03/09/2026
Tarehe 20 Desemba 2020, beki wa zamani wa Barcelona, Gerard Piqué, aliwahi kuonekana kwenye picha akiwa amevalia jezi ya Simba SC, jambo lililozua gumzo miongoni mwa mashabiki wa soka nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa mdau mmoja wa soka, ukubwa wa jina la Piqué hauishii kwenye mitandao ya kijamii pekee, bali ni miongoni mwa wachezaji waliowahi kutengeneza historia kubwa katika soka la dunia baada ya kucheza pamoja na mastaa k**a Lionel Messi, Xavi Hernández, Andrés Iniesta, David Villa na Sergio Ramos.
Mdau huyo pia amegusia maisha binafsi ya Piqué, akimtaja k**a aliyewahi kuwa mume wa mwanamuziki Shakira, ambaye amewahi kutumbuiza kwenye matukio makubwa ya Kombe la Dunia.
Akilinganisha hilo na kampeni za jezi za Yanga, mdau huyo amesema klabu hiyo imechukua baadhi ya mbinu ambazo Simba iliwahi kutumia katika kujenga chapa yake, akisema Yanga ingekuwa bora zaidi k**a ingetumia njia zake binafsi za ubunifu.
Aidha, mdau huyo ameibua mtazamo kwamba hatua hizo huenda zikawa zinatumika kuwafanya mashabiki wa Yanga kuelekeza nguvu kwenye mambo mengine, badala ya kuendelea kujadili suala la ujenzi wa uwanja.
✍️ Ameandika Mdau wa Mpira
👉 Je, unaunga mkono hoja za mdau huyu?