Poem pap

Poem pap current affairs in a poetry form

19/09/2020

KAMSA YA KEMSA

Jipu ninaliminyaa,matokeo yake USA
Twateseka wakeya,mabwenyenye mwatutesa.
Gwanangah nawakanya,siibeni zetu pesa
Kamsa napiga kemsa,serekali muko wapi?

Tunalo taka ni jibu,msiweni kwetu bubu
Nimeliminya jipu,Hamna kweli adabu
Metuacha kwenye taabu,itabidi mumetubu
Kamsa napiga kemsa,Uhuru utupe jibu.

Kweli ninyi in wakora,pesa zetu mumepora
Matumbo yenu mefura,mifuko pia mefura
Mnapo vikuna vipara,wakenya sisi twahara
Kamsa napiga kemsa,kweli ninyi mafidhuli.

Utunzi wa ustadh salijogoo
19/9/2020
Nairobi Kenya.

05/04/2020

Masai mko wapi ?

Hili swali ninalo
Nijibuni mjualo
Siulizi ya waluo
Masai mko wapi.?

Vibuyu hatuvioni
Barabarani karantini
Mmejificha mitini
Masai mko wapi?

Korona ikisha isha
Sisi tawafurusha
Mmekuwa kitupotosha
Masai tumewajua

03/04/2020

UChina Mna mambo

Ulimwengu twateseka
UChina wametuteka
Wao likula nyama
Sasa twanawa mikono.

Popo likuwa chanzo
Uhani kukiwa mwanzo
Korona meleta uozo
Wachina likula nyama
Sasa twanawa mikono

26/04/2019

china si canani

tumebaki kuwa pweke ,wakenya tunasonona
tumesha pigwa teke,katu hatutaja pona
tungekuwa na kikwete,heri sis tungepona
uchina sio canani,raila fahamu hili

canani ulo ahidi, njiani ukatuacha
kumbe likuwa hadidhi,huku kaficha kucha
wengi sisi umeudhi ,mafisadi kikumbata
uchina sio canani ,raila fahamu hili.

utunzi wa gwanangah chavasu.(salijogoo)
Nairobi Kenya
26/4/2019

Jua Kubusu Mwezi!!Yanaitwa malimwengu,yote haya ni ya mungubongo natoa kungu,jikoni mnamo vyunguhili ni shairi langu,muu...
07/03/2019

Jua Kubusu Mwezi!!

Yanaitwa malimwengu,yote haya ni ya mungu
bongo natoa kungu,jikoni mnamo vyungu
hili ni shairi langu,muulize hata mkangu
jua likibusu mwezi,waswahili mwasemaje?

Utunzi wa Gwanangah Chavasu(Salijogoo)
Nairobi kenya
7/3/2019

Je Samaki Hulala?kimya nakivunjeni,nawaomba samahaninikitambo nitungeni,kwa kutunga si mgeniniliwaacha gizani,japo kabak...
28/02/2019

Je Samaki Hulala?

kimya nakivunjeni,nawaomba samahani
nikitambo nitungeni,kwa kutunga si mgeni
niliwaacha gizani,japo kabaki moyoni
nawauliza magwiji,je samaki hulala?

k**a hulala ni vipi? hili nataka kujua
usingizi wake mfupi? ni usiku au mchana?
mwenzake wezaje kopi,kulala asokujua
nawauliza magwiji ,samaki hulala vipi?

machoye je huyafumba,nak**a ndio ni vipi
blangetiye je hujifumba?nahivyo itakuwa vipi
maji ni chake chumba,awe mrefu au mfupi
nawauliza magwiji,samaki hulala vipi?

kifudifudi au chali,ningependa mi kujua
niijue yake hali,k**a pia hutoa dua
usingiziwe ni halali,macho akiyakodoa
nauliza nijibiwe, samaki hulala vipi?

Utunzi wa Gwanangah Chavasu
(Salijogoo)
28/2/2019
Nairobi Kenya.

