Orginal Professor

Orginal Professor kurasa za orginal professor from songwe,mbozi,halambo

02/11/2023
08/07/2023

I have reached 500 followers! Thank you for your continued support. I could not have done it without each of you. 🙏🤗🎉

05/05/2023

😁😁😁😁😁

🛏️🛏️FAIDA YA KUFANYA MAPENZI AHSUBUHI🛏️Huwenda umeshawahi kusikia kuhusu umuhimu wa kushiriki tendo la ndoa asubuhi na u...
05/05/2023

🛏️🛏️FAIDA YA KUFANYA MAPENZI AHSUBUHI🛏️

Huwenda umeshawahi kusikia kuhusu umuhimu wa
kushiriki tendo la ndoa asubuhi na ukashangaa lakini ni kweli kuna faida za kufanya tendo hilo kwa afya yako na wataalamu wanasema ni moja wapo ya matibabu.

Tunakusogezea baadhi ya faida za kushiriki tendo la ndoa asubuhi kutokana na utafiti uliofanywa na Dr.Sudeshna.

Huimarisha kumbukumbu

Ngono asubuhi inaweza kusaidia ubongo wako kuwa na nguvu siku nzima na pia kukusaidia kuwa na kumbukumbu hivyo unashauriwa kushiriki kial upatapo nafasi.

Ni mazoezi tosha

Unapofanya ngono asubuhi ni k**a unafanya mazoezi kwani kuna kilo na mafuta yanapungua pindi unaposhiriki.

Huongeza kinga ya mwili

Ni vizuri kushiriki tendo la ndoa asubuhi kwani huongeza kinga za mwili sababu wakati wa tendo hilo mwili unazalisha antibodi ya IgA inayosaidia katika ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa.

Hukupa nguvu ya kazi

Baada ya tendo la ndoa mwili huwa mwepesi na tayari kwa ajili ya kufanya kazi na ndio maana mnashauri kabla hujaenda kazini ili usiende kuharibu kazi na kuonekana mvivu ni bora ukajamiiana.

Hizo ni baadhi za faida ya kushiriki tendo la ndoa asubuhi lakini unashauri uhakikishe kwamba hamtumii muda mrefu k**a ambavyo mngeweza kufanya usiku.

Doctor peter leader. Apdate

17/04/2022

UGONJWA WA PID:

PELVIC INFLAMMATIRY DISEASE PID.
Ugonjwa huu unafahamika k**a PID, ni maambukizi kwenye via vya uzazi wa mwanamke .

• PID ni miongoni kwa magonjwa hatari sana kwa mwanamke una madhara makubwa na unaambukizwa kwa njia ya kujamiiana.
Ugonjwa huu unaweza ukapelekea uharibifu mkubwa kwenye mfuko wa uzazi,mayai ,mirija ya uzazi au sehemu nyingine za uzazi wa mwanamke
Na pia Pid ni moja ya chanzo cha ugumba kwa mwanamke ambacho kinaweza kuzuilika.

•TAKWIMU ZINAONESHA
Kila mwaka,zaidi ya wanawake milioni moja nchini marekani wanapatwa na ugonjwa huu wa PID,
Matokeo yake zaidi ya wanawake 100000 wanakuwa wagumba kila mwaka.
Zaidi ya hayo idadi kubwa ya mimba zaidi ya 100000 inatungiwa kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy) inahusishwa na tatizo hilo la PID.
Kiwango kikubwa cha maambukizi ni kwa wasichana wadogo

