Mkono Wa Msanii

Mkono Wa Msanii Huu ni ukurasa wa Riwaya, Mashairi na Tenzi: ALLY S. MATOLA

Kwa Riwaya za kusisimua zenye matukio yanayogusa hisia za jamii, zinazoburudisha na kuelimisha; pia simulizi kwa njia ya Mashairi na Tenzi 'LIKE PAGE' ili usipitwe na mambo mazuri yatakayojiri.

19/04/2023

Ramadhani inaisha. Tumwombe MOLA azikubali funga zetu na tuendeleze mema yote tuliyotenda katika mwezi huu

SIMULIZI KATIKA UTENZIJIRANI (12)IMETUNGWA NA;ALLY S. MATOLA (CHANDUGU)SIMU +255678158389DAR ES SALAAM.ILIPOISHIA SEHEMU...
26/01/2022

SIMULIZI KATIKA UTENZI

JIRANI (12)

IMETUNGWA NA;
ALLY S. MATOLA (CHANDUGU)
SIMU +255678158389
DAR ES SALAAM.

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA...

"SUMU si kitu kizuri,
Epuka hii hatari,
Kuwa nayo 'sifikiri,
Ama utaangamia.

Luka mara akanena,
Machoye yamekazana,
"Wapi inapatikana?"
Swali akanitupia.

SASA ENDELEA...

SWALI lake likagonga,
Majibu nikayapanga,
Mara mamaye katinga,
Luka kamkaripia.

"Unafanya nini hapo?
Kazi kujaza makopo!
Au nikupe kichapo?
Ondoka nakuambia!"

"Mwanangu nakushangaa,
Kwenye mlango kukaa,
Unatafuta balaa,
Mashaka utanitia."

"Utapata la kupata,
Kizaazaa kuleta,
Ukumbwe jini makata,
Msiba utanachia."

Kauli ya mama Luka,
Ilinipa kush*tuka,
Mbali sana ilifika,
Alinitia udhia.

Nikajiinua wima,
Kisha nikamtazama,
Midomo ikatetema,
Hasira zilizidia.

"Hebu ondoa imani,
Kuendekeza shetani,
Jini amemweka nani?
Ondoa mbaya hisia.

"Kwani wewe umedoda?
Kwenu si wa kawaida,
Mnazuga kwa ibada,
Wachawi kupindukia!"

"Ondoka hapa mwanangu,
Ondoka kipenzi changu,
Twende huku baba yangu,"
Kwake akamvutia.

Wakaondoka kabisa,
Ndani kwao kujitosa,
Nikabaki napepesa,
Nilishindwa kutulia.

Akamwacha Zainabu,
Ameshangaa ajabu!
Kawa kimya k**a bubu,
Macho kawatumbulia.

Hakika mtoto yule,
Mwenye sifa za upole,
Hakustahili yale,
Mbele yake kutukia.

Ikabidi nimshike,
Bega la kushoto kwake,
Kwa upole nitamke,
Pale nilipomwambia.

"Usijali sana Zai,
Japo yale hayafai,
Unadanganya uhai,
Ndivyo ilivyo dunia."

"Vitu vyako weka hapa,
Palipo mlango kwepa,
Cheza acha kuogopa,
Mimi ndani naingia."

Nilipoingia ndani,
Nikajitupa sofani,
Kichwa kikawa kazini,
Vituko kufikiria.

"Mama Luka Mama Tizo,
Wamenitia mawazo,
Kunizushia mizozo,
Wala sikufurahia.

Fikira ziliniteka,
Hadi zikanipeleka,
Usingizini hakika,
Pasipo kutarajia.

Nikaota ndoto tata,
Moyo ukaenda p**a,
Mara simu ikaita,
Ndoto ikakatizia.

(26.01.2022)

ITAENDELEA...

09/01/2022

Kimya kingi siku zote, kina mshindo mkuu,
Wasiwasi msipate, ipo kazi mwaka huu,
Vitu kwenu nivilete, vyenye ubora wa juu,
Mtavuna mwaka huu.

ALLY S. MATOLA (CHANDUGU)
@ JAN 2022

27/06/2021

Wazo zuri linahitaji utekelezaji mzuri. Usipotekeleza vizuri watatokea watekelezaji wazuri, watekeleze vizuri ubaki umetahayari

Alhamdulillahi, idd sasa imefika,Tumeswali asubuhi, twamshukuru Rabuka,Tule tunywe tufurahi, bila kuvuka mipaka,  ALIYOW...
14/05/2021

Alhamdulillahi, idd sasa imefika,
Tumeswali asubuhi, twamshukuru Rabuka,
Tule tunywe tufurahi, bila kuvuka mipaka,
ALIYOWEKA RABUKA, IDD SIKU YA FURAHA.

©ALLY SELEMANI MATOLA (CHANDUGU)

19/12/2020

JIRANI (11)
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA ....

