18/06/2026
HISTORIA YA TANTINE ABETI MASIKINI
L'HISTOIRE DE TANTINE ABETI MASIKINI
ABETI MASIKINI Taswira ya Malkia, Mwanzo wa Upekee na Dhamiri ya Mwanamke wa Bara
Akiwa amezaliwa k**a Élisabeth Finant, tarehe 9 Novemba 1954 huko Stanleyville (Kisangani), Mji uliokuwa ukipitia misukosuko ya Congo iliyokuwa ikijijenga upya? ABETI MASIKINI yeye huwekwa kwenye Group adimu sana la Wasanii ambao safari yao inavuka mipaka ya jukwaa la muziki na kujigeuza kuwa hadithi ya Taifa, Bendera ya utambulisho, Tamko la kisiasa.
Baba yake Mzee Jean‑Pierre Finant, Mwanasiasa mashuhuri na shujaa wa uhuru aliyeuawa mwaka 1961, ABETI MASIKINI kalelewa katika mazingira ambayo heshima, utamaduni, upinzani na ufahamu wa historia vilikuwa kitu kimoja.
Urithi huu ulimjengea imani ya kina : Sanaa sio burudani pekee, bali ni uwepo, ni madai, na njia ya kujidhihirisha mbele ya Dunia.
Utoto ulioumbwa na upotevu, nidhamu na nia
Akiwa yatima wa Baba akiwa na umri wa miaka saba, alilelewa na Mama yake Alphonsine, Mwanamke jasiri na mwenye nidhamu. aliyemfundisha aibu njema, bidii na uvumilivu.
Mapema sana, ABETI MASIKINI alionyesha uwezo wa sauti yake ya upekee, yenye joto, pana, inayobadilika, yenye uwezo wa kutoka katika upole wa utulivu hadi mwangwi mkali wa moto.
Akiwa kijana, alijaa mirindimo ya Jiji la Kinshasa, midundo ya Soukou, harmonia za Rumba, pamoja na ushawishi wa Muziki wa Waamerika Weusi uliokuwa k**a ushawishi mkubwa Barani Africa kwa miaka hiyo ya 1970.
Kuchanua kwa nyota: kuzaliwa kwa “ABETI MASIKINI”
Mwanzoni mwa miaka ya 1970, alichukua jina la kisanii ABETI MASIKINI, likawa k**a muunganiko wa kishairi uliogeuka kuwa alama.
Akawa muasisi wa Group lake (Les Redoutables), na akaweka mtindo mseto uliochanganya Rumba, Funk, Soul, na midundo ya jadi ulio ongozana na Ngoma za kisasa.
Uwepo wake jukwaani wa kuvutia, wa Kisanii, wa kiliturujia ulimtofautisha mara moja: Abeti hakuimba tu, aliishi muziki.
Mwaka 1973, akawa mmoja wa Wasanii wa kwanza kutoka Africa Kusini mwa Jangwa la Sahara kutumbuiza kwenye Ukumbi maarufu wa L’Olympia Jijini Paris, zoezi ambalo kalirudilia tena kwa mafaanikio kwenye miaka ya 1975 na 1986.
Show hizo, zilisifiwa sana na vyombo vya habari vya Ufaransa, hadi kupelekea kuliweka jina lake kwenye ramani ya dunia ya sauti kubwa za Afrika.
Kazi iliyoongozwa kwa ubunifu, nidhamu na ujasiri.
Akiwa mchapakazi asiyechoka, ABETI MASIKINI alikua Mwandishi, Mtunzi, Producer, Kiongozi wa Group lake, kajihusisha pia na kujadili mikataba, kadhalika na ubunifu wa mavazi yake.
Alikuwa miongoni mwa Wanawake wa kwanza kabisa wa Afrika ya Kati kuchukua uongozi kamili wa Kisanii, katika ulimwengu uliotawaliwa na Wanaume.
Baadhi ya kazi zake mashuhuri:
Je Suis Fâchée : (Tamko la nguvu ya Mwanamke)
Ngblimbo : (Mchanganyiko wa Ngoma za jadi na na midundo mpya)
Maïsha : (Matembezi ya ndani yenye uzito wa kipekee)
Je t’aime, je t’adore : (Wimbo uliotikisa Bara nzima).
Urithi wake wa muziki, wenye sura nyingi, ulizunguka mapambano, hisia, kiroho na utambulisho.
Mwanamke, mama, mpenzi
Nyuma ya diva mwenye mwanga mkali, alikuwepo mwanamke mwenye hisia nyeti sana.
ABETI MASIKINI aliishi maisha ya ndoa na Gérard Akueson, ambae alikua pia Producer na meneja mwenye ushawishi, ambao uwepo wake ulikuwa wa mapenzi, kazi na msingi wa safari yake.
Mama wa watoto wane, aliwalinda dhidi ya kelele za umaarufu, akileta uzazi wake katikati ya safari ndefu na zenye kuchosha.
Dhamiri ya Mwanamke kabla ya wakati wake
Kabla hotuba za ukombozi wa mwanamke hazijawa za kawaida, ABETI MASIKINI alikuwa tayari Mwanamke huru, mwenye mikakati, anayejitawala, anayekubali mwili wake, sauti yake, na ndoto zake.
Alifungua njia kwa vizazi vya Wasanii wa k**e wa Congo mfano wa akina Tshala Muana na Mbilia Bel ambao wote wanamtambua k**a Mwanzo wa mapinduzi.
Mwisho wa utawala, kuzaliwa kwa hadithi
Akiwa na saratani, alifariki 28 Septemba 1994 huko Paris, akiwa na umri wa miaka 39 pekee.
