21/06/2026
Hotuba ya UNHCR kwa ajili ya Siku kuu ya WAKIMBIZI Ulimwenguni
*Siku ya Wakimbizi Duniani 2026
Ni siku ya kukumbuka watu walilazimika kukimbia nyumba zao kwa sababu ya vita, vurugu au mateso. Mwaka huu inatimiza miaka 75 ya ahadi ambayo dunia ilifanya: "yeyote anayekimbia kutafuta usalama ana haki ya kupata nafasi mpya".
*Msumbiji ina uhusiano gani na hili?
Msumbiji tayari imewapokea watu wengi waliokimbia kutoka nchi jirani. Na pia tuna ndugu zetu Cabo Delgado walipoteza kila kitu kwa sababu ya mzo na sasa wanajenga upya. Kwa hiyo: tunajua vizuri maana ya kuhitaji msaada.
*Ujumbe muhimu ni upi?
1.Mkimbizi siyo tu "masikini". Ni mwalimu, mkulima, mama, mwanafunzi, mfanyabiashara. Ni mtu mwenye vipaji na ndoto, sawa na sisi.
2.Ahadi inaendelea: "Mpaka kila mtu awe salama, tutaendelea kutimiza ahadi yetu". Maana yake: hatutawaacha wale wanaohitaji.
3.Kulinda husaidia kila mtu: Tunapotoa nyumba, shule, kazi kwa aliyekimbia, mtu huyo anakua na kusaidia jamii yote. Hakuna anayeshinda peke yake.
Kwa sentensi 1:
Hata baada ya kupoteza kila kitu, inawezekana kuanza upya, kuwa na tumaini na kujenga maisha mapya. Na hili hutokea tu tunaposaidiana.
✍️| Daniel Lion Benga
VD Media Maratown
VD Mǝdia Dzaleka
Maratown News