05/09/2026
Mfanyabiashara na ushawishi wa mitandao ya kijamii Mwingereza mwenye asili ya Nigeria, Igho "Tiny" Ubiribo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 43 kufuatia upasuaji wa kuongeza ukubwa wa uume akiwa mapumzikoni nchini Thailand na mke wake, kulingana na TMZ.
Ubiribo, anayejulikana pia k**a Denisi au Ego, inasemekana alifanyiwa upasuaji huo wa urembo katika kliniki moja jijini Bangkok ambapo madaktari walimchoma mililita 40 za hyaluronic acid na lidocaine kwenye uume wake. Muda mfupi baadaye, alienda kufanyiwa massage (kandandishwa) na mke wake, Danielle Simba Allen, lakini akaanza kupata maumivu makali ya kifua.
Taarifa zinasema Ubiribo alizimia mara mbili kabla ya kukimbizwa katika Hospitali ya Sukhumvit, ambapo madaktari walimfanyia huduma ya dharura ya usaidizi wa kupumua na moyo (CPR) kwa zaidi ya dakika 100. Japo walijitahidi, alitangazwa kuwa amefariki dunia.
Maafisa wa afya baadaye walithibitisha chanzo cha kifo kuwa ni pulmonary embolism — yaani gazi/sugu la damu lililoziba mishipa ya mapafu lililotokana na sindano hizo za kujaza (filler injections).