•VISABABISHI VYA PID
Kwa kawaida mlango wa uzazi (cervix) inazuia bakteria ambao wameingia ukeni wasisambae sehemu zingine za ndani za uzazi
K**a mlango wa uzazi cervix umepatwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana k**a kisonono na/au clamydia
Mlango huo wa uzazi cervix unaathirika na unakuwa na uwezo mdogo
wa kuzuia kusambaa kwa bakteria sehemu za ndani za uzazi.
PID inatokea pale vimelea vya magonjwa vinaposafiri kutoka kwenye mlango wa uzazi cervix kwenda sehemu za juu za uzazi.
Aslimia 90 ya PID husababishwa na kutotibiwa ugonjwa wa kisonono na klamidia
Visababibishi vingine vya pid
👉Kutoa mimba
👉Kujifungua
👉Vipimo kwenye mlango wa uzazi

DALILI ZA PID
zinatofautiana,zinaweza kuwa zifuatazo
👉Maumivu ya tumbo sehemu ya chini au upande wa kulia
👉Kutokwa kwa uchafu ukeni usio wa kawaida wenye rangi ya kijani au ya njano na wakati mwingine una harufu isiyo ya kawaida
👉Kichefuchefu na kutapika
👉Maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Maumivu sehemu ya kulia upande wa juu wa tumbo.

MAMBO YANAYOWEZA KUMUWEKA HATARINI MWANAMKE KUPATA PID

Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinamuweka mwanamke katika hatari ya
kupata PID ni k**a vifuatavyo

1.Wanawake wenye magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana k**a kisonono na klaimidia wako hatarini sana kupata PID
2.Wanawake ambao waliwahi kupata PID wako hatarini kupata tena.

3. Wasichana wadogo wapo hatarini kupata PID kuliko wazee.

4.Wanawake wenye wapenzi wengi wako katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na PID.

Baadhi ya tafiti zinaeleza uoshaji wa uke unachangia kupata PID.Kuosha uke( Douching) kunaweza pelekea kusukuma bakteria sehemu za juu za via vya uzazi na kuzuia kutoka kwa uchafu ambao mwanamke angeweza kutumia k**a ishara ya kwenda kuonana na wataalamu wa Afya mapema.

MADHARA YA PID

Kutokea /kujirudia kwa PID kunaweza kusababisha
kutokea kuharibika mirija ya uzazi ambayo inaweza kupelekea
•Ugumba
•Mimba kutunga kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy)
•Maumivu makali kwenye shingo ya kizazi
Kati ya wanawake nane (8) wanaougua PID mmoja(1) unakuwa mgumba

JINSI YA KUJIKINGA NA PID

PID inaweza kuzuilika kabisa ,kisababishi kikubwa cha pid ni magonjwa ya zinaa Mambo ya kuzingatia ili uweze kujikinga na PID
•Epuka kufanya mapenzi na watu wengi
•Tumia njia za uzazi wa mpango(barrier) k**a kondomu
•Tumia spermicides kwa kila tendo la ndoa hata k**a unameza vidonge vya uzazi
•Usitumie IUDs k**a unawapenzi wengi.
Note
IUDs ni vitu vinavyowekwa ndani ya uke kuzuia mimba
•Wahi matibabu ukiona dalili zozote za PID au za magonjwa ya zinaa k**a kuto=
kwa na uchafu usio wa kawaida ukeni,maumivu kiunoni nk
•Pia fanya uchunguzi wa afya ya uzazi mara kwa mara ili k**a kuna tatizo ligundulike na litibiwe kabla halijasambaa kwenda kwenye viungo vya ndani vya uzazi

Kwa kupata tibalishe itakayokuponya moja kwa moja .

Tuma neno AFYA kwenda /whatsApp
no: 0653720341

25/02/2022
ᴋᴡᴇɴʏᴇ ɴᴇᴛᴡᴏʀᴋ ᴍᴀʀᴋᴇᴛɪɴɢ ᴋᴜɴᴀ ᴡᴀᴛᴜ ᴡᴀɴᴀʜɪꜱɪ ᴛᴜɴᴀᴡᴀʟᴀᴢɪᴍɪꜱʜᴀ ɴᴏ🖐️ ʜᴀᴛᴜᴡᴀʟᴀᴢɪᴍɪꜱʜɪ ᴡᴀᴛᴜ ᴋᴜᴊᴏɪɴ 😇🤞ɴᴀ ᴡᴀʟᴀ ʜᴀᴛᴜʙᴇᴍʙᴇʟᴇᴢɪ ɴɪ ...
26/10/2021