"SIJISIKII vizuri,
Najihisi nina ngiri,
Acha nikanywe shubiri,
Naomba hapa bakia."

Beka akanitazama,
Kwa macho yenye huruma,
Kwa upole akasema,
Majibu kunipatia.

SASA ENDELEA....

"USIJALI sana kaka,
Mambo sawa nitaweka,
Kanywe dawa pumzika,
Hali nitakujulia.

K**a hali tazidi,
Usingoje sana hadi,
Uteteme kwa baridi,
Zahanati kimbilia.

K**a vipi nijulishe,
Nduguyo nikuwahishe,
Lisijezidi kasheshe,
Ugonjwa ukizidia.

Nilimsikiza vyema,
Nikamwonea huruma,
Moyoni hakunisoma,
Ukweli sikumwambia.

"Usijali naamini,
Nikishafika nyumbani,
Nitapata afueni,
Dawa nikishatumia.

"Sawa basi kaka nenda,
Usiogope k**anda,
Hili halitanishinda,
Amini nakuambia."

Tulipokubaliana,
Vizuri tukaagana,
Na yeye nikaachana,
Nami nikashika njia.

Nyumbani nikawasili,
Pote palikuwa tuli,
Ila watoto wawili,
Mlango walizuia.

Walikuwa wanacheza,
Mlangoni wamejaza,
Chupa za kuokoteza,
Hatari kuzitumia.

Ni vipande vyenye ncha,
Hovyohovyo wakiacha,
Miguu vitapekecha,
Majeraha kuwatia.

Ni Luka na Zainabu,
Watoto wenye adabu,
Licha ya zangu ghadhabu,
Wema niliwafanyia.

Nikachuchumaa kwao,
Huku ninasema nao,
Kuhusu mchezo wao,
Huku ninawatania.

"Luka na mchumba wako,
Hivi mmekosa jiko?
Oneni hapo mliko,
Mlangoni mwasikia?

Hapa mlipojiweka,
Peupe mnaoneka,
Wakiwazukia paka,
Pilau watawalia.

Wote wakatabasamu,
Kisha Luka kwa nidhamu,
"Akija nampa sumu,"
Kasema kuniambia.

Alinishangaza Luka,
Kauli alotamka,
Kichwani nikamshika,
Kisha nikamuambia.

"Sumu si kitu kizuri,
Epuka hii hatari,
Kuwa nayo 'sifikiri,
Ama utaangamia.

Luka mara akanena,
Machoye yamekazana,
"Wapi inapatikana?"
Swali akanitupia.

ITAENDELEA...

23/09/2020

SIMULIZI KATIKA UTENZI:

JIRANI (10)

MTUNZI:

ALLY SELEMANI MATOLA (CHANDUGU)

SIMU: 0678 158389
DAR ES SALAAM.

Ilipoishia...

Sana nikajitahidi,
Mawazo yasinizidi,
Nikamwachia Wadudi,
Atavyoniangazia.

Sasa endelea...

Kwa yaliyonitokea,
Moyoni nikachelea,
Kero kujiongezea,
Ofisini kubakia.

Nikazungukazunguka,
Mbele kwenye langu duka,
Kichwa changu kiliwaka,
Kwa mengi kufikiria.

Wakati natafakari,
Nikamuona Bakari,
Haraka nikafikiri,
Yafaa kumtumia.

Nikamwita aje kwangu,
Kanijia wanguwangu,
"Nambie rafiki yangu," Beka kanisalimia.

"Samahani nina shida,
Nahitaji msaada,
Ikiwa unao muda,
Ofisi nakuachia."

"Nimepata mtihani,
Hali yangu si makini,
Nataka kwenda nyumbani,
Vibaya najisikia."

"Sijisikii vizuri,
Najihisi nina ngiri,
Acha nikanywe shubiri,
Naomba hapa bakia."

Beka akanitazama,
Kwa macho yenye huruma,
Kwa upole akasema,
Majibu kunipatia.

ITAENDELEA.

03/09/2020

Tenda tendo utendapo, utende kwa makusudi,
Ukitaraji malipo, kutoka kwake Wadudi,
Sitende kwa majitapo, ili watu wakunadi,
Itafute sana pepo, siku zote jitahidi,
Tenda muda ungalipo, wewe umchaye Allah,

ALLY S. MATOLA (CHANDUGU)
DAR ES SALAAM

17/05/2020

*MOLA TUNUSURU*.

Yarabi utunusuru, na janga liloingia,
Ambalo Linatudhuru, watu tunaangamia,
Mola twangazie nuru,
suluhu kutupatia,
RABI TUONESHE NJIA, YA KUMALIZA CORONA.

'Kizazi Cha Mkatashari'
ALLY S. MATOLA {Chandugu}
DAR ES SALAAM.

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255759158385

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mkono Wa Msanii posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Mkono Wa Msanii:

Share

Category