30/05/2019
Story: NISAMEHE
Contact us: 0659146373
Author: Cleverley
Sehemu ya 4
Ilipoishia sehemu ya 3;
Wakati mama John anainua simu kujaribu kumpigia mume wake, ghafla ilisikika mlio wa mlango mtu akiwa anagonga ikifuatiwa na sauti iliyo jawa na hofu.
“Hodi, nifungulie” hii ilikuwa sauti ya k**e
“Hee! Kuna nini mbona mbio hivyo?” aliuliza mama John baada ya kufungua mlango huku akiwa katika hali ya kutaharuki
“Umepata taarifa ya mumeo (Baba John)?” aliuliza mama huyo
“Hapana kuna nini? Nini kimetokea?” yalikuwa na maswali mawili yaliyofatana kutoka kwa mama John.
************************
Endelea………….
Asubuhi ya siku inayofata k**a kawaida kila mtu akiwa katika mihangaiko yake ya kujitafutia riziki lakini ilikuwa tofauti katika familia yake John ambao yeye pamoja na mama yake na mdogo wake walikuwa katika hospital ya kijiji kwaajili ya kumuona baba yao akiwa amelazwa.
Saa tatu kamili asubuhi ndio mda maalumu wa kuruhusiwa kuwaona wagonjwa, mama John na wanae waliruhusiwa kuingia wodini.
“Habari za asubuhi mume wangu” alisalimia mama John huku akiwa anatoa chupa kwenye mfuko
“Ah! Salama tu, mmeamkaje?” alijibu baba John na kuwatupia swali
“Shkamoo baba” walisalimia watoto kwa pamoja
“marahaba hamjambo” alijibu Baba John
“Hatujambo” walijibu watoto
“Enhe! Nini kilitokea” aliuliza mama John huku akikaa kitandani
“Dah! Wakati narudi jana usiku nilikutana na vibaka watatu ila mmoja sura yake siyo ngeni kwangu lakin sikumbuki wapi nlishawahi kumuona, wameniibia simu pesa na pia walinipiga k**a unavyoona wameniumiza mguu lakini namshukuru mungu naendelea vizuri kwa sasa japo daktari amesema nimepata hitilafu kidogo kwenye mfupa lakini haujavunjika kabisa” alisema baba John wakati huo watoto wake wakiwa katika utulivu na kwenye sura za kuonesha huruma kwa baba yao
“Pole, utakuwa sawa tu karibuni. Ngoja nikuwekee chai basi” alisema mama John huku akitoa kikombe katika mfuko na kumimina chai katika chupa.
Naam ulikuwa ni muda wa mapumziko, watoto walionekana baadhi wakicheza baadhi wakiwa kantini na wasiokuwa na hela walibaki darasani japo siyo kwa kupenda kwao. Steve k**a kawaida yake alikuwa uwanjani wakicheza mpira na wenzake ilisikika sauti ya k**e ikimuiita na alipogeuka alikuwa ni Vanessa.
“We nitafute baadae bana sasa hivi nacheza” alijibu Steve huku akiwa amegeuka kwaajili ya kurudi uwanjani lakini Vanessa alimuita tena,
“Njoo mara moja nikuulize basi” alijibu Vanessa kwa sauti kubwa na yenye ukali ndani yake
“Haya sema haraka haraka” alijibu Steve huku akijikung’uta suruali yake
“Wewe mwenzio (John) leo vipi mbona hajaja” aliuliza Vanessa
“Hata sijui maana leo sijapitia kwao, atakuwa kalala huyo maana ili mvua ya saa kumi na mbili siyo mchezo” alijibu Steve kimasihara
“Haha leo si utapitia kwao ukiwa unarudi nyumbani?” aliuliza Vanessa
“Nadhani” alijibu Steve
“Basi ukifika msalimie alafu mwambie akumbuke Ijumaa mechi aje” alisema Vanessa huku akigeuka kuondoka
“poaaaaaaaaaaa” alijibu Steve nae akigeuka ili kurudi uwanjani lakini muda ulikuwa umeenda na kengele ya kuashiria muda wa kurudi darasani ulikuwa umefika, kitendo hicho kilimfanya Steve akunje sura na kutoa sauti ya hasira.
Ilitimia Saa kumi na mbili jioni, Baba yake John aliruhusiwa kurudi nyumbani ila kwa masharti ya kutokuutumia mguu huo kwa kutembele ndani ya muda wa mwezi mmoja ndipo aanze mazoezi ya kuukanyagia chini.
“Itabidi tutafute baiskel ya kukufikisha nyumbani sisi tutakuja kwa miguu maana hela niliyonayo haitoshi kupanda gari” alisema mama John huku akimpungia mtu wa baiskel k**a ishara ya kumuita.
***********
Kengele iligongwa na kufanya wanafunzi wakimbie kuelekea eneo la matangazo(mstarini).
“Hamjambo” ilikuw sauti ya mwalimu Adamu mwalimu wa michezo
“Hatujambooo, shkamoo mwalimu” baadhi ya wanafunzi waliitikia na baadhi yao walikuwa kimya
“Natoa dakika kumi ya kufanya usafi kabla ya kengele ya pili kwaajili ya kukutana kuelekea uwanjani kwenye mechi na wageni wameshafika. Haya tawanyika isipokuwa wachezaji tuu ndo wabaki hapa”alisema mwalimu huyo na kufanya wanafunzi hao waanze kukimbia kuelekea sehemu zao za kufanya usafi
“Captain” aliita mwalimu Adamu baada ya kubaki na wachezaji tu
“Naam” alijibu Captain aliyefahamika kwa jina la Abduli
“Waongoze wenzako nilipokuelekeza alafu pitia jezi pale stoo mvae kabisa, mnisubiri nakuja” alisema mwalimu huyo na kuondoka.