ᴋᴡᴇɴʏᴇ ɴᴇᴛᴡᴏʀᴋ ᴍᴀʀᴋᴇᴛɪɴɢ ᴋᴜɴᴀ ᴡᴀᴛᴜ ᴡᴀɴᴀʜɪꜱɪ ᴛᴜɴᴀᴡᴀʟᴀᴢɪᴍɪꜱʜᴀ ɴᴏ🖐️ ʜᴀᴛᴜᴡᴀʟᴀᴢɪᴍɪꜱʜɪ ᴡᴀᴛᴜ ᴋᴜᴊᴏɪɴ 😇🤞ɴᴀ ᴡᴀʟᴀ ʜᴀᴛᴜʙᴇᴍʙᴇʟᴇᴢɪ ɴɪ ᴋᴜᴋuᴘᴀ ꜰᴜʀꜱᴀ ᴛᴜ ɴᴅᴜɢᴜ ʏᴀɴɢᴜ 🫂ɪᴋɪᴡᴀ ᴜᴛᴀᴄʜᴜᴋᴜᴀ ꜰᴀɪᴅᴀ ɪᴛᴀᴋᴜᴡᴀ ᴜᴘᴀɴᴅᴇ ᴡᴀᴋᴏ ɪʟᴀ ❤️✍️ᴘɪᴀ ᴜᴋɪᴋᴀᴛᴀᴀ ᴍᴛᴜ ᴍᴡɪɴɢɪɴᴇ ᴀᴛᴀᴄʜᴜᴋᴜᴀ ꜰᴜʀꜱᴀ ✍️ɴᴀᴊᴜᴀ ʜᴀɪᴡᴇᴢᴇᴋᴀɴ ᴡᴏᴛᴇ ᴛᴜᴋᴀꜰᴀɴʏᴀ ɴᴇᴛᴡᴏʀᴋ ᴍᴀʀᴋᴇᴛɪɴɢ ✍️ɪʟᴀ ᴋᴀᴍᴀ ᴜɴᴀᴜᴡᴇᴢᴏ ᴡᴀ ᴋᴜɪꜰᴀɴʏᴀ ɴɪɴɪ ᴋɪɴᴀᴋᴜᴢᴜɪᴀ ʜɪɪ ᴀɢᴇ ꜱɪᴏ ʏᴀ ᴋᴜᴛᴀᴘᴇʟɪᴡᴀ ɴᴀ ᴀᴋɪʟɪ ᴢᴀᴋᴏ ᴢᴏᴛᴇ 🤔ᴅᴏɴᴛ ʟɪꜱᴛᴇɴ ᴛᴏ ʏᴏᴜʀ ʙʀᴏᴋᴇ ꜰʀɪᴇɴᴅ ᴀɴᴀᴇ ᴋᴡᴀᴍʙɪᴀ ᴛʜɪꜱ ᴛʜɪɴɢꜱ ɪꜱ ɴᴏᴛ ʀᴇᴀʟ muepuke🖐️ᴍᴀɪꜱʜᴀ ɴɪ ʏᴀᴋᴏ ᴊᴜᴋᴜᴍ ʟᴀᴋᴏ🧐ᴡᴀᴋᴀᴛ ᴜᴋɪᴜᴘᴏᴛᴇᴢᴀ ʜᴀᴜᴡᴇᴢɪ ᴋᴜᴜRᴜᴅɪꜱʜᴀ ᴛᴇɴᴀ ꜱᴏ ꜰᴀɴʏᴀ ᴍᴀᴀᴍᴜᴢɪ ꜱᴀʜɪʜɪ ʜᴜᴜ ɴɪ ᴋᴀᴍᴀ ᴜꜱʜᴀᴜʀ ᴛᴜ. Ofisi zipo TUNDUMA, SONGWE +255710013986 *MWAMBIE MWENZIO*

20/10/2021

P.I.D NI NINI? NA MADHARA YAKE KATIKA VIA VYA UZAZI WA MWANAMKE.