Kifo chake kilisababisha mshtuko mkubwa katika Afrika nzima hasa kwenye Inchi zinazo zungumza Kifaransa.
Lakini wahusika wakuu hawafi: hubadilika kuwa hadithi.
Hadi kwa leo hii, ABETI MASIKINI anabaki kuwa ikoni wa Utamaduni, Mwanzo wa jukwaa la kisasa, Sauti iliyofungua njia.
Hitimisho ABETI MASIKINI, Mwanamke aliyebadili jukwaa kuwa ufalme
Abeti Masikini hakuwahi kuwa Muimbaji pekee :
Alibuni nafasi,
Alifafanua upya uwepo wa Mwanamke,
Aliuweka Muziki wa Congo katika kisasa cha muziki wa Dunia.
Urithi wake ni wa mwanamke aliyekuja kutoka utoto uliojeruhiwa, na akajenga kazi ya kifalme, mitindo, mtazamo, na hadithi isiyofutika.
Version Française
ABETI MASIKINI Portrait d’une souveraine, pionnière absolue et conscience féminine du continent
Née Élisabeth Finant, le 9 novembre 1954 à Stanleyville l’actuelle Kisangani, cité traversée alors par les remous d’un Congo en pleine recomposition, ABETI MASIKINI appartient à cette caste rarissime d’artistes dont la trajectoire excède la simple scène musicale pour se muer en mythologie nationale, en étendard identitaire, en affirmation politique.
Fille de Jean‑Pierre Finant, figure politique majeure, martyr de l’indépendance exécuté en 1961, elle grandit dans une atmosphère où dignité, culture, résistance et conscience historique se confondent.
Cette filiation imprime en elle une conviction profonde : l’art n’est jamais un divertissement, mais une présence, une revendication, une manière d’exister face au monde.
Une enfance sculptée par la perte, la discipline et la volonté
Orpheline de père à sept ans, elle est élevée par Maman Alphonsine, femme de courage et de rigueur, qui lui transmet le sens de la pudeur, de l’effort et de la persévérance.
Très tôt, ABETI MASIKINI révèle une voix singulière, chaude, ample, modulée, capable de glisser de la douceur feutrée à l’éclat incandescent.
À l’adolescence, elle s’imprègne des rythmes urbains de Kinshasa, des cadences du soukou, des harmonies de la rumba, mais aussi des influences afro‑américaines qui traversent l’Afrique des années 1970.
L’éclosion d’une étoile : la naissance d’«ABETI MASIKINI»
Au début des années 1970, elle adopte le nom de scène ABETI MASIKINI contraction poétique devenue emblème.
Elle fonde son orchestre, Les Redoutables, et impose un style hybride où se croisent rumba, funk, soul, rythmes traditionnels et orchestrations modernes.
Sa présence scénique magnétique, théâtrale, presque liturgique la distingue immédiatement : ABETI MASIKINI ne chante pas, elle incarne.
En 1973, elle devient l’une des premières artistes d’Afrique subsaharienne à se produire à L’Olympia, exploit renouvelé en 1975 et 1986.
Ces passages, salués par la presse française, installent son nom dans la cartographie mondiale des grandes voix africaines.
Une carrière gouvernée par l’innovation, la rigueur et l’audace
Travailleuse infatigable, ABETI MASIKINI compose, écrit, chorégraphie, dirige son orchestre, négocie ses contrats, conçoit ses costumes.
Elle est l’une des premières femmes d’Afrique centrale à assumer une direction artistique totale, dans un univers dominé par les hommes.
Parmi ses œuvres marquantes :
Je Suis Fâchée : (Manifeste de puissance féminine)
Ngblimbo : (Fusion de rythmes traditionnels et modernité urbaine)
Maïsha : (Ballade introspective d’une intensité rare)
Je t’aime, je t’adore : (Succès continental)
Son répertoire, polymorphe, oscille entre engagement, sensualité, spiritualité et affirmation identitaire.
Une femme, une mère, une amoureuse
Derrière la diva flamboyante se cache une femme d’une grande sensibilité.
ABETI MASIKINI partagea sa vie avec Gérard Akueson, Producteur et Impresario influent, dont la présence fut à la fois passionnelle, professionnelle et fondatrice.
Mère de quatre enfants, qu’elle protège du tumulte médiatique, elle mène sa maternité dans les interstices de tournées harassantes. Cette tension nourrit une mélancolie discrète, perceptible dans ses ballades les plus profondes.
Une conscience féminine avant l’heure
Bien avant que les discours sur l’émancipation ne deviennent courants, Abeti incarne une femme libre, autonome, stratège, assumant son corps, sa voix, son ambition.
Elle ouvre la voie à des générations d’artistes congolaises de Tshala Muana à Mbilia Bel qui reconnaissent en elle une pionnière.
La fin d’un règne, la naissance d’un mythe
Atteinte d’un cancer, elle s’éteint le 28 septembre 1994 à Paris, à seulement 39 ans.
Sa disparition provoque une onde de choc dans toute l’Afrique francophone.
Mais les grandes figures ne meurent pas : elles se transfigurent.
Aujourd’hui encore, ABETI MASIKINI demeure une icône culturelle, une pionnière de la scène moderne, une voix qui a ouvert des brèches.
Conclusion ABETI MASIKINI, la femme qui transforma la scène en royaume
ABETI MASIKINI n’a pas seulement chanté :
Elle a inventé un espace,
Elle a redéfini la présence féminine,
Elle a inscrit le Congo dans la modernité musicale mondiale.
Son héritage est celui d’une femme partie d’une enfance meurtrie, qui a bâti une œuvre souveraine, une esthétique, une attitude, une légende.
BABA L.W.L