01/09/2026
Watu wanajiuliza kwa nini Konami hawaleti kadi ya Prime Ronaldo, ikizingatiwa kuwa kadi za Messi zimekuwa zikitoka kwa wingi. Je, Konami hawataki pesa? Kadi ya Ronaldo akiwa kwenye ubora wake—alipokuwa Manchester United au Real Madrid—ingewafanya watu wanunue coin kwa kiwango cha juu sana.
Nakumbuka Mwaka 2021 Ronaldo na Messi wote kwa pamoja walikua ambassador wa PES/eFootball 🔥
Suala lililopo ni kwamba kinachowakwamisha Konami ni masuala ya leseni. Ni rahisi kwa Konami kutoa kadi za sasa hivi za Ronaldo akiwa na Ureno au Al Nassr, lakini kadi zake za zamani zinahitaji ruhusa maalum, fedha nyingi, na makubaliano ya kisheria ambayo huchukua mchakato mrefu. Maswala ya leseni pia inakwamisha kupata card za za wachezaji wengine wa zamani k**a vile Zinedine Zidane na Ronaldo Nazario