NA Dr. Peter Leader,

Ndugu msomaji nimeamua kulitoa somo hili kwa upana zaidi na kwa kulichanganua ili kila mmoja apate kuelewa kuwa PID ni nini, ina dalili gani, na madhara gani!

Kwanza neno PID ni neno la kiingereza ambalo kirefu chake ni “Pelvic Inflammatory Disease”, ambalo kwa Kiswahili maana yake ni maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi.

Maambukizi katika via vya uzazi kwa kawaida hujulikana k**a PID, ni maambuki yanayoathiri viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hakika hutokana na mchanganyiko mbalimbali wa magonjwa ya zinaa, hasa yaliyosababishwa na bacteria wa Pangusa(Chlamydia) au kisonono. Ugonjwa wa PID unapokaa muda mrefu bila kutibiwa, unaweza kusababisha uharibifu mkubwa usiobadirika katika mfumo wa uzazi wa mwanamke, hasa katika mfuko wa kizazi(uterus), vifuko vya mayai(Ovaries), na mirija ya mayai(fallopian tubes).

Ugonjwa huu unapokaa muda mrefu bila kutibiwa humfanya mwanamke kupatwa na ugumba. Inaonyesha asilimia kubwa leo katika jamii, wanawake wengi wamekuwa wakisumbuka na ugonjwa huu.

Je, Nini Kinachosababisha Ugonjwa Huu Wa PID?





Ugonjwa wa kisonono pamoja na Pangusa(Chlamydia) ndio vyanzo vikuu vya maambukizi katika via vya uzazi wa mwanamke.

Mwili wa mawanamke unapokuwa na afya kamili, mlango wa kizazi huwa na nguvu ya kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.

Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa kuingia, hasa kisonono na pangusa, mlango wa kizazi hupata maambukizi na kisha hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bacteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi.



Je, Jinsi Gani PID inavyokupata?



Japo inakuwa tayari imesababishwa na magonjwa mengine ya zinaa, PID huambukizwa kwa urahisi ikiwa k**a mtu atashindwa kufuata njia za kuepukana na mienendo ama tabia mbaya. Hapa kuna mambo ambayo huwafanya wanawake kupatwa na tatizo hili kwa urahisi sana, nazo ziko k**a ifuatavyo:

Kuwa na wapenzi wengi ama kutoka nje ya ndoa
Kuanza mambo ya mapenzi mapema hasa chini ya miaka 25
Kupiga bomba ukeni yaweza kusaidia vimelea kuingia ndani na kusababisha maambukizi katika viungo vya uzazi


Je, Nini Dalili Za Ugonjwa Wa PID?





K**a ilivyo katika magonjwa mengi ya zinaa, PID inaweza kuendelea kwa kuonyesha dalili za kawaida ama kutokuonyesha dalili zozote. Hali hii yaonyesha kuwa ni vyema sana kufanya uchunguzi wa vipimo mara kwa mara kwa daktari. K**a PID ikianza kuonyesha dalili zozote, zaweza kuwa k**a ifuatavyo;

Maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
Kutokwa na uchafu ukeni, hasa wenye rangi ya njano unaoelekea kuwa kijani kwa mbali ukiwa na harufu mbaya.
Kuhisi Maumivu ama hali ya kuungua wakati wa kukojoa
Homa
Kuhisi kichefuchefu ama kutapika
Kuhisi Maumivu wakati wa tendo la ndoa ama kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
Kupata hedhi katikati ya hedhi, yaani waweza kupata hedhi mara 2 ndani ya mwezi 1.


