26/06/2026
ποΈ KITUO MAALUM CHA KULINDA HAKI ZA WATOTO KINAJENGWA MALINDI
Kila mtoto anastahili kusikilizwa, kulindwa na kutendewa kwa heshima. Hili linawezekana kwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira salama ambapo watoto wanaweza kueleza changamoto zao bila hofu.
Ujenzi unaoendelea wa Kitengo Maalum cha Kulinda Haki za Watoto (Child Protection Unit) katika Kituo cha Polisi cha Malindi, unaofadhiliwa kupitia Malindi NG-CDF, ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za ulinzi na usalama wa watoto katika eneo hili.
Kitengo hicho kitakuwa na mazingira rafiki kwa watoto, kikiwemo maktaba na ofisi maalum zitakazowezesha maafisa kushughulikia kwa haraka na kwa weledi kesi zinazohusu unyanyasaji, ukatili na unyonyaji wa watoto.
Mradi huu unalenga kuhakikisha watoto wanapata ulinzi, haki na msaada wanaostahili katika mazingira salama na yenye utu.
β Mheshimiwa Mbunge Hon. Amina Mnyazi - M.P Malindi
Malindi show biz