15/11/2023
Ameacha kitanda nyumbani yupo barabarani kutafuta afadhali ya kesho kwa watoto wake
Anatoka asubuhi na mapema anarudi usiku sana! Amechagua vita yake kupigana katikati ya mvua na jula kali
Kila akitoka anaacha mia mbili mezani madogo wakiamka wapooze njaa na vitumbua pale kwa Mama Rashidi
Unga unga mwana! Life bado ni kitendawili na mtegaji hamjui, achoki kupambana
Hana account Tiktok hajui kujisnap wala hatii huruma mitandaoni k**a Gigy Money
Ni Mama bora aliyekoswa hela lkn Mungu amemjalia moyo safi wa kuridhika na chake kidogo
Picha itumike funzo kwa wale wanawake wanaosema siwezi kuolewa na mwanaume masikini
Big up kwa wamama wote wapambanaji.