Je, Unawezaje Kutambua Kuwa una PID?



Kadri inavyoonyesha kuwa huna dalili zozote za PID, ni vyema kila mara kwenda katika zahanati ama hospitali ili kupata vipimo kuweza kukuhakikishia kuwa uko salama, na hauna maambukizi yoyote ya zinaa.

Wanawake wadogo chini ya umri wa miaka 25, mara nyingi wanapatwa na janga la maambukizi haya kwa urahisi, na inafaa wapate vipimo angalau hata mara moja kwa mwaka. Pia unapoona dalili zozote tofauti, naomba usisite kufika hospitalini ili kufanya uchunguzi na kuhakiki tatizo lako.






Hakuna kipimo maalumu cha PID, lakini hata hivyo daktari anaweza kupima maambukizi kwa kuchukua vitu vinavyotoka ukeni, ama mkojo. Vipimo hivi hupelekwa maabara kwa ajili ya uchunguzi ambao hubaini kuwa huenda una vimelea wanaosababisha maambukizi. Ikiwa k**a daktari atakuwa amefikiria tu ama kudhania, unaweza kuambiwa uende ukapate vipimo vingine zaidi, vikiwemo;

Vipimo vya Ultrasound ambavyo hurusu kuona picha ya viungo vyako vya uzazi kwa kutumia sauti za mawimbi.
Kipimo cha Endometrial biopsy, ambacho kinamaanisha kuwa kwamba daktari wako atachukua ute ute kidogo kutoka ndani ya uke kwa ajili ya upimaji mwingine zaidi.
Kipimo kupitia kifaa cha kuingiza ndani ya uke.


Je, Maambukizi Ya PID Yanaweza Kupona?



Ni vyema kufanya vipimo na kuanza matibabu mapema kadri iwezekanavyo. Vinginevy PID inaweza kuendelea na kukomaa na kusababisha madhara makubwa katika mfumo wa uzazi ambayo yaweza kushindwa kutibika. Lakini uanzapo kufanya matibabu yafaa pia hata mwenzi wako apate matibabu japo hajaonyesha dalili zozote. Ikiwa k**a hatapata matibabu, anaweza kukufanya upate tena maambukizi mara unaporudi kufanya mapenzi na yeye. Hakikisha pia unamaliza matibabu yako kulingana na maelekezo ya tabibu wako ijapokuwa unaona dalili za maambukizi zinatoweka. Kumbuka pia unapotumia vidonge kwa muda mrefu na vikashindwa kukusaidia, PID huzidi kukua na kusababisha majipu ndani ya uzazi ambayo humfanya mgonjwa kutokwa na vitu k**a usaha ukeni. Hali hii yaweza kusababisha madhara makubwa hasa katika vifuko vya mayai na kwenye mirija ya uzazi pia.



Je, Ugonjwa Huu Waweza Kutibika?



PID inapona kwa kutumia tiba za asili zenye uwezo wa antibiotic tu. Hata hivyo inafaa ieleweke kuwa upatikanaji wa tatizo hili hutegemeana na jinsi gani PID imeharibu mwili wako. Ikiwa k**a mgonjwa kawahi kupata vipimo na kuanza matibabu, basi uponaji wake utakuwa ni wa haraka pia. Lakini k**a tatizo litadumu muda mrefu, linaweza kusababisha madhara makubwa hasa ugumba kwa mwanamke.

Jinsi Gani Unaweza kuepukana na PID?



Asilimia 90% ya maambukizi katika via vya uzazi(PID) husababishwa na Kisonono pamoja na Pangusa(Chlamydia). K**a ilivyo magonjwa mengine ya zinaa, mara nyingi huambikizwa kwa njia ya kujamiiana. Japo kuepukana na maambukizi ya PID unashauriwa kuwa na mpenzi mmoja unayemwamini na kutumia Kondom wakati unapofanya tendo la ndoa. K**a nilivyosema awali pia, kuwa yafaa kutembelea katika vituo vya afya mara kwa mara ili kuhakiki afya yako. Hata k**a umeshawahi kupata aina moja ya ugonjwa wa zinaa, bado inachukua mpaka kufikia kuwa PID, hivyo unapokuwa na mazoea ya kufanya uchunguzi wa vipimo kwa ajili ya afya yako, yaweza kukusaidia kujikinga na tatizo la PID.

