kumwagiliwa kila siku hivyo akiacha ikauke wenye uhitaji wa kula mboga za majani ni wengi hivyo amlinde Mwanamke k**a mboni.
7. Mkumbushe John kuwa wabeba maono ni wengi siku hizi, hivyo amtangulize Mungu asije kuliwa kichwa na madanga wa mjini.
8. Mkumbushe John kuwa kila akimuona mwanamke analia asimuone k**a muigizaji bali kupitia kulia kwake mwanamke hujiongezea siku za kuishi kwa kuondoa machungu na mwanaume hali hii ndiyo mara nyingi humuondoa uhai kwa sababu ya kuyakumbatia machungu leo hii wanaume wengi hufa mapema na kuwaacha wake zao.......