23/10/2015
SAKATA LA KUSHUSHWA BEI YA FILAMU.
BAADHI YA VIONGOZI SHIRIKISHO NA VYAMA HATIJIELEWI.
Nawakumbiusja tu "k**a siyo TATUZI basi tambua wewe ni sehemu ya TATIZO "
BIBILIA Inasema ni kheri kuwa MOTO au BARIDI kuliko kuwa. Vugu vugu.
Niliwahi kuweka ujumbe kwenye baadhi ya mitadao ya kijamii kuashiria sumu inayoweza kutudhuru katika harakati zetu huku tukiamini SHIRIKISHO ndiyo kimbilio letu tusiokuwa na kwa kukimbilia.
Kwa namna nyingine taarifa yangu ilipingwa kuonyesha ilikuwa tofauti na maamuzi ya bodi .
Lakini kutokana na misimamo yangu na pita pita zangu pamoja na kilichotokea leo ni wazi kuwa msimamo wa BODI yetu ya SHIRIKISHO umegawanyika k**a si kututenga kabisa.
Kitendo cha JOHN LISTER kushiriki kwa uwazi kabisa kuunga mkono harakati za upande unao ongozwa na STEPS huku akijijuwa wazi kuwa yeye ni mjumbe wa BODI ya SHIRIKISHO iliyoweka msimamo wake wazi kwamba isingependa kuingiza misimamo yake katika jambo hili.
Wakati RAIS Simon Mwakifwamba akizuiwa kulizungumzia jambo hili bila kujali kwamba ,ukiachilia mbali dhamana aliyonayo yeye ni binaadamu mwenye matashi na hisia kutokana na kuwa mdau wa muda mrefu kwenye industrie hii .
Lakini pia hata upande ambao tuliuona walau una baraka za shirikisho hatukuona hata Kiongozi mmoja kushiriki vita hii hadharani licha ya kumkataza Rais Simon Mwakifwamba lakini hata wajumbe nao walikataa kushiriki kabisa kwa kuhofia kulichafua shirikisho letu pendwa .
Pamoja na mimi kufahamu wazi msimamo wa baadhi ya wajumbe wengine kuwa msimamo wao ni kuunga mkono hoja za Steps kwa dhahiri.
Je ni kipi kilijiri mpaka Mjumbe wa BODI JOHN LISTER kuamua kuishiriki vita hii hadharani ?
Pamoja na kuuweka siri msimamo wa SHIRIKISHO mnataka tuamini Huu ndiyo ulikuwa msimamo wa SHIRIKISHO ?
K**a lilikuwa na haja ya kutenda haki kwa pande zote kwa kuwa ni mzazi lilishindwa nini basi kuwa achia viongozi wake kila mmoja achague upande anaoutaka yeye kwa sababu ni haki yake kuamini hivyo ?
Wadau wenzangu wa Team wazalendo tunahitaji kujipanga sana , Lakini pia tunalitazamaje suala la bodi ,John Lister na maamuzi ya kumzuia mwaki huku baadhi ya waliomzuia tukiwaona wakifanya yao .
Je haiwezi ikawa hii ndiyo ilikuwa sababu ya kumzuia ili kulinda maslahi ya upande wa pili ?