Je, PID inaweza Kusababisha Nini?



Unapofanya vipimo na kuanza matibabu mapema, PID haiwezi kusababisha madhara yoyote mwilini mwako. Hata hivyo, ikiwa k**a utazembea na kuliacha tatizo hili likakaa kwa muda mrefu, PID inaweza kusababisha madhara yafuatayo;

Maumivu ya nyonga ama tumbo ya mara kwa mara, hasa wakati wa tendo la ndoa ama kipindi cha upevushaji mayai, kutokana na majeraha yanayokuwa katika mirija ya uzazi.
Kusababisha majeraha ndani na nje ya mirija ya uzazi ambayo hupelekea mirija kuziba.
Kubeba mimba nje ya kizazi. Yai lililorutubishwa hushindwa kufika kwenye mji wa uzazi kupitia mirija ya uzazi. Hali hii inaweza kumfanya mwanamke kuvuja damu nyingi sana.
Ugumba kwa mwanamke: PID inapokuwa sugu humfanya mwanamke kushindwa kushika ujauzito.


Je, Wawezaje Kuiondoa PID?

Ndio unaweza K**a kweli unahitaji kupona na kurudisha fraha ya ndoa yako.

By Doctor Peter Leader

Magonjwa Ya Maungio Ya Mifupa (Arthritis)ugonjwa wa joints-arthritis Leo tutazungumzia tatizo linalowapata watu wengi sa...
22/09/2021

Magonjwa Ya Maungio Ya Mifupa (Arthritis)
ugonjwa wa joints-arthritis



Leo tutazungumzia tatizo linalowapata watu wengi sana pale umri wao unapokuwa umezidi miaka 50 na hasa wale wenye miili mikubwa. Nina uhakika kuwa umewaona akina mama wenye umri mkubwa na miili mikubwa wanavyopata shida kutembea huku wakiinama toka upande mmoja hadi mwingine kila wakipiga hatua au shida wanayopata pale inapowabidi kupanda ngazi au kukuchuchumaa. Maneno k**a “ugonjwa wa kuumwa joints, nina tatizo la joints, maumivu ya joints” na maumivu ya mifupa umeyasikia mara nyingi. Tatizo hasa hapa ni nini? Ungana nami katika mada hii uujue ugonjwa huu wa arthritis.



Ugonjwa Wa Arthritis Ni Nini?


Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna yo yote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo. Neno arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla yapo zaidi ya 100. Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.



Chanzo Cha Arthritis Ni Nini?


Kusudi kuelewa chanzo cha ugonjwa huu, hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana. Fikiria goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:



maungio ya mifupa



Ligaments: Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni k**a utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.

Cartilage: Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.

Capsule: Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna ukano (synovial fluid) ambao huzalishwa na synovial membrane. Ukano ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.



Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yo yote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa gegedu inalika, upungufu wa ukano (synovial fluid), maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.



Aina Za Ugonjwa Wa Joints-Arthritis


K**a nilivyoeleza hapo juu, kuna aina zaidi ya 100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis. Katika mada yetu ya leo tutatazama aina k**a nne hivi za ugonjwa huu, tukielezea chanzo cha kila aina.

Osteoarthritis: Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa. Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka. Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber). Cartilage hii inapopoteza ubora wake, tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu. Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea, mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana.

Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka na muda. Kutaanza kutokea maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu. Joints zitakaza, hasa mapema asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida. Siku zinavyosogea ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako. Mara nyingine utaona uvimbe kwenye joint. Osteoarthritis hushambulia zaidi nyonga, mikono, magoti na uti wa mgongo.

