Fred Ngajiro

Fred Ngajiro Fred Fabian Ngajiro (born 16/06/1987) is a Tanzanian Businessperson and entrepreneur also known as Fred Vunjabei. Full Name : Fred Fabian Ngajiro

He is the founder and CEO of Vunjabei Group Limited and President of Too Much Money Company

Nimefanikiwa Kutembelea Basketball Hall of Fame, Massachusetts USA, ilikuwa ndoto iliyotimia. Nilicheza sana kikapu na S...
23/04/2026

Nimefanikiwa Kutembelea Basketball Hall of Fame, Massachusetts USA, ilikuwa ndoto iliyotimia. Nilicheza sana kikapu na Safari yangu ya basketball ilianza nikiwa nasoma Consolata Seminary Mafinga O-Level, Ruaha Sec Iringa, Galanos Sec, Club ya Hotspring Iringa na leo nimefika sehemu yenye historia ya magwiji niliyokuwa nawafuatilia tangu zamani.

Picha hii nikiwa mbele ya sanamu la Dr. James Naismith, mwanzilishi wa mchezo wa basketball mwaka 1891 hapa Springfield, Massachusetts, inanipa hisia kubwa sana. Hapa ndipo chimbuko la mchezo huu ulioleta furaha kwa dunia nzima, ndiyo maana sehemu hii huonekana k**a nyumbani kwa basketball.

Ndani ya Hall of Fame nimeona historia za legends k**a Michael Jordan (6× NBA Champion, 5× MVP), LeBron James (all-time leading scorer, 4× NBA Champion) na Kobe Bryant (5× NBA Champion, 81 points in one game), pamoja na wengine wengi walioweka records zisizofutika.

Nimevutiwa sana kuona namna credits, records na mafanikio ya wachezaji yanavyotambuliwa na kuheshimiwa. Hii imenikumbusha kuwa kazi nzuri, nidhamu na juhudi huwa hazipotei. Ndoto yangu ilikuwa kufika hapa… leo imetimia. 🏀🇺🇸✨ Legends BasketballJourney

25/03/2026

Nimempoteza baba yangu mwingine leo, tulishirikiana kumzika Baba Vunjabei mwezi uliopita lakini fumbo hili na ugumu wake umekuwa wewe mwezi huu. RIP VANGIMEMBE

K**a hujui, niliwahi kuwa mtumishi wa umma. Nilifanya kazi Serikalini na kujifunza mambo mengi sana ndani ya miaka yangu...
19/03/2026

K**a hujui, niliwahi kuwa mtumishi wa umma. Nilifanya kazi Serikalini na kujifunza mambo mengi sana ndani ya miaka yangu ya utumishi, ikiwemo kushiriki kwenye operations nyeti kadhaa zilizoniongezea uzoefu, ujasiri na ugumu wa roho

Baada ya muda, nikaona hii njia sio yangu. Nikaamua kujitoa na kwenda kupambana Kariakoo — kwa imani moja tu: IPO SIKU.

Watu wanasema Vunja ni wakishua? Je ni kweli? Baba yangu ni kweli alikuwa mdosi kiaina ila sio tajiri sana, binafsi sijawahi kubeba jukumu kubwa la kusaidia familia yangu. Nilianza na zero — sio negative. (Maana kuna wengine wanaanza na mizigo ya kifamilia, hiyo tayari ni negative). Hiyo peke yake namshukuru Mungu sana.

Kitu kikubwa nilichopewa na baba yangu — ambacho si wengi hupata — ni urithi wa elimu mbili kwa wakati mmoja:
Elimu ya DARASANI na elimu ya MTAANI
Huo ulikuwa mtaji mkubwa kuliko pesa. Mpaka leo, sijawahi kuhitaji msaada wake kwenye mtaji wala connections.

Baba yangu hakuwa muumini wa kumpa mtu mtaji wa moja kwa moja. Aliamini uanze kidogo kidogo, ujenge hasira, njaa na uchungu wa mafanikio.

Ajira yangu ya kwanza baada ya chuo kikuu ilikuwa kwenye taasisi ya fedha (sitaitaja). Nilikuwa Afisa Mikopo, na mshahara wangu wa net ulikuwa TZS 320,000. Baba alisema huna familia wala majukumu jifunze ku-SAVE

Sikuwahi kulalamika.
Kwa sababu nilijua — ni suala la muda.
Na nilikuwa naamini, kwa dhati — IPO SIKU.

The last King of Sinza

Siku ya kwanza kuingia China, hapo hali ni tete kila mchongo ukiskilizia haukubali.  Relax, kimoyomoyo sema IPO SIKU 🙏
16/03/2026

Siku ya kwanza kuingia China, hapo hali ni tete kila mchongo ukiskilizia haukubali.

Relax, kimoyomoyo sema IPO SIKU 🙏

We will, next time 🙏
12/03/2026

We will, next time 🙏

Nyimbo yangu pendwa mpk leo ni Shida ndogo ndogo nakumbuka niliipenda mpk tukaishoot Guangzhou, China, i will always be ...
10/03/2026

Nyimbo yangu pendwa mpk leo ni Shida ndogo ndogo nakumbuka niliipenda mpk tukaishoot Guangzhou, China, i will always be your number one SHABIKI young bro, HBD

Leo tunacheza mechi ya nne na ya mwisho kwenye ngwee hii ya kufuzu robo fainali tukiwa na rekodi ya kutokupoteza kwa mec...
07/03/2026

Leo tunacheza mechi ya nne na ya mwisho kwenye ngwee hii ya kufuzu robo fainali tukiwa na rekodi ya kutokupoteza kwa mechi zote 3 tulizocheza (the unbeaten) Karibuni muone game ya kibabe leo na Clouds Fm. Mpira ni uwekezaji, vilabu vinaweka hela kwa heshima ya ligi yetu SAMIA CUP.

New Levels New Devils 💸💸
03/03/2026

New Levels New Devils 💸💸

Nichukue nafasi hii kuwashukuru wote ambao kwa nafasi moja au nyingine mmeshiriki katika kumpumzisha Mzee wangu “Sisi kw...
11/02/2026

Nichukue nafasi hii kuwashukuru wote ambao kwa nafasi moja au nyingine mmeshiriki katika kumpumzisha Mzee wangu “Sisi kwa Sisi” mpaka kufika hapa tumemaliza salama na kurudi Dar.

Lakini pia wale rafiki zangu wote ambao mlishindwa kusafiri mpaka Iringa karibuni nyumbani Mbezi Beach mtaa wa kwa Mwamunyange “Vunjabei Appartments”
Siku ya Jumamosi kuanzia saa 6 Mchana tupeane mkono wa pole na kusherehekea maisha aliyoyaishi mzee hapa duniani( Miaka 71)

Mbuzi 30 zitasalimu amri ili siku yetu iende sawa not in sorrow, but in gratitude for the legacy he left in our hearts.Please come to celebrate his life and the legacy of love, unity, and hard work that he shared with us.

Big brother
06/02/2026

Big brother

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fred Ngajiro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share