Baada ya dakika 15 kengele ilipigwa tena na mda huu mwalimu aliwaamrisha wanafunzi watangulie uwanjani.
“haya kipa utakuwa wewe maana mwenzako leo hajaja” mwalimu wa michezo alianza kutoa namba za kucheza kwa wachezaji
“namba mbili, tatu, nne na tano wataongozwa na captain akifatia Juma, Khamisi na Hamadi” aliongezea mwalimu
“Upande wa kushoto na kulia ni James na Peter alafu viungo namba sita ni Kelvin na namba nane ni Joshua” alisema mwalimu huku waliotajwa wakianza kuchukua jezi
“Namba tisa na kumi ni Petro na Lucas wengine tutaanzia nje” alimaliza mwalimu na kusababisha Steve kucheka kuguna baada ya yeye na mwenzake John kutokutajwa katika kikosi kitachoanza.
Wachezaji walielekea uwanjani na kuwakuta timu pinzani wachezaji wa shule ya sekondari Manjangu wakiwa uwanjani wakipasha misuli yaani (warm up) na wao walianza kupasha misuli na kunyoosha viungo vyao kabla ya kipenga cha muamuzi wa mchezo huo kupulizwa mpira uanze. Wachezaji wa timu zote mbili walijipanga uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
“prrrrrrr” ilikuwa ni mlio wa filimbi ya muamuzi kuashiria mpira uanze na shule ya manjangu ndio walianzisha mpira huo ulioanza kwa kasi ya wachezaji wao, wachezaji wa timu ya manjangu wakionekana wako vizuri pia ukilinganisha na maumbo yao makubwa tofauti na wachezaji wa shule ya sekendari ya Mwanzini
Mpaka dakika ya arobaini na tano ya kipindi cha kwanza timu zote mbili zilichoshana nguvu kwa kutoka sare ya kutokufungana japokuwa timu wenyeji walionekana kutawaliwa kipindi cha kwanza.
“Poleni kwa mchezo, tuna mapungufu kwenye nafasi za ushambuliaji pia viungo mmepoteana na kusababisha kushambuliwa sana. Nitafanya mabadiliko kidogo kwenye nafasi ya ushambuliaji.” Aliongea mwalimu Adamu na kuwaruhusu kurudi uwanjani. Punde kipindi cha pili kilianza
Hamad!
Dakika ya sitini shule ya manjangu wanajipatia goli kutokana na mpira wa kona uliochongwa vizuri na kumkuta Bakari bila kuangalia goli aliutumbukiza nyavuni kwa kichwa maridadi. Mashabiki wa timu ya manjangu wanashangilia sana kwa goli hilo huku mashabiki wa timu ya Mwanzini wakiwa wanyonge ndani ya uwanja wao.
Dakika ya sabini na mbili timu zote zinafanya mabadiliko ya wachezaji huku timu wenyeji wakifanya mabadiliko ya wachezaji watatu kwa wakati mmoja wakiingiza washambuliaji wawili John na Steve pamoja na kiungo mmoja ambae Shabani mashabiki wa timu wenyeji walionekana kurudi kwa kushangilia baada ya mabadiloko hayo.
Inapigwa pasi maridadi kutoka kwa Steve inamkuta John ndani ya kumi na nane akibaki na kipa tu. “Prrrrrrrr” ni kipenga cha mwamuzi kuashiria ile ni penalt, ni baada ya John kuangushwa na golikipa baada ya kumpiga chenga, mashabiki wa Mwanzini wanaonekana kushangilia sana na penat inaenda kupigwa na Captain Abduli. Mwamuzi anaruhusu kwa filimbi penal ipigwe “Goooooooooooooal” ni kelele za mashabiki wa timu ya shule ya sekondari ya Mwanzin Abduli anaipatia timu yake bao la kusawazisha mnamo dakika ya themanini na tatu Mwanzin sekondari 1 na Manjangu sekondari 1.
Zimesalia dakika tatu mpira kuisha timu zote zikionekana kutawala mchezo kwa zamu, pasi inatoka kwake Petro inafika na kumkuta John, John anakokota mpira anapiga pasi inamkuta Steve “prrrrrr” Steve anachezewa madhambi karibu na penalt box inakua ni faulo kuelekea timu ya Manjangu zikiwa zimesalia sekunde kadhaa mpira kuisha. Anachukua John na kuutenga mpira kwaajili ya kupiga….. Mwamuzi anaruhusu mpira kupigwa na John anaupiga moja kwa moja “Goooooooooal” ni goli la pili kwa timu wenyeji linaloandikwa kupitia kwa mshambuliaji wao John, mashabiki wanaingia uwanjani kwa furaha.
Mpira unaekwa kati kwaajili ya kuanzishwa na hauchukui muda mwamuzi anamaliza mpira na timu wenyeji wanatoka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya timu ya Manjangu, John anaonekana akibebwa na wenzake juu juu kwa furaha.
“Hongera John” ilikuwa ni sauti ya Vanessa akimwambia John huku akimkumbatia kwa furaha kitendo hicho kilishuhudiwa na wanafunzi wengi, ilisikika sauti ikisema
“Nyie” sauti hiyo iliwafanya wawili hao kugeuka.
Je nini kitatokea? Kaa tayar kupata muendelezo usikose
****************************************
Itaendelea...Kesho(Ijumaa)
Toa maoni yako kwa kucomment au katika namba hizi 0659146373
Nisaidie kushare ili na wengine wapate kuisoma, pia usiache kulike na kucomment ikiwa k**a support yako kwangu.
Like page yetu Simulizi Za Kusisimua Tz