Rheumatoid arthritis: Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili kwa bahati mbaya kuanza kushambulia viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu. Hali hii isipodhibitiwa, huweza kusababisha ulemavu. Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho, ngozi, mapafu, midomo, damu na mishipa ya damu. Huu ni ugonjwa ambao zaidi ni wa wanawake na huwatokea zaidi wawapo kati ya umri wa miaka 40 hadi 60. Mgonjwa atasikia maumivu na kuona uvimbe kwenye joints za pande zote za mwili, yaani k**a ni magoti, yote mawili la kulia na la kushoto, yote yatashambuliwa. Viungo vinavyoshambuliwa zaidi ni vidole, viwiko vya mikono na miguu.

ugonjwa wa joints-Rheumatoid Arthritis

Athari zake huonekana zaidi asubuhi unapoamka na maumivu yanaweza kudumu kwa muda wa hadi nusu saa. Muathirika wa ugonjwa huu hujisikia mchovu muda wote, hukosa hamu ya kula na hupungua uzito.

Ugonjwa katika hatua zake za baadaye huleta matatizo katika viungo vyote vya mwili. Matatizo yanayoweza kujitokeza ugonjwa ukikua ni k**a yafuatayo:

– Macho. Ukavu, maumivu, wekundu, kutopenda mwanga na kutoona vizuri
– Midomo. Ukavu, maumivu na maambukizi ya fizi
– Ngozi. Vijinundu chini ya ngozi kwenye maeneo yenye mifupa
– Mapafu. Kushindwa kupumua vizuri
– Mishipa Ya Damu. Uharibifu wa mishipa ya damu
– Damu. Upungufu wa chembechembe nyekundu za damu

Infectious arthritis (septic arthritic): Aina hii ya arthritis inatokana na maambukizi ya bacteria kwenye synovial fluid. Maambukizi haya yanaweza kuwa pia ni ya fungus au virusi. Wadudu kutoka sehemu nyingine ya mwili iliyo karibu na maungio ya mifupa huweza kusambaa kupitia mfumo wa damu hadi kwenye joint na kuleta maambukizi. Mara nyingi mtu mwenye aina nyingine ya arthritis ndiye anayepata maambukizi ya namna hii. Mgonjwa ataanza kwanza kupata homa, maumivu na uvimbe kwenye joint. Maeneo ambayo hushambuliwa zaidi na aina hii ya arthritis ni goti, mabega, kiwiko cha mkono, kiganja (wrist) na vidole na mara nyingi ni eneo moja tu ndilo litakaloshambuliwa.

Juvenile rheumatoid arthritis (JRA): Juvenile rheumatoid arthritis (JRA) ni ugonjwa ambao huwapata zaidi vijana walio na umri ulio chini ya miaka 16 na unakuja kwa namna nyingi. Kuna aina kuu tatu za ugonjwa huu:

1. Pauciarticular JRA, huu ndiyo unaoonekana zaidi na hauna madhara makubwa ukilinganisha na aina nyingine. Mtoto atasikia maumivu kwenye joints zinazofikia nne.

2. Polyarticular JRA, huu hushambulia joints nyingi zaidi, zaidi ya nne na maumivu yake ni makali zaidi. Kadri siku zinavyoongezeka, ndivyo maumivu yatakavyozidi.

3. Systemic JRA, huu huonekana kwa nadra ambapo maumivu hujitokeza kwenye maeneo mengi na madhara yake kuwa makubwa zaidi.

Mtoto ataanza kusikia homa za vipindi ambapo huzidi zaidi nyakati za jioni. Hali hii inaweza kumtokea mtoto kwa muda mfupi au kwa wengine kwa muda mrefu sana . Mtoto atapata mauvimu kwenye maungio ya mifupa (joints), uvimbe kwenye maungio hayo na kukak**aa kwa viungo. Mtoto huyu atakosa hamu ya kula hivyo kumfanya akonde. Ugonjwa ukizidi, mtoto anaweza kudumaa (kushindwa kukua), ukuaji wa mifupa yake kuathirika na kupata matatizo ya macho (uveitis).

