11/08/2026
SALAMU ZA POLE
“Bwana ndiye aliyetupa, na Bwana ndiye aliyetwaa; jina la Bwana libarikiwe.”
— Ayubu 1:21
Tunatoa pole na rambirambi zetu za dhati kwa Mchungaji wetu MCH. PETER SUBI , familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao, Mama yake ESTER MBALU NKILA.
Katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, tunaungana nanyi katika huzuni na maombi. Tunamuomba Mungu awape faraja, nguvu, uvumilivu na amani katika kipindi hiki cha majaribu.
Tunamshukuru Mungu kwa maisha ya Mama yetu mpendwa na kwa kila jambo jema alilolitenda katika maisha yake.
“Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa.”
— Ufunuo 14:13
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, na awatie nguvu wafiwa wote.
POLE SANA MCHUNGAJI WETU.
MUNGU YUKO PAMOJA NANYI.