23/12/2025
SIMULIZI: MVUJA JASHO
MTUNZI: DANIFORDY BEN
MAWASILIANO: +255711444410
SEHEMU YA 03
TULIISHIA.
Jerinda amempeleka sofania maeneo ya fordy bar baada ya kuagizwa na mama zurufa. Je ni mzigo gani anaufikisha eneo hilo kwa ujira mrefu?
SASA TUENDELEE.
Ama hakika waghani lugha hawakukosea kusema sura siyo roho, furaha ya sofania ni kupita na kuingia sehemu ghari k**a zile ambazo aliziona kwa mbali wakati wa matembezi. Furaha yake ilimkumbusha kila muda sura ya mama zurfa ambaye kwake ama hakika alikuwa mwema kila sekunde ubongoni mwake. Hakuna hata thumuni ya kosa ingethubutu kuchafua wema wa mama zurufa kwa sofania. Jerinda alitoa maelekezo ya ishara tu kumtambulisha sofania, k**a vile wapiga debe wafanyavyo stendi kwa ile kauli yao ya kusema hii ni namba yangu nimeichora kuashiria kuwa wammpigia debe mteja. Sofania hakutambua chochote kilichokuwa kikiendelea kwake, zaidi alipewa maelekezo ya kukaa katika kiti moja wapo ndani ya saloon ile iliyojazwa nakshi haswa.
Upambaji ulianza kwa binti yule ambaye alikuwa amebuka na maisha ya ufukara, licha ya kuoga kila siku lakini haikufanya apendeze kwa muonekano wake. Hivyo ilifaa apendezeshwe zaidi ili tu kufanania na kazi aliyokuwa akiifanya. Dakika za kuhesabu muonekano wake ulianza kubadirika na urembo wake ukaanza kujidhihirisha wazi. Wakati huo jerinda alikuwa ametoka na kujipakia katika gari lake na kuondoka, kabla ya muda mchache kurejea akiwa na mifuko miwili ambayo alifika na kuiweka katika kiti kisha akawaeleza wahudumu wale kuwa ni kwaajiri ya sofania na kumkabidhi begi ambalo aliambiwa anapaswa kulilinda sana, kisha akamwambia anamsubiri garini. Punde tu baada ya kumaliza kumremba sofania akarembeka ndipo walipomkabidhi mifuko ile na kumuelekeza mahali pa kwenda nayo. Ilikuwa ni mifuko yenye nguo ghari sana, nguo ambazo alipaswa kuzivaa kwa muda huu, amahakika zilikuwa zimempendeza ila tu. Hofu ilikuwa dhidi yake kwa muonekano ule wa suruali pekee kutembea nayo maana hakuwahi kabisa kuvaa hivyo.
Ila haikuwa na namna ilimlazimu, ijapo roho yake ilikuwa ikisita sana akaihisi kuwa uvaaji huo ni nje ya maadili aliyofunzwa, sofania alitoka ndani mule akiwa mtu mwingine kabisa. Alikabidhiwa begi lake na kisha safari ikaanza kulifuata gari, hakika alibadirika haswa hali iliyomfanya mpaka jerinda kuduwazwa na muonekano ule ambao hakuwa ameutegemea kabisa.
"You look great". Alizungumza jerinda na kumuacha sofania akiwa anatabasamu tu, asijue nini maana ya kile alichokuwa ameambiwa.
Jerinda aliwasha gari na kulisogeza mita kadhaa hapa ilikuwa ni nje kabisa ya fordy bar, mahali ambapo ndipo alipaswa kuupeleka mzigo ule ambao hakuwa akijua ni nini haswa kilichokuwa ndani yake. Alipewa maelezo nini akifanya pindi aingiapo ndani mule na ni code gani azitaje, hivyo hakuwa na muda wa kusubiri alitekeleza alichoambiwa na hatimaye baada ya kukamilisha biashara ile aliyoambiwa, alitoka akiwa amebarisha lile begi la mwanzo na kuwa na jingine jeusi la lezzer, hili lilikuwa zito kiasi lakini kwa masharti aliyopewa ndivyo ilibidi afuate, hakupaswa kufungua kabisa mzigo huo. Alirudi garini na jerinda akalichapa gear kuelekea kwa mama zulfa, lakini sasa haikuwa dukani pale tena zaidi sasa mwelekeo ulikuwa nyumbani.
Mbele ya uzio mkubwa wa jumba la kifahari kulipambwa na madhari nzuri sana, juu ya kuta za fensi kulikuwa na uzio wa umeme, na kwa mbali ungetazama kwa nje jengo hili lilikuwa la ghorofa. Muda wote sofania alikuwa kimya tu akijikagua kagua namna alivyokuwa amependeza siku hii hata hakuwa na umakini wa safari ni wapi ametoka na wapi aendako. Zaidi alish*tushwa ghafla na ulio mkali wa honi, yes ni nukta chache geti likasogea upande wa kulia taratibu na gari lao likaanza kuingia ndani ya mji ule wa gharama ya juu, ughari wa jumba lililokuwa mbele ya macho ya sofania ulijaza maswali lukuki unongoni mwake, kwa ile wazawazua ninani aishiye humo ndani.
Gari liliendeshwa taratibu na kupaki upande wa kulia wa jengo hili na jerinda ndiye alikuwa wa kwanza kushuka, kabla ya sofania kufuata. Sofania kila kitu kilimshangaza hasa pale alipokuwa akishangaa geti lililokuwa likijifunga pasi kuwapo mtu, hakika kwake hii aliona k**a mi ushirikina, ila tu alikosa wa kumuuliza swali kutokana na ubusy wa muda wote kwa jerinda Walipiga hatua za taratibu kuusogelea mlango lakini kabla hawajafungua konde zito lilitua kichwani mwa sofania ambaye taratibu macho yalipoteza nuru, nguvu zikamuisha na taratibu akashuka na kutua ardhini k**a mzigo.
ITAENDELEA.
JE! nini kitaendelea unadhani na nini hatima ya mkasa huu?
Basi usikose sehemu inayofuata