Kwa sababu ya urefu wa mada hii, leo tutaishia hapa na katika muendelezo wake katika ukurasa nyingine tutaujadili ugonjwa wa gout na Tiba Za Magonjwa Ya Joints. Tunaomba maoni yako kuhusu mada hii na usisite vilevile kuuliza maswali uliyo nayo. Tutafurahi sana kupata mchango wako au kuona tumekujibu vizuri maswali yako.

https://youtu.be/R1EuNPDgH-Q
29/08/2021

https://youtu.be/R1EuNPDgH-Q

huyu ndie mwanadada anae_Trend sana mitandaoni akihitaji kuolewa hata na mwanaume anaepumua tu na yeye ajisikie ana mme na pia apate mtoto, anaumia sana miak...

Sapoti yenu ya mhimu sana kwenye channel hii kusubscribe na kuendelea kutaza apdate zote ambazo unasogezewa kila mda,👇👇👇...
25/08/2021

Sapoti yenu ya mhimu sana kwenye channel hii kusubscribe na kuendelea kutaza apdate zote ambazo unasogezewa kila mda,

👇👇👇
Msaada wa kushare ili tupate wafuatiaji kuanzia 1000 na kuendelea Asanteni

29/06/2021

*TATIZO LA UKE MKAVU KWA WANAWAKE NA TIBA YAKE*

Na, Doctor Peter Leader.

Uke mkavu; Ni tatizo ambalo husababishwa na upungufu wa homoni au kutokuwa na uwiano mzuri wa homoni ya estrogen ambayo hupelekea misuli ya uke kusinyaa na kukosa vilainishi.
Kwa kawaida uke unatakiwa kuwa na ute wa wastani ambao hufanya uke kubana kuleta joto na raha ya tendo la ndoa. Ute huo ukizidi sana au kuwa pungufu sana nalo ni tatizo.

VISABABISHI VYA UKE KUWA MKAVU ÷ √. Upungufu mkubwa wa homoni ya ESTROGEN
√.Ukosefu wa vitamin muhimu mwilini (vitamin C&E)
√.Utumiaji mafuta ama lotion zenye viambato vyenye kemikali kali (hydroquinone)
√.Magonjwa ya zinaa k**a kisonono, gonorhea na clamydia.
√.Matumizi ya sabuni za ant-bacteria kusafishia uke
√.Kuugua mara kwa mara fangasi, UTI na PID. √.Woga na wasiwasi (sexual anxiety)
√.Upungufu wa madini muhimu mwilini k**a zinki, calcium, potassium nk.

DALILI ZA UKE MKAVU
>Maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa.
>Kupungua ama kukosa
hamu ya tendo la ndoa.
>Kutofurahia tendo la ndoa kutokana na maumivu.
>Kuwa na ngozi kavu
>Maumivu ya mifupa >kusongwa na msongo wa mawazo (stress)
>Mzunguko wa hedhi kubadilika badilika kila mwezi.

MATIBABU YA UKE MKAVU
Kuna tibalishe (food supplements) maalum za asili 100% zinazotokana na mimea, matunda na mboga mboga ambazo zimetengenezwa kitaalam kwa kuzingatia mlo kamili na rafiki katika kurekebisha matatizo yote ya uke mkavu, tatizo la homoni na tatizo la uzazi kwa ujumla.

Tibalishe zetu zote zimethibitishwa na TMDA na TBS hivyo ni salama kwa Matumizi ya binadamu katika kutibu matatizo hayo.

By: Doctor Peter Leader

Address

Ichenjezya
Vwawa
342

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Orginal Professor posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share