08/01/2019

NGWINA KUACHILIWA

gwananga ninashangaa
nimebaki kuzubaa
yalotufika ni balaa
uvumi umezagaa

Ngwina kuachilia
wakenya tunalia
hatutaja si tulia
kenya kweli familia?

kweli shamba la wanyama
itabidi si kuhama
twabaki kishika tama
wenzetu wakila nyama

utunzi wa gwanagah chavasu
(salijogoo)
7/1/2019
Nairobi Kenya

27/11/2018

SIMU ZINA SUMU
sijaifunga saumu,nasiishi mi watamu
nalitunga lenye sumu,halina tena utamu
niyangu mi majukumu,napia niyangu zamu
walo hai wafahamu,simu hizi zina sumu

akili zangu timamu,muulize wangu mamu
nishikapo na kalamu,kutunga napata hamu
yahitaji na nidhamu,ili simwage damu
walokole na kafiri,simu zino zina sumu.

utunzi wa salijogoo(gwanangah chavasu)
Nairobi kenya
27/11/2018

Za mkizi Na MbogoNjoo pole baa mdogo,harakazo tajikwaawaititu au odongo,ustarabu unafaasomalia hadi kongo,sisi wamoja ja...
08/11/2018

Za mkizi Na Mbogo

Njoo pole baa mdogo,harakazo tajikwaa
waititu au odongo,ustarabu unafaa
somalia hadi kongo,sisi wamoja jamaa
hasira mkizi kali, za mbogo nazo vipi?

mbugani siende ovyo,sana aliko mbogo
tapokonya wako moyo,kikukabili mbogo
tajipata kuwa ovyo ,usipo tumia bongo
zamkizi japo kali,za mbogo takuwaje?

tamati langu shairi,gwananga kawambieni
sitamu si shubiri,hili nilowatungeni
hasira zao hatari,mukizi pia na nyati
za mkizi nae mbogo,zipi huwa hatari?

Utunzi wa Gwanangah Chavasu(Salijogoo)
Nairobi Kenya
Nov 8 2018.

AHADI NI DENIwalishanena wahenga,ahadi huwa ni deninasititiza gwananga,hili tia akiliniahadi huezi lenga,ungalipo dunian...
16/10/2018

AHADI NI DENI
walishanena wahenga,ahadi huwa ni deni
nasititiza gwananga,hili tia akilini
ahadi huezi lenga,ungalipo duniani
dawa ya deni kulipa,ahadi deni jamaa

tusianze mvutano,mwenyewe uliahidi
siwape milioni tano,wape ulowaahidi
tusisikie maneno,gushi umewapa hundi
dawa ya deni kulipa ,ahadi deni jamaa.

Utunzi wa salijogoo(gwanangah chavasu)
Nairobi Kenya
16/10/2018

12/10/2018

ASANTENI WOTE MNAO NIFUATA KWENYE UKURASA HUU.NASHUKURU SANA MOLA AWABARIKI.

current affairs in a poetry form

JORDANI HAMNA MAMBAkanani ulituahidi,njiani ukatuachawewe ni mushaidii,twalia usiku kuchamkataba ulikaidi,wenzako ukatua...
12/10/2018

JORDANI HAMNA MAMBA

kanani ulituahidi,njiani ukatuacha
wewe ni mushaidii,twalia usiku kucha
mkataba ulikaidi,wenzako ukatuacha
jordani hamna mamba,usemayo ni hekaya

muulize hata jakaya,napenda uadilifu
situngi lenyekinaya,mulizeni hata mkufu
sijui kuimba kwaya,yaitaji umakinifu
jordani hamna mamba,raila fahamu hili

sasa uko kanani,wenzako tuko jordani
muko sasa na jubilii,na huo sio utani
watuambia bora uhai,cheki katia mfukoni
jordani hamna mamba,mbona wewe ulivuka?

Utunzi wa salijogoo(gwanangah chavasu)
Nairobi kenya
12/10/2018

Address

Nairobi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Poem pap posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share