08/10/2026
Wakati Bilionea Wicknell Chivayo akiwa anaandaliwa kupelekwa katika nyumba yake ya milele, pamoja na mke wake na familia, nimegundua kitu kimoja kikubwa: umasikini ni kitu kibaya sana unapofika hatua ya kuharibu fikra za mtu.
Tofauti na picha nyingi tulizokuwa tunaona kwenye mitandao ya kijamii, maelfu ya Wazimbabwe walionekana kuomboleza, kujipanga barabarani na kushiriki katika kumuaga. Watumishi wa Mungu, waumini, wafanyabiashara na watu mbalimbali walijazana. Hapo nimeona kitu kimoja: nguvu ya uma na namna maisha ya mtu yanaweza kugusa watu wengi.
Na ukitazama safari yake ya kibiashara, Chivayo hakuwa mtu aliyefanikiwa kwa siku moja. Kampuni yake Intratrek ilihusishwa na Gwanda Solar Project ya 100MW, ambayo mkataba wake wa awali ulikuwa karibu US$172–173 million, na baadaye ukarekebishwa hadi takribani US$132 million. Pia biashara zake zilihusishwa na miradi mingine ya nishati k**a Munyati Power Station, takribani US$163 million, na Gairezi Hydroelectric Project, takribani US$128–131 million. Kwa ujumla, miradi ya nishati iliyohusishwa na kampuni zake Zimbabwe ilifikia thamani ya karibu US$1 billion.
Lakini niseme jambo moja muhimu: thamani ya mkataba si sawa na pesa alizokuwa nazo mfukoni au utajiri wake binafsi. Mikataba hiyo ina gharama za ujenzi, vifaa, wafanyakazi, financing na partners. Hakuna takwimu iliyokaguliwa hadharani inayothibitisha net worth yake halisi.
Nilichojifunza ni kwamba wakati mwingine mtu akiona mwingine amefanikiwa, badala ya kujiuliza, “Nifanye nini ili siku moja nami nifike pale?” anaweza kujiuliza, “Kwa nini yeye na si mimi?”
Na hapo ndipo tatizo linapoanzia.
Mafanikio ya mtu mwingine hayapaswi kuwa sababu ya chuki. Yanapaswa kuwa lesson, motivation na inspiration.
Usimchukie aliyekutangulia.
Jifunze kwake.
Jenga yako.
Tafuta njia yako.
Fanya kazi kwa bidii.
Maisha ni safari, si mashindano ya kumchukia aliyefika mbele yako.