23/07/2026
Mamlaka za afya nchini Ufaransa zimesema watu 5,764 wamefariki dunia kutokana na athari za wimbi kubwa la joto lililoikumba nchi hiyo huku vifo hivyo vikirekodiwa kati ya Juni 17 na Julai 2 mwaka huu.
Joto hilo limeathiri maeneo mbalimbali na kuongeza hatari kwa makundi yenye afya dhaifu hasa wazee na wenye magonjwa sugu.
Wataalamu wa hali ya hewa wanasema kuongezeka kwa mawimbi ya joto na matukio mengine ya hali mbaya ya hewa kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za binadamu, hususan uzalishaji wa gesi chafuzi unaochochea mabadiliko ya tabianchi.
Wamezitaka nchi kuimarisha hatua za kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa na kujiandaa zaidi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.